Friday, 12 August 2022

REA YATUMIA TAKRIBANI TRILIONI 3 KUFIKISHA UMEME VIJIJINI

Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Azam, Godluck Paul (kulia) akiendesha mjadala wakati wa mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau jana Agosti 11, 2022 Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA, Mhandisi Jones Olotu, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau jana Agosti 11, 2022 Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA, Mhandisi Jones Olotu (wa kwanza kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau jana Agosti 11, 2022Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu nishati vijijini wakati wa mkutano na wadau wa REA jijini Dar es Salaam jana Agosti 11, 2022 Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti, Mhandisi Elineema Mkumbo (katikati), akijibu hoja za wadau kuhusu masuala mbalimbali kuhusu nishati vijijini wakati wa mkutano wa REA na wadau wake jijini Dar es Salaam hapo jana Agosti 11, 2022

Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia, Mhandisi Advera Mwijage (kulia) akichangia katika mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau wake ukiangazia masuala mbalimbali ya nishati vijijini ambao umefika Agosti 11, 2022 Jijini Dar es Salaam na kurushwa mubashara na kituo cha Azam TV Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia, Mhandisi Advera Mwijage akichangia katika mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau wake ukiangazia masuala mbalimbali ya nishati vijijini ambao umefika Agosti 11, 2022 Jijini Dar es Salaam na kurushwa mubashara na kituo cha Azam TV

Wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari nchini wakifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Hassan Saidy (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa REA na wadau wake jijini Dar es Salaam Agosti 11, 2022

Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Nipashe, Bi. Salome Kitomali akichangia katika mkutano wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wadau wake jijini Dar es Salaam hapo jana Agosti 11, 2022.Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi, Mhandisi Jones Olotu (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti, Mhandisi Elineema Mkumbo (Wa kwanza kutoka kulia), Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia, Mhandisi Advera Mwijage (wa pili kutoka kushoto ) na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Azam, Godluck Paul mara baada ya kuhitimisha mkutano wa REA na wadau wake hapo jana Agosti 11, 2022

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA MWANDISHI WETU

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) hadi sasa umetumia takribani Shilingi trilioni 3 kwa ajili ya kazi ya kupeleka miradi ya umeme vijijini ili kuhakikisha nishati ya umeme inafika na kutumika kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ya uzalishaji, kuboresha huduma na shughuli za kiuchumi.

Hayo yamesemwa Agosti 11, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy wakati wa mkutano wa Wakala huo na wadau wake kuelezea masuala mbalimbali ya nishati vijijini uliorushwa mubashara na kituo cha televisheni cha Azam ambapo amesisitiza kuwa mradi unaoendelea hivi sasa (mradi wa usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili) pekee unagharimu kiasi cha shilingi trilioni 1.2.

Mhandisi Saidy ameongeza kuwa, kutokana na kazi zinazoendelea na mipango waliyoijiwekea, vijiji vyote nchini vitapata umeme kabla ya muda ulioelekezwa (mwaka 2025).

"Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeahidi kufikisha umeme katika vijiji vyote ifikapo mwaka 2025, sisi kama REA hatutafika huko, tutakamilisha vijiji vyote kuvipatia umeme kabla ya mwaka huo" alisema Mhandisi Saidy na kuongeza kuwa

"Wananchi wakipata nishati ya umeme itasaidia sana katika uhifadhi wa mazingira, kwani hivi sasa zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanatumia kuni na mkaa jambo ambalo linapelekea kuathiri mazingira kwa kuharibu misitu. Takwimu zinaeleza kuwa kwa mwaka mmoja, Tanzania inapoteza hekta 400 za misitu"

Ameendelea kwa kusema kuwa, REA inatumia gharama kubwa kupeleka miradi ya umeme vijijini hivyo amewataka wananchi wa vijijini kuchangamkia fursa hiyo kwa kuutumia kwa shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa REA , Mhandisi Elineema Mkumbo, amesema hali ya upatikanaji wa umeme vijijini imepanda kutoka asilimia 2 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 69.6 kufikia mwaka 2020. "Lengo letu ni kuhakikisha vijiji na vitongoji vyote nchini vinapata umeme nyumba kwa nyumba.

Mhandisi Mkumbo ameeleza kuwa, kazi ya kupeleka umeme vijijini inaenda sambamba na kupeleka umeme katika vitongoji ambapo hadi sasa zaidi ya vitongoji 27,000 vimepatiwa umeme.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA, Mhandisi Jones Olotu ameeleza kwamba, kufuatia kasi ya upelekaji miradi ya umeme vijijini na nishati hiyo kuwafikia wananchi wengi wa vijijini, Tanzania imeweka rekodi na kuongoza katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wananchi wake wamepunguza kuhama kutoka vijijini kwenda mijini na badala yake watu mijini kuhamia vijijini kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali.

"Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kubadilisha mtazamo wa watu kuhama kutoka vijijini kuja mjini, siku hizi ni kawaida kabisa watu wanahama kutoka mjini na kuhamia vijijini" alisema Mhandisi Olotu.

Mhandisi Olotu amebainisha kwamba, matokeo ya kasi ya upatikanaji umeme vijijini hivi sasa ni matokeo ya REA kuandaa mipango kabambe na mikubwa ukiwemo mpango mkubwa wa miaka mitano wa kupeleka umeme katika vijiji vyote nchini ambao REA inaendelea kuutekeleza huku vipaumbele vikiwa ni taasisi za umma ikiwemo zahanati, shule, vituo vya maji, polisi, nyumba za ibada kwa lengo la kuboresha huduma za jamii.

Akichangia katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia wa REA, Mhandisi Advera Mwijage amesema, kazi ya REA syo tu kupeleka umeme vijijini bali ni kupeleka nishati mbalimbali vijijini ili ziweze kutumika na wananchi wa maeneo hayo katika shughuli mbalimbali ambapo katika kusambaza gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani wanashirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kazi hiyo wanaifanya katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani.

Mhandisi Mwijage ameongeza kuwa, katika maeneo ya visiwa, REA imekuwa ikitumia nishati ya jua katika kupeleka miradi ya umeme ili kuhakikisha visiwa vyote nchini vinapata nishati hiyo ambapo kwa sasa mpango uliopo ni kuvipelekea umeme visiwa 36.

"Tanzania tuna visiwa 196, visiwa 53 havina makazi ya kudumu, vyenye makazi ya kudumu ni 143. Kati ya visiwa 143 vyenye makazi ya kudumu, visiwa 72 vina umeme na visiwa 71 havina umeme. Tulianza na visiwa 20 kuvipelekea umeme na sasa tuna mpango wa kupeleka umeme katika visiwa 36" alisisitiza Mhandisi Mwijage.

Akizungumzia suala la mawakala wa wauzaji mafuta vijijini ambao watakopeshwa ili kutoa huduma hiyo kwa wananchi wa vijijini, Mhandisi Mwijage amesema

"Kitu kikubwa kitakachozingatiwa kwa wauzaji na vituo vya mafuta vijijini ni usalama, mazingira ya kuuzia mafuta, eneo na kituo husika. Watakaokidhi vigezo watawezeshwa kupitia mikopo na lengo letu ni kuhakikisha kwamba katika utekelezaji wa zoezi hili walengwa na wanufaika wote watoke vijijini"

Nao wahariri wa vyombo vya habari Joyce Shebe, Salome Kitomali na Neville Meena wakizungumza katika mkutano huo wameishauri REA kuendelea kutilia mkazo suala la usawa wa kijinsia katika fursa na matumizi ya nishati, kuchangia na kukuza uchumi.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 umekuwa na desturi endelevu ya kukutana na wadau mara kwa mara kueleza na kutoa mrejesho wa masuala mbalimbali ya nishati vijijini lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau na mwananchi mmoja juu kazi zinazoendelea kufanywa na Wakala huo.
Share:

PESA ZA MAENDELEO ZA RAIS SAMIA HAIJAWAHI KUTOKEA TANGU UHURU - MBUNGE JAH PEOPLE

Mbunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe, Deo Sanga, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka pesa za maendeleo kila kona ya nchi.

Sanga amesema kuwa uwekezaji huo wa serikali ya Rais Samia kwenye miradi ya maendeleo haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.


Mbunge huyo, maarufu kama Jah People, aliongea wakati wa mkutano wa hadhara kwenye ziara ya Rais Samia mkoani Njombe, huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.


"Awamu ya 6 imemwaga mahela mengi ya maendeleo haijapata kutokea tangu nimekuwa seneta (Mbunge) wa Bunge hili Haki ya Mungu," alisema Sanga huku akitikisika mwili.


"Zimemwagika hela za maendeleo mpaka natizama nasema Mama (Rais Samia) Mungu akujaalie sana.",amesema.


Sanga pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Njombe na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mikoa ya Iringa na Njombe.


Amesisitiza kuwa uwekezaji huo wa serikali ya Rais Samia kwenye miradi ya maendeleo sekta za afya, elimu, maji, barabara, umeme na miundombinu mingine "haujapata kutokea" tangu nchi ipate uhuru.


"Miradi tuliyoipata, tumepata mabilioni na mabilioni na mabilioni," alisema.


Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, naye aliipongeza serikali ya Rais Samia kwa kuwekeza pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

Share:

MAMA MZAZI ALIPATA NAFUU BAADA YA KUKUTANA NA DAKTARI KIWANGA...“KIFAFA KILITOKOMEA”


Ama kwa hakika kila mtu hufurahia kuona wapendwa wao wakiishi kwa amani na wenye afya kila siku. Hali ilikuwa tofauti kwetu kwani mama mzazi alikuwa katika hali mbaya ya kifafa ambayo kila mara ilitukosesha usingizi kama wanawe. 


Kwa jina ni Kamau Kutoka Nyamira. Kifafa ama kwa hakika kilikuwa ni donda sugu katika familia yetu haswa kwa mama yetu mzazi. Mama alikuwa na miaka sitini na saba na hapo akaanza kuonyesha dalili za kuwa na kifafa. Kila mara alianguka na kuanza kufanya kama mtu aliyekuwa akizimia. Suala hili lilitupa mchanganyiko wa mawazo kama wanawe kwani ugonjwa ule haukumpa mama yetu fursa nzuri ya kuzeeka polepole.


Kila mara tulimpeleka hospiltalini kwani kila alipoanguka alikuwa akipoteza fahamu. Hali hii ilitufanya kupoteza hela nyingi kwa ajili ya shughuli za matibabu za mama yetu. Kila wiki angepelekwa hsopitalini ambapo tungetumia pesa nyingi ili apate nafuu. Ama kwa hakika alikuwa kipenzi chetu na hivyo hatungekata kumpeleka hospitalini ili aweze kupata nafuu. Ndugu zangu wengine nao walisema kwamba pengine ilikuwa ni uchawi ama mambo ya ushirikina yaliyomfanya mama kuwa na shida ile kwanza katika umri wake na wakati ule. Ilitupa kazi ngumu kwani hatukuwa tukimwacha nyumbani peke yake.

Alikuwa akipelekwa hadi msalani hii ilikuwan kazi ngumu iliyotokana na zimwi hili la ugonjwa wa kifafa. Tulijaribu kumtafutia tiba kutoka kwa madakatri wengine wenye tiba asilia lakini wote walikuwa kila mara wakikula pesa zetu kwani ugonjwa ule ulikuwa kila mara ukirudi kwa mama yetu swala ambalo lilikuwa likitutatanisha kama wana wake. 

Mama alianza kupoteza iamani na hata wakati mwingine akaanza kusema kwamba tumwache afariki kwani alikuwa ameishi muda wa kutosha kwenye dunia. Hatukutaka vile kwani upendo wetu kama wanawe kwake ulikuwa wa kweli na kwenye kiwango cha juu. Kila aliyesikia wito wa mama yetu hakufurahikia kabisa. Kila mtu alitaka aendelee kusishi kwani alikuwa mzuri wa kutoa wosia na kusaidia katika mambo mbalimbali ya kifamilia.

Hapo ndipo tulipatana na daktari Kiwanga ambaye rafiki wa familia alitushauri kwamba daktari huyu wa miti shamba alikuwa na uwezo tajika wa kusuluhisha shida kama zile kwa tiba yake tajika. Tulichukua nambari ya daktari Kiwanga na kuwasiliana naye kwani tulitaka afueni ya haraka kwa mama yetu mzazi tuliyemdhamini. Tulipeleka kwa daktari Kiwanga na hapo akashugulikiwa.

 Daktari Kiwanga alitupa imani kwamba hali ilikuwa shari kwani tiba ya mitishamba aliyokuwa amempea ilikuwa yenye mafanikio. Tulirejea nyumbani na kuwa na imani kwamba hali ya mama yetu ilikuwa shwari. Ama kwa hakika hakuna nlolote ambalo lilitokea tena kwa mama kwani daktari Kiwanga alikuwa kesha tupea suluhisho.

Hivyo ndivyo tulivyopata nafuu ya mama kutokana na ugonjwa wa kifafa. Daktari Kiwanga hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo. Husuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo. Ama kwa hakika daktri Kiwanga ni mtu wa kutegemewa katika jamii kwa ajili ya kusuluhisha mambo yanayowakosesha watu mbalimbali usingizi ama maisha bora yenye matamanio. Kwa mahojiano na daktari Kiwanga kwa ajili ya kusuluhisha shida zako, piga simu kwa nambari +254769404965/barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama tembelea wavuti wwww.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 12, 2022

















Share:

Thursday, 11 August 2022

TFF YAFUNGUKA UPOTOSHAJI UNAOENDELEA MIALIKO MKUTANO WA CAF JIJINI ARUSHA

Share:

MWANAMKE AJIUA KWA KITENGE CHUMBANI


Elizabeth Cheleo mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa mtaa wa Nsemulwa, Kata ya Nsemulwa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, amepoteza maisha kwa kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kipande cha kitenge alichokining'iniza juu ya kenchi.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad, na kusema kwamba baada ya uchunguzi jeshi hilo lilibaini kwamba marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.

Chanzo - EATV
Share:

DOWNLOAD/ INSTALL UPYA APP YA MALUNDE 1 BLOG..Tumeboresha zaidi

Share:

FULL POWER NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;


1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


Pia tunatibu Magonjwa mengine kama


Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767  utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

MAMA AKAMATWA TUHUMA ZA KUUA MCHEPUKO WA MME WAKE



Mtuhumiwa, Hajaratu Sini ambaye atafikishwa Mahakamani kwa mauaji.
 **
Maafisa wa Jeshi la Polisi Jimbo la Adamawa nchini Nigeria, wamemkamata mama mmoja, Hajaratu Sini (58), kwa tuhuma za kumuua kimada wa mumewe kwa fimbo kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi.

Polis imesema mshukiwa huyo ni mkazi wa eneo la Wumbirmi Tilli, uliopo jirani na serikali ya mtaa wa Michika, na anadaiwa kumuua mpenzi huyo wa mumewe aliyefahamika kwa jina la Kwada Drambi, Julai 31, 2022.

Inadaiwa kuwa mume wa mtuhumiwa Hajaratu na marehemu ambaye alikuwa ni mjane, walikuwa wakionana kwa siri ambapo Julai 31, Hajaratu aliwakamata wakiwa katika mazingira ya kutatanisha majira ya saa tisa usiku baada ya kuvamia nyumba ya mjane huyo.
Katika harakati za ugomvi, ndipo mtuhumiwa Sini alipofuatwa na mumewe na kuanza mapambano nje ya nyumba ambapo marehemu liingilia ugomvi huo na ndipo alipokamatwa na kumpiga na fimbo iliyomsababishia umauti baada ya kufikishwa hospitalini.

Kamishna wa Polisi Jimbo la Adamawa S.K. Akande, amesema mtuhumiwa anatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu kukamilia.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 11,2022















Share:

🛑 FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU KENYA 2022

Share:

Wednesday, 10 August 2022

RC CHALAMILA AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KWA MAENDELEO YA MKOA WA KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila amewataka watumishi kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kikao kikao cha Mkuu wa Mkoa na watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa tarehe 9 Agosti 2022, amewataka watumishi na viongozi wote kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha Mkoa unapata maendeleo kupitia umoja wao.

"Viongozi mnapotofautiana na mmoja wapo kumchongea maneno ya uzushi mwingine kwa mkubwa wao ujue yeye ndiye mwenye tatizo maana zipo ajenda nyingi za kuzungumza kama shule, afya, maji na barabara na si kumsema mwenzako. Kaeni kwa pamoja na zungumzeni kwa pamoja ili muwe na malengo ya pamoja" ,amesema Mh. Chalamila.

Ameongeza kuwa yote hayo ni kuepusha migogoro maana hakuna migogoro yenye visababishi viwili, siku zote migogoro mingi kisababishi ni kimoja lazima kuna mmoja ndiye sababu ya mgogoro.

"Na mimi Mkuu wa Mkoa sipendi kusikia hivyo napenda kusikia Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani na Mameya mko pamoja na kama kuna jambo linashindikana tunalirekebisha kwa njia za kitumishi zinazoeleweka", amesema Mh. Chalamila.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger