Thursday 13 May 2021

RPC MAGILIGIMBA AONYA WAVUNJIFU WA AMANI SIKUKUU YA EID EL-FITR SHINYANGA….ASHUKURU WADAU KWA USHIRIKIANO

Share:

Project Officer – SAUTI Youth Project at World Vision

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

The SAUTI YOUTH Project Officer, will be responsible of  Formation and mobilizing CVA (Citizen Voice Action) Youth groups, To empowers the youth to have the capacity to engage with the communities and monitor relevant government services and policy influence to climate change trough CVA Preparation of Monthly and quarterly project report Monitoring of the groups, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

NIMEMLIPIA ADA YA CHUO KIKUUU MCHUMBA WANGU NA BAADA YA MASOMO ETI ANATAKA KUOLEWA NA MWANAUME MWINGINE

  Sisi wanaume tunatumia nguvu nyingi katika kutafuta pesa na mtu yoyote akichezea jasho lako haki inauma sana.

Nimi naitwa Mbaraka mkazi wa Gongo la Mboto najishughulisha na Biashara ndogo ndogo hapa mjini. Katika pitapita zangu nilikutana na msichana anaitwa Rehema.Nilimfahamu Rehema kupitia kwa dada yake Zainabu ambaye alikuwa rafiki yangu sana na mteja wangu wa uhakika.

Nilivutiwa sana muonekano na tabia aliyekuwa nayo Rehema hadi ikafika hatua ya kuwa wapenzi.Kipindi nafahamiana nae alikuwa amemaliza kidato cha sita hivyo alikuwa kwa dada yake Zainabu akiwa anasubiri matokeo ya mtihani kutoka.

Kulingana na jinsi tulivyopendana dada yake alikuwa anamruhusu anakuja kazini kwangu na kunisaidia kazi mara kwa mara. Miezi 3 kupita matokeo yalitoka na yeye alikuwa miongoni mwa wenye sifa za kujiunga masomo ya Chuo Kikuu. Kwa Upande wangu nilifurahi sana kuona mke wangu mtajariwa anaenda kujiunga na masomo ya Chuo Kikuu na muda si muda alijiunga na chuo cha Makumira Arusha kwa kozi ya Sheria.

Siku ilipowadia ya kuripot chuoni niliweza kwenda nae hadi chuo na kumpangishia sehemu ambayo atakuwa anaishi. Semister ya kwanza ilipoisha mchumba wangu alirudi Dar na kufikia kwangu maana dada yake na mama yake walikuwa wanafahamu mahusiano yetu na ada ya kujiunga chuo mimi ndiyo nilimlipia mchumba wangu maana mama yake alikuwa amekosa pesa ya kumlipia hata mkopo kutoka kwa serikari hakupewa.

Baada ya likizo alirudi chuo kwa ajili ya semister ya pili ila muda wa kufunga ulipowadia Rehema hakuja Dar au kwenda kwao Mtwara bali alibaki Arusha. Mimi nilifunga safari hadi Arusha nikakaa nae kwa siku mbili tu na kurejea Dar na katika mazungumzo nilimuuliza mbona hukuja Dar akaniambia kuwa semester ya pili ilikuwa ngumu kwake.

Tangu hapo Rehema kuna muda alikuwa anakuja Dar na muda mwingine haji kabisa . Hiyo tabia iliniumiza sana ikabidi nitafute usaidizi ndipo nilikutana na rafiki yangu Amimu na kuniambia kuwa Dr.Kiwanga anaweza nisaidia kwa sababu huyo Dr ndiye alimsaidia yeye na mke wake kupata mtoto baada ya kuhangaika kwa miaka 6 wakitafuta mtoto na bila mafanikio.

Alinipatia namba ya simu ya Dr. Kiwanga ambayo ni +254 769404965. Nilipanga safari kutoka Dar Hadi Kenya kwa Dr. Kiwanga niliweza fika kwenye ofisi ya Kiwangadoctors kisha kueleza shida iliyonileta, .Ndipo niliambiwa kuwa mchumba wangu Rehema kuna Mwalimu ambaye anataka kumuoa baada ya masomo.

Kulingana na maelezo ya Dr Kiwanga asilimi 100 nilikubali maana kuna kipindi mchumba wangu alikuwa anawasiliana na mwalimu moja mara kwa mara nilikuwa nauliza anasema kuwa ni mtu anawasaidia tu wala hakuna kitu kingine.Mwalimu yule mwaka wa kwanza hadi wa nne ila kwa kuwa sikufika chuo kikuu hivyo sikuweza fahamu zaidi.

 Nikiwa ofisini kwake Dr.Kiwanga akaniambia kuwa atanisaidia na relationship spells hadi nimpate Rehema kwa muda wa masaa 48.Baada ya kutoka ofisini kwake haukupita muda Rehema alijileta hadi kwangu na kuomba tufunge ndoa haraka maana kachoka na kusumbuliwa na wanaume,bila kupoteza muda nikijulisha baadhi ya ndugu na Jamaa kisha ndoa ikawepo na kwa sasa tuna watoto wawili na Rehema kanisaidia Biashara yangu kupanda kwa asilimia 75.

Natoa uwito kwa mwenye shida ya mapenzi,kumpata mpenzi wa ndoto zako,Nguvu za kiume,mwenye nuksi na mikosi wasiliana Dr. Kiwanga kwa Namba: +254 769404965 Website: www.kiwangadoctors.com Emails: kiwangadoctors@gmail.com

Share:

Project Manager at North Mara Gold Mine Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POSITION DESCRIPTION: North Mara Gold Mine Limited is seeking to recruit one (01) Project Manager to join North Mara Gold Mine team. The successful candidate for this role will report to Engineering Manager and the role holder will be involved in initiation, planning, execution, monitoring/control and closure of capital and maintenance-based projects, to meet company business targets in accordance with Barrick […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Data Manager at ASUTA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Title:  Data Manager Job Location: Dar es salaam. Temeke District Organisation: Asasi ya Uwezeshaji Tanzania – ASUTA Asasi ya Uwezeshaji Tanzania – ASUTA working in partnership with FHI 360 on  Epidemic Control (EpiC) which is a global project funded by the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and the U.S. Agency for International Development (USAID) […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Wizara Ya Madini Kufanyia Kazi Mapendekezo Sita Ya Wachimbaji Wakubwa

 


Na Grace Semfuko, MAELEZO.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema Wizara yake itayafanyia kazi mapendekezo sita, yaliyotolewa na Wachimbaji wakubwa na wa kati wa madini kwenye kikao cha wadau wa sekta hiyo waliokutana Mei 12, Jijini Dar es Salaam.

Mapendekezo hayo ni pamoja na kuweka vivutio na sera nzuri za biashara ya Madini ili kuwavuta wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi, kufanya tafiti za madini, kuweka mazingira wezeshi ya biashara hiyo, kuwa na ulinzi na usalama wa uhakika wa biashara hiyo, uibuaji wa vipaji na mafundi wa madini wa kitanzania na uboreshwaji wa mindombinu kwenye maeneo ya migodi.

Akifungua mkutano wa siku moja wa majadiliano baina ya Serikali na Wachimbaji wa Madini wakubwa na wa kati, wenye lengo la kukuza sekta hiyo nchini, Biteko amesema Wizara yake inayafanyia kazi mapendekezo ya wachimbaji hao ili yaweze kuleta tija ya kiuchumi.

“Naomba niwahakikishie tutayafanyia kazi mapendekezo yenu yote mliyoyatoa hapa, lengo letu ni kuhakikisha biashara hii inazidi kukua na kuleta tija ya kiuchumi” amesema Waziri Biteko.

Amesema Serikali inaendelea kusimamia sekta ya madini ili iendelee kuwa na tija, kutokana na sekta hiyo kuongoza kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia saba kutoka asilimia 3.8 ya mwaka 2015, na kutajwa kuongoza kwa kuliingizia Taifa pato la kigeni.

Biteko pia amesema asilimia 52.4 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa nje ya nchi, zinatokana na mazao ya madini na hivyo kuifanya sekta hiyo izidi kuimarika kwenye mapato na kuchangia sekta nyingine katika ukuaji wa uchumi.

“Sekta ya Madini imetoka mbali, imepita katika historia ndefu sana, historia mbaya na nzuri, imetoka kwenye kundi ambalo biashara ilikuwa ikifanywa kwa kificho, leo imekuwa ni sekta ambayo biashara inafanywa kwa uwazi, mchango wake unaweza kupimwa katika maeneo mbalimbali ikiwepo kukuza uchumi wa nchi kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia 7” amesema Biteko.

Naye, Mwenyekiti wa Chemba ya Madini Mhandisi Philbert Rweyemamu ameishauri Wizara hiyo, kujadiliana na wadau ili kuangalia namna bora ya kuongeza migodi mipya ya uchimbaji wa madini, na kuongeza mitaji kutoka katika masoko ya hisa ya nchi za nje.

“Tunahitaji pesa za wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa sababu soko la hisa la Dar es Salaam halijakidhi mahitaji ya sasa, na mara nyingi pesa za kuanzisha hii miradi zinatoka kwenye masoko makubwa ya hisa ya nchi za nje, kwa hiyo tunashauri Wizara tujadiliane kwa yale ambayo tunafikiri kama yakiwekewa mkazo au yakabadilishwa, yataongeza tija na tutaona migodi mipya ikianzishwa” amesema Mhandisi Rweyemamu.


Share:

Waziri Mkuu Azitaka TPA, TRA, TASAC NA EGA Zifanye Kazi Kwa Ushirikiano

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam

Ameyasema hayo jana(Jumatano, Mei 12, 2021) alipotembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona utendaji wa bandari hiyo.

“TPA endeleeni kuiimarisha bandari yetu, hii ni sura ya uchumi wa nchi yetu, zungumzeni lugha moja ya uwajibikaji, TRA muwepo maeneo yote yanayohitaji uwepo wenu na muda wote wateja wetu wahudumiwe ili bandari yetu iendelee kuwa bora. Nchi nyingi zinatutegemea”

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ihakikishe mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS) unafanya kazi kwa ufanisi ili kupuinguza malalamiko ya wateja kuhusu mfumo huo.

“Dosari zote za mfumo wa TANCIS zifanyiwe kazi, mfumo usituharibie, mnapoona kuna madhaifu fanyeni marekebisho ya haraka, tunataka wateja waingie na kutoka kwa muda mfupi” Amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Kamishna Mkuu wa TRA apeleke watumishi katika mizani ya TANROADS iliyopo Kurasini Dar es Salam ili kurahisisha ukaguzi wa ‘seal’ pale ambapo magari yamezidisha uzito na yanahitaji kukaguliwa

“TRA kuna foleni kwenye mizani, hakuna watu, kuanzia leo peleka watumishi pale tunataka ukaguzi uwe muda wote”.

Akitolea ufafanuzi kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya uwepo wa foleni bandarini hapo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Eric Hamissi amesema suala hilo halina ukweli na hakuna dereva anayekaa bandarini kwa siku tatu.

“Hata sisi tulishangaa sana kuona ile clip, haina ukweli wowote, dereva Omari Mambo Mei 10, 2021 aliingia saa nane mchana, na ilipofika saa 10.38 alishusha mzigo na kuondoka saa 11.00 jioni”

Aliongeza kuwa kwa sasa asilimia arobaini ya eneo la bandari lipo kwenye ujenzi ikihusisha ujenzi wa njia nne za barabara na ujenzi wa gati namba moja mpaka saba lengo ni kuifanya bandari iweze kuhudumia wateja kwa ufanisi mkubwa “mpaka sasa gati namba moja mpaka tano zimekamilika na gati namba sita na saba zitakamilika mwezi Agosti,2021”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva wa malori wanaoingia na kutoka kwenye Bandari ya Dar es Salaam wamesema wanaridhishwa na utendaji kazi wa bandari kwani hawatumii muda mrefu kuingia na kutoka bandarini hapo.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Ummy : Uuguzi ni Taaluma Sio Siasa


Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wauguzi ni miongoni mwa wataalamu wa Afya wanaopaswa kuheshimiwa na kupewa thamani inayostahili na wasichukuliwe kisiasa.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani yakiyofanyika Mkoani Manyara tarehe 12 Mei,2021.

Amesema uuguzi ni fani adhimu na kuwataka viongozi wa Mikoa na Wilaya kuacha kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

“Viongozi wa Mikoa na Wilaya niwatake kuelewa kuwa uuguzi ni taalamu adhimu na muache kuamuru wawekwe ndani au kuwachukulia hatua kali ambazo haziendani na taalum yao kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi, hili tuliache mara moja,”amesema

Ameongeza “Kama Muuguzi amekosea akashitakiwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga ambapo atachukuliwa hatua kwa matakwa ya taaluma yake na sio kwa utashi wa kisiasa.”

Hata hivyo, amesema kiongozi yeyote atakayemuweka ndani muuguzi awe amethibitisha ameiba lakini kwa tuhuma nyingine akashitakiwe kwenye Baraza lao la Kitaaluma.

Pia Mhe.Ummy amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kuwakatalia wauguzi kwenda kusoma mara wanapopata fursa za kwenda kujiendeleza kielimu.

“Wauguzi lazima wathaminiwe kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wagonjwa sababu mara zote ukienda hospitali Daktari atakuona kwa muda mchache sana na wakati mwingi utakuwa na nesi katika kukuhudumia hivyo wapewe moyo,”amesema.

Amewapongeza na kuwashukuru Wauguzi kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa wimbi la ugonjwa wa Corona na amewataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuokoa maisha ya watu.

Akijibu hoja zilizowasilishwa na Wauguzi katika risala yao, Waziri Ummy amesema suala la muundo linafanyiwa kazi na lilishawasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua zaidi.

Mhe. Ummy amesema kwa sasa Madaktari na wauguzi wafanye kazi kama timu moja ili kuleta matokeo chanya kwa jamii inayowategemea na hayo ya kiutawala yataendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi.

Kuhusu posho ya majukumu, amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaangalia ni namna gani inaweka mazingira bora kwa wauguzi walioko TAMISEMI kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana.

“Ofisi yangu itahakikisha inatoa kipaumbele katika kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi wa Afya kwa kujenga nyumba za kutosha ili watumishi hao waweze kukaa kwenye vituo vyao na kufanya kazi kwa amani,”amesema.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ummy ametoa zawadi ya sh.500,000 kwa Muuguzi Aldolefina Shayo wa Zahanati ya Kilangare iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ambaye amevunja rekodi ya kuhudumia wagonjwa hamsini kwa siku bila kunung’unika na leo ameshindwa kushiriki maadhimisho hayo kwa kuwa yuko peke yake kwenye zahanati hiyo na hakuna mtu wa kumsaidia.

Waziri Ummy amesema katika ajira mpya zilizotangazwa watapelekwa wauguzi wawili na Mganga mmoja ili kuboresha zaidi huduma za Zahanati hiyo.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 13



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 12,2021


Share:

SIKUKUU YA EID -EL- FITR NI IJUMAA MEI 14


Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr ni Ijumaa Mei 14, 2021.

Amesema leo Mei 12, 2021 mwezi haujaonekana hivyo waumini wa dini ya Kiislamu wataendelea kufunga kwa siku ya 30.
Share:

Wednesday 12 May 2021

Museveni aapishwa kuiongoza Uganda kwa muhula wa sita


Rais Yoweri Museveni amekula kiapo hii leo nchini Uganda kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa sita.


Museveni ataiongoza Uganda kwa miaka mengine mitano, ikiwa ni muhula wake wa sita madarakani.

Aliingia madarakani Januari 1986 kwa mapinduzi ya kijeshi, hadi utakapofika uchaguzi mwingine 2026 atakuwa madarakani kwa miaka 40, sawa na miongo minne. Wakati huo akiwa na umri wa miaka 81.

Alishinda uchaguzi wa Januari 14, 2021 kwa kuwabwaga wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais kwa ushindi wa asilimia 58 ya kura zote.


Share:

Usichelewe .....Pakua sasa hivi App Ya Mpekuzi Ikiwa na Maboresho Mapya. Ipo PlayStore

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Zaidi ya wagonjwa Mil. 20 Watibiwa 2020/21- Serikali

 


Na Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Maghembe amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 wauguzi waliopo katika vituo vya kutolea huduma wamehudumia wagonjwa wapatao milioni 20 waliofika katika vituo hivyo kupata huduma za kiafya.

Akitoa salamu za Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Manyara. Dkt. Magembe ameyasema, huduma zilizotolewa kwa wingi ni pamoja na huduma za Nje maarufu kama huduma za Mkoba  ambazo zilihusiaha takribani watu milioni 1.2 ambazo zimejikita zaidi katika kumhudumia mama na mtoto.

Dkt. Magembe, amesema wauguzi hao walifanikiwa kuwazalisha kina mama takribani laki moja na kutoa huduma dawa ya usingizi kwa wajawazito 25,000.

Dkt. Magembe, alibainisha mahitaji ya wauguzi wa sasa ni 41,000 lakini waliopo katika vituo vya kutolea huduma ni 19,000 ambapo ni sawa na asilimia 41 ya mahitaji.

Kuhusiana na wauguzi walio ajiriwa katika mwaka wafedha wa 2017/2019  ni 3,625 ambapo watumishi hao waliajiriwa na Serikali pamoja na wadau  wa Taasisi ya Benjamini Mkapa.

"Na katika ya ajira 2,720 za kada ya afya zilizotangazwa Mei 9 mwaka huu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, jumla ya ajira za wauguzi miongoni mwake ni 954 sawa na asilimia 35 ya ajira zote zilizotangazwa."

Siku ya wauguzi husherehekewa tarehe 12 mwezi Mei ya kila Mwaka, ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Florence Nightngale, mwana takwimu na mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa. Maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani kitaifa yamefanyika mkoani Manyara na kubebwa na kauli mbiu “Wauguzi sauti inayoongoza, Dira ya huduma ya afya”


Share:

Shilingi milioni 61 kujenga barabara na makalvati 14 Wilayani Same


 Na Mathew Kwembe, Dodoma
Serikali imetenga shilingi milioni 61 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Makanya kwenda kwenye Machimbo ya Jasi Wilayani Same kwa kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita moja pamoja na ujenzi wa makalvati 14 katika mwaka wa fedha 2021/22.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Zuena Athumani Bushiri, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.David Silinde amesema serikali itatoa kipaumbele cha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami katika bajeti zijazo ili kuiboresha na kurahisisha usafirishaji wa Jasi.

Amesema kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha barabara hii inapitika muda wote na ndio maana imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara.

Naibu Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2019/20 Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Same umefanya matengenezo ya barabara ya Makanya hadi kwenye Machimbo ya Jasi maeneo korofi yenye urefu wa kilomita 3.5 kwa gharama ya Shilingi milioni 77.3.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/21 TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Same   imefanya matengenezo ya barabara hiyo kipande chenye urefu wa kilomita mbili kwa kiwango cha Changarawe kwa gharama ya Shilingi milioni 49.4.

Barabara ya Makanya hadi kwenye machimbo ya Jasi Wilayani same ina urefu wa kilomita 40.9. Kipande cha kilomita 4.5 cha barabara hii kimeinuliwa kwa kujengwa tuta kati ya kilomita 14.5 zinazotakiwa kujengwewa tuta kwa kiwango cha changarawe.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe.Silinde amesema katika mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2020/21 barabara za kutoka Rubanga, Isurwa, Butundwe, Mkoba, Kukuruma, Kamhanga, Kishinda na Mkorani zimetengewa Shilingi milioni 318.8 kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 33 na wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa kazi.

Amesema matengenezo ya barabara hii yanatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2021 na kuwa vijiji vilivyotajwa vinaunganishwa na barabara za Mkoba bridge – Isulwabutundwe – Lubanga yenye urefu kilomita 15  na Geita – Isamilo – Mkolani (Busekeseke) yenye urefu wa kilomita 18 ni barabara muhimu sana wananchi.


Share:

Jaji Imani Aboud Apendekezwa Kugombea Urais Wa Mahakama Ya Afrika


Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo.


Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu…


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania inayo imani na Jaji Imani Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kwa Taifa na kwa wanawake kuendelea kushika nyadhifa kubwa sio Serikalini tu, bali kwenye taasisi na mashirika ya kimataifa.


Majaji wengine wanaogombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon ambapo Hayati Jaji Augustino Ramadhani ndie alikuwa Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.




Share:

Uzinduzi Msimu wa Ununuzi wa Pamba Kitaifa 2021/2022; Wadau Watakiwa Kushirikiana ili Kuongeza tija ya Zao la Pamba


Msimu wa ununuzi wa Pamba kitaifa 2021/2022 umezinduliwa wilayani Busega, mkoani simiyu. Akizindua, msimu wa ununuzi wa pamba, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Mwera amesema ushirikiano wa wadau wa kilimo cha pamba utaongeza tija ya zao hilo.

“Zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya kimkakati, hivyo wadau washirikiane ili kuongeza tija”, alisema Mhe. Mwera. Katika kuleta tija ni vyema wakulima kufuata kanuni za kilimo bora ikiwemo upandaji wa pamba kwa nafasi inayotakiwa ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo, aliongeza Mhe. Mwera.

Awali, Mkurugenzi wa bodi ya pamba, Bw. Marko Mtunga amesema uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba una manufaa makubwa hivyo Busega imepewa heshima kubwa, na hii imetokana na kazi kubwa ya usimamizi mzuri wa viongozi wa Wilaya katika kilimo cha pamba. “Katika msimu wa 2020/2021, wilaya ya Busega imezalisha takribani kilo milioni 3, lakini msimu wa mwaka 2021/2022 tunategemea uzalishaji zaidi ya kilo milioni 10” aliongeza, Mtunga.  

Aidha, Mhe. Mwera amesema licha ya Wilaya kuwa na uzalishaji mzuri katika zao la pamba, lakini changamoto kubwa inayowakabili wakulima, ikiwemo wadudu. Hali hiyo imewafanya wakulima wengi kushindwa kutambua jinsi ya kukabiliana na wadudu wanaoshambulia zao la pamba, hivyo bodi ya pamba itoa elimu zaidi kwa wakulima ikiwemo elimu ya kupambana na wadudu.

Kauli mbiu ya uzinduzi wa msimu ununuzi wa pamba kitaifa 2021/2022 inasema “Tuboreshe Ubora na Usafi wa Pamba kwa Uhakika wa Soko na Malipo kwa Wakati”. Kauli ambayo imeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwa wakulima wa zao la pamba. Wanunuzi wa pamba walioshiriki uzinduzi huo wamesema wapo tayari kununua pamba na kuahidi wakulima watalipwa kwa wakati. Katika uzinduzi huo, Serikali imetoa bei elekezi ya zao la pamba kwa msimu wa 2021/2022, ambapo pamba daraja A itanunuliwa kwa Tzs 1,050 na daraja B itanunuliwa kwa Tzs 525.

Baadhi ya wa wakulima wa pamba Wilayani Busega wanasema Serikali, wakulima na wadau wengine wanapaswa kushirikiana ili kuongeza uzalishaji wa zao la pamba nchini. Kwa upande mwingine wameiomba Serikali kutoa elimu zaidi ya zao hilo ikiwemo kanuni bora za ulimaji wa zao hilo.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger