Thursday, 5 November 2020

Mamlaka yaonya Watoa huduma za maji taka


 Samirah Yusuph
Maswa. Watoa huduma za maji taka katika wilaya ya Maswa wametakiwa kuzingatia usalama wa afya wawapo katika majuku yao kwa kuvaa vifaa maalum vinavyo weza kuwakinga na uchafu ili kujilinda na magongwa ya mlipuko.
Agizo hilo limetolewa na afisa afya wa wilaya hiyo Abel Machibya kufuatia uwepo wa wa wafanyakazi wanao toa huduma hizo bila ya kuwa na vifaa kazi kwa ajili ya usalama wa afya jambo ambalo ni hatari  na linaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Machibya alisema kuwa usalama wa usafi lazima uambatane na mazingira bora kwa wale wanaofanya kazi ya kutunza huduma  za usafi kwa kulinda afya zao na kuongeza kuwa:

"watu wote wanatoa huduma za usafi katika wilaya hiyo kabla ya kupatiwa kazi hizo hujaza mkataba na moja ya kipengere katika mkataba huo ni kila anayeomba kazi ya kufanya usafi ni lazima  ahakikishe usalama wa wafanyakazi wake kwa kuwa na vifaa kinga wakati wa kazi".

 Aidha alisisitiza iwapo wafanya usafi hawana vifaa kinga wakati wa kufanya kazi zao zikiwemo za kutapisha vyoo ni marufuku kufanya kazi hiyo na ikibainika wanafanya kazi katika mazingira hatarishi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika wote kwani hali hii ikiachwa itaeneza magonjwa.

Hali iliyoelezwa na wafanyakazi hao kuwa mara nyingi hukaribiana na uchafu wa kinyesi cha binadamu, na hufanya kazi bila ya vifaa au kinga kwa kutumia mikono yao suala ambalo huwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa mengi.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wafanyakazi walioajiliwa na kampuni ya Mbiti walisema kuwa licha ya kutoa huduma hiyo muhimu katika jamii lakini viongozi wao waliowapa kazi hiyo hawajali afya zao pamoja na kuwa wanawaingizia fedha.

Walisema kuwa licha  ya kuomba kupatwa vifaa kinga wanapokuwa kwenye kazi zao lakini wasimamizi wao,wamekuwa wakiwapatia ahadi ambazo hazitekelezeki hali inayo wafanya wanaendelea kufanya kazi katika mazingira hayo hatarishi.

Ambapo hufanya kazi bila vifaa vya kuziba pua (Mask) na kuvaa mikononi (gloves) hali ambayo ni tishio kwa afya zao lakini  hiyo haijawa sababu ya wao kuacha kazi kwa sababu wanajitafutia kipato.
 
"Hii ndiyo hali yetu ya ufanyaji kazi siku zote sisi tumeajiliwa na kampuni ya usafi ya MBITI ambayo ndiyo imeingia mkataba na halmashauri ya Maswa kufanya usafi katika mji huu ikiwa ni pamoja na kutapisha vyoo vilivyojaa lakini hatupewi vifaa vya kujikinga kama ubavyoona,"alisema mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka jina lake litajwe na kuongeza kuwa:

"Kazi hii ni ngumu kwani tunakumbana na kinyesi cha binadamu kwenye hivi vyoo bila tahadhari yoyote na afya zetu zipo hatarini kupata magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko na hata kwenye jamii tunaweza kupata magonjwa kama kipindupindu na kuhara hasa kipindi hiki cha msimu wa mvua"

Aidha wafanyakazi hao walitoa lawama kwa ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya ya Maswa kwa kutosikiliza kilio chao hicho licha ya kumjulisha kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kufanya kazi bila vifaa kinga.

Akifafanua juu ya malalamiko hayo msimamizi wa kampuni hiyo Masanja Mbiti alisema kuwa malimbikizo ya madeni kutoka katika halmashauri yanapelekea kampuni hiyo kukosa fedha kwa ajili ya kununua vifaa kazi.

"Hata mie sipendi hawa wafanyakazi kufanya kazi bila vifaa kinga lakini nashindwa nifanyaje maana tunadai fedha za miezi sita hatujalipwa na halmashauri maana ndiyo tulioingia nao ubia wa kazi hii nikipata fedha nitanunua kama ilivyo kawaida nami nathamini afya za hao wafanyakazi wangu,"alisema.

Na kuongeza kuwa siku za nyuma alikuwa akinunua vifaa hivyo ambavyo ni mipira migumu ya kuvaa mikononi pamoja na barakoa kwa ajili ya wafanyakazi wake lakini sasa ni miezi sita hajalipwa fedha na halmashauri ya wilaya ya Maswa.

"Hata mie sipendi hawa wafanyakazi kufanya kazi bila vifaa kinga lakini nashindwa nifanyaje maana tunadai fedha za miezi sita hatujalipwa na halmashauri maana ndiyo tulioingia nao ubia wa kazi hii nikipata fedha nitanunua kama ilivyo kawaida nami nathamini afya za hao wafanyakazi wangu,"alisema.

Aidha alisema kuwa kuna wakati aliamua kutoendelea kufanya kazi hizo hadi hapo atakapolipwa fedha hizo lakini wafanyakazi hao waliamua kuendelea kazi bila  ya kuwa na vifaa kinga .

MWISHO
.

Share:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Afunguka Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema alikuwa anafuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 28, 2020, huku akipongeza ulivyoisha kwa amani.

Museveni ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo amesema moja ya vitu vilivyomvutiwa ni ushindi wa kishindo wa CCM katika majimbo ya Ilemela pamoja na Hai.

‘Nilikuwa nafuatilia uchaguzi kupitia Television nikaona mama mmoja wa Ilemela ameshinda kwa kishindo, mara nikaona tena Hai nako CCM imeshinda, nikasema sasa kazi nzuri imefanywa na CCM” Amesema Museven

“Wengine wanafikiri ni jambo rahisi, lakini Afrika kufaulu lazima tukumbuke jambo la mwelekeo wa kisiasa, baada ya uhuru viongozi wetu waligawanyika,  wengi wa Afrika walichukua mstari wa kuwa vibaraka wa nchi za nje wachache wakiongozwa na mwalimu Nyerere (Julius- Rais wa kwanza wa Tanzania) na wengine kama kina Mzee Kaunda na Seretse Khama walikataa.


"Kama tungefuata mstari ule mwingine wa vibaraka hawa viongozi hawangekuwa hapa,  Kusini ya Afrika yote ilikuwa chini ya wakoloni kwa hiyo mnisamehe kuwa natazama TBC 1 kujua inakwendaje uchaguzi wa 2015 nilikuwa na hofu sana hii imekuwaje? Lakini baadaye nikaona alichaguliwa kwa kura nyingi sana.”

“Safari hii nikaona tena kule Hai nikasema heee Hai, hata Ilemela haya ndiyo majimbo ambayo walitangaza kwanza Newala huko nikasema aah basi, sasa mwisho naona nikiangalia umati wa watu hapa naona vijana wengi sana lakini vijana lazima mrithi msimamo wa wazalendo ambao walitangulia wakiongozwa na Mwalimu Nyerere.” - Amesema



Share:

Rais Magufuli: Uchaguzi Umekwisha, Sasa ni Muda wa Kulijenga Taifa Letu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli  amewaeleza wananchi wa  Tanzania kuwa uchaguzi mkuu umemalizika na jukumu lililopo mbele ni kuwatumikia wananchi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020 baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma kuwa Rais wa Taifa hilo, sherehe iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Pia, Samia Suluhu Hassan, ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania ambao kwa pamoja watawaongoza Watanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano 2020-2025.

Dk. Magufuli ameapishwa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020 kwa kupata kura milioni 12 kati ya milioni 15 zilizopigwa sawa na asilimia 84.

Rais Magufuli amewashukuru watu mbalimbali waliojitokeza kwenye sherehe hizo, “nawashukuru sana na mimi kuwa Rais wa kwanza kuapishwa katika hili Jiji la Dodoma.”

Huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema “nawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuniamini na kunichagua ili niwaongoze kwa miaka mitano na kukipa ushindi mkubwa chama changu cha mapinduzi na ushindi huu si wa wana CCM pekee bali ni wa Watanzania wote”

Pia, ameipongeza, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia uchaguzi huu pamoja na kuvishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi.

Rais Magufuli amesema, baadhi ya nchi, uchaguzi umekuwa chanzo cha mgogoro na uhasama, “sisi Watanzania tumevuka salama na hii ni ishara kwamba mwenyezi Mungu ametuvusha salama kama alivyotuvusha kwenye janga corona.”

“Nawashukuru viongozi wa mataifa mbalimbali waliokuja kuungana nasi, wapo marais, mawaziri wakuu, mawaziri na mabalozi wote na wawakilishi wa taasisi za mataifa kama EAC na SADC,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo amesema “uchaguzi sasa umekwisha, uchaguzi sasa umekwisha, uchaguzi sasa umekwisha na jukumu kubwa na muhimu lililopo mbele ni kulijenga na kuleta maendeleo taifa letu na niwahakikishe Watanzania, kiapo nilichoapa na makamu wangu (Samia Suluhu Hassan), tutakienzi.”

Rais Magufuli amesema, katika uongozi wa miaka mitano, watasimamia kumaliza miradi waliyoianzisha, kusimamia rasilimali mbalimbali za taifa, kushughulikia tatizo la ajira hususan vijana na kero zinazowakabili wananchi na kuzidisha mapambano ya rushwa na ufisadi.



Share:

Usichelewe .....Pakua sasa hivi App Ya Mpekuzi Ikiwa na Maboresho Mapya. Ipo PlayStore

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

PICHA: Rais Magufuli Alivyoapishwa Jijini Dodoma Leo Kuwa Rais wa Tanzania Kwa Muhula wa Pili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za Uapisho wake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea eneo la heshma ya kupigiwa Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma leo tarehe 05 Novemba 2020.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kabla ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano katika Muhula wa pili katika sherehe zilizofanyika leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kuapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

Share:

Zitto Kabwe, Freeman Mbowe Waripoti Polisi


Mwenyekiti Chadema Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na wajumbe watatu wa kamati kuu wameripoti kituo cha polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Jumatatu Novemba 9.

Wengine ni aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Chadema) Halima Mdee na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini Godbless Lema




Share:

Mbunge wa zamani Moshi Vijijini Dr. Cyrili Chami afariki Dunia


Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Vijijini, Dr. Cyrili Chami, amefariki dunia usiku wakuamkia leo Novemba 5, 2020, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Chami alihudumu kama mbunge wa Moshi Vijijini kuanzia mwaka 2005, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa Mbunge, Rais wa Awamu ya nne, Mh Jakaya Kikwete, alimeteua Januari 4, 2006, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.

Alihuduma katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje kabla ya Februari 12, 2008, kuhamishwa na kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  kabla ya kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.


Share:

Dkt. Magufuli Aapishwa Kuwa Rais wa Tanzania

Rais John Magufuli ameapishwa leo Alhamisi Novemba 5, 2020 kuendelea na wadhifa huo kwa mhula wa pili.

Ameapishwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma katika tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya kula kiapo na kusaini hati ya utii alikabidhiwa katiba na mkuki na ngao.

Mbali na Rais Magufuli, makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan naye alikula kiapo.



Share:

MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA TANZANIA ...MITANO TENA



Dk. John Pombe Magufuli ameapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mhula wa pili.

Dk. Magufuli ameapishwa leo Alhamis Novemba 5, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma katika tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya kula kiapo na kusaini hati ya utii alikabidhiwa katiba na mkuki na ngao ambapo pia Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan naye alikula kiapo.

Rais Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28.10.2020.

Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

Hii ni awamu ya pili kwa rais Magufuli kuongoza Tanzania, yeye ndiye alikuwa rais wa tano kuiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 na sasa anatarajia kuongoza mpaka mwaka 2025.

Share:

BARAZA LA MAWAZIRI KUKOMA SHUGHULI ZAKE LEO


Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas

Na Richard Mwaikenda,  Dodoma

BARAZA la Mawaziri limekoma leo kuendelea na shughuli za kikazi mara atakapoapishwa Rais Mteule, Dk. John Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk Magufuli.

Dk Abbas alisema kuwa kisheria ni kwamba Baraza la Mawazili la 2015-2020 mwisho wake ni mara tu Rais Mteule atakapoapishwa kushika kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Majukumu yote yatafanywa na makatibu wakuu wa wizara hadi atakapotangaza baraza jipya.
Share:

LIVE: Sherehe Ya Uapisho Wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Magufuli, Uwanja Wa Jamuhuri Dodoma


Sherehe Ya Uapisho Wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Magufuli, Uwanja Wa Jamuhuri Dodoma


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi November 5



Share:

WATANZANIA WATEGEMEE MAGEUZI MAKUBWA KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

kulia Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akikagua gari iliyotoka site aina ya fuso lenye kufanya kazi ya kubeba kokoto,mchanga na mawe katika kazi za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, gari hilo lina uwezo wa kubeba tani kumi na tano, kushoto ni kaimu mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali.  
Aliyesimama Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya, akikagua mtambo aina ya Wheel loader wenye kazi ya kuchota kifusi, alipotembelea katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukagua mitambo hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akitoa maelekezo ya kutumika kwa mtambo mpya unaotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili isipate kutu wakati wa mvua.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiendelea na ukaguzi wa Mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma leo.

Katibu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema, watanzania wategemee mageuzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji, kwani serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekata hiyo.

Bw. Kusaya ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa na ziara ya kikazi katika ofisi za Tume ya Taifa yaUmwagiliaji, ambapo amesema Serikali ina mpango wa kuboresha mundombinu yote chakavu katika sekta ya umwagiliaji na kufufua skimu za zamani na kuongeza skimu mpya.

Alisema pia ikiwemo kuongeza vyanzo vipya vya maji katika maana ya kujenga mabwawa na kutumia vyanzo asili vilivyopo kama mito, mabwawa  ya asili na maziwa hivyo mkulima atanufaika na kilimo cha umwagiliaji katika mazao ya biashara na chakula.

Sambamba na hilo, amesema Serikali pia imeona umuhimu wakuongeza wataalamu wa sekta hiyo katika ngazi za wilaya na itafikia ngaz iya kata na kijiji ili kuweza kumfikia mkulima kwani kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo cha uhakika na mkombozi kwa mkulima.

“wakulima watapata huduma za uhakika zaidi na kunufaika na kilimo cha umwagiliaji” Alilisita.

Awali, alipokuwa akizungumza na menejimenti yaTume ta ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Kusaya amewataka watumishiwa Tumeya Taifa ya umwagiliaji kufanya kazi kwa ushirikiano,na uhakika ili kuweza kufikia malengo ya mageuzi makubwa yenye tija katika sekta ya umwagiliaji.

Na baada ya hapokatibu Kusaya alikagua mitambo iliyopo katika ofisi za Tume hiyo inayotumika kujengea na kuboresha miuondombinu ya umwagiliaji.

                      

Share:

Biden apata mafanikio yatakayomwezesha kushinda kiti cha rais wa Marekani


Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden amepiga hatua muhimu kuelekea kupata ushindi baada ya kunyakua majimbo tete ya Michigan na Wisconsin usiku wa kuamkia leo.

 Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa pamoja na mgombea mwenza Harris Kamala, Biden amesema hawezi kujitangazia ushindi lakini ana matumaini kuwa zoezi la kuhesabu kura litakapomalizika wataibuka kuwa washindi. 

Kwa kunyakua majimbo hayo mawili, Biden amefikisha kura 264 za Baraza maalumu la wajumbe wanaomchagua rais dhidi ya 214 za rais Doanld Trump anayewania muhula wa pili.

 Trump amezungumzia mafanikio hayo ya Biden kwa hasira na tayari amewasilisha ombi la kufungua shauri dhidi ya matokeo hayo ikiwa ni pamoja na kutaka kura kuhesabiwa tena na katika baadhi ya majimbo ametaka zoezi la kuhesabu kura kusitishwa.



Share:

Wednesday, 4 November 2020

WANAFUNZI SITA WA UDSM WASHINDA TUZO KWENYE SHINDANO LA TEHAMA LA HUAWEI


Wanafunzi sita wa Kitanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefuzu kushiriki shindano la Huawei la TEHAMA Duniani baada ya kufanya vizuri katika fainali za Mashindano ya TEHAMA ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Huawei. hafla ya utoaji Tuzo kwa washindi ilifanyika Mtandaoni siku ya jana Oktoba 29, 2020.

Shindano hilo linalenga kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji kwenye TEHAMA kuonyesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, kuhimiza utafiti wa TEHAMA, na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Timu 13 zilizoshinda ni timu kutoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Lesotho, Mauritius, Zambia. Timu hizo zitashindana na timu kutoka mabara mengine ikiwemo Marekani katika mashindano ya dunia Mwezi Novemba.

Miongoni mwa timu zilizopewa tuzo kwenye hafla hiyo ni timu 10 zilizoshiriki upande wa Network Track zikiwemo timu kutoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na Lesotho. Timu hizo zitaenda kushiriki mashindano ya Dunia baada ya kuchuana vikali kupata wawakilishi kwa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara. Timu za Nigeria, Mauritius na Zambia zenyewe zilishinda upande wa Cloud Track.

Timu ya Tanzania ilikuwa na wanafunzi 9 ambao waligawanyishwa katika timu tatu. Timu mbili kati ya hizo zimefanikiwa kufika kwenye fainali za dunia, timu ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Zaidi ya timu 40 zilizoshiriki, na timu nyingine ilishika nafasi ya 4 na hivyo kupata nafasi ya kushiriki fainali za dunia.

Timu hizo zimeundwa na wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Washindi wa nafasi ya kwanza ni Mpoki Abel Mwaisela, Hongo Kelvin and Henry Kihanga na washindi wa pili ni Aghatus Biro, John Lazaro na Elisante Akaro.

Hafla hiyo ya utoaji tuzo imeashiria miaka mitano mfululizo ya kushiriki kikamilifu Shindano la TEHAMA la Huawei kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, shindano hilo limekuwa likivutia zaidi ya wanafunzi 50,000 kutoka nchi 14 za Afrika yakiwa na Kauli mbiu ya “Connection, Glory and the Future” na Uelewa mpya kuhusu TEHAMA kama vile Cloud computing, AI, mitandao ya simu na intaneti.

Katika hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini, viongozi wa tasnia, na wanafunzi, Makamu wa Rais wa Huawei Afrika Mashariki na Kati, Hou Tao aliangazia shauku ya wanafunzi kujifunza, ambayo inahitajika sana ili kuhakikisha mifumo ya Kidijiti inafika Afrika nzima katika zama ambazo ujuzi wa mahali pa kazi tayari unahamia mtandaoni.

Uzoefu wa kimataifa unaonyesha kuwa hili ni eneo muhimu ambapo ushirikiano wa umma na taasisi binafsi unaweza kuwa na mchango mkubwa. "Bwana Hou anasema," Kama kampuni ya binafsi inayohudumia soko la Afrika kwa zaidi ya miaka 20, Huawei imejitolea na itabaki kuwa mshirika wa kuaminika wa serikali na taaluma katika kujenga vipaji na wanataaluma wa TEHAMA, kuimarisha uwezo na kuongeza uwezo wa watu wa dijiti. . ”

Akiongea kama mwakilishi wa waalimu wa Chuo Kikuu, Prof.Funso Falade, Rais wa Jumuiya ya Elimu ya Uhandisi Afrika (AEEA) aligusiachangamoto kadhaa dhidi ya mafunzo ya wahandisi barani Afrika kama ufadhili, kuchoka kwa akili, na ushirikiano dhaifu wa vyuo vikuu / tasnia. Pia alisifu jitihada zinazofanywa na Huawei katika kukabiliana na changamoto hizi.

“Fursa za kukuza ujuzi zinazotolewa na Kampuni ya Huawei zinaambatana na lengo na matarajio ya AEEA kwa wanafunzi wetu na eneo muhimu ambapo sasa tunahitaji utaalam mwingi barani Afrika kuliko wakati wowote kabla, hasa ukizingatia changamoto zilizoletwa na janga la COVID-19 kwenye mfumo wetu wa elimu, ”aliongeza.

Shindano la TEHAMA la Huawei ni moja ya tukio kubwa la aina yake. Miongoni mwa nchi zinazoshiriki, Zambia, Kenya, Tanzania, na Afrika Kusini zilifanya sherehe ya ufunguzi wa kitaifa au tuzo ambapo mawaziri na maafisa wengi katika sayansi na elimu walizungumza kupongeza kazi inayofanywa na Shindano hilo na mchango wa Huawei katika kukuza vipaji vya Sayansi na teknolojia Afrika.

Share:

GGML YAANZISHA BUSTANI YA KUVUTIA MJINI GEITA

Share:

JUMUIYA YA MARIDHIANO YAMSHUKURU MUNGU UCHAGUZI KUFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, kumshukuru Mungu kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa amani na utulivu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Askofu Oswald Mlay na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Askofu Evance Chande. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

MWENYEKITI wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.

Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, akiwa pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.

 Aidha, Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali iliyoshinda iongoze vema.

"Tunashukuru Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni kuungana kuendelea  kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze salama.

Katika chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila mmoja  haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la kawaida,"amesema Sheikh Alhad. 

Ameshauri upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuiya hiyo inaweza kuweka mambo sawa.

"Kubwa tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu, tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo, tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani, kuirejesha ni ngumu sana."

Amesema viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu  kwa wema wake  aliotutendea. na kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia. 

Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu  nchi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu  na sasa iko salama hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger