Monday 15 May 2023

MSANII MAARUFU CHAP CHAP ANAIOMBA SERIKALI, WADAU MSAADA WA MATIBABU

...

Msanii maarufu wa nyimbo za utamaduni  wa kikundi cha Shinyanga Arts Group Fadhili Mungi maarufu Chap Chap (44) mkazi wa Msikamano kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga anaiomba serikali na wadau mbalimbali msaada wa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua kutokana na kwamba hawezi kumudu gharama za awali za matibabu shilingi 3,945,000/= 

Jinsi ya kutuma mchango
Kwa njia ya simu, Tuma mchango wako  kwa M-Pessa 
Namba. 0747956257 RAYMOND GLEYDA
➡️Kwa M-Koba tumia
Namba 1403815 CHAPCHAP FAMILY

Msanii Chap Chap  ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam kwa  zaidi ya miezi miwili akisumbuliwa na ugonjwa kwa kutokwa na usaha puani, maumivu makali ya kichwa , kutokwa na vipande vya nyama na maumivu mengine.

Kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji (TDFAA) Mkoa wa Shinyanga Neema Philipo Mushi  amesema kwa mujibu wa taarifa za madaktari anahitaji takribani shilingi Milioni 4 ili aweze kufanyiwa upasuaji ambapo kwa sasa anaendelea kutumia dawa za kutuliza maumivu shilingi 98,000/= kila mwezi na kwamba miezi kadhaa amekuwa akiteseka.

Chap Chap anaiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia ili pate matibabu kwani hana uwezo wa kifedha wa kufanikisha matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.

Kwa njia ya simu, Tuma mchango wako  kwa M-Pessa 
Namba. 0747956257 RAYMOND GLEYDA
➡️Kwa M-Koba tumia
Namba 1403815 CHAPCHAP FAMILY
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger