Picha haihusiani na habari hapa chini
****
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia.
ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.
Kamanda Konyo amesema majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa Polisi na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.
0 comments:
Post a Comment