Friday 26 April 2024

WAKULIMA VIJANA WAELEZA FAIDA ZA MATUMIZI YA MBEGU BORA

...
 
Mkulima kijana kutoka jijini Arusha anayefahamika kwa jina la Edward Jacob anayejihusisha na kilimo cha Mbogamboga na Matunda ameeleza faida za matumizi ya Mbegu bora na matarajio yake kuelekea Bajeti ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 itakayosomwa Bungeni jijini Dodoma mnamo Mei 02 na Mei 03, 2024.

Miongoni mwa faida nyingi alizoeleza ni pamoja na kupata mazao yenye ubora, yasiyoharibiwa kirahisi na wadudu pamoja na kupata mavuno ndani ya muda mfupi.


Sambamba na faida hizo Edward pia ameeleza matarajio yake kwa Bajeti ya kilimo kwa Mwaka 2024/2025 kuwa ni kuendelea kupata mbegu hizo zinazozalishwa na taasisi zinazotambulika nchini pamoja na kupata pembejeo kwa urahisi zaidi ili kuendelea kupata mazao bora.


Kwa upande wake, Agnes Sachi ambaye pia ni kijana anayejihusisha na Kilimo cha Mbogamboga jijini Arusha ameeleza namna kulima kwa kutumia mbegu na miche bora kulivyomnufaisha na matarajio yake kuelekea bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2024/2025.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger