Tuesday, 17 January 2023

WAZIRI NDALICHAKO AHIMIZA ELIMU YA USALAMA NA AFYA KWA WATU WENYE ULEMAVU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akizindua kitabu maalum cha watu wasioona chenye maudhui ya usalama na afya mahala pa kazi mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa kwa wajasiriamali wasioona jijini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria, Mhe. Yahya Masare (Mb), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Rasheed Maftah na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona, Bw. Omari Amas.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akimkabidhi Fimbo nyeupe na kitabu maalum cha watu wasioona chenye maudhui ya usalama na afya mahala pa kazi kwa mjasiriamali asiyeoona Bi. Fadhila William wakati wa mafunzo hayo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akihutubia wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kwa watu wasioona yaliyofanyika katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.


Sehemu ya watu wasioona wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akieleza jambo wakati wa mafunzo hayo.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona, Bw. Omari Amas,akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kwa watu wasioona yaliyofanyika katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya washiriki mara baada ya kuzindua mafunzo ya usalama na afya kwa watu wasioona yaliyofanyika katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.

..................................

Na;.OWM – KVAU -DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameutaka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) kuweka mkazo wa kukuza uelewa wa masuala usalama na afya kwa Watu wenye Ulemavu.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya usalama na afya kwa watu wasioona Mkoa wa Dodoma.

Amesema mafunzo OSHA imekuwa ikitekeleza program ya mafunzo kwa makundi mbalimbali ikiwamo wajasiriamali na wachimbaji wa madini na kwa mwaka 2022 walifikiwa watu 11,204.

“Niipongeze Taasisi ya OSHA kwa kuendelea kuona umuhimu wa kutoa mafunzo haya na kuandaa chapisho kwa ajili ya watu wasioona, naagiza hakikisheni mnachapisha nakala za kutosha na kuzisambaza mikoa mingine na haya mafunzo muendelee kutoa hata kwenye maeneo mengine ili kuwezesha wafanyakazi na Watu wenye Ulemavu kuzingatia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi,” amesema.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema masuala ya usalama na afya yana umuhimu sana katika maendeleo na ustawi wa watu duniani hivyo yanapaswa kupewa uzito unaostahili.

“Mathalani takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO) za mwaka 2022, zinaonesha kuwa watu milioni 2.9 hupoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 400 huumia kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi duniani kote na Tanzania ikiwemo,” amesema.

Vile vile, Prof. Ndalichako amesema magonjwa na ajali zitokanazo na kazi huisababishia dunia hasara ya zaidi ya asilimia tano ya pato lake ghafi la mwaka na hivyo kuhimiza uwajibikaji ili kubadilisha hali hiyo kupitia mafunzo hayo ambayo ni nyenzo muhimu ya kutusaidia kupunguza ajali na magonjwa katika sehemu za kazi ili kuongeza tija kwenye uzalishaji.

Naye, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema mafunzo hayo kwa watu wasioona ni utekelezaji wa mwongozo wa ujumuishwaji na uimarishwaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu nchini na taasisi hiyo ina jukumu la kuimarisha usalama na afya kwenye shughuli zao.

“Pamoja na kutoa mafunzo leo tumekuja na fimbo 100 kwa ajili yao na tutawapatia na kitabu maalum kilichochapishwa kwa nukta nundu na tumetengeneza baada ya kutembelea maeneo yao ya kazi na kuona shughuli wanazofanya,”amesema.

Mwenda amesema watu wenye ulemavu wanapofanya kazi kwenye mazingira hatarishi kuna hatari ya kuongeza ulemavu na mafunzo hayo ni muhimu katika kutengeneza kinga ili hali hiyo isiongezeke.

“Tunawafundisha wenzetu hawa ili washiriki vyema kwenye shughuli za kiuchumi, kwa kuwa takwimu za ILO za mwaka 2017 inaonesha asilimia moja hadi saba ya pato la taifa la nchi yeyote hupotea kwa kukosekana ujumuisho wa watu wenye ulemavu, hivyo tukitengeneza miundombinu mizuri wana uwezo wa kuzalisha na pato likaonekana katika kujenga nchi,”amesema.

Awali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona, Bw. Omari Amas, amepongeza serikali kupitia OSHA kwa kuona umuhimu wa kuwapatia elimu hiyo ambayo itasaidia wajikwamue kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Khadija Taya, amesema mafunzo hayo yataleta chachu kwa watu wenye mahitaji maalum kujikwamua kiuchumi na kuchangamkia fursa mbalimbali.
Share:

GGML YAONGEZA UDHAMINI KWA GEITA GOLD FC MSIMU WA 2022/2023


Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Geita FC, Pole Zengo, wakionyesha mkataba wa udhamini uliosainiwa kati ya pande hizo mbili. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Geita, Constantine Kanyasu (CCM), Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi (wa tatu kulia), na Kaimu Meneja Mwandamizi wa Masuala ya Jamii wa GGML, Moses Rusasa (wa kwanza kulia), wakitazama (wa pili kulia).

Na Mwandishi wetu 

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeongeza mkataba wa udhamini kwa Klabu ya Geita Gold Football Club (GGFC) wenye thamani ya Sh milioni 800 kuanzia tarehe 16 Desemba 2022.


GGML ilipata haki ya kipekee kama wadhamini wakuu wa Klabu kwa mechi na matukio yote yanayohusiana na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022-2023 (NBC Premier League) kwa mujibu wa makubaliano hayo.


Katika msimu wa 2020/21, Klabu ya Geita Gold FC ilitimiza malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mechi za kimataifa.


Geita Gold, iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ilipata mafanikio hayo kwa mara ya kwanza baada ya kushika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita.

Katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika hivi karibuni kwenye Makao makuu ya Halmashauri ya Mji wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alisema kuwa makubaliano hayo yameifanya GGML kuwa wadhamini wakuu wa klabu ya Geita Gold Football Club.


"Msimu uliopita, GGML ilikubali kudhamini klabu ya Geita Gold Football Club kwa Sh milioni 500; hata hivyo, kwa mwaka 2022, udhamini wetu umeongezwa hadi Sh milioni 800.


"Kama ilivyotajwa kwenye MOU, GGML ingependelea udhamini huu kuwezesha ununuzi wa basi la Klabu, milo ya timu na vifaa vya michezo. Tunatarajia udhamini wetu utarahisisha ushiriki wa timu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2022-2023, pamoja na shughuli nyingine za klabu,” alisema.


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya utiaji saini alifurahishwa kuona pande hizo mbili zikitia saini makubaliano hayo kwa kuwa yatakuwa na ushawishi chanya mkoani Geita.


“Geita Gold Football Club ni kielelezo cha sifa chanya za mkoa wa Geita. Timu imefanikiwa kutambulisha wilaya na mkoa wetu. Kwa sasa kila mtu anafahamu eneo la kijiografia ya mkoa wetu,” alisema na kuzitaka pande hizo mbili kufikiria kuunda Chuo cha michezo mkoani Geita ili kuibua vipaji vya vijana.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi, alipongeza GGML kwa kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya klabu ya Geita Gold FC.


"Ufadhili huu wa GGML katika klabu hii umekuwa na matokeo chanya. Shauku na juhudi za wachezaji ni matokeo ya uwekezaji wa GGML. Tunashukuru kwa dhati kutokana na msaada huu," alisema.




Share:

Video Mpyaa Kabisa : JUMA MARCO - LUBHIMBI


Hii hapa ngoma mpya ya Msanii maarufu wa Nyimbo za asil Juma Marco kutoka Kahama inaitwa Lubhimbi 'Mpaka' ...Ngoma ya moto sana!! Tazama hapa chini
Share:

Monday, 16 January 2023

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU

Share:

YANGA SC YAUSONGELEA UBINGWA, YAICHAPA IHEFU FC 1-0


*********** 

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM 

KLABU ya Yanga Sc imefanikiwa kulipa kisasi kwa kuichapa Ihefu Fc kwa bao 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, tumeshuhudia mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Kalala Mayele ameweza kuongeza kalama yake ya mabao baada ya kufunga kwenye mechi hiyo. 

Mchezo wa kwanza mzunguko wa kwanza Yanga iliharibiwa Unbeaten ya 50 na kufikia 49 kwa kufungwa bao 1-0.
Share:

MAMA AWACHOMA MOTO WATOTO WAKE KISA WAMEDOKOA MBOGA 'DAGAA & NYANYA CHUNGU'



Watoto waliochomwa moto
Picha ya Mwanamke Scholastica Peter mwenye umri wa Miaka 28 akiwa katika ofisi ya Mtendaji kata ya Ibinzamata.

Na Mapuli Misalaba, SHINYANGA

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Scholastica Peter mwenye umri wa Miaka 28 mkazi wa mtaa wa Bugwandege kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, amewajeruhi watoto wake wawili kwa kuwachoma moto kwenye mikono kwa kile alichodai alikuwa akiwaonya baada ya kukomba mboga.


  Waandishi wa habari wamefika eneo la tukio na kuzungumza na Mama huyo ambaye amekiri kuwachoma moto watoto hao, akisema alifanya hivyo kama hatua ya kuwaonya, kwa sababu wana tabia ya udokozi wa mboga.

“Hawa watoto wana tabia ya udokozi ile siku nilipika mboga tukala usiku tukaibakiza asubuhi nikatoka nikaenda kutembeza mboga nikakuta wameikomba mboga yote ilikuwa ni mboga ya dagaa nilichanganya na nyanya ntole/chungu sasa nilikuwaga nawakanya hawasikii hiyo siku nilishikwa na hasira mara ya kwanza niliwapiga na ya pili hii mara ya tatu kulikuwepo jiko lilikuwa na moto na kulikuwepo na jiko ambalo nilikuwaga natolea mkaa baada ya kuwapiga nikasogeza hilo jiko ndiyo nikawa nawababua na kijiko”,amesema Scholastica.

Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kata ya Ibinzamata Victor Kajuna amesema kuwa taarifa hizo amezipata leo kutoka kwa wananchi waliochukua jukumu la kuwabeba watoto na kuwapeleka katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata.

“Leo majira ya saa nne asubuhi niliwapokea wananchi kutoka mtaa wa Bugwandege walifika wakiwa wameongozana na mama mmoja pamoja na watoto wake wawili wakaeleza kuwa baada ya watoto hao kuwaona wanaendelea kuishi bila msaada”,amesema.

Diwani wa kata ya Ibinzamata Mheshimiwa Ezekiel Sabo amekemea kutokea kwa tukio hilo huku akiwaomba wananchi wa kata hiyo kuacha tabia ya kutoa adhabu kali kwa watoto wao,kwani kwa kufanya hivyo ni ukatili.

“Taarifa hii ya watoto kuchomwa moto nimeipokea kwa masikitiko makubwa sana lakini nakemea swala hili lisijitokeze tena katika kata ya Ibinzamata kwa sababu jamii ikifikia hapo basi tutakuwa tumefika pabaya sana na niviombe vyombo vya serikali vifuatilie ili ukatili huu usijirudie tena”, amesema Sabo.

Kwa upande wake Afisa elimu wa kata ya Ibinzamata Mackrine Shija amewaomba wazazi na walezi kuacha tabia ya kutoa adhabu kubwa kwa watoto.

Msaidizi wa kisheria kutoka Community Edification Organization kata ya Ibinzamata Robert Said amesema kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.

Share:

BAKARI KHAMIS : "USICHUKULIE POA UNAPOONA WATU WANAGOMBANA TUZUIE MAUAJI"


Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bakari Hamis
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bakari Khamis.

**
Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog
Wakati wanaharakati wa haki za wanawake na watoto wakiendelea kupaza sauti jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Bakari Hamis amesema ni vyema jamii ikajikita katika kuzuia ukatili badala ya kujitokeza baada ya tukio kufanyika.


Mwenyekiti huyo wa Mtaa wa Mabambasi ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 16,2023 wakati akitoa neno kwenye msiba wa mkazi wa mtaa huo Bi. Asia Mdadila (85) aliyefariki dunia jana Jumapili baada ya kuanguka Jumamosi na kulazwa hospitali ambapo mazishi yamefanyika leo mchana.

Khamis amesema bado matukio ya ukatili dhidi ya wanawake yanaendelea katika jamii ikiwemo wanandoa kuuana jambo ambalo amesema mwarobaini wake ni jamii kuzuia vitendo hivyo wanapoona dalili mbaya kabla havijatokea.

“Wananchi acheni kunyamaza mnaposhuhudia matukio ya ukatili,msichukulie poa mambo haya. Utakuta mke na mme wanapigana kila siku lakini nyinyi mnanyamaza tu, matokeo yake mauaji yakitokea mnaanza kusema hawa walikuwa wanapigana kila mara, ama tuliwaona wanagombana tukaona tusiingilie mambo ya watu, au tulisikia tu mtu anapiga kelele”,amesema Khamis.


“Ndugu zangu naomba tuishi kwa amani na utulivu, tusinyamazie tunapoona dalili za ukatili wa kijinsia. Nawasisitiza sana sana kuzingatia uvumilivu na kufuata sheria. Unapokuwa umepatwa na jambo lolote lile vipo vyombo mbalimbali vya kutatua mambo kuanzia katika ofisi za serikali za mitaa,kata, wilaya,mkoa na kitaifa.

“Hakuna sababu za raia yeyote kujichukulia sheria mkononi, mnakumbushwa sana kufuata sheria zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria na miongozo ya dini hairuhusu mtu kuua”,ameongeza Khamis.

Khamis amesema uongozi wa Mtaa huo unaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia mikusanyiko mbalimbali kuachana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Share:

KAZI IMEANZA, HAKUNA KUSUBIRI....TAYARI SOPHIA MJEMA KATUA LUMUMBA




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema amewasili Ofisini kwake Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam leo Jumatatu tarehe 16 Januari, 2022.


Ndugu Mjema akizungumza na watumishi na maafisa wa idara yake amewataka kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na wakati wote kuhakikisha wanakuwa mfano bora katika kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya CCM na Mwenyekiti wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Amesisitiza kazi kubwa iliyopo mbele ni kuendelea kuyasema mazuri yanayofanyika kwa wananchi ili wayafahamu, kueleza uzuri wa CCM, kuwasikiliza wananchi kero au changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wetu kupitia mafunzo. Kazi zote hizi hazipaswi kusubiri, tuanze sasa na tuendelee mbele.


#CCMImara #RaisNiSamia #KaziIendelee
Share:

WANAWAKE LAKI MOJA, MASHIRIKA YAGEUKA MBOGO MAUAJI YA WANAWAKE SHINYANGA...."NI UPUUZI MKUBWA KUSEMA NILISIKIA TU AKIPIGA KELELE"

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi, Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani.

Na Kadama Malunde & Elizabeth Cosmas - Malunde 1 blog

Taasisi ya Wanawake Laki Moja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Shinyanga yamelaani matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yanayoendelea mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla huku wakiitaka jamii kupaza sauti kupinga vitendo hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Januari 16,2023 katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe amesema Taasisi hiyo inasikitika kuona vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kutokea katika jamii.

“Tumekuwa tukipata taarifa na kuhusu matukio ya kikatili ikiwemo wanawake kuuawa kwa kupigwa na waume zao, matukio haya yanatokea kwenye maeneo yetu lakini jamii haitoi ushirikiano kuripoti matukio kwa wakati vitendo vya ukatili vikifanyika”,amesema Ndagiwe.

“Wananchi wamekuwa wakishuhudia matukio ya ukatili lakini wanakaa kimya, hawatoi taarifa. Ni upuuzi mkubwa kusema ‘Nilisikia akipiga kelele’ inasaidia nini sasa wakati mtu tayari ameshapoteza maisha, ungepaza sauti hayo mambo yasingetokea, wanawake wasingeuawa”,ameeleza Ndagiwe.

Mwenyekiti huyo wa Wanawake Laki Moja ameomba viongozi wa serikali za mitaa kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa mstari wa mbele kutokomeza matukio ya ukatili kwani baadhi yao hawafanyi kazi ya ulinzi na usalama ipasavyo.

“Viongozi wa ngazi za juu hawana tatizo, tatizo ni viongozi wa huku chini ambao ni wenyeviti wa vitongoji, vijiji, mitaa baadhi yao wanalegalega katika suala la ulinzi na usalama wa wanawake na watoto, wengine wanadiriki kumaliza kesi kienyeji kwa kupeana pesa badala ya kupeleka kesi kwenye vyombo vya kisheria”,ameongeza Ndagiwe.

Amewashauri wanandoa kuvunja ukimya wanapofanyiwa au kuona dalili za kufanyiwa ukatili kwa kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali na Dawati la Jinsia na Watoto ili kukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives amesema Mauaji ni ukiukwaji wa haki za binadamu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha wanawake na watoto wanalindwa.

“Wanandoa mkishafikia hatua ya kuambizana kuuana hiyo ni hatua mbaya sana. Ukitishiwa kuuawa usinyamaze kwani ipo siku atatimiza anachokisema. Pia tunaomba viongozi wa dini waendelee kupaza sauti kutoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika jamii”,amesema Mbugani.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na serikali katika kutokomeza vitendo vya kikatili huku akiwahamasisha wananchi kutoa ushahidi kwenye kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia badala ya kupeana pesa kumaliza kesi hizo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi akizungumza na Waandishi wa Habari 
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akizungumza na Waandishi wa Habari 
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani.
Share:

UDHIBITI WA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU KATIKA WILAYA YA MVOMERO

Share:

Sunday, 15 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 16,2023



Magazetini leo Jumatatu January 16, 2023











































Share:

TAZAMA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 MARUDIO

Taarifa kwa Umma Kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Kuhusu Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza kwa Wanafunzi waliofanya Mtihani wa Marudio Tarehe 21-22 Disemba 2022.


Share:

MWANAMKE AFARIKI DUNI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA MAMBA AKIOGA MTONI

 

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Modesta Shido (31) mkazi wa Ubaruku Mbarali Mkoani Mbeya amekutwa amefariki kwa kushambuliwa na Mamba sehemu a kiunoni wakati akioga Mtoni katika Mto wa Mkoji uliopo katika Kijiji cha Lyala Mkoani Mbeya.

Akithibitisha tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amesema limetokea Mnamo tarehe 09.01.2023 majira ya saa Tisa Mchana huko katika Kijiji cha lyala Kata ya Luhanga Mbarali ambapo Chanzo cha kifo ni kuoga Mtoni na kupelekea kung na Mamba katika Mto wa Mkoji.


Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa Wananchi kuacha kuwa na tabia ya kuoga mtoni.
Share:

KENYA YAWASIMAMISHA KAZI WACHEZAJI 14 NA MAKOCHA WAWILI KWA KUPANGA MATOKEO LIGI YA TAIFA


Shirikisho la soka nchini Kenya limewasimamisha kazi wachezaji 14 na makocha wawili kwa tuhuma za upangaji matokeo baada ya kupokea taarifa kuhusu udanganyifu katika ligi ya taifa.

Miongoni mwa waliosimamishwa Ijumaa ni wachezaji sita kutoka Zoo Kericho FC, ambayo ilipatikana na hatia ya kupanga matokeo na kitengo cha uadilifu cha FIFA mnamo 2021 na kufukuzwa kutoka kwa Ligi Kuu ya Kenya.

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) lilisema kuwa limewasimamisha kazi washtakiwa hao, akiwemo mchezaji mmoja kutoka kwa Tusker ya Ligi Kuu ya Kenya, hadi kesi hiyo ichunguzwe rasmi.

“Shirikisho la Soka la Kenya limepokea ripoti za siri zinazodai kuhusika kwa wachezaji na maafisa mbalimbali katika shughuli za upangaji matokeo,” shirika hilo lilisema kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti yake.

“Katika juhudi za kulinda uadilifu wa ligi … shirikisho limewasimamisha mara moja watu hawa kusubiri uchunguzi wa suala hilo na idara ya uadilifu ya FIFA na FKF.”

Shirika hilo liliwashauri wanachama wote wa FKF “kuepuka mawasiliano yoyote yanayohusiana na michezo” na wachezaji na makocha waliosimamishwa katika kipindi cha kusimamishwa.

Mnamo Februari 2020, FIFA ilipiga marufuku wachezaji wanne wa Kenya – mmoja kwa maisha – kwa “njama ya kimataifa” ya kurekebisha mechi za ligi.

Waamuzi watano wa Kenya walisimamishwa baadaye kutokana na kashfa hiyo hiyo.

Kenya ilirejea katika kandanda ya kimataifa mwezi Novemba baada ya kusimamishwa na FIFA Februari 2022 kwa madai ya ubadhirifu wa fedha na kuteua kamati ya muda.

Mnamo 2004, FIFA ilisimamisha Kenya kwa miezi mitatu kwa kuingiliwa na serikali, lakini hali ilibadilishwa baada ya nchi hiyo kukubali kutunga sheria mpya
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger