Sunday, 22 May 2022

BARRICK KUENDELEA KUTEKELEZA SERA YA USHIRIKISHWAJI WATANZANIA KATIKA MNYORORO WA UCHUMI WA MADINI (LOCAL CONTENT)


Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akizungumza kwenye jukwaa la kwanza la utekelezaji wa ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya Madini, lililofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof Idris Kikula, akizindua jukwaa la kwanza la utekelezaji wa ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya Madini, lililofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia matukio
Baadhi ya Wadhamini wa jukwaa hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof ldris Kikula.
***

Kampuni ya Madini ya Barrick, imeanza kutekeleza kwa vitendo , sera ya Serikali inayoyataka makampuni ya madini kushirikisha Watanzania katika mnyororo wa uchumi wa madini ambapo hadi kufikia sasa takribani asilimia 70% ya watoa huduma katika migodi yake inayoendesha nchini ni Watanzania.


Kampuni imeanza kutekeleza sera kwa vitendo katika maeneo ya ajira, utoaji wa zabuni, sambamba na kuendesha miradi ya kusaidia jamii katika maeneo yanazozunguka migodi yake nchini kupitia sera ya kampuni ya kuhudumia jamii (CSR).

Hayo yamebainishwa wakati wa jukwaa la kwanza la utekelezaji wa ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini linalofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Barrick, tayari imeanzisha programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani,(Local Business Development Programme (LBD) inayosimamiwa na mgodi wa North Mara, ambayo ni mhimili wa kusimamia kanuni hii na kuhakikisha watanzania wananufaika nayo kwa asilimia kubwa kwa kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji katika sekta ya madini, na fursa zilizopo kwenye sekta hii na tayari baadhi ya wafanyabiashara wamepatiwa mafunzo katika awamu ya kwanza.

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow, alisema wakati wa uzinduzi wake kuwa programu hii inadhihirisha jitihada endelevu za Barrick, katika kujenga uwezo wa watu wa ndani.

“Tangu migodi ianze kufanya kazi, tumekuwa tukishirikiana na wakazi wa maeneo yanayozunguka migodi yetu kwa kutengeneza fursa za uchumi endelevu kupitia mkakati wa usambazaji wa bidhaa za ndani kwa ajili ya uchumi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla,” alisema.

Alisema Programu hiyo ya maendeleo ya biashara za ndani italeta mabadiliko makubwa kwenye mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini na kuimarisha makampuni ya ndani sambamba na kutumia fursa zilizopo kwenye mnyororo huo wa thamani.


Serikali ya Tanzania, iliunda sera ya Local content mwaka 2015 ikilenga sekta ya madini, mafuta na gesi ili kuhakikisha uchimbaji wa madini na mapato yake yanawanufaisha watanzania.


Sera hiyo na kanuni zake inalenga kupanua uwanda wa kibiashara kwenye uchumi wa Tanzania, kutengeneza nafasi za ajira kwa kuhamasisha maendeleo ya taaluma na uwezo wa watanzania kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.

Share:

EDWIN SOKO AIBUKA KINARA WA TUZO YA HAKI YA KUPATA HABARI NA HAKI YA KUJIELEZA

Edwin Soko
Maria Sarungi 

Kampuni ya SK Media imetoa tuzo haki ya kupata habari na haki ya kujieleza kwa mwaka 2021 / 2022, ambapo Edwin Soko ameibuka kuwa mshindi  wa kwanza wa tuzo hizo.

SK Media wametangaza tuzo hizo kwa kumtangaza Edwin Soko kuwa mshindi wa kwanza kwa kutetea kundi la waandishi wa habari wanaopata madhila  ya kukamtwa na Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine yanayowagusa waandishi wa habari.


Mshindi wa pili wa tuzo hizo ni Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye amepata tuzo kwa kupaza sauti za wananchi na kuiwezesha jamii kuwasiliana kurahisi kupitia mtandao wa Maria space kupitia mtandao wa twitter.

Mshindi wa tatu, wamegongana Boniface Jacob na Martine Mases ambao walifuatilia kesi ya Freeman Mbowe hatua kwa hatua kwa kutumia simu ya kiganjani.

Washindi hao watapata vyeti na zawadi nyingine mbalimbali.

 

Share:

Saturday, 21 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 22,2022



Share:

TAKUKURU KUINGIA KAZINI UNUNUZI WA PAMBA

Mrajis msaidizi wa ushirika mkoa wa Geita, Doreen Mwanri, akizungumza na wajumbe wa chama kikuu cha ushirika wa mazao Chato.
Baadhi ya wajumbe wa Chama Kikuu cha Ushirika wa mazao Chato (CCU)wakiendelea kupokea maelekezo ya viongozi wa ushirika
Na Daniel Limbe, Chato

MSIMU wa ununuzi wa zao la pamba ukiwa umefunguliwa rasmi nchini, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru)wilayani Chato mkoani Geita imesema imejiandaa vyema kufuatilia vitendo vyote vya rushwa kwa viongozi wa vyama vya msingi (Amcos).

Aidha imewaonya viongozi wa Amcos 53 zinazounda ushirika wa mazao wa "Chato Co-Operative Union (CCU) kutojihusisha na wizi wa pembejeo za wakulima pamoja na fedha za ushirika huo.

Kaimu kamanda wa Takukuru wilaya ya Chato, Felix Vedastus, ameyasema hayo leo,mbele ya wajumbe zaidi ya 100 ambao wameshiriki mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa Ushirika wa CCU.

Hatua hiyo ni baada ya Mrajisi msadizi wa Ushirika mkoa wa Geita, Doreen Mwanri, kuzilalamikia baadhi ya amcos ambazo zinadaiwa kupata hasara kila msimu, huku baadhi ya wajumbe wakidaiwa kuiba pembejeo za wakulima.

Mbali na hilo, Mwanri, amedai serikali haitawaonea huruma baadhi ya makatibu wa amcos ambao watabainika kujihusisha na wizi wa fedha za ununuzi wa zao la pamba, kwa kuwa hali hiyo isipodhibitiwa inaweza kufifisha jitihada za serikali kuinua ushirika nchini.

"Lazima mtambue kuwa fedha zinazoletwa kwenu kununua pamba ni mkopo...na mnapaswa kuzilejesha kwa mujibu wa sheria...haiwezekani makatibu wachache watuharibie ushirika wetu kwa tamaa zao binafsi hatutakubali"amesema.

Kadhalika amesisitiza umoja miongoni mwa wajumbe na viongozi na kujiepusha na vitendo vya kuhujumu ushirika huo kwa kuwauzia pamba safi makampuni ya watu binafsi badala ya CCU, ambacho ndiyo chama kikuu cha ushirika huo.

Mkutano huo maalumu umeandaliwa na Mrajis wa ushirika mkoa wa Geita ili kutekeleza takwa la kisheria la kuwachagua viongozi wa Chama hicho ambapo wajumbe hupaswa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitatu.
Share:

Friday, 20 May 2022

SHIRIKALA THUBUTU AFRICA LAZINDUA MRADI WA HISANI KATIKA JAMII


Viongozi mbalimbali wa kata zilizolengwa na mradi huo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy)

Na Suzy Luhende,Shinyanga
Shirika lisilo la kiserikali la Thubutu Africa Initiatives (TAI) limezindua mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy) kwa ajili ya kuhamasisha jamii ya manispaa ya Shinyanga kuweza kutumia rasilimali zao katika kutatua baadhi ya changamoto zao bila kusubili fedha za serikali na wadau wengine.


Mradi huo umezinduliwa leo Mei 20,2022 mjini Shinyanga na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyewakilishwa na Chila Moses ambaye ni afisa Mipango na uratibu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ambaye amesema ni jambo zuri kuwepo kwa mradi huo, kwa kuwa unaleta mbinu ya moja kwa moja ya kutatua matatizo ya jamii husika zinazo wazunguka.


"Ninawaomba wote tuliopo hapa tukawahamasishe wananchi ili waweze kujitolea na kuweza kufanikisha mradi huu kwani mpango huu ni mzuri wa kuleta maendeleo na kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii",amesema Chila.


Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Manyama amesema ni jambo la kawaida limezoeleka la utoaji kuhusu maendeleo ya wengine ila ni wakati wa jamii yenyewe kutatua changamoto zao kwa kutumia rasilimali walizonazo katika maeneo yao.


" Mfumo huu umefanikiwa na kwa nchi za wenzetu kwa kiwango kikubwa kwa jamii yenyewe kutatua matatizo yao bila kusubili nguvu ya serikali na wahisani wa maendeleo,ni wakati wa kubadili tabia za jamii yetu ili iweze kujitoa zaidi kwa rasilimali zao kusaidia maendeleo binafsi kwa kuwashirikisha wenyewe", amesema Jonathan.


"Mradi huu utafanyika katika manispaa ya Shinyanga na utalenga kata nne ambazo ni kata ya Lubaga, Old Shinyanga, kata Mwamalili, kata ya Mjini, ambapo kata ya Lubaga tunatarajia kujenga choo cha watoto wa kike katika shule ya msingi Lubaga"amesema Manyama.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la TVMC Mussa Ngangala ambaye pia ni mjumbe baraza la NGO Taifa (NACONGO) amesema yeye binafsi alishawahi kujitolea kuondoa changamoto kivuko mtaa wa kitangili,lakini aliambiwa ni kihelele na wananchi,lakini baada ya kufanikisha kuondoa tatizo hilo alianza kusikia maneno kuwa huyu kijana anajitahidi kufanya maendeleo ya mtaa wetu.


Diwani wa kata ya Lubaga ,Reuben Dotto amesema ametiwa moyo kwa mradi huo kuanza kutekelezwa katika kata ya Lubaga na atahakikisha anakamilisha matundu ya vyoo katika shule ya sekondari kata ya Lubaga bila kusubili fedha za serikali bali kutumia ushirikishwaji wa wananchi wenyewe.


Afisa maendeleo ya Jamii Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga John Tesha amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu ili kuondoa changamoto mbalimbali ndani ya jamii, bali yapo yanayowezekana kwa wanajamii wenye bila kusubili serikali, hivyo wananchi wakishirikishwa wanaweza kujitoa kwa ajili ya maendeleo, hata kwenye harusi jamii inajitoa haiwezi ikashindwa kwenye suala la kimaendeleo.

Afisa maendeleo wa mkoa wa Shinyanga 
Tedson Ngwale amesema suala hili ni jambo la msingi, kwani rasilimali kubwa ni wananchi, hivyo nguvu ya wananchi inaaminika wakitaarifiwa tu kuna changamoto ya kitu furani watatoa ushirikiano na mradi huu umepokelewa na mkoa kwa sababu serikali inaamini nguvu ya wananchi


Katika uzinduzi huo pia ulifanyika uchaguzi wa kamati ya jamii ya wanashinyanga ya kusimamia mradi huo ambayo itasimamiwa na mwenyekiti aliyechaguliwa Joseph Ndatala ambaye amesema atafanya kazi kwa uaminifu na kamati yake ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Mgeni rasmi Chila Moses ambaye ni afisa Mipango na uratibu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, aliyemwakilisha katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary wakati wa uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy)
Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( community Philanthropy).
 Mkurugenzi wa shirika la TAI Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.
 Mkurugenzi wa shirika la TAI Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.
 
Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Afisa Mradi kutoka shirika la TAI. Paschalia Mbuguni akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo
Wajumbe wa kamati ya kusimamia kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii Joseph Ndatala akizungumza baada ya kuchaguliwa.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akichangia hoja juu ya mradi huo
Diwani wa kata ya Lubaga Reuben Dotto akichangia hoja kwenye uzinduzi wa mradi huo
Share:

CHUO CHA IFM CHAZUNGUMZIA TUKIO LA MOTO ULIOTOKEA CHUONI HAPO

Share:

WATANZANIA WATAKIWA KUYATUMIA MAKUMBUSHO KWA KULETA AJIRA NA KUJIFUNZA

Mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha Drt Gwakisa Kamatula akiwa pamoja na mgeni rasmi Mchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wageni wengine katika siku ya maadhimisho ya makumbusho duniani yaliyofanyika viwanja vya Azimio la Arusha .

Na Rose Jackson,Arusha

Watanzania wametakiwa kuyatumia Makumbusho kama njia mojawapo ya kuleta ajira na kujifunza Ikiwa ni pamoja na kuwa kielelezo muhimu katika historia ya nchi kwani yamebeba historia kubwa ya nchi ya Tanzania.


Hayo yamesemwa na Mchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Valeriani Vitalis wakati akiwa mgeni Rasmi katika kilele cha siku ya Makumbusho duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha yenye kauli mbiu isemayo 'Nguvu ya makumbusho katika kuelimisha na kuburudisha jamii'.


Amesema makumbusho yanaweza kuleta ajira kwani yana historia na elimu mbalimbali ambazo zina uwezo wa kuwafanya watanzania kuweza kujifunza na kujiajiri.


Ameeleza kuwa maeneo ya makumbusho yamesheheni historia mbali mbali za Taifa hivyo yanahitaji maboresho makubwa yanayo paswa kwenda na wakati ili yaweze kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema amefurahishwa na maboresho yanayoendelea katika Makumbusho hayo na kuongeza kuwa Makumbusho yakiboreshwa yatasaidia kuunga mkono kwa vitendo juhudi za baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage nyerere katika kutunza na kuenzi utamaduni wa Taifa.

Kwa upande wake mkurugenzi Makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt. Gwakisa Kamatula amesema makumbusho ni sehemu sahihi ya kuwarisisha na kuwafundisha vijana kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii kisiasa na kiuchumi.


Dkt Gwakisa ametoa rai kwa watanzania kutembelea makumbusho yaliyopo nchini ili kuweza historia na kujifunza urithi wa asili tuliorithi kwa vizazi vilivyotangulia nchi.


Kwa upande wao baadhi ya washiriki walioshiriki katika makumbusho hayo wamesema kupitia maadhimisho hayo wameweza kujifunza historia na elimu mbali mbali za makumbusho ya Taifa.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wanafunzi wa ngazi mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kujionea historia ya Taifa la Tanzania.

Share:

JINSI NILIVYOMKAMATA MCHEPUKO WA MKE WANGU KIRAHISI

Share:

EWURA YAWATAKA WAFANYABIASHARA WA GESI MAJUMBANI KUHAKIKISHA WANAKUWA NA MIZANI


Meneja wa Ewura Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Long'idu akitoa elimu ya gesi za majumbani kwa Wakala na Wasambazaji wa Gesi za Kampuni ya Taifa.


Na Rose Jackson,Arusha

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imewataka wauzaji wa gesi za kupikia kuhakikisha wanakuwa na mizani za kupima gesi kwani kutokuwa na mizani ni kosa la kisheria.

Hayo yamesemwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Long'idu wakati akitoa elimu kwa Wauzaji na wasambazaji wa gesi za kupikia majumbani semina iliyoandaliwa na kampuni ya taifa Gesi na kufanyika jijini Arusha.


Amesema kuwa ni kosa la kisheria wauzaji kuuza gesi bila kuwa na mizani hivyo wanapaswa kuhakikisha wanakuwa na mizani ili kuepuka hatua Kali za kisheria kwa wale watakaobainika kutokuwa na mizani hizo.


Aidha amedai kwa sasa bado wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao wanauza mitungi ya gesi bila kupima jambo ambalo ni kinyume na sheria kwani uzito unatakiwa kuonekana kabla ya mtumiaji kufikisha nyumbani na kuanza matumizi.


"Mwananchi unatakiwa kuhakikisha kuwa umeona muuzaji akiwa amepima na umejiridhisha kabisa kuwa ni kiwango hicho lakini Kama ni pungufu basi pia utaona", aliongeza Meneja huyo.


Aliongeza kuwa wafanyabiashara wa uuzaji wa mitungi hiyo ya gesi wakifuata sheria basi changamoto hizo za changamoto za ujazo hafifu zitaisha kabisa kwa wananchi.


aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanakuwa waaminifu na kuachana na tabia ya kupunguza gesi kwani endapo watakamatwa sheria itawafikisha mahakamani.


"Tulifanya msako Moshi na tumeshawafikisha mahakamani wafanyabiashara wawili niwaombe tu ninyi wafanyabiashara wanaofanya hivyo waache kwani ni hatari sana ndani ya jamii", aliongeza.

Naye Bw Joseph Nzumbi ambaye ni meneja mauzo wa Taifa Gesi alisema kuwa bado kwa mikoa ya Kaskazini kuna changamoto ya ujazaji wa mitungi ambayo imejazwa mitaani bila kufuata taratibu hivyo kuwa na hatari kwa watumiaji .


Amewataka wananchi kuangalia ujazo na kifuniko cha juu ambacho hakijafunguliwa pindi wanaponunua gesi ili kuweza kubaini gesi ambazo hazijachakachuliwa.


Share:

TAKUKURU YABAINI DOSARI UJENZI SHULE MPYA ZA USULE, BUTENGWA, KITUO CHA AFYA SALAWE, BARABARA MANISPAA YA SHINYANGA

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 20,2022
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 20,2022

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imebaini dosari katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya wasichana Butengwa, ujenzi wa barabara za changarawe zilizo chini ya TARURA katika Manispaa ya Shinyanga na ujenzi wa shule mpya ya Usule na ujenzi wa Kituo cha Afya Salawe katika halmashauri ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kazi zilizofanywa na TAKUKURU katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 (Januari – Machi 2022) leo Ijumaa Mei 20,2022 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa amesema miradi hiyo ni sehemu ya miradi 18 ambayo TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha shilingi 13,794,801,486/= zilizotolewa na Serikali.

“TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za serikali katika miradi ya maendeleo 18 mkoani Shinyanga yenye thamani ya shilingi 13,794,801,486/= iliyoletewa fedha za Serikali ambayo ni miradi sita ya sekta ya afya, mitano sekta ya miundombinu, miwili elimu na mitano sekta ya maji. Kati ya hiyo 18 minne ilikuwa na dosari na 14 haikuwa na dosari”,amesema Mussa.


“Kati ya miradi mine iliyokuwa na dosari miradi mitatu dosari zake zilikuwa ndogo kiasi kwamba TAKUKURU ilitoa ushauri wa namna ya kuzifanyia marekebisho dosari husika kwa mamlaka husika”,ameeleza.

Ameitaja miradi iliyobainika kuwa na dosari ndogo ndogo ni mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Butengwa Manispaa ya Shinyanga, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Usule halmashauri ya Shinyanga, ujenzi wa Kituo cha Afya Salawe katika halmashauri ya Shinyanga na ujenzi wa barabara za changarawe zilizo chini TARURA Manispaa ya Shinyanga.


“Baadhi ya dosari zilizobainika kwenye mradi wa barabara baadhi ya maeneo katika barabara ya Bugweto – Ipeja kutokuchongwa na kushindiliwa vizuri,baadhi ya maeneo ya pembeni katika barabara ya Butengwa – Ning’wa kuharibika mapema kutokana na kutokushindiliwa vizuri na kutengenezwa wakati wa mvua”,amefafanua.

“Kwenye mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Butengwa tulibaini msingi ulichimbwa kwenda chini urefu wa sentimita 70 badala ya sentimeta 90 kama BOQ inavyoonesha na kwenye mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Usule tulibaini kutokuwekwa njia za kupita watu wenye ulemavu kwenye baadhi ya majengo. Kwa upande wa ujenzi wa Kituo cha afya Salawe tulibaini dosari katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambapo uchunguzi umeanzishwa”,ameongeza Mkuu huyo wa TAKUKURU.

Amesema miradi 18 iliyokaguliwa bado utekelezaji wake unaendelea na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na mmoja umeanzishiwa uchunguzi na kwamba wametoa elimu ya utekelezaji bora wa miradi hasa inayotumia Force Account kwenye maeneo ya uandikaji wa kumbukumbu za manunuzi,utunzaji nyaraka za miradi na utunzaji vifaa vya ujenzi.

Katika hatua nyingine amesema Dawati la uchunguzi la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga limepokea taarifa 48 za malalamiko ambapo zinazohusu Rushwa ni 35 na tayari 17 uchunguzi wake unaendelea, 13 umekamilika na 5 uchunguzi wake umefungwa kwa kukosa ushahidi.


“Kesi zinazoendelea mahakamani ni 18 kati ya hizo kesi mpya ni tatu na katika kipindi cha mwezi Januari – Machi kesi 6 ziliamuliwa mahakamani na kesi 4 zilishinda kwa watuhumiwa kutiwa hatiani na kulipa faini”,amesema Mussa.


Mussa amesema kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni 2022 TAKUKURU mkoa wa Shinyanga imepanga kukamilisha majukumu yake kwa kufanya uchunguzi na kujielekeza zaidi kwenye ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa thamani halisi ya fedha iliyoletwa.


Ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha miradi yote inayoendelea ikamilike kwa ubora na kama wataona vitendo vyovyote vinavyoashiria mashaka/ ubadhilifu wa miradi hiyo watoe taarifa kwa kufika Ofisi za TAKUKURU zilizopo Shinyanga au wapige simu namba 0738150196 au 0738150197 , Ofisi ya TAKUKURU Kahama 0738150198 na Ofisi ya Kishapu 0738150199




Share:

MBUNGE LUGANGIRA:’KONGOLE KWA WABUNIFU WA NELSON MANDELA’



Mbunge wa Viti Maalum Asasi za Kiraia na Mashirika yasio ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira (Kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Kilimo, Sayansi ya Chakula na Usalama wa Lishe (CREATES-FNS) Bibi. Rose Mosha akielezea kuhusu bidhaa za Nutrano, Omega 3 na Super Grow wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu tarehe 19 Mei, 2022 jijini Dodoma.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (Kushoto) akipata maelezo kuhusu ugali Cooker ubunifu uliofanywa na Mwanafunzi wa Shahada ya Umahili kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Tuse Mwasambili (kulia) alipotembelea banda la Chuo hicho tarehe 19 Mei, 2022 jijini Dodoma.


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (kulia) akiangalia bidhaa ya Uji Tayari wenye Virutubisho (Instant Porridge) ulioandaliwa na Bi. Rufina Fredrick wakati wa maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo tarehe 19 Mei,2022 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Ndg. Waziri Salum (Kulia) akimsikiliza Mbunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Philipina Shayo katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo tarehe 19 Mei, 2022 Dodoma.


. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (mwenye koti la kijivu) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanafunzi walioshiriki maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania leo tarehe 19 Mei,2022 jijini Dodoma (Caption na Lorietha Laurence:NM-AIST).

.......................................................

Na Lorietha Laurence:NM-AIST, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalum Asasi za Kiraia na Mashirika yasio ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira ametoa kongole kwa wabunifu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kuzalisha bidhaa za kuimarisha lishe.

Ametoa pongezi hizo leo 19 Mei, 2022 alipotembelea banda la taasisi hiyo uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania ambapo alipata maelezo kuhusu bidhaa za Nutrano na Omega 3 zinazaotatua matatizo ya utapiamlo: Buheri wa Afya inayotatua magonjwa nyemelezi na Super Grow chakula cha Samaki.

“bidhaa ni nzuri na zimejikita zaidi katika kuimarisha lishe ,natamani bidhaa hizi zingawafikia walengwa hususani mikoa ambayo imeadhiriwa na utapiamlo” alisema Mhe. Neema

Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Kilimo, Sayansi ya Chakula na Usalama wa Lishe (CREATES-FNS) kilichopo chini ya taasisi hiyo Bibi. Rose Mosha ameahidi kufanyia kazi ushauri huo ili kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Bibi. Rose alieleza kuwa bidhaa hizo zimefanyiwa tafiti na wanafunzi wa NM-AIST waliofadhiliwa masomo yao na kituo hicho ikiwa ni kusimamia kauli mbiu ya Elimu kwa Jamii na Viwanda ( Academia for Society and Industry) kwa kuangalia changamoto zinazoikabili jamii na kuzifanyia tafiti kisha kutoa suluhisho.

Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw. Waziri Salum amewataka wabunifu hao kutumia fursa ya kuomba ufadhili kupitia programu za ufadhili unaotolewa na Mamlaka hiyo ili kuzifanya bunifu hizo kwenda mbele zaidi.

“tumie fursa ya kuomba ufadhili kupitia programu za ufadhili zinazotolewa na ofisi za TEA ambazo hutangazwa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo ili kuendeleza bunifu zenu ” alisema Mkurungezi wa Miradi Ndg. Waziri

Ameongeza kuwa , baadhi ya wabunifu ni wanufaika wa ufadhili huo akiwemo Mbunifi wa Chujio la Maji la Nanofilter Profesa Askwar Hilonga ambaye mara kwa mara amekuwa akipata ufadhili kupitia ubunifu wake huo uliosaidia jamii ya watu wa Arusha kupambana na magonjwa ya tumbo pamoja na kutoa ajira kwa wanawake na vijana 130.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela imefanikiwa kuleta wabunifu 18 wakiwa na bunifu mbalimbali ikiwemo Ugali Cooker, Mfumo wa kumsaidia mtu asiyeweza kuona, bidhaa za Tunda la Kweme, unga wa virutubisho, chujio la maji la nanofilter, mfumo wa kuchuja maji taka, buheri wa afya, Nutrano , Omega na nyinginezo nyingi.
Share:

Thursday, 19 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 19,2022


Magazetini leo Alhamisi May 19,2022


Share:

BENKI YA EQUITY YAZINDUA KAMPENI YA ‘ISHI KISASA PESA MZIGO’'


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya Equity (T) Isabella Maganga ( katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Ishi Kisasa Pesa Mzigo'. Kampeni hiyo inahamasisha utumiaji wa huduma za Kibenki kidijitali kama njia mbadala wa kupata huduma za kibenki pamoja Shughuli zote zinaweza kutatuliwa kwa wakati na kwa usalama kwa kukamilisha miamala yao na malipo kwa kutumia simu zao kiganjani, kadi zao za benki na Internet Banking popote pale walipo. Kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Malipo, Victor Wairimu na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Grace Magige.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya Equity (T) Isabella Maganga ( katikati), Meneja Mwandamizi Kitengo cha Malipo, Victor Wairimu na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Grace Magige wakizidua Kampeni ya 'Ishi Kisasa Pesa Mzigo'. Kampeni hiyo inahamasisha utumiaji wa huduma za Kibenki kidijitali kama njia mbadala wa kupata huduma za kibenki pamoja Shughuli zote zinaweza kutatuliwa kwa wakati na kwa usalama kwa kukamilisha miamala yao na malipo kwa kutumia simu zao kiganjani, kadi zao za benki na Internet Banking popote pale walipo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Equity wakipiga picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger