Monday, 15 May 2023

MERIDIANBET KASINO YAJA NA MCHEZO WA ZOMBIE APOCALYPSE

 


Sloti ya Zombie Apocalypse

 

Tambua kwamba Meridianbet Kasino ya Mtandaoni Inakujali Zaidi wewe mteja kila siku, kwa ofa, bonasi na promosheni kibao ili kuhakikisha unaenjoy sana. Sloti ya Zombie Apocalypse inakuja na mizunguko ya bure, Jackpot na ushindi mkubwa kwa mara moja.

 

Hatua za Ushindi.

 

Mchezo huu una mistari 20 ya malipo, ushindi wote hulipwa kutoka kushoto kwenda kulia, isipokuwa alama ya Bonasi. Kwenye mstari wa ushindi ni ushindi mkubwa pekee unaolipwa. Pori hubadilisha alama zote isipokuwa ishara ya Bonasi.

 

Dau la chini kuanzia Tsh 10 sawa na 1.00 PTS.

 

Jinsi ya Kucheza Sloti hii ya Kasino ya Mtandaoni

 

Ili kushinda Zaidi kwenye mchezo huu wa kasino ya mtandaoni, bonyeza kitufe cha kubashiri na ujaribu kukisia kama kadi/karata inayofuata ni nyekundu au nyeusi ukipatia ushindi wako utaongezwa mara mbili Zaidi na kama utakosea basi ushindi wako utafutwa.

 

Sloti ya Zombie Apocalypse inakupa nafasi ya kupata mizunguko ya bure pale tu unapoanza kucheza, mizunguko hii inaipata kwenye namba hizi 9,10,11,12,13,14 au 15. Kila alama ya Wild inayoonekana kwenye mzunguko ina nyongeza mara 2 au 3.

 

Kasino hii ya Mtandaoni ina Jackpot za aina 3 tofauti za Jackpot ambayo mchezaji anaweza kutarajia ushindi. Mchezaji anapobofya spin, asilimia kadhaa ya hisa zake huingia kwenye sehemu ya jackpot. Jackpot inayoendelea inakua, inakuwa kubwa zaidi na zaidi, hadi mchezaji mmoja atashinda. Zawadi ya jackpot huhamishiwa moja kwa moja kwenda akaunti ya pesa ya mchezaji.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko 50 ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:

MSANII MAARUFU CHAP CHAP ANAIOMBA SERIKALI, WADAU MSAADA WA MATIBABU


Msanii maarufu wa nyimbo za utamaduni  wa kikundi cha Shinyanga Arts Group Fadhili Mungi maarufu Chap Chap (44) mkazi wa Msikamano kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga anaiomba serikali na wadau mbalimbali msaada wa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua kutokana na kwamba hawezi kumudu gharama za awali za matibabu shilingi 3,945,000/= 

Jinsi ya kutuma mchango
Kwa njia ya simu, Tuma mchango wako  kwa M-Pessa 
Namba. 0747956257 RAYMOND GLEYDA
➡️Kwa M-Koba tumia
Namba 1403815 CHAPCHAP FAMILY

Msanii Chap Chap  ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam kwa  zaidi ya miezi miwili akisumbuliwa na ugonjwa kwa kutokwa na usaha puani, maumivu makali ya kichwa , kutokwa na vipande vya nyama na maumivu mengine.

Kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji (TDFAA) Mkoa wa Shinyanga Neema Philipo Mushi  amesema kwa mujibu wa taarifa za madaktari anahitaji takribani shilingi Milioni 4 ili aweze kufanyiwa upasuaji ambapo kwa sasa anaendelea kutumia dawa za kutuliza maumivu shilingi 98,000/= kila mwezi na kwamba miezi kadhaa amekuwa akiteseka.

Chap Chap anaiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia ili pate matibabu kwani hana uwezo wa kifedha wa kufanikisha matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.

Kwa njia ya simu, Tuma mchango wako  kwa M-Pessa 
Namba. 0747956257 RAYMOND GLEYDA
➡️Kwa M-Koba tumia
Namba 1403815 CHAPCHAP FAMILY
Share:

BIBI ALIA MACHOZI BAADA YA KUBEBA UJAUZITO WA UZEENI


Ninamuita bibi kwa kuwa ni mdogo wa mzazi wa kike wa baba yangu mzazi yeye anaishi huko kwao kijijini ambako huwa tunakwenda marachache sana kumtembelea kwasababu za umbali na changamoto za usafiri wa kutufikisha kwake, amebahatika yeye mpaka umri wake wa miaka 64 bado yupo hai na mume wake pia bado yupo wanaishi pamoja japokuwa hawajawahi kupata mtoto yoyote yule enzi za ujana wao.

Yeye babu anao watoto wawili wa nje ya ndoa aliozaa kwa ruhusa ya bibi kabisa baada ya wao kujaribu sana mitishamba mingi na kila kona ya hospitali lakini hawakuwahi kupata tiba ya kuwaponya na kumpa bibi , mtoto hata mmoja wa kujivunia.

Kwakuwa bibi hakuwa na mtoto hata mmoja alipenda sana wajukuu wa dada yake kukaa nao pale kwake angalau tumpe faraja na kuzungumuza naye pale anapokuwa hayupo na furaha au anapokuwa mpweke  tu bila ya kuwa na mtu yoyote.


Sasa mimi zikuwahi kuishi kwake huko muda mrefu kwa sababu za kishule ilinibidi zinguzuke kila kona za huku na huko kupambana na masomo kwanza , na nilipomaliza nilisaidiwa na daktari BAKONGWA nikapata ajira ijapokuwa haikuwa serikalini lakini nilipata ajira ya kampuni lenye mshahara mzuri tu na mkataba mrefu wa kutosha. Likizo yangu mmoja ya kikazi nikaamua kumtembelea sasa bibi huko kwake nikajuwa anaendeleaje , mwenyewe nikajipanga na vijizawadi vyangu vichache kisha nikafunga safari mpaka kijijini hapo kwai nikajue wanaendeleaje.


Bibi alinipokea kwa machozi , furaha na kushangazwa kwa maana sasa ilikuwa ni muda mrefu hatujaonana na nimerudi sasa nikiwa mtu mzima mwenye mindevu na kazi tayari ya kuajiriwa nimekwisha ipata.


Baada ya salamu , nimazungumzo nidvyo yakafuata tukacheka na baadaye nidpo alipofunguka kuwa na yeye alitamani sana angalau kwenye umri wake ujanani angepata mtoto walau saizi angeitwa bibi na watoto wa watoto wake kabisa.Mimi sikuwahi kujua kama bibi hakuwa na mtoto hilo kwangu lilikuwa geni nadhania wazazi walinificha zamani kwa sababu za umri wangu mdogo.

Nikamwambia bibi mbona hata saizi unaweza kupata mtoto kama umeamuwa sema ni umri tu ndio umekukimbia wa kulea lakini kwa habari ya kuzaa bado iko ndani ya uwezo wake, yeye akajibu haiwezekani kwa kuwa ametumia mitishamba ya kila aina na hospital zote kubwa amezunguka lakini hakupata msaada.

Kwa upendo wa bibi ule na jinsi alivyokuwa anahadithia nilitamani kutokwa na machozi , ndipo nikaamua kumuuliza tena bibi uko tayari upate mtoto hata kwenye umri huu bibi akajibu ndiyo mjukuu wangu, hapo sikumjibu chochote nikanyamaza na kumuaga nikapumzike.

Nilipoingia chumbani tu nikanakiri nambari za daktari za whatsapp +243990627777 kwenye simu yangu kutoka kwenye tovuti zake https://bakongwadoctors.com na kufanya naye mazungumzo ya kiundani ,nikamwambia shida aliyo nayo bibi yangu na umri wake yeye daktari akasema hilo linawezekana ila atanipatia dawa ya bibi na babu kusudi la kuwaponyesha wote wawili.

Alinipa maelekezo kisha akanitumia dawa nilipozipokea nikakuta kikaratasi chenye maelekezo ya dawa hizo ambazo ziliwataka watumie masaa 26 tu kisha washiriki tendo la ndoa daktari aliweka dawa ya bibi kushika ujauzito na babu kumpa nguvu ya tendo la ndoa kwa umri wake mkubwa, mimi nikawapatia dawa zao.

Walipofuata maelekezo ya dawa kabla hata ya mimi sijamaliza likizo yangu ya wiki tatu tayari nilimuacha bibi anaujauzito wa wiki mbili, na furaha isiyomuisha asante sana daktari kwa faraja uliyotuletea kwetu.


Share:

Sunday, 14 May 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 15,2023
























Share:

SERIKALI KUJA NA SERA YA ELIMU YENYE MASLAHI KWA TAIFA




WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Bi. Mtumwa Idd Hamad,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba,akichangia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Mbunge wa Jimbo la Buyungu Aloyce Kamamba,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi.Rose Maliki,akichangia wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwa na viongozi mbalimbali wakifatilia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akichangia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiteta jambo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.



WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,amesema kazi ya kukusanya maoni ya kuboresha mitaala na sera ya elimu inaendelea, watachakata maoni yote ili kupata kitu kizuri chenye tija kwa taifa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Mei 14, 2023 Jijini Dodoma wakati wa kufunga Kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu lililofanyika siku tatu.

Amesema kuwa nia ya Serikali ni kufanya maboresho makubwa kwenye sekta ya elimu hivyo kamati haitaacha maoni yoyote ambayo yanatija katika kuboresha mfumo wetu wa elimu nchini.

“Niwahakikishie hakuna maoni yatakayoachwa yote tutazingatia na tutayabeba kwa ajili ya utekelezaji nashukuru kuna baadhi ya maoni yametolewa ufafanuzi hapahapa''amesema Prof.Mkenda

Aidha amesema Wizara itazingatia maoni yaliyotolewa na wadau kwenye kongamano hilo na malengo yaliyopo ukusanyaji maoni utaendelea hadi Mei 31, 2023.

“Tumejiwekea malengo ifikapo Mei 31, tuwe tayari kusonga mbele, tulikuwa tunasikiliza kwa makini sana maoni nimeona hakuna upinzani katika mambo muhimu ya mageuzi ya sera.” “Kuna maoni elimu ya awali iwe ya lazima ni suala ambalo hata kamati ya bunge walisisitiza na sisi tumesema tunalipokea tunalichakata na kuliangalia, hatuwezi kusema kwa haraka kwamba litakuwa lazima lazima tuangalie uwezekano wa utekelezaji,”amesema Prof.Mkenda

Hata hivyo amesema baadhi wameshauri elimu ya lazima iwe miaka 11 ambayo inajumuisha elimu ya awali nayo iwe lazima na sera ya mwaka 2014 ilikuwa inataka elimu ya lazima iwe miaka 10 lakini utekelezaji ulikuwa miaka 7 na kubainisha kuwa watalichakata jambo hilo kwa umakini mkubwa.

Waziri Mkenda amesema kwenye mapitio ya sera yamegusa hadi vyuo vikuu na suala la mitaala litaendelea kuwa endelevu.

“NACTVET wanakamilisha utafiti waliofanya kwa waliohitimu vyuo vya ufundi vya VETA wapo wapi na wanafanya nini, na kuchunguza kwenye magereji, hoteli wameajiri wangapi kutoka VETA.” Ameongeza kuwa “tunataka tutengeneze elimu ya kiujitegemea na tutengeneze uwepo wa wahitimu wenye uelewa na wenye jeuri ya kuhoji na katika bajeti tumetenga tayari kuwaandaa walimu kuendana na mabadiliko hayo tija ipatikane” amesema.

Hata hivyo amesema kuwa watahakikishie katika mafunzo ya amali hasa tunataka tusiyafanye watu wakayadharau na ndio maana hasa ya kuanza na vyuo vya ufundi, mafunzo ya amali sio ya waliofeli bali waliofaulu vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Deogratius Ndejembi,amesema kama TAMISEMI haitakuwa kikwazo katika kutekeleza sera mpya ya elimu itakayopitishwa.

Ameongeza kuwa “mpaka sasa tuna shule 9 za ufundi na kupitia mradi wa SEQUIP tuna kiasi cha bilioni 300 tuna kwenda kujenga shule za ufundi katika karibu Halmashauri zote ambazo hazikufikiwa na vyuo vya VETA tunakwenda kujenga madarasa hayo” amesema Mhe. Ndejembi.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo,amesema wao kama wawakilishi wa wananchi Bungeni watahakikisha wanasimamia maoni yote ya wadau yanafanyiwa kazi kikamilifu ili tija ya kuanzisha zoezi hilo ifanikiwe na baada ya miaka mitano tija ianze kupatikana.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Bi. Mtumwa Idd Hamad amewashukuru viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanziabar kwa miongozo wanayowapa ambayo inarahisisha utendaji kazi wao.

Amesema mabadiliko yanayofanywa yataleta tija kubwa kuhakikisha vijana wanaozalishwa wanakuwa na uelewa wa kutosha na wanaoajirika na wenye uwezo wa kujiajiri wenyewe kutokana na ujuzi wanaoupata.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Dk Angelina Mabula amesema kuwa Wizara yake itawapa ushirikianao wapi mnataka viwanja kwa ajili ya vyuo vya ufundi sisi tutawapatia watanzania tuko mikononi salama kwenye mikono ya Rais Suluhu Hassan na maono yake yatatimia.

Awali,Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,amesema michango iliyotolewa na wadau itazingatiwa kwenye uchakataji ili kuwa na sera na mitaala bora.
Share:

KITUO CHA KULEA WATOTO WENYE ULEMAVU CHA ST.JUSTIN CHAPATA MSAADA WA DOLA 10,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVEP KWA UFADHILI WA BARRICK

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko (kushoto) akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 Msimamizi wa Kituo kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin kilichopo mjini Musoma, Sista Juliana Kitela,katika hafla iliyofanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.
Watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin kilichopo mjini Musoma,walezi wao na wafanyakazi wa kituo hicho wakifurahi baada ya kukabidhiwa msaada wa hundi ya dola 10,000 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara ,Apolinary Lyambiko,katika hafla ilifanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea wakati wa hafla hiyo.
Msimamizi wa Kituo kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St. Justin Sista Juliana Kitela akiongea wakati wa hafla hiyo
Mwanzilishi wa Kituo hicho, Sista Magreth John akiongea wakati wa hafla hiyo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko akipokelewa kwa furaha na watoto alipowasili kituoni hapo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha St.Justin wakionyesha umahiri wa kucheza ngoma wakati wa hafla hiyo.
Shirika la ya Nos Vies en Partage Foundation (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za kimarekani 10,000 kwa kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin, kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara kwa ajili ya kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto hao uwezo wa kujitegemea katika jamii.


Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.


Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika kituo hicho ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko, alisema kuwa kila robo ya mwaka NVEP ina utaratibu wa kuelekeza misaada katika masuala yanayolenga kuleta tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji, na kwamba hadi sasa limeshasaidia mashirika 12 nchini Tanzania.


Aliongeza kusema kuwa Shirika hili [NVEP] linajikita kutafuta fedha ili kusaidia makundi maalumu katika jamii kama vile wanawake, watoto na mengine yenye uhitaji wa ukuaji wa kiuchumi,


“Leo tunakabidhi msaada wa Dola 10,000 katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu cha St. Justin kupitia NVEP. Kituo hiki ni sehemu muhimu ya jamii yetu, kimeonesha kuwathamini watoto hawa kwa jinsi walivyo bila kuwabagua kwa rangi, dini au kabila,” alisema Lyambiko.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo hicho, Sista Juliana Kitela, ameishukuru Kampuni ya Barrick, akisema msaada huo utapunguza changamoto zikiwemo za kitengo cha jiko katika kituo hicho, ili kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto hao uwezo wa kujitegemea katika jamii.


Sista Juliana. amebainisha kuwa Kituo cha St. Justin kinalea watoto wenye ulemavu wa viungo, mtindio wa akili na wasiosikia kwa kuwapatia huduma maalumu na muhimu, zikiwemo za chakula, malazi, matibabu, elimu na mafunzo ya useremala na ushonaji.


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika hicho, Ernest Mwita, ambaye ni mlemavu wa akili alishukuru Barrick kwa kujitoa kuwasaidia ili waweze kuwa katika mazingira bora ya kuishi na kupata maarifa.


Kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St. Justin, kilianzishwa mwaka 2006 na kinaendeshwa na Shirika la Masista Moyo Safi wa Maria Afrika wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma.Kwa sasa kituo hiki kina wafanyakazi 25 na kinahudumia watoto 110, ambapo 75 wanaishi kituoni na 35 wanaishi kwa wazazi na walezi wao nje ya kituo.

Share:

WAZIRI DKT MABULA AINGIA MTAANI KUKAGUA UTEKELEZAJI MAELEKEZO YAKE

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua orodha ya wananchi waliohudumiwa katika eneo la Ndachi jijini Dodoma alipokwenda kukagua utekelezaji wa maelekezo yake ya kuzitaka idara za ardhi kwenda kuwahudumia wananchi katika maenreo yao mwishoni mwa wiki.

**************

Na Munir Shemweta, WANMN

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amefanya ukaguzi katika mtaa wa Ndachi jijini Dodoma kuangalia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa idara za ardhi nchini kuhakikisha zinawafuata wananchi angalau mara mbili kwa wiki kwa lengo la kutoa huduma za sekta ya ardhi.

Dkt Mabula alifanya ukaguzi huo mwishoni mwa wiki katika eneo hilo la Ndachi ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinasogezwa karibu badala ya huduma hizo kupatikana ofisini pekee.

Mbali na juhudi hizo, kwa sasa Wizara ya Ardhi inabadilisha mifumo yake kutoka analogia kwenda digitali ambapo moja ya hatua kubwa iliyofikiwa ni utaratibu wa kuwapelekea wamiliki wa ardhi ankara za malipo kupitia ujumbe wa simu za kiganjani.

Katika ukaguzi huo, Dkt Mabula alianzia ziara yake ofisi ya Mtendaji Kata iliyopo eneo la Ndachi Boda ambapo aliwakuta watendaji wa sekta ya ardhi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma wakitoa huduma kama alivyoelekeza.

"Nimekuja kuangalia kuona maelekezo yangu kuwa badala ya wananchi kwenda kila mara ofisi za jiji kupata huduma basi ofisi hiyo ipange walau mara mbili kwa wiki kwenda katika mitaa kusikiliza changamoto za ardhi nimekuja hapa kuangalia kuona kama hilo limetekelezwa’’ alisema Dkt Mabula.

‘’Mkienda katika mitaa muende na ofisi, yaani idara zote za sekta ya ardhi kwa lengo la kusikiliza kero, kutoa hati na kama ipo haja ya kwenda eneo la mgogoro basi muende na mtoe tangazo kama mtakuwa mahala fulani’’. Alisema Waziri wa Ardhi

Hata hivyo, Waziri Dkt Mabula akiwa katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Ndachi alipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakidai kuna mtu aliyemilikishwa kiwanja eneo la Ndachi Mnadani kwa maelezo kuwa kimetokea kwenye shamba lake jambo walilodai siyo kweli.

Kufuatia hali hiyo, Dkt Mabula àliongozana na walalamikaji pamoja na wananchi wengine kwenda kuliona eneo la shamba hilo ambapo akiwa katika eneo hilo walalamikaji walidai mmiliki huyo alipatiwa eneo hilo kiulaghai kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa jiji.

Kufuatia madai hayo, Dkt Mabula alimpigia simu mkuu wa idara ya ardhi wa halmashauri ya jiji la Dodoma Bw. Maduhu Ilanga na kuweka sauti kubwa ili wananchi wasikie moja kwa moja ambapo mkuu huyo wa Idara alieleza utaratibu mzima uliotumika hadi mdaiwa kumilikishwa pamoja na mgogoro uliopo katika eneo hilo.

Mkazi wa Ndachi Bw. Joel Said Katala alimueleza Waziri wa Ardhi kuwa, Dodoma ina changamoto kubwa haswa halmashauri jiji la Dodoma kutokana na watendaji wake kutosimamia ukweli na kuangamiza wananchi huku wakijua ukweli ambapo aliongeza kwa kusema kuwa, watendaji hao hutengeneza uongo kwa sababu wao ni wa mwisho kuzungumza na viongozi.

Mkazi mwingine Shaban Haruna, alisema changamoto ya eneo linalolalamikiwa imetokana na serikali kutangaza uwepo mabadiliko katika eneo hilo kutoka mashamba kuwa makazi huku wananchi wakiwa tayari walishaanza kuishi. Hata hivyo, alisema mkuu wa wilaya ya Dodoma tayari ameunda kamati itakayoshughulikia umilikishaji kwenye maeneo hayo.

Naye Salum Iddy Juma ambaye ni Mwenyekiti wa shina namba moja eneo la Ndachi Mnadani alieleza kuwa, katika mchakato mzima wa utwaaji shamba alilomilikishwa mlalamikiwa, kamati inayosimamia zoezi hilo haijahusishwa jambo alilolieleza kuwa linatia shaka.

Baada ya kupata maelezo kuhusiana na mgogoro huo, Dkt Mabula aliwaeleza wananchi kuwa, pamoja na wizara yake kupitia idara ya ardhi jiji la Dodoma kuwafuata wananchi katika maeneo yao lakini migogoro ya ardhi itaisha tu iwapo wananchi watazingatia sheria kanuni na taratibu na kuacha kuwa na haraka kujenga nyumba bila kuwa na vibali.

"Sasa hivi jiji la Dodoma linakuwa kwa kasi na fursa ziko nyingi na watu wanakimbilia, kuweni na subira katika ujenzi, fuateni taratibu" alisema Dkt Mabula.

Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alielekeza ujenzi unaoendelea eneo linalolalamikiwa kusitishwa hadi hapo ufumbuzi wa mgogoro wa eneo hilo utakapopatikana.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisikiliza kero za baadhi ya wananchi aliowakuta eneo la Ndachi Dodoma wakati akikagua utekelezaji wa maelekezo yake ya kuzitaka idara za ardhi kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneo yao mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi alipokwenda eneo la Ndachi Mnadani jijini Dodoma kusikiliza mgogoro wa ardhi wakati akikagua utekelezaji wa maelekezo yake ya kuzitaka idara za ardhi kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneo yao mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasili eneo la Ndachi jijini Dodoma alipokwenda akikagua utekelezaji wa maelekezo yake ya kuzitaka idara za ardhi kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneo yao mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

Tanzia : LE MUTUZ AFARIKI DUNIA


Mmiliki wa 'Le Mutuz' Blog, William Malecela, maarufu kama Mr Super Brand amefariki dunia leo Mei 14, 2023 jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Le Mutuz Tv, Deusdedith Innocent amethibitisha taarifa za kifo hicho.

Share:

WALIMU WAKAMATWA TUHUMA ZA WANAFUNZI KUFA KWENYE TANKI LA MAHARAGE


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watumishi watatu wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa uchunguzi wa tukio la vifo vya wanafunzi wawili wa kidato cha nne wa shule hiyo.


Watumishi hao wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa ni mkuu wa shule hiyo, mwalimu wa zamu pamoja na mtunza stoo wa shule hiyo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Simoni Maigwa imesema wanafunzi hao walifariki dunia Mei 12 shuleni hapo baada ya kuingia ndani ya tenki la kuhifadhia maharage baada ya sehemu ya chini ya kutolea maharage kuziba.


Wanafunzi waliofariki dunia ni Edson Gabriel Mosha (17) na Godwin John (17) ambao wote ni wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.


"Wanafunzi hawa baada ya kuingia kwenye tenki kwa lengo la kutoa maharage kwenye tenki hilo baada ya sehemu ya chini inayotolea maharage kuziba, kwa hiyo baada ya kuingia ndani walikosa hewa na baada ya kutolewa walikimbizwa kituo cha afya Kirua Vunjo ambao ilibainika wameshafariki," amesema.


Miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mawezi kwa uchunguzi zaidi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger