Monday, 6 July 2020

Nafasi ya kampuni za simu katika kukuza teknolojia Tanzania

...
Na Mayala Francis, DIT
Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia maendeleo makubwa kwenye sekta ya teknolojia hasa linapokuja suala la matumizi ya simu.

Hakuna ubishi wowote kwamba intaneti kwa njia ya simu imeleta tija kubwa katika shughuli zetu. Katika ulimwengu wa biashara imesaidia watu kuwasiliana na kufanya kazi pamoja hata kama wako maeneo tofauti. 

Vivyo hivyo intaneti kwa njia ya simu pia imezesha kuwasiliana na wapendwa wetu kwa namna mbalimbali na kwa urahisi, jambo ambalo halikuwezekana miaka michache iliyopita. Ni jambo lisiloshangaza kwamba katika baadhi ya maeneo duniani, watu sasa wanatumia muda mwingi mtandaoni kuliko miaka ya nyuma. 

Nchini Tanzania, idadi ya wananchi wanaopata mtandao wa mtandao wa intaneti imeongezeka mara dufu kati ya mwaka 2013 na 2019 na kufikia asilimia 46. Sehemu mafanikio haya imewezeshwa na kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi kama Tigo Tanzania. 

Kampuni kama Tigo zimekuwa bunifu na kutumia maendeleo yaliyopo kuwapa wateja wake huduma za uhakika katika dunia ya kidijitali. Tigo inataja huduma bunifu kama Tigo Rusha inayowapa wateja wake uwezo wa kununua muda wa maongezi na vifurushi toka kwa mawakala na vituo vya mauzo. Wakati huo huo Tigo hutoa huduma kwa mteja masaa 24 kupitia simu na mtandao wa WhatsApp. 

Sekta ya mawasiliano ya simu ni muhimu katika kupanua wigo wa Watanzania wengi zaidi kufurahia huduma za kiteknolojia. Tuendelee kuiunga mkono sekta hii na kuipa nafasi kukua zaidi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger