Saturday, 10 December 2022

JINSI TGNP ILIVYOADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA...GEMMA ATAKA KILA MMOJA ALINDE MTOTO

Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali leo Jijini Dar es Salaam akizungumza na wananchi wakati wa Maadhimisho ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambayo hufanyika kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kila Mwaka ambapo amesema ukatili unaofanyika kwenye jamii na ndani kwenye familia ndio unaowadhuru watoto na wanawake ndio unaowanyima haki zao za Msingi.


Amesema kumekuwa na taaarifa za kingono kwenye sekta ya usafiri hasa kwenye magari ya watoto kwa hiyo usalama wa watoto upo hatarini sana hivyo kila mtu awe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsi dhidi ya watoto na wanawake.


"Ni jukumu letu Kila mmoja katika jamii ajisikie kuwajibika kumlinda mtoto ili afurahie utoto wake, ujana wake pamoja na kufurahia uzee wake", amesema Gemma.


Akizungumzia kuhusu ufuatiliaji wa sheria ya Ngono amesema kuwa watafuatilia sheria ya rushwa ya ngono, ambayo inakaribia kwenda kujadiliwa bungeni ambayo ina kipengele cha sheria Rushwa ya ngono ni sawa na uhujumu uchumi.


Amesema kuwa Takwimu za Jeshi la Polisi za Januari hadi Desemba 2021 zinaonesha kulikuwa na kesi 5899 za ubakaji, matukio ya ubakaji 1677 na Matukio ya mimba za utotoni 1114 .


Pia amesema kuwa jamii sijionee aibu kukemea matendo ya ukatili wa kijinsia kwani yamefika hadi ngazi ya Familia.


Kwa upande wake Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Builders of Future Africa Brenda Mgallah amesema kuwa ukatili ni jambo la kukemewa katika jamii hivyo kila mmoja awe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia.


Naye Mwakilishi wa Serikali ya Mtaa wa Mabibo, amesema kuwa wanashirikiana na TGNP, viongozi wa dini kutoa elimu makanisani na misikitini katika kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi ya mtaa na familia na tayari wameanzisha mabaraza la kata kwa ajili ya kusimamia na kupinga ukatili ya kijinsia maeneo yote yanayoizunguka jamii.


Kauli mbiu ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kila uhai una thamani, tokomeza Mauaji ya wanawake na watoto.


Ukatili dhidi ya watoto umekuwa ni sehemu ya maisha ya watoto wengi nchini ambapo asilimia nane ya wanawake na watoto wenye umri wa Miaka 15 hadi wanapata ukatili wa Kingono na wanaofanya ukatili huo ni ndugu wa karibu.
Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akizungumza na vituo vya Taarifa na Maarifa, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kuhusu taswira halisi ya namna walivyoweza kukabiliana na ukatili wa kijinsia wakati alipokuwa anafanya ufunguzi wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya hiyo Leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP Subira Kibiga akimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Builders of Future Africa Brenda Mgallah akizungumza namna wanavyoshirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kutoa Elimu kwa jamii kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Makini Janeth Johnakizungumza kuhusu namna wanavyitoa elimu hasa kwa watoto wa kike waliopo mashuleni namna ya kujitambua na kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe mbalimbali wakichangia mada kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Baadhi ya viongozi kutoka Serikalini, mashirika, vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akiwa kwenye picha za pamoja na Makundi mbalimbali kama vile viongozi kutoka Serikalini, Mashirika na Taasisi, vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na Wananchi mbalimbali wakiwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akiwasili kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.

Maandamano yakiendelea
Burudani zikiendelea
Share:

TBS YASHIRIKI TAMASHA LA VIPODOZI 2022 DAR ES SALAAM

Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bi. Hidaya Kabelege akitoa elimu kuhusu madhara ya vipodozi vyenye viambata sumu na usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi kwa wananchi waliotembelea banda la TBS lililopo katika tamasha la siku ya vipodozi 2022, lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam mapema leo.

*****************

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Tamasha la Siku ya Vipodozi 2022 katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam ambapo wananchi wameweza kutembelea kwenye banda la TBS na kupewa huduma.

TBS imetoa elimu kuhusu madhara ya vipodozi vyenye viambata sumu na usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi kwa wananchi ambao wameweza kutembelea kwenye Tamasha hilo.

Share:

TVMC YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUTOA ELIMU NSALALA...."WANAOJIGAMBA BAADA YA KUACHIWA BADO TATIZO"


Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Shinyanga Mussa Ngangala akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata ya Nsalala Halmashauri ya Shinyanga.


Na Shinyanga Press Club Blog

Jamii imetakiwa kuendelea kuwafichuaa watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na kuwa chanzo cha umasikini kwenye familia na kuharibu ndoto za watoto kwa kuwakatisha masomo kutokana na kupata ujauzito katika umri mdogo pamoja na kukomesha ndoa za utotoni.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Nsalala Mkurugenzi wa Shirika la TVMC lenye makao makuu yake Manispaa ya Shinyanga Mussa Ngangala,amesema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wameamuaa kuwafikia wananchi vijijini ili kutoa elimu itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo ambavyo bado ni changamoto kwenye jamii.

Ngangala amesema kila mtu ana wajibu wa kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha anakuwa salama wakati wote anapokuwa nyumbani na shuleni,kutokana na vitendo vya ukatili kuisababishia hasara serikali kwa kutumia fedha nyingi kuhudumia madhura wa ukatili.

Kwa upande wa mimba na ndoa za utotoni,Mussa ameiomba jamii kuacha kuwalinda watu wanaoharibu ndoto za watoto wao kwa kuwakatisha masomo baada ya kupata ujauzito,badala yake wawe mstari wa mbele kutoa taarifa kwa viongozi ili wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha matukio hayo.

“Bado tuna changamoto kubwa ya mimba na ndoa za utotoni sasa ni jukumu letu sisi sote kama wazazi kupinga vitendo hivyo ili viweze kukoma na kuwawezesha watoto kufikia ndoto zao, hakikisheni mnafuatilia mienendo ya watoto wenu wanapokuwa nyumbani hasa wakati wa likizo pia kujua changamoto wanazokumbana nazo wanapokwenda shule”, amesema Ngangala.

Nao baadhi ya wakazi wa Kata ya Nsalala Juliana Paul na Kazimili Shuhuli wamesema vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni tatizo kubwa na kuiomba serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na kuchukuwa hatua kali.

Wakazi hao wa Nsalala wamesikitishwa na kitendo cha watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwemo wanaowapa mimba wanafunzi kuachiwa huru na kuonekana mitaani wakitoa maneno ya majigambo jambo ambalo wamesema linaongeza machungu kwa madhura wa ukatili kutokana na kukaa muda mfupi na kurejea tena mitaani na kuiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria ili liwe fundisho kwa wengine.
Mkazi wa Kata ya Nsalala Kazimili Shuhuli akitoa maoni yake jinsi ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Cloudi Malunde kutoka MC Entertainment akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kata ya Nsalala.
Juliana Paul akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mkutano unaendelea
Wananchi wa Nsalala wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Share:

MWIMBAJI NGULI WA RHUMBA ELIZABETH TSHALA MUANA AFARIKI DUNIA


Habari za kifo chake zimewekwa asubuhi ya leo kwenye mtandao wa Meta na mtayarishaji na mwandani wake, Claude Mashala.

‘’Mapema asubuhi ya leo Bwana mwema amefanya uamuzi wa kumuita tena Tshala Muana. Mola mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa Duniani. Kwaheri Mamu kutoka kwangu’’

Juni mwaka jana 2020, kulitokea uvumi kwamba amefariki, lakini badala yake akalazwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa kiharusi.

Élisabeth Tshala Muana Muidikay (aliyezaliwa 13 Mei 1958), anayejulikana kwa jina lake la kisanii kama Tshala Muana, alikuwa mwandishi na mpiga densi wa Kikongo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anachukuliwa kuwa ‘’Malkia wa Mutuashi’’, muziki wa kitamaduni na densi kutoka eneo lake la asili la Kasai, katikati mwa nchi ya DR Congo.

Mara nyingi watu humuita "Mamu National", mama wa taifa.

Anajulikana kwa nyimbo kadhaa kama vile "Karibu Yangu", "Malu", "Tshianza", "Tshibola" na zingine nyingi.

Amefanya ziara nyingi nje ya nchi, ameshinda tuzo kadhaa katika eneo la kitaifa, bara na kimataifa na amerekodi zaidi ya albamu 20.

Muziki wake umeonekana katika rekodi maarufu ya muziki ya 1987 ya La Vie est Belle na Aya ya Yop City.

Share:

TTB YAADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU WA TANZANIA KWA KUSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA SANAA

Picha ya Pamoja, Dkt. Soumya Manhunath Chavan na watumishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mkuu wa Kituo cha Kutolea Taarifa kwa Watalii cha Bodi ya Utalii kanda ya Pwani, Alistidia Karaze akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Dkt. Soumya Manhunath Chavan mfuko wenye zana za kutangazia utalii mara baadaya kufungia maonesho ya sanaa.


Mmoja ya wasanii walioshiriki Maonesho ya Sanaa.

************************

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika maonesho ya Sanaa ya Uchoraji wa Picha mbalimbali zinazoonyesha mandhari ya vivutio vya utalii vya Tanzania, Maonesho haya yana lengo la kukuza kazi ya Sanaa ili wasanii waweze kujikwamua kiuchumi na jamii iweze kuitambua na kuithamini kazi ya sanaa ya uchoraji.



Maonesho haya ya siku tatu yameandaliwa na Jumuiya ya Kihindi inayoitwa Arthshakti Foundation kama sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania, Maonesho ya Sanaa yanafanyika katika Mgahawa wa Chill a& Lime uliopo jijini Dar es salaam, Kuanzia leo Disemba 9 – 11, 2022.



Akiongea mara baadaya ufunguzi wa Maonesho Mkuu wa Kituo cha Kutolea Taarifa kwa Watalii cha Bodi ya Utalii kanda ya Pwani, Alistidia Karaze amesema”

Tunawashuri vijana wanaochipukia katika sanaa ya uchoraji, kuendelea nayo pasipo kukta tamaa kwani Sanaa ya uchoraji ni njia mojawapo ya kutangaza utalii kupitia picha vile vile na kukuza uchumi na kuongeza ajira”.
Share:

Friday, 9 December 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 10,2022










Share:

MCHUNGAJI AWASHAURI WAKE ZA WATU KUOMBEA MICHEPUKO YA WAUME ZAO IOLEWE


Mchungaji anayezingirwa na utata James Ng’ang’a amewashauri washirika wa Kanisa lake la Neno Evangelism kuwaombea mipango ya kando ya waume zao wapate kujaliwa bwana zao.

Akihubiri katika ibada kanisani mwake hivi karibuni, Ng’ang’a aliwaambia wanawake walioolewa kuacha kuomba mabaya kuwapata hawara za waume zao, bali wanapaswa wawaombee nao pia waolewe.

"Nasikia mnasema mpango wa kando akufe. Wamama wanapenda hiyo sana. Sema bwana Yesu bariki mpango wa kando mpatie bwana yake," alisema pasta huyo.

 Zaidi ya hayo, Ng'ang'a aliwatetea mpango wa kando akisema, hawapaswi kulaumiwa kwani mara nyingi ni wanaume ndiyo huwavizia.

"Bwana yako ndiye mpango wa kando, ndiye anatanga tanga tanga. Basi kwanza ua bwana yako... Na umesema Yesu asifiwe, hatujaitwa kuua," aliongeza.

Via Tuko News
Share:

GGML YAWAAGA WAHITIMU WA MAFUNZO TARAJALI


Baadhi ya wahitimu wa mafunzo tarajali kutoka GGML wakiwa na vyeti vya kuhitimisha mafunzo waliyoyapata kwenye kampuni hiyo kwa mwaka 2021/2022

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imewaaga wahitimu 26 wa mafunzo tarajali waliokuwa wakifanya mafunzo katika kampuni hiyo kwa mwaka 2021/2022.


GGML hutekeleza programu ya mafunzo tarajali kila mwaka kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu inayohusika na ajira, vijana, na watu wenye ulemavu pamoja na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Chama cha Waajiri Nchini (ATE). Hii ni mojawapo pia ya mkakati wa kampuni ya GGML kunufaisha jamii ya Tanzania kutokana na shughuli za uchimbaji dhahabu.


Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wahitimu hao mkoani Geita, Meneja Mwandamizi anayesimamia kitengo cha Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo kutoka GGML, Dkt Kiva Mvungi amewapongeza wahitimu hao kwa kufikia hatua hiyo muhimu katika fani walizozisomea.


“Tunawapongeza kwa kupata fursa hii. Kampuni yetu imekuwa ikitoa nafasi hizi kila mwaka na wahitimu wengi wa vyuo vikuu wamekuwa wakituma maombi yao. Kwa ambao mlichangamkia fursa za ajira zilipotangazwa, tunawapongeza kwa kuwa wafanyakazi wa kudumu wa kampuni hii. Kwa ambao bado hamjapata ajira, endeleeni kutuma maombi yenu kila GGML inapotoa nafasi za kazi,”


Dkt Mvungi alisisitiza, “Kukamilisha programu hii ni mwanzo sasa wa kuonesha ukomavu wenu mnapoitwa katika udahili wa kazi. Asimilia kubwa ya vijana waliopitia programu hii wameajiriwa na makampuni mbalimbali, bila shaka nanyi mtaajiriwa pia hapa GGM au kwingineko. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini hapa nchini inapata wafanyakazi wenye uzoefu.”


Kwa upande wake Mhandisi Ruth Mugurusi ambaye ameajiriwa katika kitengo cha ulipuaji cha GGML ameshukuru kupata fursa hiyo akiwa katika mchakato wa kuhitimu mafunzo yake.


“Mimi ni Mtanzania ambaye naishukuru sana GGML kwa kunipatia fursa hii. Baada tu ya kuhitimu masomo yangu ya Chuo Kikuu, nilituma maombi na kuanza mafunzo haya. Namshukuru Mungu nikiwa katika kipindi cha mafunzo haya, zilitangazwa nafasi na mimi na wenzangu tukatuma maombi na kufaulu usaili na leo hii hatimaye tumeajiriwa na GGML. Nawashauri wahitimu wengine wa mafunzo haya, waendelee kutuma maombi yao kila nafasi zinapotangazwa kwa kuwa GGML ni kampuni inayotoa fursa kwa watu wote wakiwemo wanawake,” alisema Mhandisi Mugurusi.


Tangu programu hii ianze mwaka 2009 hadi hivi sasa jumla ya wahitimu 168 wamenufaika ambapo kati ya hao wasichana ni 58 na wavulani ni 110. Asilimia kubwa wameajiriwa na GGML katika vitengo vya uchenjuaji dhahabu, uhandisi, ufundi, ulipuaji na uchimbaji madini na baadhi yao wameajiriwa katika makampuni mengine ndani na nje ya nchi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger