Monday, 20 June 2022

BRELA YAFANYA USAFI SOKO LA MBAGALA ZAKHEIM

...

 

Watumishi na Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakifanya usafi katika Soko jipya la Mbagala Zakheim lilipo katika wilayani  Temeke Jijini Dar es Salaam leo Juni 20,2022 ikiwia ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza rasmi Juni 16 hadi 23,2022. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO.

Na: hughes Dugilo, DAR.

katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (BRELA) imetoa mwito kwa wafanyabiashara kote nchini kurasimisha biashara zao ikiwemo kufanya usajili ili kufanya shughuli zao na  kutambulika kisheria.

Mwito huo umetolewa leo Juni 20,2022 na Ofisa Habari wa Wakala huo Bi. Christina Njovu katika soko Jipya la Mbagala Zakheim walipokuwa wakifanya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi Juni 16 na yanatarajia kufikia tamati Juni 23, mwaka huu.

Ameeleza kuwa licha ya BRELA kufanya usafi sokoni hapo pia inawapa fursa wafanyabiashara hao kupata elimu juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwemo usajili wa Biashara na Leseni.

"Leo tumefika hapa kufanya usafi katika soko hili, huu ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza wiki iliyopita hivyo BRELA tumekuwa  tukifanya kazi mbalimbali za kijamii na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi zetu"

"Hii ni fursa kwa wafanyabiashara wa soko hili la Zakheim  kuifahamu BRELA na kazi zake ili sasa wapate kurasimisha kazi zao kwa kusajili biashara zao,"amesema Njovu.

Ameongeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja BRELA imeendelea kutoa huduma zake za papo kwa hapo katika viwanja vya Ofisi zake zilizopo katika mtaa wa Shaban Robert na Sokoine Jijini Dar es Salaam na kwamba zoezi hilo litakamilika Juni 23,mwaka 2022. 

PICHA: BRELA WAKIFANYA USAFI










Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger