Wednesday, 21 December 2022

TBS YAKABIDHI LESENI NA VYETI VYA UBORA 42 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA KANDA YA ZIWA

...
Kaimu Katibu Tawala (Mwanza) Bw. Patrick Kurangwa akikabidhi vyeti na leseni za ubora 42 kwa wazalishaji wa bidhaa kutoka mikoa iliyopo kanda ya Ziwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hiiti B. Sillo uliyopo Jengo la TMDA jijini Mwanza mapema leo.

Bw. Kurangwa aliwapongeza wazalishaji hao na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri wa TBS kwa kuendelea kuzalisha bidhaa bora.Kaimu Katibu Tawala (Mwanza) Bw. Patrick Kurangwa akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni za ubora iliyofanyika katika ukumbi wa Hiiti B. Sillo uliopo jengo la TMDA jijini Mwanza.Meneja Kanda ya Ziwa (TBS) Mhandisi Joseph Ismail Mwaipaja akitoa neno la utangulizi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala Mwanza Bw. Patrick Kurangwa katika hafla ya utoaji vyeti na leseni za ubora iliyofanyika katika ukumbi wa Hiiti B. Sillo uliopo jengo la TMDA jijini Mwanza.

Mhandisi Mwaipaja alitoa wito kwa wajasiriamali wadogo kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha ukizingatia Serikali inatenga fedha kupitia TBS kwa lengo la kuwapatia leseni ya kutumia alama ya ubora bila gharama yoyote.Kaimu Katibu Tawala (Mwanza) Bw. Patrick Kurangwa akipata maelezo kutoka kwa wazalishaji waliopata vyeti na leseni za ubora alipotembelea bidhaa zao katika hafla ya utoaji vyeti iliyofanyika ukumbi wa Hiiti B Sillo uliopo jengo la TMDA jijini Mwanza.

Katika hafla hii TBS imetoa vyeti na leseni 42 kwa wazalishaji wa bidhaa mbambali katika leseni hizo leseni 8 ni kwa wajasiriamali wadogo waliothibitishwa bure na TBS. Kaimu Katibu Tawala (Mwanza) Bw. Patrick Kurangwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wazalishaji waliopokea vyeti na leseni za ubora kutoka mikoa iliyopo kanda ya Ziwa katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Hiiti B. Sillo uliyopo Jengo la TMDA jijini Mwanza mapema leo.

*********************

SERIKALI kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) itahakikisha miongozo na taarifa muhimu kuhusiana na ubora na usalama wa bidhaa zinapatikana kwa wakati na kuhakikisha bidhaa zenye ubora hafifu zinaondolewa sokoni lakini pia kuendelea kutoa elimu elekezi wakati wa kaguzi mbalimbali viwandani na katika masoko;

Ameyasema hayo leo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Patrick Kurangwa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti na leseni za ubora 42 wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba, 2022 kutoka mikoa iliyopo kanda ya Ziwa.

Amesema wajibu wetu sote kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa viwandani, zinazingatia kanuni bora za uzalishaji ambazo hazitachafua wala kuharibu sifa halisi za bidhaa husika.

"Kwakulitekeleza hili Serikali imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa kisekta (kama ninyi hivi leo) kwa lengo la kulinda afya za watumiaji na mazingira katika mkoa wetu wa Mwanza, Kanda ya ziwa na maeneo mengine nchini". Amesema Bw.Kurangwa.

Kwa upande wake Meneja Kanda ya Ziwa (TBS) Mhandisi Joseph Mwaipaja amesema TBS kanda ya ziwa imeweza kutoa jumla ya vyeti na leseni Arobaini na mbili (42). Kati ya hizo, leseni na vyeti vipatavyo nane (8) sawa na (19.05%) vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo.

Aidha Vyeti na leseni hizo vinahusisha bidhaa mbalimbali kama vile; chakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vifaa vya makenika, vibebeo pamoja na vifungashio.

Pamoja na hayo amewaasa wazalishaji waliopata leseni na vyeti vya ubora kuwa mabalozi wazuri katika matumizi ya Viwango ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania tupo uchumi wa kati.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger