Mtuhumiwa, Hajaratu Sini ambaye atafikishwa Mahakamani kwa mauaji.
**
Maafisa wa Jeshi la Polisi Jimbo la Adamawa nchini Nigeria, wamemkamata mama mmoja, Hajaratu Sini (58), kwa tuhuma za kumuua kimada wa mumewe kwa fimbo kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi.
Polis imesema mshukiwa huyo ni mkazi wa eneo la Wumbirmi Tilli, uliopo jirani na serikali ya mtaa wa Michika, na anadaiwa kumuua mpenzi huyo wa mumewe aliyefahamika kwa jina la Kwada Drambi, Julai 31, 2022.
Inadaiwa kuwa mume wa mtuhumiwa Hajaratu na marehemu ambaye alikuwa ni mjane, walikuwa wakionana kwa siri ambapo Julai 31, Hajaratu aliwakamata wakiwa katika mazingira ya kutatanisha majira ya saa tisa usiku baada ya kuvamia nyumba ya mjane huyo.
Katika harakati za ugomvi, ndipo mtuhumiwa Sini alipofuatwa na mumewe na kuanza mapambano nje ya nyumba ambapo marehemu liingilia ugomvi huo na ndipo alipokamatwa na kumpiga na fimbo iliyomsababishia umauti baada ya kufikishwa hospitalini.
Kamishna wa Polisi Jimbo la Adamawa S.K. Akande, amesema mtuhumiwa anatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu kukamilia.
0 comments:
Post a Comment