Sunday 29 November 2020

Iran yaishtumu Israel kwa kuhusika katika mauaji ya mwanasayansi wake mkuu

...


Iran imeinyooshea kidole cha lawama Israel kuhusika katika mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkuu wa nyuklia na mwanajeshi Iran, na kuahidi kulipiza kisasi kwa wale waliohusika na mauaji hayo.

Mohsen Fakhrizadeh aliuawa katika operesheni ya kushangaza Kaskazini mwa Tehran. Kwanza gari ndogo lililipuka barabarani, mbele ya gari lake, kabla ya kushambuliwa kwa risasi.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, ameishutumu moja kwa moja Israel kwa kuhusika katika mauaji hayo.

Jina la Mohsen Fakhrizadeh lilitajwa mnamo mwezi Aprili 2018 na Waziri Mkuu wa Israeli katika hotuba yake kwenye televisheni. Benyamin Netanayhu alimshtumu kuwa mmoja wa maafisa wakuu wa mpango wa nyuklia wa Tehran. "Kumbukeni vizuri jina hili: Fakrizadeh", Bw. Netanyahu alisema wakati huo.

Mwanasayansi huyo mwandamizi pia alikuwa kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger