Sunday 28 April 2024

KAMPENI YA USALAMA BARABARANI YA AMEND YAWAFIKIA WAENDESHA BODABODA HALE WILAYA YA KOROGWE

...











Na Oscar Assenga,KOROGWE.

KAMPENI ya Usalama barabara inayotolewa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana an Shirika la Amend Tanzania kupitia Ubalozi wa Uswis nchini umewafikia waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda eneo la Hale wilaya ya Korogwe huku ikieleza zaidi ya waendsha Bodaboda kati ya 5 mpaka 10 wanapoteza maisha kwa siku katika Mkoa wa Tanga.


Huku ikibainishwa kwamba wengine wakipata ulemavu kutokana na ajali za barabarani na kubwa ambalo limekuwa likichangia wa na kutokuzingatia sheria za usalama wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto pamoja na kuendesha mwendokasi.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Hamis Mbilikila wakati wa utoaji wa elimu katika kampeni ya usalama barabarani iliyokuwa ikitolewa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Amend kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswis Tanzania iliyofanyika Hale wilayani Korogwe .

Hali hiyo inachangia kwa asilimia kubwa kupelekea kupoteza nguvu kazi kubwa ya vijana kutokana na asilimia kubwa kujiajiri kupitia sekta hiyo bila kuwa na elimu ya sheria za usalama barabarani wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.

Alisema ajali hiyo zinatokana na asilimia kubwa kutokuzingatia sheria za usalama barabarani hivyo uwepo wa mafunzo hayo ambayo yanatolewa na Shirika hilo kwa mkoa huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali zinazotokana na madereva hao wa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Aidha alisema kwamba mafunzo hayo wanaamini yatakuwa na tija ka madereva hao ambao huku akiwataka pia kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi ajali zinazopotekea kweye maeneo yao badala yake watoe taarifa kwenye mamlaka husika.

“Ndugu zangu bodabda ajali zinapotkea msijichukulie sheria mkonono mtoe taarifa mkoa wa Tanga ni wa kimkakati tumeona mambo mengi yanafanyika kuna bomba la mafuta kuna wageni wengi Bandari yetu imefunguka kuna njia inaunganisha nchi jirani na Kenya na hapa hale ni barabara kuu kuna watu wengi wanapita hivyo ni lazima tufuate sheria za usalama barabara”Alisema

Aidha aliwataka waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuacha kujichukulia sheria za usalama barabarani kutokana na kwamba hawawezi kujua watakumbana na jambo gani lakini pia madhara ya ajali ni kupoteza maisha na vifo .

“Vijana wengi wanapoteza maisha kupitia vyombo hivyo pikipiki zimekuja kutusaidia na asilimia kubwa kwenye vijiji pikipiki ni muhimu hivyo kutokana na adhari hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Amend kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswis wameona wawape mafunzo hayo ili tuweze kujua sheria za usalama barabarani”Alisema

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Miradi kutoka Shirika la Amend Tanzania Scolastica Mbilinyi alisema lengo lao ni kupeleka mafunzo kwenye maeneo mbalimbali ili kuwafikia watu wengi sana kwenye kampeni ya usalama barabarani na sasa wanayafikia maeneo ya pembezoni ambao ni mpango kazi wa dunia kupunguza ajali angalau kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

“Tulianza wilaya ya Tanga na baadae Mkanyageni wilaya ya Muheza walianza leo tupo Hale wilaya ya Korogwe na tumepanga kupeleka elimu hii kwenye maeneo mengi kwa sababu wengi hawana elimu ya usalama barabarani na itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi zaidi baada ya kupata elimu hii”Alisema

Afisa Mradi huyo aliwataka bodaboda wafuata sheria za usalama barabarani ikiwemo wahakikishe wanatembea spidi inayotakiwa na sehemu kwenye matuta waweze kupunguza mwendo ikiwemo kuhakikisha pikipiki walizokuwa nazo zimekamilika kwa sabababu itawasaidia kupunguza ajali kwa asilimia kubwa .

“Lakini sisi tunatoa elimu ya usalama barabarani kwa shule za Sekondari,Msingi na kwenye Jamii pamoja na madereva wa pikipikimaarufu kama bodabda na tumekua tukishirikiana na Jeshi la Polisi na mafunzo hayo yanaratibiwa na Jeshi hilo”Alisema

Naye kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Amend Tanzania Ramadhani Nyanza –aliwashukuru kwa bodaboda kwa mwitiko mzuri wao waliojitokeza kwa wingi huku akieleza mikakati yao baada ya kutoka Hale watakwenda Korogwe,Mombo, Segera, Handeni na Kilindi kwani hilo ni kundi kubwa lipo kwenye hatari kwa ajali ni bodaboda.

“Barabara zetu mnaziona kila siku mnaingia barabarani hakuna njia za waendesha pikipiki ni hiyo hiyo moja kisheria kama kuna sehemu wanatembea 50 nao wanatembea hivyo hivyo wanapiga honi muwapishe kwa hiyo mkijiweka kwenye hali ya kudharaulika na watu wanawafanya hivyo wao mnapoamua kuwatoa huko ni kampeni ya usalama barabarani hao wakiwa salama askari watakuwa salama na abiria wao”Alisema

Akizungumza na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Isa Juma ambaye ni bodaboda kituo cha Hale alisema wanashukuru wamepata elimu hiyo nzuri na kuna mambo mengi wamejifunza ambayo watayatumia ili kuondokana na ajali za barabarani.

Alisema pia mafunzo hayo yamewapa mwanga wa kuona namna nzuri ya kutumia sheria za usalama barabarani kwani kuna vitu vingi walikuwa hawavijui na wameelezwa hivyo vitakuwa chachu kwao kuepukana na ajali .
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger