Thursday, 23 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 23,2022

Magazetini leo Alhamis June 23 2022











Share:

Wednesday, 22 June 2022

MREMBO MWENYE UMBO MATATA 'KIUNO CHA NYIGU' AZUNGUMZIA UREMBO WAKE


Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), Poshy Queen.


Poshy Queen; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye amekuwa akizungumziwa mno juu ya kutengeneza shepu matata aliyonayo, lakini mwenye anasema hajawahi kufanya jambo kama hiyo.

Poshy Queenn anasema kuwa umbo lake matata (kiuno cha nyigu) linatokana na asili ya familia yake kwani hata mama yake ana shepu kuliko hata yeye.


Kwa baadhi ya watu wanaojua familia ya Poshy Queen ambao ni wenyeji wa jijini Mbeya wanasema ni kweli ni asili yao kwani ndugu zake nao wamejaaliwa shepu kama ilivyo kwa wanawake walio wengi kutoka jijini Mbeya.

STOLI: SIFAE LPAUL
Share:

MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022...FAHAMU KUHUSU SENSA

 




Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Utangulizi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti 2022. Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo. Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012. Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

 

Maana ya Sensa ya Watu na Makazi

Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

 

Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-

  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

 

Madodoso ya Sensa

Sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa zilizopita itatumia aina mbili kuu za madodoso. Dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na Dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.

Madodoso Mengine ni:-

  • Dodoso la Taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waliolala mahotelini/nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini; na

  • Dodoso la Wasio na Makazi maalum ambalo ni mahsusi kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo mbalimbali, kwenye madaraja na maeneo mengine.

 

Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022

Utekelezaji wa sensa ya watu na makazi hufanyika katika awamu kuu tatu kuu ambazo ni Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu, Wakati wa Kuhesabu Watu na Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu.

Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu

Kipindi kabla ya kuhesabu watu kinajumuisha Uandaaji wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa na nyaraka nyingine, Utengaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu na Uzalishaji wa Ramani, Uandaaji wa Nyenzo (Madodoso na Miongozo mbalimbali); Uhamasishaji, Sensa ya Majaribio ifikapo tarehe 29 Agosti 2021 ikiwa ni mwaka mmoja kamili kabla ya Sensa yenyewe; Kuunda kamati za sensa; kufanya mikutano na wadau wa takwimu; kufanya manunuzi, kufanya uchaguzi wa aina ya teknolojia itakayotumika, kuajiri wadadisi na wasimamizi, usambazaji wa vifaa; na kufanya maandalizi ya Tathmini ya Sensa.

 

Kipindi cha Kuhesabu Watu

Kipindi cha kuhesabu watu kinajumuisha kazi kuu na ya muhimu katika zoezi hili ya kuhesabu watu.

 

Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu

Kipindi baada ya kuhesabu watu kinajumuisha Uchakataji wa Taarifa za Sensa, Uchambuzi, Utoaji wa Matokeo ya Awali, Usambazaji wa matokeo ya mwisho, uhamasishaji wa matumizi ya takwimu kwa watumishi wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.

 

Maandalizi ya sensa ya watu na makazi 2022 yalianza 2018, ikiwa ni kutenga maeneo ya kuhesabia watu, kutayarisha nyaraka muhimu za sensa kama vile madodoso, miongozo, fomu za kudhibiti ubora na kufanya sensa ya majaribio.

 

Kwa sasa maandalizi ya sensa yamefikia katika hatua zifuatazo;

  1. Kuandaa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022;

  2. Kutenga Maeneo katika wilaya 5 za mkoa wa Dodoma ambazo ni Bahi, Chamwino, Kondoa, na Chemba; na Wilaya moja ya Mkoa wa Singida (Singida Mjini);

  3. Kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu inaendelea katika mkoa wa Singida katika wilaya za Manyoni, Ikungi; na mkoani Dodoma katika wilaya za Mpwapwa na Kongwa.

  4. Kufanyika kwa ziara moja ya kimafunzo nchini Kenya kwa ufadhili wa UNFPA ambao wamefanya sensa ya kidigitali hivi karibuni na kujifunza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya sensa kwa mafanikio. Matumizi ya teknolojia hii itasaidia kupunguza gharama za kufanya sensa na kupunguza muda wa kutoa matokeo ya sensa.

  5. Kuandaa rasimu ya Dodoso la Sensa na nyaraka nyingine muhimu kama vile miongozo ya kufundishia, miongozo ya makarani wa sensa, miongozo ya wasimamizi wa sensa na miongozo ya waratibu wa sensa mkoa na wilaya.

 

Maswali Yatakayoulizwa katika Sensa ya mwaka 2022

Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ina moduli kumi na nne ambazo zitatumika kukusanya taarifa za watu na makazi yao nchi nzima.

 

Maswali yatakayoulizwa yatahusu:-

  1. Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, n.k.);

  2. Maswali yanayohusu ulemavu;

  3. Taarifa za Elimu;

  4. Maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi

  5. Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva)

  6. Shughuli za kiuchumi

  7. Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA

  8. Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya

  9. Vifo vitokanavyo na uzazi

  10. Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali

  11. Maswali ya kilimo na mifugo

  12. Mifuko ya hifadhi ya jamii.

 

Tofauti ya Sensa ya Mwaka 2022 na Sensa zilizopita:-

Katika sensa ya mwaka 2022 inatarajiwa kuwa na vitu vipya kama vile;

  • Kutenga maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za kitongoji/mtaa na upatikanaji wa taarifa za kitakwimu katika ngazi za kitongoji/mtaa pamoja na kuwa na mipaka ya kudumu katika ngazi hizo;

  • Matumizi ya Vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji wa sensa kwa lengo la kupunguza gharama;

  • Nyongeza ya maswali yatakayowezesha upatikanaji wa taarifa zaidi za kitakwimu ikilinganishwa na Sensa ya Mwaka 2012:-

  1. Taarifa za kidemografia (umri wakati wa ndoa ya kwanza);

  2. Maswali yanayohusu ulemavu (Kichwa kikubwa, Mgongo wazi, Kifafa/Epilepsy, Mbalanga/storiasis na Usonji/autism);

  3. Maswali ya uhamaji kulingana na mapendekezo ya IOM (International Organization of Migration);

  4. Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho NIDA, vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo, Mzanzibari mkazi, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva);

  5. Maboresho ya maswali ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na idadi ya kaya ziliko kwenye sekta isiyo rasmi;

  6. Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA

  • Takwimu za nyumba (orodha, hali ya umiliki na aina ya nyumba)

  • Maswali ya kilimo na mifugo

 

Hitimisho

Matarajio ya Ofisi ni kujipanga vizuri kwa kutumia rasilimali chache zilizopo ili kukamilisha kwa wakati shughuli zote za maandalizi ikiwamo:-

  1. Kazi ya utengaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu katika ngazi ya kitongoji na mtaa ambayo ndiyo msingi wa kufanikisha sensa kwa ubora

  2. Uandaaji wa nyaraka za sensa;

  3. Uundaji wa vikosi kazi/units kwa lengo la kugawana majukumu; na

  4. Ufanyaji wa Sensa ya majaribio tarehe 29 Agosti 2021

Share:

OJADACT YALAANI MAUAJI YA WATOTI GEITA

 


TAMKO  LA  KULAANI MAUAJI YA WATOTO MKOANI GEITA, JUNI   22 2022


OJADACT  inalaani  matukio  ya  mauaji  yanayoendelea  Nchini  husasani  matukio  mawili  ya  mauaji  ya  watoto  yaliyotokea  Mkoani  Geita,  tukio la kwanza  lilihusisha  kifo  cha  aliyekuwa  Mwanafunzi wa Darasa  la saba  Johson  Thomas (14) katika  shule  ya Msingi Buhalahala , Halmashauri  ya Mji  Geita, Mkoa wa Geita, aliyekutwa  amefariki na mwili wake ukiwa pembeni  mwa Mto baada  ya kupotea Juni 2, 2022.


Tukio la pili ni  tukio la  kuuawa kwa mtoto  Dorcas Mathias  mwenye  umri  wa  Miaka (7)  aliyekuwa  Mwanafunzi wa Chekechea Shule ya Msingi Ibambi Wilaya ya Nyahg’wale Mkoani Geita  baada ya  kuvamiwa na watu  watatu  wakati akiwa  aanachunga  mbuzi na  mwenzake.


Kamanda  wa Polisi  Mkoani Geita Henry Mwaibambe alisema  baada  ya  mwili huo kufanyiwa  uchunguzi na Daktari alibainika  kuwa,Dorcas alibakwa, kulawitiwa na kisha  kuuawa na  baadaye akavunjwa  shingo. Jeshi  la Polisi  limewafikisha  Mahakamani watuhumiwa   watatu Mathias Shilole (52),Mganga wa tiba  asili na Mkazi waKilimanajro Nyangwale na  LucyMdelema kwa tuhuma za kujihususha  na mauaji  hayo.


OJADACT imebaini sababu mbalimbali za  maujai   hayo  ni  pamoja na 


1.Imani  za kishirikina  kwenye  jamii zinahusishwa na  kujipatia utajiri kwa njia nyepesi


2.Ukatili kwenye jamii  unaombatana  na malezi mabaya  ya  jamii  isiyo na  staha


OJADACT  inatoa  rai  kwa  jamii  kutojihusisha na   vitendo  vya  uvunjifu wa  sheria na badala  yake jamii iwe  mlinzi wa mtoto kwa kutoa tarifa  inapoona  viashiria  vya  ukiukwaji wa haki za mtoto ikiwemo haki ya  kuishi .


 Serikali na wadau  mbalimbali wanendelee  kufanya kazi  kwa pamoja  ya kumlinda mtoto.          


 Edwin Soko

 Mwenyekiti

 OJADACT

 *22.06.2022

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 22,2022


Magazetini leo Jumatano June 22 2022

Share:

Monday, 20 June 2022

MWANAFUNZI WA CHUO CHA SAUT ANUSURIKA KICHAPO AKIDAIWA KUTUPA MTOTO MCHANGA

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut) Mwanza aliyetambulika kwa jina moja la Judith amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi akidaiwa kujifungua na kumtupa mtoto nyuma ya nyumba anayoishi.

Mwanafunzi huyo anayesoma shahada ya sheria mwaka wa tatu chuoni hapo anadaiwa kutenda tukio hilo leo asubuhi Jumatatu Juni 20, 2022 nyumbani kwake mtaa wa Silivin Sweya jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Silivini, Rajabu Ramadhan amethibitisha kutokea tukio hilo akibainisha kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa Polisi.

"Baada ya kukuta mwili wa kichanga umetupwa tulifanya msako wa kujua mtu aliyekuwa na ujauzito na tulimbaini mwanafunzi wa Saut ambaye baada ya kumchunguza tumekuta ana dalili za kutoa mimba kwani alikuwa akitokwa na damu," amesema Ramadhani.
 
Via Mwananchi

Share:

HAMIS AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI TUHUMA ZA KUIBA MAHINDI DEBE 2

NB- Picha haihusiani na Hamis wa kwenye hii habari chini

**
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis Hassan, mkazi wa Kijiji cha Kambuzi, Kata ya Litapuga wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuiba debe mbili za mahindi.

Inaelezwa kuwa kabla ya tukio hilo la mauaji, wananchi marehemu walimtuhumu kuiba debe mbili za mahindi mali ya Emmanuel Malela, na kiongozi wa mtaa huo aliwaagiza watu wanaomshikilia wamfikishe kituo cha polisi Kanoge ila wakajichukulia sheria mkononi.

Watu hao watano wanaotuhimwa kutekeleza mauaji ya Hamisi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na kupitia kitengo cha upelelezi walibainika kukimbilia mkoani Tabora na kurudishwa Katavi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili.

Chanzo - EATV
Share:

BRELA YAFANYA USAFI SOKO LA MBAGALA ZAKHEIM

 

Watumishi na Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakifanya usafi katika Soko jipya la Mbagala Zakheim lilipo katika wilayani  Temeke Jijini Dar es Salaam leo Juni 20,2022 ikiwia ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza rasmi Juni 16 hadi 23,2022. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO.

Na: hughes Dugilo, DAR.

katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (BRELA) imetoa mwito kwa wafanyabiashara kote nchini kurasimisha biashara zao ikiwemo kufanya usajili ili kufanya shughuli zao na  kutambulika kisheria.

Mwito huo umetolewa leo Juni 20,2022 na Ofisa Habari wa Wakala huo Bi. Christina Njovu katika soko Jipya la Mbagala Zakheim walipokuwa wakifanya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi Juni 16 na yanatarajia kufikia tamati Juni 23, mwaka huu.

Ameeleza kuwa licha ya BRELA kufanya usafi sokoni hapo pia inawapa fursa wafanyabiashara hao kupata elimu juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwemo usajili wa Biashara na Leseni.

"Leo tumefika hapa kufanya usafi katika soko hili, huu ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza wiki iliyopita hivyo BRELA tumekuwa  tukifanya kazi mbalimbali za kijamii na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi zetu"

"Hii ni fursa kwa wafanyabiashara wa soko hili la Zakheim  kuifahamu BRELA na kazi zake ili sasa wapate kurasimisha kazi zao kwa kusajili biashara zao,"amesema Njovu.

Ameongeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja BRELA imeendelea kutoa huduma zake za papo kwa hapo katika viwanja vya Ofisi zake zilizopo katika mtaa wa Shaban Robert na Sokoine Jijini Dar es Salaam na kwamba zoezi hilo litakamilika Juni 23,mwaka 2022. 

PICHA: BRELA WAKIFANYA USAFI










Share:

TANZANIA YAKOPESHWA SH. BILIONI 195 KUJENGA MRADI WA MAJI DIDIA ,ISELAMAGAZI, TINDE NA MANISPAA YA SHINYANGA


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen (kushoto), wakibadilishana mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen (kushoto), wakionesha wanahabari na wadau walioshuhudia utiwaji Saini mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen (kushoto), wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen, akiongea wakati wa hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, wakati wa hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Mhandisi Anthony Sanga wakati wa hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD baada ya hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Stephanie Mouen, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe. Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba, wakiwa katika picha ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango, na Shirika la Maendeleo la KImataifa la Ufaransa – AFD, wakati wa hafla ya utiaji Saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 195 uliotolewa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Shinyanga (SHUWASA), Jijini Dar es Salaam.


.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam)

……………………………………..

Na Eva Ngowi, Dar es Salaam

Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Ufaransa (AFD), imetia saini mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wa Euro milioni 75 sawa na takriban shilingi bilioni 195 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Mkoa wa Shinyanga.

Akiongea baada ya kusaini mkataba huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel M. Tutuba, alisema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kutoa huduma za uhakika na endelevu za upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Shinyanga.

Bw. Tutuba alisema kuwa mradi huo utaboresha afya, ustawi wa jamii na hali za maisha ya wanufaika wa mradi huo kwa kuboresha na kuimarisha miundombinu iliyopo na kuongeza ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma bora kupitia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

“Hii ni ajenda kubwa inayoendana na hatua za Serikali, kupitia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano unaotoa vipaumbele pamoja kuboresha upatikanaji na usamabazaji wa Maji na huduma za usafi wa mazingira mijini na vijijini na utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira na ufadhili huu wa AFD utachagia kufikia moja ya vigezo vya Mpango huo wa kuongeza asilimia ya watu wa mijini wanaopata huduma ya maji safi”. Alisema Bw. Tutuba

Bw. Tutuba aliongeza kuwa Mradi huo ukikamilika utaongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa asilimia 95 katika Manispaa ya Shinyanga na baadhi ya miji midogo katika Wilaya ya Shinyanga, na itawanufaisha wananchi zaidi ya 306,566.

“Uzalishaji wa maji utaongezeka kutoka mita za ujazo za sasa ambazo ni 25,877 kwa siku, hadi 33,944; na kuongeza nafasi za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika maeneo yanayozunguka mradi” alisisitiza Bw. Tutuba

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Tutuba alizitaka taasisi zitakazotekeleza mradi huo (Wizara ya Maji na SHUWASA) chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Sanga, watumie uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Sekta ya Maji Tanzania, Programu ya huduma endelevu za Maji na usafi wa Mazingira vijijini na miradi mbalimbali ya maji na usafi wa mazingira iliyofadhiliwa na AFD ili kutoa huduma nzuri kwa ajili ya wananchi wa Shinyanga na nchini kwa ujumla.

Aliihakikishia Serikali ya Ufaransa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan iko tayari kuendelea kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo kwa faida ya wananchi wan chi hizo mbili na itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.

Kwa upande wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaoui alisema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika sekta hiyo ambapo katika kipindi cha miezi mitano tu iliyopita kuanzia mwezi Februali, Ufaransa imeipatia Tanzania Euro milioni 330 kiasi ambacho ni kikubwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.

“Nchi zetu mbili zina urafiki ambao umekuwa ukikuwa kama inavyojidhihirisha katika miradi ya kimaendeleo tunayofadhili ikihusisha mkataba tuliosaini leo. Tutaendelea kushirikiana hasa katika sekta hizi tatu ambazo ni Maji na Usafi wa Mazingira, Nishati na Usafirishaji na Uchukuzi.” Alisema Mhe. Hajlaoui

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzania Bi. Stephanie Mouen, alisema kusainiwa kwa mkataba huo ni moja ya malengo ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa.

Alisema kuwa tangu mwaka 2014 Serikali ya Ufaransa imewekeza zaidi ya euro bilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo duniani kote ikiwa ni jitihada ya nchi hiyo kuziwezesha nchi zinazoendelea kuondokana na uhaba wa maji na uharibu wa mazingira.

Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, alisema anashukuru kushuhudia kusainiwa kwa mkataba huu wa maji na usafi wa mazingira kwani utakwenda kusaidia wananchi wa Shinyanga ambao hivi sasa wanapata maji kwa wastani wa asilimia 60.

Hivyo kukamilika kwa mradi huu kutawezesha maji kufikia asilimia 95 au Zaidi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo imeelekeza kufikia mwaka 2025 huduma ya maji mijini ifikie asilimia 95 na maji vijijini ifikie asilimia 85.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa nchi yetu ya kuweza kuaminiwa na nchi mbalimbali, marafiki ambao sasa wanatukopeha kwa masharti nafuu ili kuweza kutekeleza miradi hii ya kimkakati na kuhakikisha kwamba tatizo la maji katika maeneo mbalimbali linamalizika.” Alisema Mhandisi Sanga

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Mhandisi Yusuph Katopola, alisema "msaada huu ambao wamekuwa wakitupatia Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Maji pamoja na AFD uendelee kuwepo mpaka mwisho wa kukamilika kwa mradi huu"

“Sisi SHUWASA tuna furaha sana kupokea fedha hizi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu wa Maji safi na usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Shinyanga lakini pia miji midogo ya Tinde, Didia na Isalemagazi maalumu kwa ajili ya kuendeleza huduma za maji safi na Usafi wa Mazingira.” alisema Mhandisi Katopola
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger