Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut) Mwanza aliyetambulika kwa jina moja la Judith amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi akidaiwa kujifungua na kumtupa mtoto nyuma ya nyumba anayoishi.
Mwanafunzi huyo anayesoma shahada ya sheria mwaka wa tatu chuoni hapo anadaiwa kutenda tukio hilo leo asubuhi Jumatatu Juni 20, 2022 nyumbani kwake mtaa wa Silivin Sweya jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Silivini, Rajabu Ramadhan amethibitisha kutokea tukio hilo akibainisha kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa Polisi.
"Baada ya kukuta mwili wa kichanga umetupwa tulifanya msako wa kujua mtu aliyekuwa na ujauzito na tulimbaini mwanafunzi wa Saut ambaye baada ya kumchunguza tumekuta ana dalili za kutoa mimba kwani alikuwa akitokwa na damu," amesema Ramadhani.
Via Mwananchi
0 comments:
Post a Comment