Mwanamke mmoja aitwaye Maria Matheo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kumvizia mumewe GABRIEL NGUWA (80) akiwa amelala na kumkaba shingoni hadi kifo.
Chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu baina ya wanandoa hao hususani nyakati za jioni mwanamke anapokuwa amelewa na kuanza kumtuhumu mumewe kuwa hana msaada katika maisha yao.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Bugweda kijiji cha Budushi tarafa ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
0 comments:
Post a Comment