Thursday, 28 July 2022

KAMPUNI YA APS YAGAWA TAULO ZA KIKE 'KIPEPEO PAD' SHULE YA WASICHANA JANGWANI

Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company) inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike maarufu kwa jina Kipepeo Pad imetoa na kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam.

Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika shuleni hapo Julai 27,2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani ambaye ametumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao wa kike kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao huku akiishuru Kampuni ya APS kwa kutoa msaada huo wa taulo za kike.


Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu Mkurugenzi wa kampuni ya Kipepeo Pad Janeth Dutu aliyeambatana na mwakilishi wa Taasisi ya Girls Chapter amesema uhitaji wa taulo za kike kwa mabinti bado ni mkubwa katika shule mbalimbali huku akiwasihi kuzingatia matumizi sahihi ya taulo za kike na kujitunza ili watimize ndoto zao
Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani akizungumza wakati Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company) inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike maarufu kwa jina Kipepeo Pad ikitoa na kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Kampuni ya  APS , Janeth Dutu akizungumza na wanafunzi wa shule Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Kampuni ya  APS , Janeth Dutu akizungumza na wanafunzi wa shule Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam


Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company) inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike maarufu kwa jina Kipepeo Pad, Janeth Dutu akifurahia jambo baada ya kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Share:

Wednesday, 27 July 2022

CWT BAGAMOYO YAENDELEA KUTOA MISAADA KWENYE SHULE MBALIMBALI



Na Elisante Kindulu - Chalinze
CHAMA Cha walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya BAGAMOYO kimeendelea kutoa misaada mbalimbali mashuleni ikiwa ni pamoja na kusaidia vifaa vya ujenzi.

Hatua ya kusaidia vifaa vya ujenzi imekuja baada ya shule ya Sekondari ya Dunda kuezuliwa na upepo kwa choo cha wanafunzi wa kike na hivyo kufanya vijana hao kupata changamoto kupata huduma hiyo muhimu.

Vifaa hivyo vilikadhidhiwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Bagamoyo, Mwl. Hamisi Kimeza pamoja na Katibu wake Mwl. Shaaban Tessua katika viwanja vya shule hiyo hivi karibuni.

Katibu Tessua alisema kwamba vifaa hivyo  vya upauaji ni hatua ya mwanzo tu ya msaada wao huku vifaa vingine vikiwemo mifuko ya saruji kupitia CWT mkoa wa Pwani kitengo cha walimu wanawake nayo itafuata.

Katika hatua nyingine CWT Wilaya ya Bagamoyo imeendelea kutoa majiko ya gesi kwa ajili ya walimu mashuleni ikiwa ni sehemu ya Mchango wake ili walimu waweze kupata huduma ya pamoja ya  chakula wawapo mahala pa kazi.

Akikabidhi majiko hayo akiwa na baadhi ya wajumbe wa CWT wa  kamati ya utendaji ya Wilaya, Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Bagamoyo Mwl. Hamisi Kimeza alisema, lengo la kutoa majiko hayo ni kuongeza mshikamano na upendo kwa walimu wawapo mahala pa kazi, kwani chakula ni eneo mojawapo la kuwakutanisha wote kwa wakati mmoja.

Lakini Mwenyekiti huyo aliwaeleza walimu kuwa chama Wilaya hakitakuwa na fedha za kujaza gesi baada ya ile ya awali kumalizika , badala yake akawashauri watafute namna ya kupata fedha hata kuchangia fedha zinazorejeshwa mashuleni kwa ajili ya posho ya vikao vya kichama mahala pa kazi.

Naye Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Bagamoyo, alisema kuwa wamefanya zoezi Hilo katika awamu mbili kwa baadhi ya shule ,lakini lengo Ni kuzifikia shule zote za halmashauri ya Chalinze pamoja na Bagamoyo zilizopo wilayani Bagamoyo.
Mwenyekiti wa CWT ,Wilaya ya Bagamoyo Hamisi Kimeza(kushoto) na Katibu wa Chama hicho wa Wilaya, Shaaban Tessua(kulia) wakikadhi mbao kwa walimu wa shule ya Sekondari Dunda ili kusaidia matengenezo ya choo kilizoezuliwa na upepo shuleni hapo.

Share:

RADI YAUA WATU 22



NCHINI India imeripotiwa vifo vya watu 20 waliouawa na radi ikiwa ni ndani ya masaa 24 katika miji nane iliyo Mashariki mwa Jimbo la Bihar nchini humo.

Radi hizo ziliambatana na mwanga mkali ambapo Mkuu wa Jimbo la Bihar Nitish Kumar amewataka wananchi kufuatilia kwa ukaribu ushauri wa Mamlaka inayohusika na majanga nchini humo.


Mamia ya watu hufariki kila mwaka kutokana na radi ambazo mara nyingi hutokea kipindi cha mvua za Monsoon.

Sababu kubwa iliyotolewa ambayo inasababisha idadi kubwa ya vifo kwa raia wa India karibu kila mwaka kutokana na radi ni ule utamaduni wa watu wengi wa India kufanya kazi nje tofauti na mataifa mengine.

India imerekodi idadi ya radi milioni 18 kwa kipindi cha kuanzia Aprili 2020 hadi Machi 2021

Aidha siku ya jumanne Kumar alitangaza kiasi cha Rupee 40,000 ambayo ni sawa na Dola 5,008 kwa kila familia iliyofiwa.


Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba India imeripoti jumla ya radi milioni 18 katika kipindi cha Aprili 2020 hadi Machi 2021 na hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Climate Resilient Observing System Promotion Council ambalo pia limebainisha kuwa rekodi hizo ni ongezeko la 34% ukilinganisha na rekodi zilizopita katika kipindi kama hicho.
Share:

TANZANIA YANG’ARA UCHAGUZI MKUU WA UMOJA WA WATOA HUDUMA ZA POSTA KUSINI MWA AFRIKA (SAPOA)

Ujumbe wa Tanzania kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa SAPOA Bwana Janras Serame Kotsi (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mhandisi Kulwa Fifi, Kaimu Meneja wa Biashara mtandao, Bwana Constantine Kasese, Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara, Janras Kotsi (SAPOA) na Elia Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa.
Bwana Constantine Kasese,Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara za Shirika, aliyemwakilisha Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania akimpongeza Bwana Elia Madulesi mara baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Utawala ya SAPOA na baadae Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo jijini Cape Town,Afrika ya Kusini wakati wa vika vya SAPOA vinavyoendelea.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia za Kidijitali wa Afrika ya Kusini Mheshimiwa Phillemon Mapulane (Mb) katika aliyekaa,akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Utawala ya SAPOA. Waliokaa kulia kwake ni Bwana Festus Hangula, Mwnyekiti wa Bodi na kushoto kwake ni Bwana Elia Madulesi, Makamu Mwenyekiti.Waliosimama kutoka kushoto ni Cornelius Ramatlhakwane, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Botswana (Mjumbe), Bibi Nomkhita Mona, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Afrika Kusini(Mjumbe) na Bwana Janras Kotsi Mtendaji Mkuu wa SAPOA

****
Cape Town, South Africa


Tanzania kupitia Shirika la Posta nchini imechaguliwa kuingia kwenye bodi ya Utawala ya Umoja wa Watoa Huduma za Posta Kusini mwa Afrika (SAPOA) kwenye uchaguzi wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 20 unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Durbanville, ulioanza tarehe 25-28 Julai, 2022, jijini Cape Town, Afrika ya Kusini. 

Katika mkutano huo Bw. Elia P.K.Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania amepata nafasi hiyo ya kuiwakilisha Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Utawala ya Umoja huo, nchini Afrika Kusini.

Uchaguzi huo uliofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Mwaka wa SAPOA, uliohusisha nchi zilizo katika Umoja huo ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Vilevile, katika Bodi hiyo Bw. Madulesi, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwenye Bodi hiyo, huku nafasi ya Mwenyekiti Ikienda kwa Ndugu Festus Hangula, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Namibia. 

Wengine waliochaguliwa kuingia kwenye Bodi hiyo ni Cornelius Ramatlhakwane, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Botswana, Bibi Nomkhita Mona, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Afrika Kusini na Bibi Elizabeth Mamosehlela Letsoela, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Lesotho.

Shirika la Posta Tanzania linahudhuria Mkutano Mkuu wa 20 wa Mwaka wa SAPOA na jukwaa la Posta la SAPOA likifanyika sambamba na Mkutano huo. 

Shirika la Posta limewakilishwa na Bw. Constantine Kasese, Kaimu Meneja Mkuu, Uendeshaji wa Biashara ambaye alimuwakilisha Bwana Macrice Mbodo Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kwenye Mkutano huo, Bw. Kulwa Fifi, Kaimu Meneja wa Biashara Mtandao na Bw. Elia P.K. Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
27 Julai, 2022

Share:

Tuesday, 26 July 2022

BASI LA SHULE LAUA WATU 10 WAKIWEMO WANAFUNZI 8 ..RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE

Ajali ya basi
Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kufuatia basi la wanafunzi wa Shule ya King David Mtwara lenye namba za usajili T 207 CTS lililopata ajali asubuhi ya leo Jumanne, Julai 26, 2022 eneo la Mikindani Mtwara likiwa na wanafunzi na kuua watu 10 wakiwemo wanafunzi nane wa shule hiyo.


Kamanda wa Polisi Mtwara Nicodemus Katembo amesema Wanafunzi waliofariki dunia ni wanane, Dereva mmoja na Mwangalizi mmoja, majeruhi ni 19.


Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Samia ameandika: “Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbukia shimoni. Nawapa pole wafiwa, mkuu wa mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu na kuwaponya majeruhi.


Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitakujia hivi punde.
Share:

MVUA YAUA WATU 310



Takribani watu 310 wamefariki dunia na wengine 300 wamenusurika kifo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko nchini Pakistan.

Mamlaka ya Taifa ya Kusimamia Majanga (NDMA) imetangaza taarifa hiyo na kueleza kwamba wanawake na watoto 175 ni miongoni mwa wahanga wa janga hilo.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa watu 64 wamefariki dunia Mashariki mwa Mkoa wa Punjab, 62 wamefariki Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Khyber Pakhtunkwa na zaidi ya watu 70 wapoteza maisha Kusini mwa Mkoa wa Sindh.


Aidha, mamlaka hiyo imeongeza kuwa nyumba 8,979 na takribani madaraja 50 yameharibiwa kwa kusombwa na maji ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.


Taarifa inaeleza kuwa Jeshi la wanamaji la Pakistan linaendelea na operesheni za kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko sambamba na kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hatarishi zaidi.


Mamlaka ya hali ya hewa ya Pakistan imetabiri kuwa mvua kali zilizoanza kunyesha Juni 14, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya nchi zitaendelea kunyesha kwa muda wa siku kadhaa nchini humo.


Mnamo 2021 mamia ya watu walifariki dunia na kujeruhiwa ambapo nyumba nyingi zilibomoka kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kali za msimu zilizonyesha katika maeneo mbalimbali ya Pakistan.
Share:

HATIMAYE MWILI WA MAREHEMU ULIOHIFADHIWA MOCHWARI MIAKA 6 WAZIKWA



Familia moja mjini Kisii nchini Kenya sasa inaweza kupumua baada ya kumzika jamaa yao ambaye amekuwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa zaidi ya miaka sita iliyopita.

Tangu 2017, familia ya Mzee Joseph Abuga Oribo imekuwa katika majonzi tokea mwanao alipofariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Lakini mipango ya maziko ilisitishwa kufuatia zuio la mahakama kuhusu mzozo wa ardhi ya ekari tatu ambayo haukuwa umetatuliwa.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya mjukuu wa marehemu pia kuugua katika hospitali ya Keroka na hatimaye kuaga dunia.

Mwili wa mjukuu huyo pia ulizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu huku kukiwa na mkwamo katika shughuli za mazishi na ilibidi Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi kuingilia kati ili mwili huo kuachiliwa na kufanyiwa mazishi.

Mjane Dinah Moraa alieleza furaha yake kuona mume wake mwenye umri wa miaka 85 pamoja na mjukuu huyo wakizikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Iranya Nyamache.

Chanzo - EATV
Share:

AZIKWA AKIWA HAI AKICHIMBA CHOO



Mwanaume mwenye umri wa miaka 30, amezikwa akiwa hai Jumatatu, Julai 25, akichimba choo katika Shule ya Sekondari ya Jean Marie, Kaunti ya Nandi nchini Kenya.

Josphat, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaume watatu waliopewa kandarasi ya kuchimba choo katika shule hiyo, alikwama baada ya kuta za choo hicho kuporomoka akiwa ndani mwendo wa saa nane kamili mchana.

Nicholas Odungo, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi hicho cha uchimbaji alisema kisa hicho kilitokea wakati watatu hao walikuwa wakimalizia kazi yao.

Choo kilikuwa cha futi 30. Odungo na wenzake walikuwa wamekwenda kupata chamchana wakati tukio hilo lilitokea.

"Tulikuwa tumeenda kula chakula cha mchana na tukamwambia aendelee kuchimba. Tulirudi muda mfupi baadaye ili kumsaidia kuondoa udongo na tukiwa katika harakati za kufunga kamba kuta zikazama," Odungo alisema kama alivyonukuliwa na K24.

Josephat, baba wa watoto watatu bado amekwama kwenye vifusi huku juhudi za uokoaji zikiendelea. Wakaazi wenye mfadhaiko sasa wanatoa wito kwa serikali ya kaunti na ya kitaifa kusaidia katika juhudi za uokoaji.

“Inasikitisha sana kwamba tulikuwa tunamalizia kazi yetu kabla hatujalipwa lakini kilichotokea kimetuathiri sana, tunaomba kikosi cha uokoaji na wasimamizi wa maafa waje kumuokoa Josphat ambaye amenaswa tangu saa 2:00 usiku," mkazi mmoja alisema.

Chanzo - Tuko news
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 26,2022

















Share:

Monday, 25 July 2022

MAKAMBA ATAKA WAKANDARASI WAZAWA KUONESHA WELEDI

 

Waziri wa Nishati January Makamba akitoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotekelezwa mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) kuja Chongoleani Tanga jana katika kijiji cha Sojo, kata ya Ugusule, wilayani Nzega Mkoani Tabora ambapo kinajengwa kiwanda cha kuandaa mabomba ya kusafirisha mafuta hayo kwenda jijini Tanga

Na Mwandishi wetu, Tabora

WAKANDARASI wazawa waliopewa kazi katika mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja Chongoleani (Tanga) wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili serikali iendelee kuwaamini na kuwapa kazi nyingine.

Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Nishati January Makamba alipofanya ziara maalumu kutembelea eneo kinapojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta ghafi ya mradi huo.

Alisema kiwanda hicho kinachojengwa katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilayani Nzega Mkoani hapa kinatakiwa kukamilika haraka kwa ubora na weledi unaotakiwa ili kazi ianze kutokana na umuhimu wake kwa uchumi wa taifa.

Alibainisha kuwa makampuni ya ndani yanaposhiriki katika miradi mikubwa kama hiyo wanapata uzoefu na nchi inapata manufaa lakini wanapofanya vibaya au kuchelewesha kazi wanakwamisha juhudi za serikali na kutokuaminika.

 ‘Miradi huu una manufaa makubwa kwa serikali, hivyo wakandarasi wa ndani wanaposhirikishwa wanapaswa kufanya kazi kwa weledi na viwango ili iwe rahisi kupata kazi nyingine zinazotekelezwa hapa nchini’, alisema.

Waziri Makamba aliongeza kuwa matarajio ya serikali ni mradi huo kuanza kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu hivyo akaagiza kila mkandarasi aliyepewa kazi katika mradi huo kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Alizitaka kampuni zote kushirikiana ili kuharakisha utekelezaji wake, alitaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni Milembe Construction Company Ltd (ya wazawa), ECOP (East African Crude Oil Pipe line) na ISOAF ambao wamepewa kazi ya kutengeneza kiwanda hicho.

Mbunge wa Jimbo la Bukene Seleman Zedi ambapo mradi huo upo, aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika kijiji hicho na kuwapelekea umeme wa uhakika katika eneo hilo, sasa wananchi wameanza kunufaika kwa kupata ajira.

Aliongeza kuwa serikali pia imewapatia kiasi cha sh mil 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo ili kuboresha huduma za afya kutokana na muingiliano wa watu wengi aidha alisema halmashauri pia inatarajia kupata tozo ya huduma kiasi cha sh bil 1.8 kutokana na mradi huo.

Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian alisisitiza kuwa dhamira yao ni kuona mradi huo ukiwanufaisha wakazi wa Mkoa huo katika nyanja zote ikiwemo ajira, kupata fursa ya kutoa huduma za chakula, ulinzi na mengineyo.


Share:

SAMIA APONGEZWA KWA MAAMUZI YA KULETA MAGEUZI VYOMBO VYA DOLA


*Samia aagiza mageuzi kwenye majeshi ya ulinzi na usalama

* Mchujo mkubwa waja, wenye vyeti feki wasio na sifa kumulikwa

* Mifumo ya nidhamu, ajira, maadili kufumuliwa

* Mahusiano ya majeshi ya ulinzi na usalama na raia kuchunguzwa

* Jeshi la Polisi laanza kusukwa upya 

* Mageuzi makubwa ya haki jinai kufanyika nchini

* Wengi wafurahia maamuzi ya Rais Samia kufungua vyombo vya dola

Mwandishi Wetu

AMRI Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan, amepongezwa ndani na nje ya nchi kwa uamuzi wake wa kuagiza mageuzi makubwa kwenye majeshi ya ulinzi na usalama nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuimarisha haki jinai nchini.

Katika mageuzi hayo makubwa yatakayoanza kwenye Jeshi la Polisi Tanzania, muundo wa majeshi hayo itapitiwa upya, ikiwemo mfumo wa ajira, mafunzo, maadili na upandishaji vyeo.

Mahusiano ya vyombo vya dola na wananchi yataangaliwa upya, ikiwemo utoaji wa haki kwa wananchi.

Rais Samia, ambaye wiki ijayo amefanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa zaidi kwenye jeshi hilo baada ya kupokea mapendekezo ya kamati aliyounda kupitia upya mundo wa vyombo vya dola nchini.

"Tutaanza na Polisi, wakimaliza wakileta ripoti tutafanya marekebisho halafu tunakwenda majeshi mengine," alisema Rais Samia wakati wa uapisho wa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Camillus Wambura.

"Serikali sasa tunakuja na jicho jingine ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania."

Rais ameunda kamati ya watu 12 na Sekreterieti ya watu 5 kufanya kazi hiyo ya kupitia mifumo na utendaji wa vyombo vya dola, itakayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohammed Chande (Mwenyekiti) na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue (Makamu Mwenyekiti).

"Nimeunda kamati kushauri njia bora ya kuleta mabadiliko ya Utendaji kazi wenye matokeo bora kwenye vyombo vya haki ya jinai," alisisitiza.

Pamoja na mambo mengine, Rais Samia ameagiza ufanyike mchujo kwenye vyombo vya dola ili kubaini wenye vyeti feki na waliopewa nafasi kwenye majeshi pasipokuwa na uwezo stahiki.

"Vitendo vinafypfanyoka barabarani na polisi hudhani kuwa kweli wamehitimu masomo," alisema Rais Samia.

Taasisi nyingine za haki ya jinai ambazo zitamulikwa kwenye mageuzi ya Rais Samia baada ya jeshi la polisi ni pamoja na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Nyingine ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Jeshi la Magereza na majeshi mengine ya ulinzi na usalama.


Pongezi zamiminika ndani, nje ya nchi

Uamuzi ya Amri Jeshi Mkuu Rais Samia ya kuvifumua vyombo vya ulinzi na usalama nchini umepongezwa na wadau mbalimbali nje na ndani ya nchi 

Balozi wa zamani wa Norway nchini Tanzania, Bi Hanne-Maria Kaarstad, amesema uamuzi wa Rais Samia kufanya mageuzi kwenye vyombo vya dola nchini ni jambo la muhimu sana.

Pia amepongeza uteuzi wa Jaji Chande na Balozi Sefue kuongoza kamati hiyo ya kupendekeza mageuzi hayo, akisema kuwa watumishi hao wa umma waandamizi wastaafu wana weledi mkubwa.

Semkae Kilonzo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Policy Forum, amesema uamuzi huo ni hatua nzuri.

"Hawa watu wawili (Jaji Chande na Balozi Sefue) ni wabobezi kwenye maeneo yao. Uadilifu wao unawazidi wengi waliopitia nafasi hizo," Kilonzo alisema.

"Kama wateule werevu wa Rais waliopo sasa wamesoma alama za nyakati, Rais ana malengo ya kuleta mageuzi mapana."

Naye Amne Suedi, mwanasheria binafsi, amesema kuwa ana matarajio kuwa timu iliyoundwa na Rais Samia Italeta mageuzi ya haki jinai nchini.

Mwanasheria mwingine, Deogratias Melkior Njau, amesema kuwa tangu Rais Samia aingie kwenye madaraka amechukua hatua kadhaa zinazoonesha nia ya dhati ya kujenga upya misingi ya utawala bora Tanzania.

Getrude Mollel, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano, amesema kuwa Rais Samia anaipeleka nchi njia sahihi kwa kutoa kipaumbele kwa masuala ya haki jinai.

"Jeshi la Polisi limekumbwa na tuhuma nyingi za rushwa na matumizi ya madaraka kinyume na sheria, mambo ambayo yamechafua taswira ya jeshi hilo," alisema.


Share:

BENKI YA EXIM YAWEKA KAMBI LINDI,MTWARA,YATOA MSAADA WA MADAWATI,YAJIZATITI KUKUZA BIASHARA NA KILIMO


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti (kushoto walioketi) sambamba na viongozi waandamizi wa benki ya Exim akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (katikati) Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (Kulia walioketi) na Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda(Kulia) wakiwa wameketi katika moja ya madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Mtwara yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini. Wengine ni maofisa wa mkoa huo, wafanyakazi wa benki hiyo na wanafunzi.


Mbunge wa jimbo la Mchinga, mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete (kushoto) akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (kulia) kwa ajili ya kusaidia kuondoa adha ya upungufu wa mawadati katika shule mbalimbali za jimboni kwake ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa ugawaji wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbalimbali hapa nchini kupitia mpango wake wa kusaidia jamii ujulikanao kama Exim Cares. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (wa tatu kulia)na maofisa wengine kutoka serikalini na benki hiyo.


Mbunge wa jimbo la Mchinga, mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa viongozi waandamizi wa benki ya Exim akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (katikati walioketi), Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (wa pili kulia walioketi) wakati wakati wa makabidhiano ya madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya jimbo la Mchinga yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.


Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi watakaonufaika na msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya jimbo la Mchinga yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na wateja wa benki ya Exim mkoa wa mkoa huo wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikuwa wakiwemo viongozi waandamizi wa mkoa huo pamoja na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (katikati) wakati wa hafla hiyo.


Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki ya Exim kutoka mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye hafla hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikuwa wakiwemo viongozi waandamizi wa mkoa huo pamoja na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (kulia) wakati wa hafla hiyo.


Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (kushoto walioketi) Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo (wa pili kushoto walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani Mtwara wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

.................................

Lindi na Mtwara: Julai 25, 2022: Benki ya Exim Tanzania imeelezea adhma yake ya kukuza na kuchochea ukuaji wa kiuchumi katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kukuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kukuza sekta ya kilimo, biashara na elimu katika mikoa hiyo

Katika kuthibitisha adhma yake hiyo, viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwemo Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo pamoja na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Stanley Kafu mwishoni mwa wiki walitoa msaada wa madawati 200 katika mikoa hiyo sambamba na kuandaa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya wateja wa benki hiyo Mkoani Mtwara.

Hatua hiyo ilitoa fursa kwa benki hiyo kuelezea huduma zake mpya, fursa za biashara pamoja na mkakati wake katika kukuza sekta za elimu pamoja na kilimo husasani kupitia zao la korosho.

Akizungumza kuhusu matukio hayo, Lyimo alisema yameweza kutoa fursa kwao kukutana na wateja wao, viongozi waandamizi wa serikali na wadau wengine muhimu mkoani humo hivyo kutoa wasaa kwao wa kutambulisha huduma mpya sambamba na kupokea mrejesho kuhusu mahitaji ya wateja wao hususani kipindi hiki ambacho mikoa hiyo ipo kwenye mkakati wa kuboresha zaidi sekta ya kilimo na bandari ya Mtwara.

“Mikoa ya Mtwara na Lindi ni miongoni mwa mikoa muhimu sana kwetu kibiashara na hiyo ndio sababu mikoa hii ilikuwa ni miongoni mwa mikoa ya awali kabisa kufungua matawi yetu. Katika kipindi chote cha uwepo wetu katika mikoa hii tumekuwa na mchango mkubwa kwa wakazi wa mikoa hii kwa kutoa huduma zinazowalenga haswa ikiwemo mikopo ya kilimo, biashara, mikopo ya watumishi na sasa tumekuja na huduma mahususi kwa ajili ya wajasirimali,’’ alisema.

Zaidi alisema hali ya uchumi katika mikoa hiyo kupitia uboreshwaji wa bandari ya Mtwara inazidi kutoa fursa kubwa kwa benki hiyo kuhudumia wateja wengi zaidi wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wa kati kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanatumia bandari hiyo.

“Uwepo wa benki ya Exim katika visiwa vya Comoro unatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande hizi mbili kufanya biashara kwa urahisi zaidi kwa kuwa Exim tunawahakikishia huduma za uhakika za kifedha ikiwemo mikopo,’’ alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Stanley Kafu alisema mchango wa benki hiyo katika mikoa hiyo haujaishia katika utoaji wa huduma za kifedha tu bali pia imekuwa mdau muhimu wa maendeleo ya kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii ujulikanao kama Exim Cares

“Serikali kupitia viongozi mbalimbali wanafanya jitihada kubwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na kilimo hivyo ni jukumu letu sisi kama taasisi za kifedha kuunga mkono jitihada hizo za serikali. Kupitia mkakati huu uliozinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwishoni mwa mwaka jana tumeweza kutoa msaada wa madawati katika mikoa mbalimbali hadi sasa ikiwemo mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Lindi na Mtwara na bado tunaendelea mikoa mingine zaidi.’’ alisema Bw Kafu.

Akizungumzia hatua hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliipongeza benki ya Exim kwa msaada wa madawati katika mkoa wake huku akibainisha kuwa msaada huo utasaidia katika kukabiliana na upungufu wa madawati katika baadhi ya shule zilizopo mkoani humo.

“Msaada huu umekuwa na tija kubwa kwenye mkoa wetu kwa kuwa tuna uhitaji wa madawati kutokana na muitikio mkubwa wa agizo la Mheshimiwa Rais la ujenzi wa madarasa. Tuna miradi mingi ya ujenzi wa madarasa ambayo inakwenda sambamba na hitaji la madawati hivyo tunawapongeza sana wenzetu wa Exim kwa kutuunga mkono kwenye hili,’’ alisema.

Kuhusu ukuaji wa biashara, Brigedia Jenerali Gaguti alisema uboreshwaji wa bandari ya Mtwara unaoshuhudiwa hivi sasa imekuwa ni kivutio kikubwa cha wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo visiwa vya Comoros, hivyo wananchi wa mkoa huo wanahitaji huduma bora za kifedha ili waweze kushiriki kikamilifu kutumia fursa za kibiashara zitokanazo na uwepo wa bandari hiyo.

“Ndio maana nimeguswa sana kusikia kwamba benki ya Exim tayari imeshaanza kujitanua zaidi nje ya mipaka ya nchi. Tafsiri yake ni kwamba wafanyabiashara wetu na wale wanaotoka nje ya nchi ikiwemo visiwa vya Comoros tayari wanaunganishwa na huduma za benki ya Exim…hongereni sana.Ni matumaini yangu kwamba wafanyabiashara mkoani Mtwara watachangamkia zaidi huduma za Exim ili waweze kunufaika na huduma za benki hii wanapofanya biashara kimataifa,’’ alisema.

Akizungumzia msaada wa madawati 100 aliyoyapata kwenye jimbo lake, Mbunge wa jimbo la Mchinga, mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha madawati hayo yanakabidhiwa katika Shule zenye uhaba na kutunzwa vyema kwa lengo la kuleta tija iliyokusudiwa hususani kukabiliana na uhaba uliopo unaotokana na mwitikio wa wazazi kupeleka watoto shule kufuatia sera ya elimu bila malipo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger