Monday 28 March 2016

Mechi ya Taifa Stars na Chad Yaota Mbawa........Chad Wamejitoa Kwenye Mashindano Kwa Madai Kwamba Hawana Fedha

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Shirikisho la Soka la Chad, limetangaza kuiondoa timu yake ya taifa katika mechi za kuwania kufuzu Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Gabon mwakani.

Tanzania na Chad zilikuwa zicheze leo, mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali hizo. Katika mchezo wa kwanza, Stars iliifunga Chad bao 1-0, mchezo uliofanyika kwenye mji wa N’Djamena.

Mtandao wa Twitter wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF ulithibitisha jana kupokea taarifa ya Chad na tayari limetangaza adhabu ya kuisimamisha nchi hiyo.

“Shirikisho la Soka la Chad limeondolewa kushiriki mashindano yajayo ya Afcon na linatakiwa kulipa faini ya Dola 20,000,” ilisema taarifa hiyo ya CAF kwa kifupi.

Kujitoa kwa Chad kumevuruga msimamo wa Kundi G la michuano hiyo kwani kwa mujibu wa Kanuni za Mashindano ya CAF, Ibara ya 58 inasema: “Ikiwa timu itajitoa kwenye mashindano hatua za awa li za makundi, matokeo yote yatafutwa (pointi, mabao ya kufunga na kufungwa).

Ibara ya 59 ya kanuni hizo za mashindano inasema Kamati ya Maandalizi itatoa adhabu kali kulingana na uzito wa timu kujitoa.

Kwa hatua hiyo, Misri iliyoshinda mabao 5-1, Nigeria 2-0 na Tanzania 1-0 zitakuwa zimepoteza matokeo hayo.

Kwa mujibu wa kanuni, Misri sasa itakuwa na pointi nne ikifuatiwa na Nigeria pointi mbili na Tanzania itabakia na pointi moja.

Michezo itakayobakia ni ya Misri kuifunga Tanzania 3-0 na sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria wakati Taifa Stars inabakiwa na pointi moja ya suluhu na Nigeria. Nigeria itabakia na pointi mbili za Tanzania na Misri kabla ya mchezo wao wa kesho kwenye mji wa Alexandria.

Mratibu wa timu ya Taifa, Msafiri Ahmed Mgoyi alikiri kuziona taarifa za Chad kutocheza mchezo na kusema: “Tumezipata taarifa hizo lakini bado tunaendelea kujiandaa kama kawaida mpaka pale tutakapopata taarifa rasmi kutoka TFF ambao wanapokea maelekezo kutoka Caf.”

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi alisema jana kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa iwapo Chad itashindwa kucheza mchezo, uamuzi wa mwisho utatolewa na chombo husika kinachosimamia mashindano hayo.

“Hadi sasa timu ya Chad haijatua nchini kwa ajili ya mechi ya kesho. TFF itatoa taarifa kamili leo usiku (jana) baada ya kikao cha maandalizi ya mchezo. Kwa mujibu wa kanuni za CAF Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Caf ndiyo inatoa uamuzi,” alisema Malinzi.

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco alisema jana kuwa benchi la ufundi na wachezaji kama ilivyo kwa watu wengine nao wamezipata taarifa hizo ingawa haziwezi kuathiri saikolojia yao kwa namna yoyote ile.

“Sisi kwa upande wetu tunafahamu mechi ipo kama kawaida kwani hatujapewa taarifa yoyote kutoka kwa TFF, hivyo kama ni kweli au la haiwezi kuvuruga mipango na maandalizi yetu kama timu, ingawa ufafanuzi zaidi tunausubiri,” alisema Morocco.

Wakati hali hiyo ikitokea, mashabiki wa soka walikwishaanza kukata tiketi za mchezo kati ya Sh25,000 ikiwa ni kiingilio cha juu na Sh5,000.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger