Monday, 13 February 2023

Picha : MKUTANO WA MWAKA WA WATOA HUDUMA WA SEKTA YA UTANGAZAJI TANZANIA



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji Tanzania unaofanyika Jijini Dodoma Februari 13 na 14,2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew


Kauli mbiu ni Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza uchumi wa kidigitali
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji Tanzania unaofanyika Jijini Dodoma Februari 13 na 14,2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji Tanzania unaofanyika Jijini Dodoma Februari 13 na 14,2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete.


Picha : Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

TAMCODE YAWATAKA WATANGAZAJI WA REDIO KURIPOTI KWA UANGALIFU NA UMAKINI MASUALA YA UTAMADUNI, SIASA NA DINI

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 13,2023





























Share:

Sunday, 12 February 2023

YANGA SC YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA WAARABU, YACHAPWA 2-0 NA US MONASTIR


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeshindwa kuibuka na ushiindi mbele ya timu ya US Monastir ya nchini Tunisia baada ya kupokea kichapo cha mbao 2-0 kwenye mchezo huo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Olympic Rades, Yanga imekuwa ikishindwa kumiliki mpira kwa muda mrefu hivyo kuwapa nafasi US Monastir kucheza mpira kwa uhuru na kuweza kupata mabao mawili ya haraka katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Yanga Sc ilirudi kipindi cha pili kutafuta mabao bila mafanikio licha ya kuwapumzisha baadhi ya wacheaji na kuingiza igizo jipya .

Mabao ya US Monastir yamefungwa na nyota wao Mohamed Saghraoui dakika ya 10 ya mchezo na bao la pili likifungwa na Boubacar Traore dakika ya 16 na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Share:

BABU ANYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, MWILI WAKE WATUPWA ZIWA VICTORIA



Mtu moja aliyetambulika kwa jina la Musa Robert anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 76 mkazi wa Kijiji cha Kasheka kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amekutwa amefariki dunia pembezoni mwa ziwa Victoria katika kitongoji cha Kisenya Kijiji cha Katwe kata ya Katwe wilayani humo huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.


Ofisa mtendaji Kijiji cha Katwe, Ezekiery Galula akizungumuza na Mwananchi February 12, 2023 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeleta simanzi kwa wananchi wa maeneo hayo.


Amesema alipata taarifa kutoka la raia wema waliopita maeneo hayo wakiwa wanakwenda kufanya shughuli za kujipatia kipato ndipo walipoona mwili huo na kutoa taarifa.


Mdogo wa marehemu Manyindo Robert (74)  amesema sehemu za siri kwenye mwili wa marehumu kaka yake zilikuwa zimenyofolewa na hazijulikani zilipo licha na viungo vingine kuwepo.

Chanzo - Mwananchi
Share:

Video Mpya : KIMWAGA MASABHO - PESA NA MAPENZI

Share:

SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK BULYANHULU KWA KUFANIKISHA MIRADI YA KIJAMII SHINYANGA NA GEITA

Sehemu ya nyumba za walimu katika chuo cha VETA cha Bugarama zikiwa katika hatua ya Mwisho kukamilika,mradi wote wa VETA umegharimu shilingi milioni 961
Muonekano wa majengo ya sekondari la Igalula
Wakurugenzi wa TAMISEMI, Bw. John Cheyo- Sera na Mipango (kulia) na Vicent Kayombo-Elimu wakisikiliza taarifa ya miradi ya kijamii ya Barrick Bulyanhulu.
Kaimu Meneja wa Mahusiano ya jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii.
Mwonekano wa bweni la wasichana la shule ya sekondari Bugarama lililojengwa na fedha za CSR zilizotolewa na Barrick Bulyanhulu,pia imejengwa nyuma ya matron,vyumba vya madarasa na uzio.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwingiro, Antony Fabian akisoma risala kwa ujumbe wa TAMISEMI ulipotembea shule hiyo kuona maendeleo ya miradi ya fedha za uwajibikaji kwa jamii za Barrick Bulyanhulu.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango-OR-TAMISEMI, Bw,John Cheyo akitembelea moja ya wodi ya kituo cha afya cha Bugarama ambacho kimejengwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii za mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa Maofisa wa TAMISEMI na Barrick Bulyanhulu baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Bugarama
 ****

Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga umepongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya kijamii yenye kuboresha maisha ya wananchi kwa ufanisi mkubwa kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambayo tayari imeanza kuchochea kasi ya maendeleo katika maeneo hayo.



Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango-OR-TAMISEMI, Bw,John Cheyo, wakati alipoongoza ujumbe wa maofisa wa TAMISEMI kutembelea miradi ya afya na elimu iliyotekelezwa kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii zilizotolewa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika Halmashauri za wilaya ya Msalala na Nyang’hwale katika mikoa ya Shinyanga na Geita.


Bw.Cheyo, alisema amefurahi kuona miradi mbalimbali imekamilika na miundo mbinu ya elimu na afya imejengwa kwa viwango vya kuridhisha kwa kutoa huduma bora kwa Wananchi na kuchochea kufanikisha mipango ya Serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi hususani katika sekta ya elimu na afya.


“Nawapongeza Barrick Bulyanhulu na Watendaji wa Serikali kwa kusimamia ujenzi wa miradi hii na natoa wito kwa watumiaji wa majengo na vifaa vilivyonunuliwa mahospitalini kuvitunza ili vidumu na kuendelea kuhudumia wananchi wengi zaidi katika kipindi cha muda mrefu.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mahusiano ya jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, alieleza ujumbe huo kutoka TAMISEMI kuwa miradi ikishapitishwa na halmashauri husika,mgodi unatoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kufanikisha mradi zinatolewa sambamba na kufanya ufuatiliaji kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango na muda uliopangwa.


Baadhi ya miradi mikubwa ambayo ujumbe huo ulitembea ambayo imejengwa kwa fedha za CSR za Barrick Bulyanhulu ni sekondari ya Mwingiro,Shule ya mchepuo wa kingereza ya Kharumwa,ujenzi wa madarasa na kuboresha maabara katika shule za sekondari za Kayenze, Igalula, Busulwangili,Bugarama,Chuo cha VETA Bugarama,chuo cha wauguzi cha Ntobo na kituo cha afya cha Bugarama.


Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwingiro, Antony Fabian akiongea kwa niaba ya wafanyakazi waliopo katika maeneo ya mradi na Wananchi alishukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Serikali kwa kufanikisha miradi hii mikubwa ambayo inaendelea kuboresha maisha ya wananchi.


Share:

REA KUSAMBAZA MITUNGI 100,000 YA GESI YA KUPIKIA VIJIJINI


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akizungumza wakati wa Semina ya Kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akiongoza Semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa kamati yake iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati jijini Dodoma.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Judith Kapinga akichangia mjadala wa nishati ya kupikia wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wabunge iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katka ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati


Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Stephen Byabato akitoa majumuisho ktk Semina ya Kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati.

******************

Serikali imeandaa mpango wa kutoa ruzuku ambayo kwa ajili ya kusambaza majiko na mitungi ya gesi yakupikia 100,000 katika maeneo ya vijijini katika mikoa 25 ya Tanzania Bara.


Mkurugenzi Mkuuwa REA, Mhandisi Hassan Saidy alisema hayo Katika Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika tarehe 10 Februari 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati Jijini Dodoma.


“Pia tuna mpango wa kusambaza majiko banifu 200,000 yanayo tumia kuni na mkaa kidogo ilikupunguza uvunaji wa miti na gharama zake zitakuwa nafuu” alisema Mhandisi Saidy.


Mhandisi Saidy alisema kuwa utekelezaji wa Mpango huo utatumia utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wasambazaji wa bidhaa na teknolojia za nishati bora na salama ya kupikia pamoja na kuwajengea uwezo wasambazaji hao ili waweze kupunguza bei ya majiko hayo na kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi maeneo ya vijijini.


Akitoa majumuisho katika Semina hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Wakili Stephen Byabato alisema kuwa Serikali imeandaa mpango wa kutoa ruzuku kwa wasambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia na bidhaa nyingine za nishati bora ya kupikia kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa hizo katika maeneo ya vijijini.


Aidha, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dustan Kitandula alipongeza Wizara ya Nishati kwa kubuni miradi ya kusambaza nishati safi na salama ya kupikia maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini.


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Judith Kapinga aliitaka Serikali kwa kushirikiana na wasambazaji wa Mitungi ya gesi ya kupikia kuweka utaratibu ambao utawezesha wanachi wengi wa vijijini kutumia gesi hiyo.


“Tuweke mkakati na wasambazaji wa gesi ili ifike vijijini na iwe rahisi kwa wananchi kupata bidhaa hiyo” alisisitiza.


Vile vile wajumbe wa Kamati hiyo wameishauri Serikali iandae mpango utakaowezesha kupunguza gharama za majiko na gesi ya kupikia katika maeneo ya vijijini.


Akichangia katika Semina hiyo, Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu alipendekeza kuwe na punguzo la bei kwa mitungi ya gesi ya kupikia kwa wananchi wa vijijini.


“Serikali imetofautisha bei ya umeme maeneo ya mijini na vijijini na kwenye gesi napo wafanye hivyo hivyo ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kutumia gesi kwaajili ya kupikia” alisema.


Kwa upande wake Mbunge wa Msalala, Mhe. Idd Kassim Idd alihoji kuwa Serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa Mitungi ya gesi ya kupikia inapatikana maeneo ya vijijini.


“ Bei ya mitungi ya gesi ipojuu kulinganisha na vipato vya wa nanchi wengi wa vijijini” alisema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger