Friday, 18 March 2022

ASASI ZA KIRAIA ZAJENGEWA UWEZO KUHUSU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA PEPFAR


Leo tarehe 16 Machi 2022 viongozi wa bodi na wasimamizi wakuu wa asasi za kiraia 36 kutoka asasi 5 nchini Tanzania wamepewa mafunzo jijini Arusha kuhusu utawala na uongozi bora ili kuweza kutekeleza miradi ya PEPFAR na kuimarisha usimamizi wa mashirika yao.

Hili ni hitimisho la mafunzo haya kwa meneja mradi, wasimamizi wa fedha na wajumbe wakuu wa bodi 108 kutoka asasi za kiraia 18 katika mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Morogoro, Njombe, Ruvuma na Shinyanga.

 Mafunzo haya yameandaliwa na FHI 360 kupitia mradi wa EpiC kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Mafunzo haya kwa mameneja miradi na wajumbe wakuu wa bodi za asasi za kiraia yamekuja baada ya kufanyika upembuzi yakinifu katika asasi hizi na kuonekana kwamba kuna umuhimu wa kuzipatia mafunzona kuzi Imarisha katika maeneo yote ya usimamizi wa miradi hasa eneo la utawala na uongozi bora kama ilivyo onekana katika matokeo ya upembuzi yakinifui “readiness review” yaliyofanywa ili kutambua uwezo wa asasi za kiraia katika nyanja mbalimbali.

Hatua hii ni utekelezaji wa lengo la nne la mradi wa EpiC “Kuzijengea uwezo asasi za kiraia na kuziwezesha kupata ufadhili wa moja kwa moja kutoka kwa wafadhili pamoja na utekelezaji wa miradi ya PEPFAR.”

“Wafadhili hawawezi kuweka hela nyingi kwenye mashirika yasiyo wajibika. Wajumbe wa bodi, wakurugenzi na meneja ni lazima kuwajibika kwenye mambo yote katika shirika.” Alisema Bernard Ogwang, Mkurugenzi wa Mradi wa EpiC.

Wakurugenzi na meneja wa mashirika, wasimamizi wa fedha na wajumbe wakuu wa bodi mbali na kuhudhuria mafunzo haya ya utawala na uongozi bora, pia wamekutana na wakuu wengine kutoka kwenye asasi za kiraia mbalimbali ambapo wameshirikishana uzoefu wa namna bora ya kuongoza na kutekelezaji miradi ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.

“Niko kwenye bodi kwa zaidi ya miaka kumi ila hatujawahi kupata mafunzo ya utawala na uongozi bora. Mafunzo haya yameleta chachu na mwanga, yatabadili utekelezaji wetu ikiwemo uwajibikaji wa bodi na kufuatilia utekelezaji wa miradi.” alisema Juma Mwesigwa, Mkurugenzi wa asasi ya HUHESO.

EpiC ni mradi wa kimataifa wa miaka mitano unaotekelezwa na shirika la FHI360 kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), uliojikita katika kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Hii ni kupitia kutoa msaada wa kitaalamu na huduma za moja kwa moja katika kuondoa vikwazo vilivyopo kufikia 95-95-95, na kuhamasisha usimamizi wa kujitegemea wa miradi ya VVU/UKIMWI kitaifa kwa kuboresha programu za utambuzi wa hali ya maambukizi ya VVU, kinga, matunzo na tiba.

Share:

MIKIDADI ASHINDA MILIONI 10 ZA BIKO


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kushoto akifurahia tukio la kumkabidhi Nuru Mikikadi (katikati) Sh Milioni 10 zake alizoshinda kwenye droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Biko iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulia ni Flamiana Msilu, Meneja Uhusiano wa CRDB Tawi la Premier lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga picha Wetu.
Mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Nuru Mikidadi, akifurahia pesa zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko droo iliyofanyika Jumapili iliyopita. Makabidhiano ya fedha zake yalifanyika katika benk ya CRDB, Tawi la Premier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Nuru Mikidadi, akifurahia pesa zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko droo iliyofanyika Jumapili iliyopita. Makabidhiano ya fedha zake yalifanyika katika benk ya CRDB, Tawi la Premier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu.
Share:

Thursday, 17 March 2022

MRADI WA MAJI KIBARA WAWAONDOLEA ADHA WANANCHI KUTEMBEA KM 30 KUFUATA MAJI ZIWANI


Mradi wa Maji Kibara
Meneja RUWASA wilaya ya Bunda,William Boniface


Na Dinna Maningo,Bunda.

WANANCHI kijiji cha Kibara kata ya Kibara wilayani Bunda mkoa wa Mara,wamepata huduma ya maji ya bomba ambapo awali walilazimika kutembea umbali km 30 kufuata maji Ziwa Victoria na hivyo kuathiri shughuli zao za kijamii.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari,Mwenyekiti wa kamati ya Jumuiya ya watumiaji wa maji kata ya Kibara,Robert Mgono alisema kuwa mradi wa maji Kibara ulianzishwa 1972 na ulistisha kutoa maji baada ya miundombinu ya maji kuchakaa.

"Wateja wanaotumia maji ya bomba ni 263 bado maeneo mengine hayajasambaziwa maji wanachota kwenye  vituo mbalimbali vinavyotoa huduma ya maji na wengine wanachota kwenye visima vya asili,mradi ulisimama baada ya miundombinu kuchakaa tunaipongeza Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)wametujengea mradi na maji yamesambwazwa kwenye vituo 29 vya kutolea maji", alisema Mgono.

Mkazi wa kijiji hicho Lucy Paul alisema kuwa upatikanaji wa huduma hiyo ya maji umewezesha kufanya shughuli za kilimo kwa wakati kulima bustani za mbogamboga kwakuwa kuna maji ya kutosha kumwagilia,aliomba kuongezwa kwa vituo vingine vya maji  na kuyasambaza majumbani ili kuwafikia wananchi wote.

Fundi Mradi Evodis Rwegasha alisema kuwa bado kuna changamoto ya mapato yatokanayo na huduma ya maji kwakuwa watu wengi wamechimba visima na wanachota maji ya bomba pindi tu kunapotokea kiangazi baada ya visima kukauka hali ambayo inashusha mapato ya fedha kwakuwa shughuli zote za uendeshaji wa mrandi yakiwemo malipo ya umeme na malipo mengine hutegemea fedha ambazo wananchi hulipa wakati wanapochota maji.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi William Boniface,alisema kuwa mradi wa maji Kibara unahudumia watu 21,000 umegharimu sh. Milioni 558,kuna vituo 29 vya maji,nakwamba katika mwaka wa fedha 2021/2022 wilaya hiyo ya Bunda imepatiwa Bilioni 5.9 kutekeleza miradi ya maji 15 ambayo itakamilika juni 20,2022.
Share:

TCCIA MWANZA YAKUTANA NA WANACHAMA WAKE KUPOKEA MAONI


Mwandishi wetu -Mwanza

Chemba ya wafanyabishara wenye viwanda na kilimo TCCIA Mkoa wa Mwanza imekutana na wanachama wake na kupokea maoni ya kuboresha utendaji kazi wake

Mwenyekiti wa TCCIA Mwanza Gabriel Mugimi ameiambia Malunde 1 Blog kuwa, dhamira ya kikao hicho ni kupokea maoni toka kwa wanachama wake ili kuweza kubaini changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabishara na wakulima Mkoa wa Mwanza.

Mugimi aliongeza kuwa, kazi ya TCCIA ni kuhakikisha wanachama wake wanakuwa na elimu pana juu ya sheria zinazosimamia biashara na kilimo Nchini Tanzania kwani kujua sheria husika ni jambo la muhimu sana.

"Tuna imani kuwa, kupokea maoni na ushauri toka kwenu wanachama kutasaidia kuifanya taasisi yetu ya TCCIA kuwa imara na yenye nguvu",alisema.

Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo waliibuka changamoto mbalimbali zikiwemo umuhimu wa elimu kwa wafanyabishara na maafisa wa mamlaka za serikali.

Justine Nelson kutoka taasisi ya Victoria Polybags alisema kuwa, kuna changamoto kubwa ya utozwaji wa kodi toka kwa maafisa wa TRA kwani inachangia kuua biashara badala ya kuendeleza.

Naye Bakari Kaoabi Mwenyekiti wa wavuvi ziwa Victoria alisema kuwa, baadhi ya sheria za uvuvi zinarudisha nyuma jitihada kukuza uchumi wa Nchi.

Pia alibainisha kuwa kuingiliana kwa wizara ndani ya sekta ya uvuvi kunarudisha nyuma jitihada za kukuza uvuvi Nchini hivyo ni vyema TCCIA Mkoa wa Mwanza ikaingilia kati.

Kikao hicho kilihusisha wanachama wa TCCIA wa Mkoa wa Mwanza na kimefanyika kwenye ukumbi wa Nyanza Jijini Mwanza.
Share:

Wednesday, 16 March 2022

TaSUBa YAELEZEA MAFANIKIO YAKE NDANI YA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA MADARAKANI

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani

******************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeeleza mafanikio waliyoyapa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madaraka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akieleza mafanikio hayo Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye amesema mambo mengi yafanyika katika taasisi hiyo na yenye tija kwa jamii ambapo katika mwaka mmoja huo Taasisi imepata fedha ya Maendeleo kutoka serikalini kwa ajili ya ukarabati wa majengo kiasi cha shilingi Milioni 150 pamoja na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kiasi cha shilingi milioni 100.

"Tumepata hiyo fedha tumeboresha miundombinu na tumeongeza miundombinu kwa maana hiyo pia hata udahili wa wanachuo umeongezeka kwasababu mwaka huu wa masomo 2021/22 tumedahiri takribani anachuo 695 lakini wale ambao wamefika na kujisajili ni 533 kulinganisha na huko nyuma ambapo kipindi ambacho tulidahili wanachuo wengi hawakuzidi 350". Amesema Dkt.Makoye

Amesema Royal Tour imechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza Taasisi hiyo ndani na nje ya nchi kwa kuwa TaSUBa ilikuwa moja ya sehemu ambazo utayarishaji wa documentary ya kutangaza nchi na vivutio vyake ilifanyika.

"Ndani ya mwaka huu mmoja tayari Rais ameshafika kwenye taasisi yetu katika zoezi la kurekodi filamu ya Royal Tour, kwa upande wetu tulifarijika sana kwasababu hii nchi ni kubwa lakini Rais aliona ni vyema kufika kwenye taasisi yetu". Amesema

Dkt.Makoye amesema Tamasha kubwa la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililofanyika Novemba, 2021 lilikuwa na mafanikio makubwa, lilivutia watazamaji takribani 70,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema katika Tamasha hilo la Sanaa na Utamaduni takribani vikundi 80 vya ndani ya nchi yetu vilikuja kushiriki na vingine vitano kutoka nje ya nchi virishiki , vilikuja vichache kutoka nje ya nchi kutokana na janga la Uviko 19.

Pamoja na hayo Dkt.Makoye amesema Taasisi hiyo inamategemeo makubwa kwasababu ukiangalia hata kwa upande wa fedha wanazoletewa kutoka serikalini nayo imeongezeka.

Share:

MBARONI KWA KUMUUA MAMA NA MWANAYE KISHA KUWACHOMA MOTO




Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Ali Makame Hamadi

Watu wawili ambao ni Dutu Maige (30) na Yusuph Sitta (32) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Katavi kwa tuhuma za kumuua mama na mtoto wake mwenye umri wa miezi minne kisha miili yao kuifukia kwenye shimo katika pori la Kalilankulu lililopo wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.

Akitoa taarifa kwa njia ya maandishi Kamanda wa Polisi Mkoa Ali Makame Hamadi ameseme walipokea taarifa Machi 8 mwaka huu kutoka kwa Paschal Masheku mkazi wa kijiji cha Sante Maria kuwa binti yake huyo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu Julai 2021 akiwa amebeba mtoto wake.

Kamanda Hamad amesema baada ya taarifa hiyo walianza upelelezi wa kina ambapo Machi 9, 2022 walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao waliohusikana na tukio hilo.

Akiendelea kuelezea tukio hilo amesema mtuhumiwa ni mume wa marehemu na walizaa mtoto mmoja na chanzo cha tukio hilo ni kugombea mpunga ambao ni gunia 60 na walikuwa wakishtakiana mara kwa mara kwa watendaji wa kijiji ili kujua nani mmiliki halali wa mpunga huo.

Pia amesema awali miili ya marehemu hao ilikutwa kwenye pori ikiwa imeharibika kwa kushambuliwa na fisi na baadae ilifanyiwa uchunguzi na madaktari wa magereza kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kuzikwa.

Watuhumiwa hawakuishia hapo baada ya mazishi yaliyofanywa na jeshi la polisi,wao warirudi tena baadae na kufukua miili ya marehemu kisha kuichoma moto na kuipeleka sehemu nyingine ili kupoteza ushahidi.

Chanzo - EATV
Share:

VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA KUTANGAZA KUPITIA SHIRIKA LA NDEGE EMIRATES KUTAZAMWA NA ABIRIA WAPATAO MILIONI 90.2

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas kuhusu kuitumia ndege hizo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo husafirisha abiria milioni 90.2 kwa kila mwaka, Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya Shirika hilo lililopo katika Mji wa Dubai, Wa pili kulia ni Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz pamoja na Balozi mdogo wa Tanzania Dubai, Idd Bakari.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas jinsi vivutio vya utalii vya Tanzania vitajulikana klupitia ndege hizo kwani Emirates husafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka, Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya Shirika hilo lililopo katika Mji wa Dubai, Wa pili kulia ni Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Dubai, Idd Bakari


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akimuonesha picha ya baadhi ya vivutio vya utalii vya Zanzibara Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kuona picha ukutani ya Zanziba iliyowekwa katika Ofisi za makao makuu ya Shirika la ndege la Emirate , wa kwanza kulia ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai , Mhe. Idd Bakari



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas kuhusu kuitumia ndege hizo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania mara baada ya kufanyika kwa mkutano leo katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Dubai, Wa pili kulia na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo.
Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Idd Bakari


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada mkutano uliofanyika baina yao wa kutangaza vivutio vya utalii kupitia ndege za Emirates. Wa pili kulia na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hiloMuhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Bakari Iddy

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kufanyika mkutano wa kuitumia ndege za Shirika hilo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo hunasafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka,


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungmza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kufanyika mkutano wa kuitumia ndege za Shirika hilo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo hunasafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka,


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada mkutano uliofanyika baina yao wa kutangaza vivutio vya utalii kupitia ndege za Emirates. Wa pili kushoto na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Bakari Iddy


............................................................


Mwandishi Wetu, Dubai.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ambapo vivutio hivyo vya utalii vitaweza kutazamwa na abiria wapatao milioni 90.2 ambao husafiri kila mwaka kwa kutumia ndege hizo



Aidha, Dkt.Ndumbaro amesema Tangazo hilo litakuwa likitazamwa na mamilioni ya abiria hao kila wakati ndege za Shirika hilo zitakapokuwa zikiruka (take off)


Dkt. Ndumbaro amebainisha hayo leo katika Mji wa Dubai alipokutana viongozi wa Shirika hilo ambalo mbali ya kusafirisha abiria milioni 90.2 duniani kote pia husafirisha abiria wapatao milioni 20 ambao huunganisha ndege nyingine


Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kutaandaliwa makala tano (Documentaries ) za kuelezea vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Zanzibar, Serengeti, Ngorongoro pamoja na Mlima Kilimanjaro

'' Shirila la ndege la Emirates ni Shirika kubwa sana Duniani lengo letu kama nchi ni kuhakikisha abiria wapatao milioni 90.2 wanaviangalia vivutio vyetu kisha wanavipenda halafu wanatembelea Tanzania'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro



Katika mazungumzo hayo amesema Uongozi wa ndege hizo umeonesha utayari wa kushirikiana katika kuitangaza Tanzania kiutalii na ifika mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wataingia makubaliano (MOU) baina ya Tanzania na Shirika hilo

Akifafanua mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro amesema kati ya abiria watakaoangalia vivutio wengi wao watavutiwa na hatimaye sehemu ya watu hao waweze kuja kutembelea Tanzania


" Shabaha yetu kubwa kama nchi ni kuhakikisha tunafikia watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025, Tunaamini tutalifikia lengo hilo" amesisitiza Dkt.Ndumbaro

Ameongeza kuwa Tanzania inategemea utalii wake wa Wanyamapori kwa asilimia 100 hivyo kupitia mkakati wa kutumia wa kutangaza vivutio vingine vya utalii kama vile utalii wa fukwe, utalii wa utamaduni pamoja na utalii wa ikolojia utaweza kujulikana dunia kote na kuwa chachu ya watalii wengi kuanza kumiminika nchini Tanzania.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas amesema Shirika la Emirate lipo tayari kufanya kazi na Tanzania katika kuhakikisha vivutio vya utalii vya Tanzania vinajulikna pande zote za Dunia

'' Tutakapofikia makubaliano tutahakikisha pia matangazo ya vivutio vya Utalii wa Tanzania vinawekwa kwenye Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii ikiwemo facebook, instagram pamoja na twitter ya Shirika hili ambayo imekuwa ikifuatiliwa na watu wengi Duniani,

Kwa upande wake, Balozi Mdogo wa Dubai, Mhe. Idd Bakari amesema mazungumzo yamekuwa na tija na hivyo kupitia Shirika hilo idadi ya watalii itaongezeka kupitia matangazo yatakayokuwa yakiruka wakati ndege za Shirika hilo zitapokuwa zikiruka

'' Mazungumzo haya baina yetu na Shirika la Emirates yataipaisha Tanzania vivutio vya utalii vitaweza kujulikana Duniani kote kuwa vipo Tanzania na hivyo watalii wengi watweza kuitembelea Tanzania

Katika mazungumzo hayo Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Balozi Mdogo wa Tanzania, Mhe.Idd Bakari
Share:

DKT. MABULA ATAKA SEKTA YA ARDHI KUPEWA KIPAUMBELE


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 15 Machi 2022Sehemu ya washiriki wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila iliyofanyika katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 15 Machi 2022.Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (KOICA) Kyuchoel Eo akizungumza wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 15 Machi 2022.Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Benelith Mahenge akizungumza wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida tarehe 15 Machi 2022.Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (KOICA) Kyuchoel Eo akitoa hati kwa baadhi ya wananchi wa Ikungi wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila uliofanywa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mkoani Singida tarehe 15 Machi 2022.

*****************

Na Munir Shemweta, WANMM SINGIDA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Ageline Mabula amewataka wananchi kuipa kipaumbele sekta ya ardhi kwa kuwa sekta hiyo ikitumiwa vizuri itawezesha kuchochea mapinduzi kichumi.

Aidha, aliwataka wananchi na taasisi zote zinazomiliki ardhi nchini kuhakikisha zinatimiza wajibu wa kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka kwa maendeleo endelevu.

Dkt Mabula alisema hayo tarehe 15 Machi 2022 wakati wa hafla ya utoaji hatimiliki za kimila kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Zaidi ya hati 5,050 zimeandaliwa kupitia mradi wa matumizi ya ardhi uliotekelezwa kwa pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women) na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (KOICA).

‘’Mimi na Wizara yangu tunaamini kuwa ardhi ikitumiwa vyema kwa maana ya kupangwa, kupimwa na kumilikishwa itawezesha kuchochea mapinduzi makubwa na ya haraka ya kiuchumi kwa mwananchi mmoja mmoja kwenye mikoa yetu na taifa kwa ujumla’’ alisema Dkt Mabula.

Waziri wa Ardhi aliwaambia wananchi wa Ikungi waliopokea hati katika hafla hiyo kuwa, wamenufaika kwa kupata nyaraka za kumiliki ardhi alizoziekeza kuwa zina faida kubwa katika maisha yao ya kila siku.

Alitaja baadhi ya manufaa hayo kuwa, ni kuwa na usalama wa miliki za ardhi, uhakika wa milki, kupunguza migogoro na kutumia hatimiliki kama dhamana katika taasisi mbalimbali kama vile taasisi za fedha, vyombo vya kisheria sambamba na kupandisha thamani ya ardhi.

‘’ Nitoe rai kwa wananchi wote kuwa na tabia ya kutumia na kuchangamkia fursa kama hizi zinapotokea katika maeneo yetu ili kuweza kupata manufaa kama haya’’ alisema Dkt Mabula.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida Justice Kijazi alisema, mradi wa uandaaji na utekelezaji mpango wa matumizi bora ya ardhi uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Japan (KOICA) katika halmashauri yake ulifanikisha kuandaliwa kwa hati za kimila 5,050 na ulilenga kunufaisha wananchi wa Ikungi hasa wanawake na wasichana.

‘’ Halmashauri yetu ya Ikungi ina jumla ya vijiji 101 na kati ya hivyo vijiji 68 tayari vimepimwa huku vijiji 28 vikiwa vimefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi na tayari hati 5,050 zimeshakamilika kwa ajili ya kupatiwa wananchi’’ alisema Kijazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Japan (KOICA) nchini Tanzania Kyuchoel Eo alisema Shirika lake litaendelea na juhudi za kusaidia wanawake na wasichana katika wilaya ya Ikungi ikiwa ni mikakati yake ya kuunga mkono usawa wa jinsia katika masuala ya ardhi.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Benelith Mahenge alieleza umuhimu wa upangaji na upimaji ardhi katika mkoa wake kwa kueleza kuwa ardhi ni jambo la msingi kwa kuwa kila kiumbe duniani kinaitegemea.

‘’Viumbe vyote vinategemea ardhi na sote ni mashahidi migogoro inayoongoza ni ya matumizi ya ardhi na kwa bahati mbaya ardhi haiongezeki hivyo tukipata miradi kama hii tutatatua au kupungiuza migogoro ya ardhi’’ alisema Mahenge.
Share:

Tuesday, 15 March 2022

Dkt. TAX AELEZA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA YA WIZAYA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax akiwa kwenye kikao na Waandishi wa habari katika ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma ambapo ameeleza mafanikio ya Mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita katika Wizara hiyo ikiwemo kuimarisha ulinzi wa mipaka ya Tanzania.

Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 Blog-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja wa awamu ya sita imeingia kwenye mafanikio mengi ikiwemo kuhakikisha kuwa nchi ipo salama na amani inalindwa na kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi. 

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax katika kikao chake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita tangu Rais Samia Suluhu Hassan aliposhika madaraka ya kuiongoza Tanzania. 

Amesema,Licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo ,Wizara hiyo imeendelea kuwa kinara  kwenye utoaji mafunzo ya kijeshi katika Vyuo na shule za kijeshi ndani na nje ya nchi,utoaji mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa JKT na utoaji huduma za matibabu kwa wanajeshi na familia zao ,vijana wa JKT,watumishi wa Umma na wananchi.

"Tunaendeleea kustawi pia katika uhawilishaji wa Teknolojia kwa ajili ya kuzalisha mazao ya msingi,udumishaji wa ushirikiano kitaifa na kimataifa katika sekta ya ulinzi,utatuzi wa migogoro ya ardhi,ujenzi wa makao makuu ya ulinzi wa taifa na utoaji wa kipaumbele katika uendelezaji miradi ya kielelezo na kimkakati na ulipaji madeni ya wazabuni waliotoa huduma mbalimbali,"amesema.

Amefafanua kuwa kama lilivyo jukumu la Wizara hiyo katika kulinda taifa dhidi ya maadui toka ndani na nje ya nchi,itahakikisha nchi inakuwa salama na kulinda amani ikiwa ni pamoja na kuimarisha mshikamano baina yake na wananchi wake.

Amesema,Kwa kipindi cha mwaka mmoja, Serikali imeiwezesha Wizara hiyo kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa weledi,umakini na mafanikio hivyo kuwezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kulipa madeni yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 175 kwa wazabuni waliotoa huduma mbalimbali.

"Hii imejenga imani kwa Serikali na kuiwezesha Wizara kuendesha majukumu yake ya msingi kwa ufanisi,na tutaendelea kusimama zaidi katika kulinda amani ambapo wizara hii kupitia JWTZ inaendelea kuondoa changamoto chache katika baadhi ya mipaka hususani Kusini na hivyo tupo salama,"amefafanua Waziri huyo.

Akifafanua kuhusu migogoro ya ardhi iliyotatuliwa na Wizara hiyo ambayo inahusisha maeneo ya jeshi na wananchi ,Dkt.Tax amesema migogoro ipatayo 74 tayari imeshughulikiwa huko Arusha.

Kadhalika Serikali pia imeendelea kudumisha ushirikiano wa kimataifa na kitaifa kupitia sekta ya ulinzi hususani kushirikiana na umoja wa mataifa (UN),Umoja wa Afrika(AU)na Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC)katika operesheni mbalimbali za Ulinzi wa amani kwa kupeleka vikosi na usaidizi,waangalizi wa Jeshi na makamanda katika nchi zenye migogoro.

"Chini ya Serikali ya awamu ya sita , JWTZ linavyo vikosi vya Ulinzi wa amani katika nchi za Lebanon,Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo na Jamhuri ya kati,Jeshi hili pia linashiriki katika kamisheni ya SADC (SAMIM)katika kupambana na ugaidi huko Msumbiji,"ameeleza

Pamoja na hayo ameeleza kuwa ili kuwa na Taifa imara , Serikali imeendelea kutoa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa mujibu wa sheria na vijana wa kujitolea kwa lengo la kujenga uzalendo na ukakamavu ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi adhima ya kuwajengea vijana stadi na uwezo wa kujitegemea.


Share:

ANUSURIKA KUFA KWA KUPIGWA CHUMA KICHWANI NA MKEWE...AZINDUKA NA KUSAMEHE HOSPITALINI


Mwanamke aitwae Zainabu Mahomoka 35 ambaye ni Mkulima kutoka kijiji cha Makonjiganga Wilayani Liwale mkoa wa Lindi amenusurika kushitakiwa Mahakamani kwa kosa la kumjeruhi Mumewe aitwae Hemedi Nyanyweleka kwa kumpiga na chuma kichwani.

Tukio hilo lililotokea March 4 2022 mchana kutokana na ugomvi kati ya wanandoa hao huku chanzo kikielezwa kuwa ni ulevi uliopindukia wa Mume huyo ambako kulimpa hasira Zainabu na kumpiga Hemedi na chuma kichwani kulikomsababishia kupoteza fahamu.

Akiwa Hospitali baada ya kuzinduka Hemedi alipoelezwa kuwa Mke wake anatakiwa kufunguliwa mashtaka Mahakamani ili kujibu shitaka la kujeruhi…. Mwanaume huyu aliomba asipelekwe Mahakamani kujibu shtaka hilo kwani amemsamehe.
Share:

WAFANYABIASHARA MKOANI DODOMA WAHIMIZWA KWENDA KUFANYA MAKADIRIO NA KULIPA KODI ZAO STAHIKI


Afisa Msimamizi Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Edwin Iwato (kushoto) akimuelimisha Mfanyabiashara wa vipuri vya magari na vilainishi kuhusu kwenda kufanya makadirio ya kodi mapema ikiwemo kutoa risiti za kodi za kielektroniki za (EFD) wakati alipomtembelea katika duka lake lililopo katika barabara ya Bahi mjini Dodoma wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Maya Magimba (kulia) akimuelimisha Mfanyabiashara wa vipuri vya magari na vilainishi kuhusu kutundika Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) katika sehemu ya wazi wakati alipomtembelea katika duka lake lililopo katika barabara ya Bahi mjini Dodoma wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Enny Mwanga (kulia) akimuelimisha Mfanyabiashara wa vipuri vya magari na vilainishi kuhusu umuhimu wa kutoa risiti za kodi za kielektroniki za (EFD) kwa wateja anaowauzia bidhaa wakati alipomtembelea katika duka lake lililopo katika barabara ya Bahi mjini Dodoma wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Philipo Eliamini (kushoto) akichukua taarifa kutoka kwa Mfanyabiashara wa vipuri vya magari na vilainishi wakati alipomtembelea katika duka lake lililopo katika barabara ya Bahi mjini Dodoma wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Barnabas Masika (kulia) akiwaelimisha Wafanyabiashara wa vipuri vya magari na vilainishi wakati alipowatembelea katika maduka yao yaliyopo katika barabara ya Bahi mjini Dodoma wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.


Na Mwandishi Wetu-DODOMA.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka Wafanyabiashara mkoani Dodoma ambao mpaka sasa hawajafanyiwa makadirio kufika mapema katika ofisi za TRA kwa ajili ya kufanyiwa makadirio na kulipa kodi zao za malipo ya kodi katika Awamu ya Kwanza.

Wito huo umetolewa jana mjini Dodoma na Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa TRA, Bw. James Ntalika wakati wa mwendelezo wa Kampeni ya Utoaji Elimu kwa Mlipakodi ya kuwatembelea Wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi maarufu kama “Mlango Kwa Mlango” yenye lengo la kuwapatia elimu ya kodi ikiwemo kusikiliza na kuzitatua kero zao.

Bw. Ntalika alisema kwamba, ili kuepuka kero na msongamano katika ofisi za TRA wakati wa makadirio ni vema wafanyabiashara wakafika mapema katika ofisi za TRA kupatiwa makadirio yao na kwenda kulipa kodi zao stahiki kabla au mnamo tarehe 31 Machi mwaka huu.

“Kwa sasa tunachokizangatia katika utoaji wa elimu ya kodi ni kuwakumbusha wafanyabiashara wote kwenda kupata makadirio ili waweze kulipa kodi zao stahiki kwa wakati, na tunawahimiza wafanya hivyo ili kuwaondolea usumbufu wa kulipa siku ya mwisho”, alisema Ntalika.

Kwa upande wao baadhi ha Wafanyabiashara wametoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na zoezi la kupatiwa elimu ya kodi ikiwemo kukumbushwa kwenda kufanya makadirio na kulipa kodi ambapo wamesema kwamba, zoezi hilo ni zuri kwani linawajengea uwezo wa kielimu kuhusu masuala ya kodi na wengine wao wameiomba TRA kuwasogezea huduma ya kufanyiwa makadirio ili kuwapunguzia muda na umbali wa huduma hiyo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea na kampeni yake ya utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango ikiwa na lengo la kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari na kukuza wigo wa walipakodi nchini ambapo zoezi hilo kwa sasa lipo katika mikoa ya Dodoma na Manyara kuanzia tarehe 07 Machi, 2022 hadi tarehe 18 Machi, 2022.
Share:

Monday, 14 March 2022

MWANAMKE BIKRA MWENYE UMRI WA MIAKA 56 ACHOKA KUWA SINGO,SASA ANATAKA MME


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina Alvera Uwitonze mwenye ulemavu wa miguu, amefunguka na kusema amechoka kuwa single kwani sasa anaona ni kama anazeeka bila kuwa na mume.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56, alisema kuwa hajawahi kuwa katika uhusiano wa mapenzi na mwanaume yeyote hapo awali na sasa anatafuta mtu wa kumuoa.

Katika mahojiano na Afrimax English, alisema anajuta kutowapa wanaume nafasi ya kuwa naye walipomkaribia wakati akiwa msichana mdogo.

“Walikuwa wakija hapa na kuniuliza wanioe nikawakatalia wote, niliogopa atakuja mwanaume kunipa ujauzito wakaniacha mimi na mtoto na kuendea mtu mwingine,” alisema Alvera.


Alvera aliendelea kueleza kwamba alipata mwanaume ambaye alikubali kumuoa lakini kwa masharti kwamba amlipe Ksh 22,000 (yaani mwanamke alipe pesa ambazo ni sawa na Tsh 446,000).

“Ninaishi kijijini ndanindani kabisa na hakuna njia ya kupata pesa za aina hiyo. Lakini nikipata, bado nitampa kwa sababu niko mpweke na pia nataka kuwa na familia yangu,” alisema.

Alvera, aliyezaliwa akiwa mzima wa afya bila ulemavu, alisema baada ya kuugua, wazazi wake walimpeleka kwa mganga badala ya hospitali hali iliyosababisha ugonjwa wake aliokuwa nao kuzaa ukilema.

Kwa sasa anaishi pekee yake huku akitegemea shughuli za kilimo shamba ili ajipatie kipato, anajipikia na ana redio ya zamani ambayo inamsaidia kutoa upweke.

Ameeleza kuwa, wanaume wengi wanasema kuwa muda wa kumuoa umepita na wanapendelea wanawake wabichi na ambao hawana ulemavu.
Share:

NYWELE NA NYUSI ZA BINTI ZAGOMA KUOTA MIAKA 23 SASA BAADA YA KUNYOLEWA NA BABA YAKE


Picha ya Kampire Josepha

Unaambiwa Bi Kampire Josepha (28) amekuwa akiishi bila nyusi na style ya para kichwani baada ya kunyolewa nywele na baba yake akiwa na miaka mitano ambazo hazijaota mpaka leo.

Kwa sasa imepita miaka 23 Kampire Josepha kuishi bila nywele hizo na kupitia mahojiano aliyofanya nchini Rwanda, anasema familia yake inaamini kubaki na upara na kutoota nywele inasabishwa na imani za kishirikina.

Aidha bibi yake amesema mjukuu wake alizaliwa na nywele ila baada ya kunyolewa hazijamuota tena, pia wamehangaika kwa mganga wa kijiji aliyewapa dawa za mitishamba kupaka ili ziote lakini imeshindikana.
Share:

INSTAGRAM YAZIMWA URUSI


Watumiaji wa mtandao wa Instagram nchini Urusi wamepewa taarifa kuwa huduma hiyo imesitishwa kuanzia saa sita usiku Jumapili ya March 14 2022 baada ya Mmiliki wake Meta Platforms kutangaza wiki iliyopita kuwa itawaruhusu Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Ukraine kutuma ujumbe wakushinikiza Wavamizi wakirusi wauawe.

Emails kutoka kwa Mdhibiti wa Mawasiliano wa Serikali ya Urusi iliwataka Watumiaji kuhamisha picha na video zao kutoka kwenye mtandao huo wa Instagram kabla ya kuzimwa ikiwa ni siku 2 baada ya Kampuni ya Meta ambayo pia inamiliki Facebook (FB) kusema mabadiliko ya muda mfupi katika sera yake ya matamshi ya chuki yanahusu Ukraine pekee kufuatia uvamizi wa Urusi wa Februari 24.

Kampuni hiyo ilisema itakuwa vibaya kuwazuia Waukraine kuonyesha hisia zao na hasira kwa vikosi vya kijeshi vinavyoivamia, kauli ambayo ilipokelewa kwa hasira na Serikali ya Urusi na kuifanya kufungua uchunguzi wa jinai dhidi ya Kampuni ya Meta.
Share:

BASI LA KILIMANJARO LAPATA AJALI



Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Kilimanjaro linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tunduma, kupata ajali asubuhi ya leo Jumatatu Machi 14, 2022.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Senjele ya Pili mkoani Songwe ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
Share:

LETSHEGO AFRICA DELIVERS DOUBLE GROWTH IN PROFITS,BUILDING THE LETSHEGONATION TO SUPPORT ECONOMIC DEVELOMENT ACROSS FOOTPRINT

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger