Saturday 5 March 2016

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi kwa mwaombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;
1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
2. Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
3. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi

Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=
3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni Tshs 50,000/=

Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.

Imetolewa na: 
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi
4 Machi, 2016

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger