Monday, 6 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 7,2022


Magazetini leo Jumanne June 7,2022



Share:

MISA - TANZANIA YAENDELEA KUWANOA WAANDISHI WA HABARI WA REDIO ZA JAMII KUANDAA VIPINDI VYENYE MRENGO WA KIJINSIA


Meneja wa Mradi kutoka Misa Tanzania Bi.Neema Kasubiro akifafanua jambo kwa washiriki
Mwasilisha mada mwandishi mkongwe Abubakar Famau.
Mwasilisha mada mwandishi mkongwe Abubakar Famau.
Mtayarishaji vpindi Edward Lucas kutoka kituo cha redio Mazingira akielezea mafanikio na changamoto katika uandaaji wa vpindi vya usawa wa kijinsia katika kituo hicho.
Mtayarishaji vpindi Glory Kusaga kutoka kituo cha redio Uvinza akielezea mafanikio na changamoto katika uandaaji wa vpindi vya usawa wa kijinsia katika kituo hicho.
TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) imeendelea juhudi zake za kuwanoa waandishi wa habari ili kukuza usawa wa kijinsia kupitia vipindi vya radio za kijamii nchini.


MISA TANZANIA kwa kushirikiana na Vikes inaendesha mradi wa kuwajengea uwezo waandishi kutoka katika radio za kijamii nchini ili kutengeneza vipindi vitakavyoleta mabadiliko katika usawa wa kijinsia ikiwemo uhuru wa kujieleza miongozi mwa wanawake.


Akizungumza baada ya kikao kazi cha kupata mrejesho kutoka kwa waandishi kutoka mikoa mbalimbali nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki,Meneja mradi huo Neema Kasubiro amesema katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo kuna mabadiliko yanayoonekana katika uandaaji wa vipindi vya usawa wa kijinsia.


“Baada ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari, wapo waliofikia hatua ya kuanzisha vipindi katika radio zao hili waweze kufanyia kazi elimu wanayoipata kuhusu usawa wa jinsia katika maudhui ya vipindi vya radio zao” alifafanua.


Neema amesema mradi huo utekelezaji wake umegawanyika katika awamu mbalimbali na kwa awamu hii ilianza January na itakamilka mwaka 2024 ikitarajiwa kujikita Zaidi katika kuboresha ubora wa maudhui katika mada za jinsia.


Akizungumza baada ya kusikiliza vipindi mbalimbali vilivyoandaliwa na waandishi hao,mwandishi mkongwe nchini Abubakar Famau amesema kwamba ili sauti za wanawake zisikike katika vyombo vya habari ni lazima waandishi wawe tayari kushirikisha jamii katika uandaaji wa vipindi vyao.


“Kama tutawashirikisha kwa kiwango kinachotakiwa nina uhakika lengo la kupata uhuru wa kujieleza kutoka kwa kundi kubwa la wanawake litatimia” alisema Famau.


Pia  Famau amewataka waandishi na watangazaji wa vipindi vya redio nchini kufuata misingi ya uzalishaji wa vipindi hivyo ikiwemo matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili ili waweze kufikisha ujumbe kwa wasikilizaji kama ilivyokusudiwa.


Famau amebainisha kwamba bado kuna matatizo katika matamshi na uchaguzi usio faa wa maneno kwa baadhi ya watangazaji wa redio nchini.


Hata hivyo kwa upande wa waandishi wa habari washiriki wa mradi huo wamebainisha kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo bado kuna changamoto zinazohitajika kutatuliwa ili kutimiza malengo.


Mratibu wa vipindi kutoka kituo cha radio cha Mazingira kilichopo wilayani Bunda,mkoani Mara Lucas Edward amesema ufinyu wa waandishi wa habari wa kujikita katika habari za jinsia imekuwa changamoto kubwa katika utekelezaji.


Kwa upande wake Glory Kusaga,mtangazaji wa kituo cha radio cha Uvinza toka mkoani Kigoma amesema uwepo wa mfumo dume katika jamii bado unaathiri ushiriki wa wanawake katika maudhui ya redio hivyo kuwa kikwazo kwa watayarishaji.


“Tunahitaji sana sauti za jinsia zote zisikike katika vipindi vyetu,lakini bado kuna wanawake hawawezi kuongea kwenye redio hadi wapate ruhusa za waume zao”amesema akiongeza kuwa hali hiyo husababisha wanawake kushindwa kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao katika vyombo vya habari.

5. 

Share:

Hureeeeeee!!! SERENGETI GIRLS YAFUZU KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA KWANZA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake U-17 (Serengeti Girls) imefanikiwa kufuzu Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cameroon mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Serengeti Girls limefungwa na Neema Paul dakika 47 na kuifanya Tanzania itinge Kombe la Dunia litakalochezwa Oktoba mwaka huu nchini India kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia mchezo wa awali kushinda 4-1 ugenini.

Serengeti Girls leo saa 3 usiku watatua kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es salaam, wakitokea hapa Zanzibar baada ya kufuzu Kombe la Dunia.


Tanzania ileeee World Cup ya Wanawake U-17.

Hongereni Serengeti Girls kuzidi kuitangaza Tanzania Kimataifa .

Imeandaliwa na Aabubakarkisandu Zanzibar.
Share:

MKE WANGU KANIAMBIA SIRI YA KUSHANGAZA AJABU!

Share:

Sunday, 5 June 2022

BARRICK BULYANHULU YAENDELEA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA KIJAMII MSALALA ….YATENGA BILIONI 1.9 KUFANIKISHA MIRADI YA JAMII 2022


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Cheick Sangare (Kulia) akibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala,Mhe. Mibako Mabubu, ambapo mgodi huo umetenga shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya kijamii kwenye halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka huu (2022).
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Cheick Sangare (Kulia) akibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mhe. Mibako Mabubu,ambapo mgodi huo umetenga shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya kijamii kwenye halmashauri hiyo.Wengine pichani ni Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Halmashauri hiyo na Wafanyakazi wa Barrick.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mhe. Mibako Mabubu akiongea katika hafla hiyo.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Msalala,Leonard Mabula,akiongea katika hafla hiyo.
Washiriki katika hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali.

**
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, umesaini mkataba wa makubaliano na Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC)  Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ambapo umetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii kupitia bajeti ya fedha zilizotengwa kufanikisha miradi ya kusaidia jamii (CSR) katika kipindi cha mwaka 2022.


Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika katika mgodi wa Bulyanhulu na kuhudhuriwa na viongozi wa mgodi wa Bulyanhulu na watendaji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala na wafanyakazi wa mgodi huo.

Akiongea katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mhe. Mibako Mabubu, aliipongeza Barrick Bulyanhulu kwa mchango mkubwa inaotoa kufanikisha jitihada za Serikali kuboresha huduma za kijamii na miundo mbinu katika wilaya hiyo.


Hivi karibuni Kampuni ya Barrick , ilitangaza kuwa itatumia dola 6 kwa kila wakia ya dhahabu inayouzwa na migodi yake miwili nchini katika kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu na upatikanaji wa maji safi ya kunywa katika jamii zinazowazunguka.


Wakati huo huo, imetoa hadi dola milioni 70 kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya kitaifa ya kuongeza thamani, ikijumuisha mafunzo yanayohusu madini, ukuzaji ujuzi na vifaa vya kisayansi katika vyuo vikuu vya Tanzania, pamoja na miundombinu ya barabara.

Hii ni kwa mujibu wa masharti ya msingi ya makubaliano ya mfumo wa Barrick na Serikali, ambayo yalihusishwa na kuanzishwa kwa ubia wa pamoja na Twiga. Twiga inasimamia mgawanyo wa 50/50 wa faida za kiuchumi zitokanazo na migodi pamoja na uongozi wake.

Rais wa Barrick na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Bristow, alisema mpango wa uwekezaji ulikuwa mageuzi ya hivi karibuni ya ushirikiano wenye mafanikio makubwa baina ya kampuni na Serikali.


Barrick, imetumia zaidi ya dola bilioni 1.9 katika kodi, mishahara na malipo kwa wafanyabiashara wa ndani katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Angalau 73% ya bidhaa na huduma za migodi hiyo zinapatikana ndani ya nchi na inatoa kipaumbele kwa kuajiri wazawa wa Tanzania.
Share:

'NYUMBA ZA IBADA,MAENEO YA STAREHE KINARA KWA KELELE'-NEMC


MENEJA wa Uzingatiaji wa Sheria na Ufuatiliaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC),Ndimbumi Mboneke,akizungumza wakati wa warsha ya Maofisa Mazingira wa Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.
...........................

Na Mwandishi Wetu_DODOMA

MENEJA wa Uzingatiaji wa Sheria na Ufuatiliaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC),Ndimbumi Mboneke,ameeleza kuwa nyumba za ibada na maeneo ya starehe yanaoongoza kwa kulalamikiwa kuwa kinara wa kelele.

Hayo ameyasema wakati wa warsha ya Maofisa Mazingira wa Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.

Mboneke amesema kuwa siku za hivi karibuni kumekuwapo na kero kubwa ya kelele, kutoka kwenye maeneo mbalimbali.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko mengi sana tukiyachambua hayo malalamiko ya kelele mengi ni kutoka kwenye baa na nyumba za ibada, kiasi ni kutoka kwenye viwanda hasa vile vinavyotumia teknolojia ambazo sio nzuri,”ameeleza

Amefafanua Kuwa kelele zina athari kubwa kwenye afya ya binadamu na mazingira.

“Watu washindwe kulala na akishindwa kulala anashindwa kufanya kazi zake za siku kwasababu anakuwa hajapata usingizi vizuri, Wanafunzi wanashindwa kusoma, wazee wanaathirika ambao ni wagonjwa na wanapata athari za kiafya,”amesema

Hata hivyo amesema kuwa kuna kanuni za usimamizi wa mazingira, kelele na mitetemo ya Mwaka 2015 ambazo zimeweka viwango vya juu vinavyoruhusiwa kuzalisha kelele.

“Hivyo viwango vimetofautina kwa muda, lakini pia kuna maeneo kama ya shule, chuo na maeneo tofauti, maeneo ya kazi, maeneo ya biashara,”amesema

Alitolea mfano viwango vya sauti vya juu katika shule na vyuo ni decibel(kizio cha kupima kiwango cha sauti) 45 kwa mchana na 35 kwa usiku huku kwenye makazi ni 50 kwa mchana na 35 kwa usiku.

Aidha amesema kuwa kutokana na tatizo hilo upo mwongozo wa kusimamia kelele na mitetemo ambao ulizinduliwa Septemba 2021, kila taasisi iliyopo kwenye mwongozo imepewa majukumu yake ya kusimamia masuala hayo ambapo msimamizi Mkuu ni Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Hata hivyo Mboneke ametoa A wito kwa kila mdau anayehusika kusimamia mwongozo huo awajibike kwa majukumu yake yaliyoainishwa.
Share:

TASAF IMEDHAMIRIA KUMPELEKA MWANANCHI WA KAWAIDA KATIKA UCHUMI WA KATI - Mhe. Londo


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dennis Londo (Mb) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ilongero, mkoani Singida wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ilongero, mkoani Singida wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) ilipotembelea kijiji hicho kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).


Wananchi wa Kijiji cha Ilongero, mkoani Singida wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo (Mb) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).


Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ilongero, Josephine Komba akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya kijiji hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa TASAF.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakimsikiliza mmoja wa wanufaika wa TASAF (hayupo pichani) Kijiji cha Ilongero wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji hicho.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo (Wapili kutoka kushoto) akisikiliza Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya kijiji cha Ilongero wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa TASAF. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi akitoa utambulisho kabla ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo (Mb) kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Ilongero wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa TASAF.


Mnufaika wa TASAF, Bi. Tatu Sima akielezea namna alivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji cha Ilongero wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa (TASAF) katika kijiji hicho.


Mnufaika wa TASAF, Bi. Pili Mohamed akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji cha Ilongero wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa (TASAF) katika kijiji hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Ilongero, mkoani Singida wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) ilipotembelea kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika kijiji hicho. Wengine ni baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo.

***************************

Na. Veronica E. Mwafisi-Singida

Tarehe 05 Juni, 2022



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Dennis Londo (Mb), amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini umedhamiria kikamilifu kumpeleka mwananchi wa kawaida katika uchumi wa kati.

Mhe. Londo amesema hayo wakati wa ziara ya kamati yake katika Kijiji cha Ilongero Wilayani Singida iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini katika Kijiji hicho.

Mhe. Londo amesema kupitia miradi inayotekelezwa na TASAF, Kamati yake ina uhakika itatoa ajira kwa wananchi wanaoishi katika kaya maskini, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kaya kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, lengo la Serikali kuzinyanyua kiuchumi kaya maskini kupitia TASAF ni kuhakikisha Tanzania ya Viwanda inaanza na wananchi wanyonge.

“Sisi kama wawakilishi wenu ambao tunafanya kazi kwa karibu sana na Ofisi ya Rais ambayo imepewa dhamana ya kuisimamia TASAF, tunaahidi kuendelea kufanya nao kazi bega kwa bega ili kuhakikisha lengo la TASAF la kuboresha maisha ya kaya maskini nchini linatimia,” Mhe. Londo amesisitiza.

Kwa upande wake, mnufaika wa TASAF wa Kijiji cha Ilongero Bi. Tabu Sima amesema ruzuku ya TASAF alipoipata kwa mara ya kwanza aliitumia kuchimba msingi wa nyumba yake anayoishi hivisasa.

Bi. Sima ameongeza kuwa, anaishukuru TASAF kwani ruzuku anayoipata imemuwezesha kusomesha watoto wake na kuendeleza biashara zake ambapo hata soko analofanyia biashara zake limejengwa na TASAF.

Naye Bi. Pili Mohamed mnufaika mwingine wa TASAF katika Kijiji cha Ilongero Wilayani Singida amesema, kabla ya kuanza kunufaika na TASAF alikuwa akiishi katika nyumba ya tope lakini mara baada ya kuanza kupokea ruzuku na kwa kupitia vikundi vya kuweka na kukopeshana walivyoanzishiwa aliweza kufyatua tofali `na kujenga nyumba bora anayoishi hivisasa.

Akizungumzia mchango wa TASAF katika Kijiji cha Ilongero, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa, TASAF imefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kujenga mabwawa mawili pamoja na kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Kijiji hicho.

“Ni heshima kubwa kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutatua tatizo la maji kupitia mpango wa TASAF, ambalo lilikuwa likiwakabili wananchi wa Kijiji cha Ilongero kwa muda mrefu,” Mhe. Jenista ameeleza.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wako mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Singida.
Share:

SAGINI AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA UJENZI WA JENGO HARAKA NA KWAMBA WIZARA HAIRIDHISHWI NA KASI YA UJENZI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Uhamiaji Mtwara,tarehe 4 Juni 2022, ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Mtwara.Katika ziara hiyo ameambatana na Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt Anna Makakala.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akizungumza kwenye kikao na Mkandarasi baada ya kukagua jengo la Idara ya Uhamiaji Mtwara.

............................................

Na Mwandishi wetu,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amemuagiza mkandarasi wa ujenzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mtwara kukamilisha ujenzi huo ndani ya mwezi mmoja na kwamba Serikali haijaridhishwa na kasi ya ukamilishaji wa ujenzi huo.

Naibu Waziri Sagini amemuagiza Mkandarasi na Mshauri Mwelekezi wa mradi huo kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio siku ya Jumatatu tarehe 06 Juni wakiwa na mpango kazi wa kukamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi Juni 2022. Aliwakumbusha kuwa kazi ya umaliziaji inahitaji umakini mkubwa.

Aidha alisisitiza kwamba Wizara inahitaji watendaji wa idara ya Uhamiaji waanze kutumia jengo hilo mapema kwani kwa sasa wanatumia ofisi zilizotawanyika.

“Tabu yetu ni kasi ndogo ya Mkandarasi kukamilisha kazi ya ujenzi wa maeneo yaliyobakia. Kinachosikitisha ni kwamba wizara haijashindwa kumlipa Mkandarasi. Fedha zipo, lakini Mkandarasi yuko nyuma ya muda pamoja na kuongezewa muda zaidi.” alisema

"Nimeelekeza mkandarasi afike na mpango kazi Dodoma na kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili wakubaliane namna ya kukamilisha kazi kabla mwaka wa fedha 2021/2022 haujamalizika” alisema.

Naibu Waziri Sagini alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara Juni 4, 2022 baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Uhamiaji ikiwa ni moja ya ziara yake mkoani humo.

Aidha, Naibu Waziri Sagini ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa kukubali kuwapatia ofisi baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wizara inaendelea kuwajengea ofisi.

Pia Naibu Waziri Sagini amevipongeza Vyombo vya Usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani vilivyopo mkoani Mtwara kwa utendaji kazi wao ukiondoa tukio moja lililolitia doa jeshi la polisi miezi kadhaa iliyopita. Alivitaka vyombo vyote kusimamia nidhamu ya askari, wakaguzi na maofisa wake ili matukio kama hayo yasijitokeze tena.

Aidha aliahidi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Uongozi wa Waziri Mhandisi Hamad Masauni itatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira na utendaji kazi wa vyombo hivyo.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amesema Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Uhamiaji Mtwara umejengwa kwa kiwango kizuri lakini kasi yake hairidhishi kwani Idara ilitegemea ujenzi huo kukamilika Februari mwaka huu.

“Jengo limejengwa kwa kiwango kizuri lakini tunapima matokeo. Ukiangalia tupo kwenye asilimia 65 lakini tunahitaji ifikapo Agosti 2022 ujenzi uwe umekamilika” alisema.
Share:

Saturday, 4 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 5,2022








Share:

Friday, 3 June 2022

ANAYETAKA BANGI IHALALISHWE SASA ANAGOMBA URAIS


Mgombea wa nafasi ya Urais nchini Kenya kea tiketi ya Chama cha Roots George Wajackoyah
**

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imepitisha jina la George Wajackoyah kuwania Urais wa nchi hiyo baada ya kumzuiwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kutokidhi vigezo

Mwanasiasa huyo kutoka chama cha Roots amekuwa maarifu nchini humo kutokana na sera yake ya kutaka matumizi ya bangi yahalalishwe.

Mapema wiki hii, usajili wake wa kugombea urais ulikataliwa na tume ya uchaguzi IEBC kwa kukosa sahihi za kutosha, ambapo alihitajika kuwa na sahihi elfu mbili ambapo amewasilisha tena sahihi hizo na kuruhusiwa kugombea
Share:

NESI AKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA KITANDANI KWAKE




Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Gerald Musabila
**
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Gerald Musabila amesema, mamlaka hiyo imemkamata nesi msaidizi wa zahanati ya Kariakoo, Salum Shaban mkazi wa Tabata Relini akiwa na kilo 174.77 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin.

Kamishna Musabila amesema kuwa madawa hayo yalikutwa juu ya kitanda chake nyumbani kwake Tabata Relini huku yeye akiwa amelala chini.

"Upekuzi uliofanyika nyumbani kwake zilipatikana Paketi 162 zenye unga uliodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya zikiwa ndani ya viroba sita vilivyokuwa nyumbani kwa mtuhumiwa na paketi moja ya unga huo iikuwa kwenye mfuko mmoja wa Nailoni" ameeleza Kamishna Musabila.

Inaelezwa kuwa uchunguzi wa kitaalam wa mkemia Mkuu wa Serikali imethibitisha kuwa unga huo ni madawa ya kulevya aina ya Heroin na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Chanzo - EATV
Share:

JINSI YA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA YAKO

Share:

MKE AMKATA MMEWE SEHEMU ZA SIRI KWA WEMBE

 Picha haihusiani na habari hapa chini

****


Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo  amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia.

ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Konyo amesema majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa Polisi na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.

Share:

Thursday, 2 June 2022

SERIKALI KUANDAA KANUNI ZA UDHIBITI WA BEI YA DAWA NA VIFAA TIBA


********************

Na WAF, Bungeni, Dodoma.

Serikali ipo mbioni kuandaa kuani za kudhibiti bei za dawa nchini na tayari rasimu ya kanuni hizo zimeshawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali lilioulizwa na Mheshimiwa. Mhandisi Mwanaisha Ng’anzi Ulenge (Mbunge Viti Maalum) Bungeni, Jijini Dodoma.

Mhe. Ulenge amehoji Serikali ina mpango gani wa kutoa bei elekezi ya vifaa vya tiba haswa akilenga vya macho, pua na koo.

Akijibu Kuhusu Vifaa tiba, Dkt. Mollel amesema kuwa bei elekezi za vifaatiba zitaandaliwa mara tuu baada ya kukamilika kwa kanuni za bei za dawa elekezi.
Share:

TANROADS YAFUNGA MASHINE ZA KUHESABU IDADI YA MAGARI KWENYE BARABARA KUU NA MIJINI


Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George akikagua Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) mara baada ya kukifunga katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es salaam.

Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George akizungumza na waandishi wa habari katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) ambayo wameifunga hivi karibuni. Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) ikiwa imefungwa katika barabara ya Morocco-Mwenge Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)wamefanikiwa kufunga Mashine ya kuhesabu idadi ya magari barabarani (Inductive Loop Vehicle Counters) katika barabara ambazo magari yyanapita kwa wingi ili kusaidia katika usanifu na ujenzi wa barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 02,2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mfumo wa Usimamizi wa Rasirimali za Barabara TANROADS, Mhandisi Mussa George amesema kwa kawaida TANROADS inakuwa na utaratibu wa kuhesabu magari kwa kutumia watu hivyo kupitia kifaa hicho kitawarahishishia ufanyaji kazi na kuepuka muda na gharama kubwa.

Amesema kupitia teknolojia hiyo inasaidia kupata data ambazo zinauharisia kuliko mwanzo walivyokuwa wanatumia watu ambapo mara nyingi hutumia kwa muda tu wakati mashine hiyo itatumika kwa masaa 24 na kuleta data zilizo sahihi.

"Lengo la kuhesabu magari , Huwa tunatumia taarifa za magari kwenye kufanya usanifu wa barabara na kufanya mateengenezo pia .Siku zote unapofanya usanifu wa barabara lazima ujue idadi ya magari yanayopita kwenye hiyo sehemu na baada ya kupata idadi ya magari na aina ya magari ndo inakusaidia kwenye tabaka la barabara kwamba barabara unayoijenga iwe ya aina gani". Amesema Bw.George.

Aidha amewataka watanzania hasa madereva kuhakikisha wanalinda miundombinu inayotekelezwa na serikali na itakapotokea mtu au watu wakifanya uharibifu kwenye miundombinu hii basi watachukuliwa hatua.

"Kanda ya Ziwa tulipata kesi tatu za uharibifu na wizi wa hizi mashine na kwa hapa DDar es Salaam tulipata kesi moja na kwa bahati nzuri maaskari walikuwa karibu walijaribu kusaidia ,tunawaomba wanancchi tuzilinde hizi mashine". Amesema

Pamoja na hayo amesema wamenunua mashine hizo 150 kwa nchi nzima na inashauriwa mashine hizo zifungwe kwenye barabara za lami ambapo kwasasa wamefunga mashine 50 kwaajili ya kuanzia ambazo wamezifunga nchi nzima na kipaumbele cha kwanza wameipa barabara kuu pili barabara za mijini ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefunga mashine 16.

Share:

TISA WAKAMATWA WAKISAFIRISHA VIUNGO VYA BINADAMU KIGOMA..KUNA MGUU NA MBAVU ZA MTU

 

Vifaa vya Uganga walivyokamatwa navyo watu waliokutwa na viungo vya binadamu


Na Fadhili Abdallah - Malunde 1 blog Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imewatia mbaroni watu tisa wakituhumiwa kujihusisha na usafirishaji na uuzaji wa viungo vinavyohisiwa kuwa ni sehemu ya mwili wa binadamu huku ikielezwa kuwa vilikuwa vitumiwe kwenye mambo ya kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,James Manyama alisema hayo akitoa  taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma ambapo alisema kuwa watu hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii Kijiji cha Kanyonza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma baada ya kuzuia katika kuzuizi cha polisi Kihomoka.

Kamanda Manyama alisema kuwa awali watu watatu  walikamatwa katika kuzuizi hicho cha polisi wakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 948 DQU aina ya Pro Box (mchomoko) wakielekea Mwanza kwenye kijiji cha Nyahunge ambako walikuwa wakipeleka kwa mteja aliyekuwa akihitaji viungo hivyo.

Alisema kuwa baada ya kuwahoji watuhumiwa waliwataja waliokuwa wakipelekewa viungo hivyo wakazi wa Mwanza ambao ni wenyeji wa Kigoma sambamba na watu waliowapa viungo hivyo kutoka wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo jumla ya watu wote waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo wamefikia tisa.

“Kwa sasa tunafanya uchunguzi zaidi na kuwahoji watuhumiwa kujua kama viungo hivyo vimefukuliwa kwenye kaburi gani na  ni mwili wa nani au kuna mtu aliuawa na viungo vyake kuchukuliwa, viungo vilivyopo ni sehemu ya mbavu na mguu mmoja,”alisema kamanda huyo wa Polisi mkoa Kigoma.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger