Habari za kifo chake zimewekwa asubuhi ya leo kwenye mtandao wa Meta na mtayarishaji na mwandani wake, Claude Mashala.
‘’Mapema asubuhi ya leo Bwana mwema amefanya uamuzi wa kumuita tena Tshala Muana. Mola mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa Duniani. Kwaheri Mamu kutoka kwangu’’
Juni mwaka jana 2020, kulitokea uvumi kwamba amefariki, lakini badala yake akalazwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa kiharusi.
Élisabeth Tshala Muana Muidikay (aliyezaliwa 13 Mei 1958), anayejulikana kwa jina lake la kisanii kama Tshala Muana, alikuwa mwandishi na mpiga densi wa Kikongo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Anachukuliwa kuwa ‘’Malkia wa Mutuashi’’, muziki wa kitamaduni na densi kutoka eneo lake la asili la Kasai, katikati mwa nchi ya DR Congo.
Mara nyingi watu humuita "Mamu National", mama wa taifa.
Anajulikana kwa nyimbo kadhaa kama vile "Karibu Yangu", "Malu", "Tshianza", "Tshibola" na zingine nyingi.
Amefanya ziara nyingi nje ya nchi, ameshinda tuzo kadhaa katika eneo la kitaifa, bara na kimataifa na amerekodi zaidi ya albamu 20.
Muziki wake umeonekana katika rekodi maarufu ya muziki ya 1987 ya La Vie est Belle na Aya ya Yop City.
0 comments:
Post a Comment