Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Gerald Musabila
**
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Gerald Musabila amesema, mamlaka hiyo imemkamata nesi msaidizi wa zahanati ya Kariakoo, Salum Shaban mkazi wa Tabata Relini akiwa na kilo 174.77 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin.
Kamishna Musabila amesema kuwa madawa hayo yalikutwa juu ya kitanda chake nyumbani kwake Tabata Relini huku yeye akiwa amelala chini.
"Upekuzi uliofanyika nyumbani kwake zilipatikana Paketi 162 zenye unga uliodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya zikiwa ndani ya viroba sita vilivyokuwa nyumbani kwa mtuhumiwa na paketi moja ya unga huo iikuwa kwenye mfuko mmoja wa Nailoni" ameeleza Kamishna Musabila.
Inaelezwa kuwa uchunguzi wa kitaalam wa mkemia Mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa unga huo ni madawa ya kulevya aina ya Heroin na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Chanzo - EATV
0 comments:
Post a Comment