Thursday, 19 January 2023

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA MJI WA TINDE...AONYA WEZI WA MAJI, WANANCHI KUBAMBIKIWA BILI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde utakaogharimu shilingi Bilioni Bilioni 5.2 utanufaisha wananchi 60,000 katika vijiji 22 vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Dkt. Mpango ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde leo Alhamis Januari 19, 2023 katika Tangi la Maji  la Buchambi - Tinde Kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.


Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi Dkt. Mpango pindi mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na Shelui utaogharimu shilingi Bilioni 24.4 utakapokamilika jumla ya Wananchi 180,000 wa Tinde, Shelui na vijiji jirani watanufaika na mradi huo.

“Sekta ya Maji ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa viwanda na kupambana na umaskini, na katika mradi huu wa maji wa Tinde utakuwa na faida kwa wananchi na kuwaepusha kupoteza muda mrefu wa kufuata maji safi salama, pamoja na kutopata magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu,”amesema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango utekelezaji wa miradi ya maji ipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 97 na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi kwa sababu maji ni muhimu.


Amesema Tangu mwaka 2015 hadi 2019 Jumla ya Miradi ya Maji ambayo Serikali imeitekeleza ni 1,423, vijijini 1,268 na Mijini 155, na kuwataka wananchi waitunze miundombinu ya miradi hiyo pamoja na vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kulinda uoto wa asili.

“Napenda kuwakumbusha wananchi kushirikiana kutunza miundo mbinu ya maji na kutunza mazingira kwa kupanda miti na maua kwenye maeneo yetu ili kunusuru nchi yetu iliyoathiriwa na ukataji miti bila kupanda mipya. Nataka miti mingi zaidi ipandwe hapa tulipo. Ni lazima turejeshe uoto wa asili, hili suala la kuhifadhi mazingira kwenye vyanzo vya maji ni lazima, ni lazima tulinde vyanzo vya maji. Uharibifu wa vyanzo vya maji ni hatari, tutunze vyanzo vya maji, msione Ziwa Victoria ni kubwa linaweza kukauka, tukikosa maji tutakufa, tusichukulie kawaida hili”,amesema Dkt. Mpango.


Katika hatua nyingine Dk, Mpango ameviagiza vyombo vya dola, pamoja na Kamati za ulinzi na usalama kuwasaka wale wote ambao wamekuwa wakijihusisha na wizi wa maji wakiwemo wawekezaji wakubwa na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwatoza faini.


“Lakini wapo watu wanachepusha maji, wanaharibu vyanzo vya maji, Wawekezaji wakubwa waache kuiba maji, bali wachimbe visima vya maji na siyo kutuibia maji, na wale ambao wanachepusha maji waache, wote waliofanya hivyo wabomoe hivyo vizuizi walivyoweka kwani kila mwananchi anahitaji maji. Wizara ya Maji na Bonde mlishughulikie hili.

Kumekuwa na wizi wa maji, kokote nchini hili iwe mwisho, wakubwa acheni kuiba maji, ni ajabu tena wanaoiba maji ni wawekezaji wakubwa na mnawatoza faini ndogo, nawaonya muache, vyombo vya usalama vifuatilie kubaini wezi wa maji, hao wawekezaji wanaoiba maji wachimbe visima vya maji, wavune maji”,amesema Dkt. Mpango.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Shinyanga baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde.

“Nimefurahi kusikia watumishi idara ya maji yamebadilika, lakini masikio yangu kwa wananchi bado kuna malalamiko ya wananchi kubambikiwa bili za maji, na hapa mbadiike, wananchi wanasema wakati mwingine wasoma mita hawasomi mita, wanakadiria, nataka wabadilike, watoe bili kadiri wananchi walivyotumia”, ameongeza Dkt. Mpango.


Dkt. Mpango pia ameagiza Wakaguzi pamoja na Baraza la uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabwawa yote ya taka sumu migodini ili kusijetokea tatizo kama lilivyotokea katika bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui.
Wakazi wa Tinde

Pia amemwagiza Mthamini Mkuu wa Serikali kukamilisha uthamini haraka juu wa waathirika wa Tope wa bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui ,ili walipwe fidia zao haraka na kuendelea na maisha yao.


Kwa upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania, Bw. Binaya Srikanta Pradhan amesema serikali ya Indi itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya maji

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kwa wananchi na kubainisha kuwa katika Mkoa wa Shinyanga kuna miradi ya maji 18 ya kimkakati ambayo inatekelezwa, na wilaya ya Shinyanga kuna miradi mitatu yenye thamani ya Sh.bilioni 1.9.

  Waziri Aweso mradi huo wa Maji ya Tinde unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili ambapo wananchi wataanza kupata huduma ya maji safi na salama ingawa tayari maji hayo yameanza kutoka katika mji wa Didia.

Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum, amepongeza utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa maji jimboni kwake , na kueleza kuwa katika jimbo hilo lina vijiji 126 na mpaka sasa kutakuwa na vijiji 89 ambavyo vinapata huduma ya maji safi na salama, na kusalia vijiji 37 ambavyo navyo vipo kwenye mchakato wa kupata maji.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akisoma taarifa ya Mradi huo wa Maji ya Ziwa Victoria, amesema katika mji huo wa Tinde vitahudumiwa vijiji 22 na kunufaisha wananchi elfu 60, ambapo pia maji hayo yanahudumia na wananchi wa Shelui wilayani Iramba mkoani Singida na una gharama ya Sh.bilioni 24.4.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa Tangi la Maji la Buchama - Tinde lenye ujazo wa lita 1,150,000
Muonekano wa Tangi la Maji la Buchama - Tinde lenye ujazo wa lita 1,150,000
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, akimwelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuhusu Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Tinde na vijiji jirani wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipanda mti katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akimwagilia maji kwenye mti aliopanda katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Muonekano wa mti wa Mzaituni uliopandwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (mwenye tai nyekundu katikati) akiondoka katika Tangi la maji la Buchambi - Tinde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na kikundi cha ngoma ya Kisukuma

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Shinyanga baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
 Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
 Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde

Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
 Balozi wa India nchini Tanzania, Bw. Binaya Srikanta Pradhan akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
 Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde

Kaimu Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa Tinde






Kwaya kutoka Wizara ya Afya ikitoa burudani
Kwaya kutoka Wizara ya Afya ikitoa burudani
Mrisho Mpoto akitoa burudani
Kikundi cha burudani cha Mama Ushauri kikitoa burudani
Waswezi wakitoa burudani
Kundi la Mabulo ya Jeshi likitoa burudani.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Wednesday, 18 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 19,2023










Share:

MRADI WA REST WAZINDULIWA DODOMA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa rasmi mradi unaoshughulikia masuala ya afya ya uzazi kwa vijana na wanawake unaojulikana kama Reproductive Equity Strategy in Tanzania (REST) unaoendeshwa na shirika lisilo la Kiserikali la Deutsche Stiftung Weltbevolkerung (DSW) - Tanzania ambao utafanya kazi kwenye Wilaya tatu za Mkoa ikiwa ni pamoja na Dodoma mjini, Bahi na Mpwapwa.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki katika uzinduzi wa mradi unaoshughulikia masuala ya afya ya uzazi kwa vijana na wanawake. Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

****************************

Mkoa wa Dodoma umezindua rasmi mradi unaoshughulikia masuala ya afya ya uzazi kwa vijana na wanawake unaojulikana kama Reproductive Equity Strategy in Tanzania (REST) unaoendeshwa na shirika lisilo la Kiserikali la Deutsche Stiftung Weltbevolkerung (DSW) - Tanzania ambao utafanya kazi kwenye Wilaya tatu za Mkoa ikiwa ni pamoja na Dodoma mjini, Bahi na Mpwapwa.

Akizindua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali ya Awamu ya Sita imetoa kipaumbele katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu yake ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora ya afya.

“Matokeo ya sensa ya mwaka 2022 yanaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya hospitali 676, vituo vya afya 1,466 na zahanati 7, 965. Tanzania Bara pekee ina hospitali 662, vituo vya afya 1,430 na zahanati 7,680 na mkoa wetu wa Dodoma una vituo vya afya 69 na zahanati 402. Hivyo ni muhimu sana kuendelea kuhamasisha wananchi hususan wakina mama wajawazito kutumia vituo vya afya kwa ajili ya kupata huduma, mpango wa Serikali ni kutokomeza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ifikapo mwaka 2025” Amesema Mhe. Senyamule.

“Nitoe rai, mkafanye kazi kwa ufanisi mkubwa maana tunataka kila unachokifanya Dodoma, kifanyike kwa ufanisi kwani tunakwenda kuifaharisha Dodoma kwa mradi huu” Ameongeza Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la DSW Bw. Peter Owaga, amesema “Mradi huu unatekelezwa kwenye mikoa minne ya Tanzania ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza kwa kushirikiana na mashirika 11 yasiyo ya Kiserikali. Kwa mkoa wa Dodoma unatekelezwa katika Wilaya tatu ikiwemo Dodoma mjini, Bahi na Mpwapwa chini ya mashirika ya Dodoma Youth Development Organization (DOYODO), Women Wake Up (WOWAP) na Family Engage for Action Foundation (FAEAF) wakiongozwa na Shirika la DSW Tanzania.

Lengo la mradi huu ni kusaidia wanawake na wasichana kupata na kutumia huduma za afya ikiwemo afya ya uzazi ili kuleta ustawi wao na kuweza kutimiza matarajio na malengo ya maisha yao. Mradi huu pia utasaidia utekelezaji wa sera na miongozo mbalimbali ya afya ya uzazi ikiwemo kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Baadhi ya kazi za Mradi huu ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Watoa Huduma wa Afya kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi ikiwamo utoaji wa huduma rafiki kwa Vijana na Jinsia, utoaji wa Mafunzo ya Afya ya Uzazi na Stadi za Maisha kwa Vijana Balehe katika Shule za Sekondari, Vyuo na walioko nje ya mfumo rasmi wa shule, kutoa mafunzo kwa Vyombo vya Habari kuhusiana na Masuala ya Afya ya uzazi na Jinsia katika kusaidia kutoa elimu kwa jamii, kutumia njia za ubunifu ikiwamo michezo, Sanaa na vikaragosi katika kuelimisha jamii.
Share:

MAMA AUAWA KWA KUCHOMWA SHINGONI NA ANAYEDAIWA KUWA MME WAKE...AACHA WATOTO WATANO



Na John Walter-Manyara 

Sabina Barma (28) mwenye watoto watano ameuawa kwa kuchomwa shingoni kwa kitu chenye ncha Kali na mtu anayetajwa kuwa ni mumewe.

Marehemu ameacha watoto watano wa mwisho akiwa ana umri wa Mwaka mmoja ambaye alikutwa akinyonya ziwa la mama yake bila kujua kuwa  alishafariki dunia.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Gisigisi Kijiji Cha Saydoda kata ya Ufana Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara John Masong Manonga amesema tukio hilo lililotokea Januari 14, 2023 kijijini hapo limewastua wengi kwani marehemu alikutwa akiwa na majeraha shingoni.


Wananchi wa kitongoji cha Gisigisi wameiomba serikali imtafute mtuhumiwa na kumchukulia hatua stahiki ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu kama hiyo.
Inaelezwa na Mmoja wa mashuhuda  kuwa mwanamke huyo alikuwa amefungwa mikono na kuteswa na kuchomwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali na  maeneo mbalimbali ya mwili wake, kwa kuwa marehemu alikutwa na kamba mkononi.
 

Mume anayetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo aliyetajwa kwa jina Moja la Nada, waliyezungumza naye wanasema walimpigia simu lakini alijibu yupo safarini na baadaye simu yake iliiita bila kupokelewa.


Wazazi wa marehemu wamesema baada ya tukio hilo wameitenga familia hiyo na kuamua kuuchukua mwili wa Mtoto wao na kwamba watamzika wenyewe nyumbani kwao na kuwachukua watoto wote kuishi nao.
Share:

PASTA MATATANI TUHUMA ZA KUMBAKA RAIA WA KIGENI NA KUMTAPELI PESA


Jeshi la Ulinzi nchini Uganda limemkamata pasta na maafisa watatu wa polisi kufuatia kisa cha mwanamke mmoja raia wa kigeni kudaiwa kubakwa na kutapeliwa pesa zake.

Kukamatwa kwa mchungaji huyo kunajiri baada ya kituo cha NTV-Uganda wikendi iliyopita kufanya mahojiano na mwathiriwa.

Katika mahojiano hayo, mwathiriwa kwa jina Anda alifichua uyahawani ambao alitendewa na nabii Joseph Collins Twahirwa muda mfupi baada ya kuwasili nchini Uganda mnamo Disemba 11, 2022. Twahirwa alikuwa amemwalika Anda kwenda nchini Uganda kwa likizo.

Punde alipowasili nyumbani kwa pasta huyo, inasemekana alimpokonya pasipoti yake na kumwibia KSh37, 203 na €400(KSh53,698) kabla ya kumbaka. 

Raia huyo wa Latvia mwenye umri wa miaka 36, alisema Twahirwa alimwambia alitaka kupata mtoto na kisha alimsukuma kitandani na kumbaka usiku wa Disemba 11, 2022.

 Anda pia alisimulia masaibu aliyopitia alipojaribu kwenda kupiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Jinja Road na, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID).

Katika Kituo cha Polisi cha Jinja Road, maafisa walimtaka mtalii huyo awanunulie mafuta ya gari lao au ashiriki ngono nao. Polisi hao pia waliungana na wafuasi wa Twahirwa kumtesa raia huyo wa kigeni. 

Anda aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alipokonywa simu yake na mawasiliano yote aliyokuwa nayo na Twahirwa kwenye mitandao ya kijamii yalifutwa ili kujaribu kuharibu ushahidi wa uhusiano wao.

 Maafisa wa kituo hicho pia walidaiwa kumvua viatu kwa nguvu miguuni na kumtandika kabla ya kumtupa ndani ya seli.


Baadaye aliachiliwa na kuamriwa kufuta kesi dhidi ya Twahirwa.

 Alipokimbia kwa CID, maafisa hao walimwambia Anda kwamba anacheza na mwanaume mwenye uhusiano na watu wenye ushawishi. 

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa CID alisema kuwa maafisa hao watatu walikamatwa Jumapili, Januari 15, na wanatazamiwa kufikishwa kortini.

 Twahirwa ambaye alikuwa ameachiliwa kwa bondi wakati taarifa hiyo ilipeperushwa, pia anashikiliwa na polisi na atafikishwa kortini ndani ya saa 48.

Claire Nabakka, ambaye ni naibu msemaji wa polisi, alithibitisha kwamba dhamana ya Twahirwa ilifutwa na kwamba pasta huyo wa Epikaizo Ministries International yuko chini ya ulinzi wa Jeshi. 

Polisi pia walitoa wito kwa waathiriwa wa pasta huyo pia kujitokeza na kuwasilisha ripoti kwa CID ili kusaidia katika uchunguzi zaidi.

 Kisa cha Anda kimeharibu sifa ya maafisa wa polisi nchini humo pamoja na wachungaji wa kipentekoste.

Chanzo - TUKO NEWS
Share:

TAZAMA HAPA MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA IDARA YA UHAMIAJI

Share:

NAMNA YA KUJIKINGA NA MAADUI ZAKO


Hakuna ubishi kuwa kila binadamu ana ndoto kubwa za kufanikiwa kimaisha, lakini ukweli ni kwamba sio kila mwenye ndoto inaweza kutimia na pengine inaweza kutimia ila kwa kuchelewa sana.


Ndivyo maisha yalivyo, wakati mwingine hayakupi kile unachota na wakati mwingine yanakupata ambacho hukutarajia, ndilo fumbo kubwa ambalo lipo katika maisha ya kila siku hapa duniania.

Jina langu ni Zakayo kutokea Nyanza nchini Kenya, mwaka 2017 nilipata kazi katika kampuni mmoja ya kimaaifa ya kuuza vinywaji baridi, kwa hakika kazi hii ilikuwa ni nzuri na yenye mashahara mzuri ajabu.

Nilikuwa najisemea kimoyo moyo kuwa endapo nitafanya kazi hii kwa miaka miwili tu, basi nitaweza kujenga nyumba hata mbili, kununua gari na mambo mengine makubwa ya kimaendeleo.

Hata hivyo, miezi saba tu katika ajira ile, mambo yalianza kubadiika, kuna wafanyakazi wenzangu ambao walikuwa ni rafiki zangu, walianza kunipiga vita ya chini kwa chini.

Walienda kusema maneno ya uongo kwa Bosi wangu na kutaka anifukuze kazi, lakini nikiwa nao wanajidai ni watu wema kwangu, ingawa mwanzo sikuweza kubaini hilo hadi AfricanDoctors walipokuja kunisaidia.

Ilifikia wakati nikasimamishwa kazi kwa mwezi mmoja, nilikaa na nyumbani na kuumia sana, nilijua tu kuna watu wameanza kunipiga majungu pale kazini bila mimi kujua.

Niliamua kuchukua uamuzi wa kuwasiliana na AfricanDoctors na kuwaeleza kuwa nimekuwa nikipigwa sana vita kazini kwangu na watu ambao nahisi ni wafanyakazi wenzangu. Basi walinifanyia tiba zao na kuniambia hilo halitokuja kutokea tena katika maisha yangu na wote walihusika lazima watapata dawa yao.

Baada ya kurejea kazini, siku hiyo Bosi waliitisha kikao na kusema kuwa amekuja kubaini kuwa tuhuma alizopewa dhidi yangu zilikuwa za uongo, hivyo akawataja waliompa taarifa zile.

Sikuweza kuamini kabisa maana wote wawili waliotajwa ni rafiki zangu ambao hata nyumbani kwangu walikuwa wanakuja, Bosi akasema kutokana wameongea uongo mkubwa kiasi cha kugharimu maisha ya wengine, basi Ofisi imefikia hatua ya kuwafukuza kazi.

Tangu wakati huo nimekuwa nikipata huduma mbalimbali kutoka kwa AfricanaDoctors hasa hiyo ya kijikinga na maadui maana sio kwenye kazi tu wapo, hata kwenye biashara, kilimo, ufugaji, familia, siasa, ujasiriamali na mengineo.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:

Tuesday, 17 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 18,2023









Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger