Wednesday 31 May 2023

UTEKELEZAJI WA SERA YA BAJETI UFANYIKE KUANZIA NGAZI YA SERIKALI ZA MITAA

...

WADAU wa Maendeleo ya Jinsia wameiomba Serikali kuhusu utekelezaji wa sera ya Bajeti ufanyike kuanzia ngazi ya Serikali za mtaa kabla haijaenda halmashauri na wananchi wajiridhishe vile vipaumbele vyao ili kuleta picha nzuri kwenye jamii na kuleta usahihi wa mambo.

Akizungumza leo Mei 31,2023 Jijini Dar es Salam wakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zinazoandaliwa na TGNP Mtandao wakati wakiichambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia, Bw.Hancy Obote amesema fedha nyingi hazijakwenda kwenye matumizi ambayo yanawalenga wananchi moja kwa moja .

"Hatujaona fedha ikienda moja kwa moja kwenye vifaa tiba kwa maana kusaidia wanawake wakati wa kujifungua, tumeona fedha imenunua magari 102 ya kwenda kwajili ya matumizi ya ufuatiliaji wa madawa, vitu ambavyo havigusi wananchi moja kwa moja". Amesema

Kwa upande wake masuala ya Bima ya Afya, washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo wamesema bima ya afya kwa wananchi wa kawaida ni changamoto kwasababu ya gharama kubwa ambazo ni ngumu kuzimudu.

Aidha wamesema suala la Matibabu bure kwa wazee na watoto wenye umri chini ya miaka mitano suala hilo linaonekana halipo kwani kuna gharama lazima aweze kulipia ili apate matibabu.








Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger