Tuesday, 7 July 2020

Hakuna Kuhuisha Hati Za Miaka 33 Kwa Wamiliki Wa Ardhi Wasioendeleza Viwanja- Waziri Lukuvi

Na Munir Shemweta, WANMM GEITA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Makamishna Wasaidizi wa Ardhi katika ofisi za ardhi za mikoa nchini kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi wasioendeleza viwanja vyao tangu kumilikishwa hawahuishi miliki zao za miaka 33 ili kupatiwa za miaka 99.

Lukuvi ametoa kauli hiyo jana mkoani Geita wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Geita ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi hizo nchini. Uzinduzi wa ofisi ya ardhi Geita umeenda sambamba na ule wa mkoani Kagera uliofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula.

Alisema, kuna wamiliki wa ardhi katika maeneo mbalimbali katika mikoa wameshindwa kuchukua hati za viwanja na wengi viwanja vyao ni vya miaka 33 na kutolea mfano wa mkoa wa Geita wenye zaidi ya wamiliki 30,000 huku baadhi yake wakishindwa maendelezo yoyote jambo alilolieleza limeikosesha  serikali mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.

" Nawaagiza Makamishna Wasaidizi wa ardhi wa mikoa kuhakikisha  wamiliki woteb wa ardhi wasioendeleza maeneo yao wasihuishwe hati zao, kama kwa muda wa miaka 33 umeshindwa kuweka hata tofali huwezi kujenga tena, hatukutoa ardhi kwa mtu kama land bank" alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi,  wananchi walioendeleza viwanja vyao Makamishna wa mikoa  wanatakiwa kuhakikisha hati zao za miaka 33 zinahuishwa na kupatiwa zile za miaka 99 ili waweze kuzitumia kwa shughuli za kiuchumi kama kuchukua mikopo ya muda mrefu benki.

Sambamba na hatua hiyo, Waziri Lukuvi aliwataka Makamishna Wasaidizi wa ardhi katika ofisi za ardhi za mikoa kumpatia gharama halisi za upimaji kufuatia usambazaji vifaa vya upimaji uliofanywa na wizara yake kwenye ofisi hizo.

Alisema, kwa sasa gharama za upimaji katika halmashauri mbalimbali za wilaya hazina uhakika kutokana na kila eneo unapofanyika upimaji kuwa na kiwango chake alichokieleza kuwa kinawaumiza sana wananchi hasa wale wanyonge.

" haiwezekani serikali inunue vifaa vya zaidi ya bilioni 3 halafu mwananchi anaumizwa, yaani vifaa vya upimaji vinakodishwa na halmashauri kwa makampuni kwa gharama ya shilingi laki mbili na nusu   kwa siku na gharama hizo anazibeba mwananchi ni lazima gharama zishuke sasa" alisema Lukuvi

Aidha, Waziri wa ardhi alisema, kuanzia mwakani wizara yake itaanza mradi mkubwa wa kupima kila kipande cha ardhi na hati kutolewa kwa mfumo wa kidijitali unaowezesha mwananchi  kumilikishwa hati ya kielektroniki ya kurasa moja.

Akizungumzia suala la urasimishaji makazi katika maeneo mbalimbali nchini,  Waziri Lukuvi aliagiza wananchi wote waliojenga maeneo hatarishi kama vile mabondeni wasirasimishiwe na badala yake maafisa mipango miji waangalie upya ramani zake ili wazirekebishe.

" aliyejenga eneo hatarishi asipewe hati na wapanga miji mrudi kutoa ramani, mvua zimeshusha hadhi yenu na kuonesha mafuriko, futeni katika mpango wenu maeneo yaliyoathirika msiyapange na walio mabondeni wasirasimishiwe" alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema kupitia uzinduzi wa ofisi ya ardhi, mkoa huo sasa utafaidi kwa kusogezewa  huduma za sekta ya ardhi karibu ambapo awali zilikuwa zilikuwa zikipatikana ofisi ya kanda uliyokuwemo mkoa wa Mwanza na kutolea mfano upatikanaji hati ulilazimu mwananchi kusafiri hadi Mwanza na kumuingizia gharama.

Mkuu huyo wa wilaya ya Geita alibainisha kuwa, kupatikana kwa huduma zote za sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita sasa miji katika mkoa huo itapangika vizuri na maeneo yaliyoiva kimji itapangiliwa vizuri.

Naye Mbunge wa Bukombe ambaye ni Waziri wa Madini Doto Biteko aliishukuru Wizara ya ardhi kwa uamuzi wa kufungua ofisi za ardhi za mikoa pamoja na kutatua migogoro ya ardhi na kubainisha kuwa uzinduzi wa ofisi hiyo ni furaha kwa wana Geita kwa kuwa hatakuwa wakisafiri tena umbali mrefu kufuata huduma ya ardhi Mwanza.



Share:

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mpya Wa Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watano








Share:

Habari Zilizopo Latika Magazeti ya Leo Jumanne July 7





















Share:

Monday, 6 July 2020

Taarifa Kwa Umma: Uteuzi Mpya wa Makatibu Tawala 06 wa Wilaya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa wilaya Sita hapa nchini.


Katika uteuzi huo Hassan Ngoma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Singida kuchukua nafasi ya Wilson Shimo ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

 
Kamana Simba ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Longido mkoani Arusha kuchukua nafasi ya Toba Nguvila ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Naye Faraja Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha kuchukua nafasi ya Abbas Kayanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Karatu.


Bahati Joram ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro kuchukua nafasi ya Lameck Lusesa, huku Salum Mtelela  akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Bunda mkoani Mara kuchuku nafasi ya Jonas Nyehoja aliyestaafu.


Uteuzi mwingine ni wa Augustino Chazua ambaye anakuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo mkoani Morogoro  na anachukua nafasi ya Robert Selasela.

Wateule wote wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dodoma Jumatano keshokutwa saa Nne asubuhi.



Share:

Nafasi ya kampuni za simu katika kukuza teknolojia Tanzania

Na Mayala Francis, DIT
Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia maendeleo makubwa kwenye sekta ya teknolojia hasa linapokuja suala la matumizi ya simu.

Hakuna ubishi wowote kwamba intaneti kwa njia ya simu imeleta tija kubwa katika shughuli zetu. Katika ulimwengu wa biashara imesaidia watu kuwasiliana na kufanya kazi pamoja hata kama wako maeneo tofauti. 

Vivyo hivyo intaneti kwa njia ya simu pia imezesha kuwasiliana na wapendwa wetu kwa namna mbalimbali na kwa urahisi, jambo ambalo halikuwezekana miaka michache iliyopita. Ni jambo lisiloshangaza kwamba katika baadhi ya maeneo duniani, watu sasa wanatumia muda mwingi mtandaoni kuliko miaka ya nyuma. 

Nchini Tanzania, idadi ya wananchi wanaopata mtandao wa mtandao wa intaneti imeongezeka mara dufu kati ya mwaka 2013 na 2019 na kufikia asilimia 46. Sehemu mafanikio haya imewezeshwa na kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi kama Tigo Tanzania. 

Kampuni kama Tigo zimekuwa bunifu na kutumia maendeleo yaliyopo kuwapa wateja wake huduma za uhakika katika dunia ya kidijitali. Tigo inataja huduma bunifu kama Tigo Rusha inayowapa wateja wake uwezo wa kununua muda wa maongezi na vifurushi toka kwa mawakala na vituo vya mauzo. Wakati huo huo Tigo hutoa huduma kwa mteja masaa 24 kupitia simu na mtandao wa WhatsApp. 

Sekta ya mawasiliano ya simu ni muhimu katika kupanua wigo wa Watanzania wengi zaidi kufurahia huduma za kiteknolojia. Tuendelee kuiunga mkono sekta hii na kuipa nafasi kukua zaidi.


Share:

HAWA NDIYO MAKATIBU TAWALA WA WILAYA SITA WALIOTEULIWA MUDA HUU


Share:

WANAWAKE WATAKA KUUZA ALIZETI YAO KAMA BIDHAA BADALA YA MALIGHAFI


Viongozi na wajumbe wa kikundi cha Mkombozi na Tumaini wakionesha alizeti
Na Sumai Salum- Meatu

Vikundi vya wanawake vya Tumaini Group na Mkombozi Group vilivyopo kata ya Sakasaka wilayani Meatu mkoani Simiyu wamesema hawatauza tena alizeti kama malighafi bali watauza kama bidhaa kutokana na tathmini walizoziona kwenye zao hilo.


Hayo waliyabainisha wakati wanapoendelea na maandalizi maonesho ya Nane Nane yanayotarajia kufanyika kwa mwaka wa tatu sasa kama ilivyo agizo la serikali katika mkoa wa Simiyu ifikapo Agosti 8 mwaka huu.

Walidai kuwa kuuza malighafi kumewachelewesha kufikia malengo ya kundi hilo pamoja na maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwani wamekuwa wakipata pesa kidogo ukilinganisha na mafuta ya zao hilo.

“Tumekusudia tuuze alizeti zetu baada ya kuchakata mafuta na kwa gunia moja linatoa lita 17 za mafuta na ukiuza unapata shilingi 60,000/= au 55,000/=/= na ukiuza alizeti bila kusindika unapata 30,000/= ambayo ni hasara kwa mkulima na kikundi, kwa gunia zetu 12 kikundi kitapata faida kubwa itatusaidia kusomesha watoto na maandalizi ya mashamba kwa mwakani” alisema Bi. Christina mhasibu wa Mkombozi Group

“Mradi huu wa alizeti tuliofadhiliwa na REDESO umetupatia manufaa kwani mwaka jana tulipouza mafuta ya alizeti pesa zile zilitusaidia wanakikundi kwani tulikopeshana kwa lengo la kuanzisha miradi ya mtu binafsi wakati tusipokuwa na alzeti tukakopeshana pesa kila mtu 50,000 kwa liba ya 10% wapo waliolima pamba,karanga na hata mahindi pia na vinatusaidia”,alisema Mwenyekiti kikundi cha Tumani Bi.Elizabeth Bisha.

Mbali na hayo, Afisa maendeleo ya jamii kata ya Sakasaka wilayani Meatu mkoani Simiyu Bi. Mbuke Jaulula aliwataka akina mama wakulima wa vikundi vilivyoko katika kata hiyo kuendelea kuwapa wanawake na wanajamii wengine elimu juu ya ulimaji wa zao la alizeti licha ya kuwa linasitahimili ukame bali pia ni zao lenye faida kwa kutoa mafuta na hata chakula cha mifugo lakini pia kwa mwezeshaji wa kikundi hicho ambaye ni REDESO apate mrejesho mzuri dhidi ya matarajio yao wanayoyategemea baada ya kuwawezesha wanakikundi.

“Mwaka huu tumewezeshwa na REDESO mbegu bora za alizeti kwa vikunndi vinne na tumevuna gunia 2 hadi 3 kwa hekali kwa magunia ya debe 6 na tutanufahika pakubwa hivyo niwasihi wanajamii wa kata ya sakasaka hasa wanawake wa jamii hii ya kisukuma kwa kuwa bado kuna mila kandamizi, kupitia kilimo hiki tuwe na amasa zaidi ya ufugaji wa kisasa ikilinganishwa na kuwa tunaishi pembezoni mwa hifadhi na kukosa sehemu ya malisho kwa kulima zao hili tutapata chakula cha mifugo pia na hawatahangaika”aliongeza Bi. Jaulula.

Kwa upande wake Mratibu miradi na Meneja kutokea asasi isiyokuwa ya kiserikali REDESO inayofanya kazi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na baadhi ya kata za wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw. Charles Buregeya amewapongeza wanakikundi hao huku akiwataka wasiridhike kwa mavuno hayo bali waendeleze bidii na jitihada katika uzalishaji ili waweze kufikia angalau gunia 7 hadi 8 kwa hekali moja kama inavyoshauliwa kitaalamu.

“Lakini pia kijasiriamali mmeonesha ukomavu kwani kuuza alizeti peke yake hautapata tija ukilinganisha na mafuta ila ninachotaka mkizingatie ni kuhakikisha mmeboresha uzalishaji,usindikaji na vifungashio ili tuweze kuingia kwenye ushindani na pia tuhakikishe tunatafuta masoko ili tuweze kuingia kwenye soko la ushindani, na pia shukrani kwa serikali kupitia maendeleo ya jamii kwa ushirikiano wanaotupatia”,alisema Buregeya.
Viongozi na wajumbe wa kikundi cha Mkombozi na Tumaini
Mratibu miradi na Meneja kutoka asasi isiyokuwa ya kiserikali REDESO inayofanya kazi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na baadhi ya kata za wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw. Charles Buregeya akizungumza
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Sakasaka wilayani Meatu mkoani Simiyu Bi. Mbuke Jaulula akizungumza
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Sakasaka wilayani Meatu mkoani Simiyu Bi. Mbuke Jaulula na Mratibu miradi na Meneja kutoka asasi isiyokuwa ya kiserikali REDESO inayofanya kazi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na baadhi ya kata za wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw. Charles Buregeya wakipiga picha ya pamoja na viongozi wa vikundi vya Mkombozi na Tumaini
Share:

TCRA YAIFUNGIA KWANZA TV KWA MIEZI 11

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha Kwanza Online TV  kwa muda wa miezi kumi na moja (11) baada ya kusikiliza shauri la ukiukaji wa kanuni za utangazaji kufuatia taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa Instagram



Share:

MGODI WA WDL WATAKA KUUZWA KINYEMELA



Waziri wa Madini Doto Biteko akijipaka kitakasa mikono baada ya kupimwa joto kwenye mgodi wa Williamson Diamond Limited alipokuwa kwenye ziara yake Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjla akipimwa joto kabla hajaingia kwenye ukumbi wa mkutano katika mgodi wa Williamson Diamond Limited nyuma yake ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula.
Waziri wa Madini Doto Biteko akifafanua jambo kwenye kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga


Baadhi ya washiriki walioshiriki kikao cha Waziri wa Madini katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.


Baadhi ya washiriki walioshiriki kikao wa Waziri wa Madini katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo kwenye kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akiwa ameongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila mara baada ya kikao katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.


Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akielekea kwenye gari mara baada ya kikao katika mgodi wa Williamsoni Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza jambo kwenye kikao kilichofanyika katika mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.


Muonekano wa mgodi wa madini ya Almasi wa Wiliamson Diamond Limited uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga.



Na Tito Mselem ,Shinyanga 

Waziri wa madini Doto Biteko amesikitishwa na kitendo walichokifanya uongozi wa mgodi wa madini ya Almasi wa Williamson Diamond Limited (WDL), uliopo Mwadui katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga cha kutaka kuuza kinyemela mgodi huo bila  Serikali kupewa taarifa.



Hayo yamesemwa  Julai 5, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko alipofanya ziara yake kwenye mgodi huo mara baada ya kuona matangazo ya kuuzwa kwa mgodi huo kwenye mitandao ya kijamii.



Waziri Biteko, alisema Serikali inaubia wa asilimia 25 katika mgodi wa WDL, haiwezekani utakekuuzwa bila mmbia wake kufahamu   kitendo hicho ni kukiuka taratbu na Sheria za nchi.



“Serikali inaubia wa asilimia 25 kwenye mgodi huu kama mnataka kuuza mgodi lazima mtoe taarifa serikalini na mpate kibali, kwa mantiki hiyo serikali inapaswa kuwaadhibu kwa kutaka kuuza mgodi bila kibali huko ni kuhujumu nchi,hivi mlituuliza serikali hatuna uwezo wa kununua mgodi na kuuendesha?,” alisema Waziri Biteko.



Kutokana na kitendo hicho, Waziri Biteko ameuagiza uongozi wa mgodi huo kufikia Julai 10 mwaka huu wawe wametoa maelezo kwa maandishi kueleza sababu za kutaka kuuza mgodi huo bila mmbia wake ambaye ni Serikali kujua na pia, kutoa taarifa ya kuwapunguza kazi wafanyakazi kisha kuwalipa nusu mshahara.



Alisema wafanyakazi waliopunguzwa kazi kwa kutumia kigezo cha ugonjwa wa Corona utaratibu uliotumiwa haufai na wao kama Wizara ya Madini hawakubaliani nao kutokana na kulipwa mishahara nusu jambo ambalo linawapa wakati mgumu na kusababisha migogoro isiyo ya lazima.



Aidha, Waziri Biteko, alisema sababu ambazo wanazitoa mgodi huo za kusitisha shughuli za uzalishaji na kutaka kuuza mgodi huo ni kushuka kwa bei ya almasi duniani iliyosababishwa na ugonjwa wa corona, ambapo alieleza kuwa sababu hizo hazina mashiko ila wawe wakweli kama wamefilisika ijulikane.



Waziri Biteko alisema sababu kubwa ambayo ingefanya mgodi huo kufungwa ni kushuka kwa uzalishaji na siyo uendeshaji, huku akihoji kama mgodi hauna fedha za kujiendesha wangesema badala ya kuweka matangazo kwenye mitandao mgodi unauzwa wakati serikali haina taarifa.

kwenda mitandaoni.



Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi huo Mhandisi Ayoub Mwenda, alikiri kuwa hawakutoa taarifa Serikalini juu ya kutaka kuuzwa kwa mgodi huo, huku akieleza kuwa walifunga mgodi huo April 8 mwaka huu kutokana na kushindwa kujiendesha na ameahidi kufuata maelekezo yote ambayo yametolewa na Waziri wa Madini.



Mhandisi Mwenda alisema walikuwa wanazalisha vizuri kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambapo kwa mchanga waliokuwa wameuzalisha walikuwa mbele kwa asilimia tatu na almasi walizokuwa wamezikusanya walikuwa mbele kwa asilimia 9.1kulingana na bajeti yao waliyokuwa wameiweka.



Alisema tatizo la Corona limeuathiri sana mgodi huo na kusimama kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na kushuka bei ya masoko ya nje ambapo kabla ya Corona bei ilikuwa dola 246 kwa karati moja ambapo Machi mwaka huu waliuza karati moja dola 135 ambayo ilikuwa haiwezi kutosheleza gharama za uzalishaji.



Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba ameipongeza Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanazozifanya ambapo wamesaidia nchi kuingia katika uchumi wa kati.

Share:

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Alegeza Masharti Ya Kukabiliana Na Corona

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelegeza kwa kiasi fulani sheria kali zilizokuwa zimewekwa kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19

Akilihutubia taifa  hilo leo Jumatatu katika Jumba la Harambee jijini Nairobi, Rais Kenyatta ametangaza kuondoa marufuku ya safari ya watu kuingia au kutoka katika kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera kuanzia kesho Jumanne.

Hata hivyo amesema kuwa agizo la kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri litaendelea kuwepo kwa kipindi cha siku 30 zijazo.

Vile vile, Rais Uhuru Kenyatta amesema makanisa na misikiti itafunguliwa lakini waumini wasiozidi 100 ndio watakaoruhusiwa kuhudhuria ibada na kwa muda usiozidi saa moja. Shule za Jumapili na madrasa zitasalia kufungwa kwa muda wa siku 30.

Hali kadhalika Rais wa Kenya amesema safari za ndege za ndani ya nchini zitaanza Julai 15, huku zile za kimataifa zikitazamiwa kuanza Agosti Mosi, lakini kwa kufuata tahadhari za kiafya.


Share:

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Amuwakilisha Rais Dkt. Magufuli Malawi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera  muda mfupi baada ya kusimikwa rasmi  kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi leo Julai 06,2020 kwenye Sherehe iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kamuzu,  Lilongwe nchini Malawi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Share:

Benard Membe Arudisha Kadi Ya Uanachama CCM

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Tanzania,na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Benard Membe,amerejesha kadi ya uanachama wa Chama hicho.

Membe amerejesha kadi hiyo leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020 nyumbani kwake Rondo mkoani Lindi.

“Leo saa 6 na nusu mchana mimi na mke wangu nikisindikizwa na mamia ya wananchi wa Rondo, tumerejesha kadi zetu za CCM kwa wenyewe. Nimemwandikia KM (katibu mkuu) wa CCM kuhusu tukio hilo na kukishukuru chama kwa mema yote kilichonitendea. Nawatakia kila la heri viongozi na wanachama wote,” ameandika Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter


Tarehe 28 Februari 2020, Kamati Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuzwa uanachama Membe kwa madai amekuwa akikiuka taratibu na miongozo ya chama hicho



Share:

Nafasi ya Kazi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola




Share:

Rais Magufuli awasimamisha kazi viongozi wa polisi, Afisa Usalama kwa uzembe

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Usalama wa Wilaya hiyo mkoani Arusha kwa kushindwa kutumiza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli amesema kuwa viongozi hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukabiliana na dawa za kulevya, hadi maofisa kutoka makao makuu walipofika na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha bangi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amempandisha cheo James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Akitangaza uamuzi huo wa kumthibitisha Kaji pamoja na kumuapisha, Rais Magufuli amesema anachotaka kuona ni matokeo ya kazi wanazofanya wasaidizi wake.


Share:

Monitoring & Evaluation Officer Job vacancy at Plan International

The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are most affected. Working together with children, young people, our supporters […]

The post Monitoring & Evaluation Officer Job vacancy at Plan International appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger