Saturday, 4 July 2020

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Wa Wakurugenzi Nane




Share:

Picha : GREYSON KAKURU ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA


Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Greyson Kakuru aliyechaguliwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi leo Julai 4, 2020.

Na Damian Masyenene - Shinyanga Press Club Blog
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) leo Julai 4, 2020 imefanya mkutano wake mkuu wa uchaguzi kutimiza matakwa ya kikatiba, ambapo imepata safu mpya ya uongozi.

Katika uchuguzi huo uliosimamiwa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila umefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa, mjini Shinyanga.

Nafasi zilizokuwa zinagombaniwa ni Wajumbe watano wa kamati tendaji, Mweka hazina, Katibu Msaidizi, Katibu Mtendaji, Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa klabu hiyo.

Uongozi uliomaliza muda wake baada ya kudumu madarakani kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2015 - 2020, ni Mwenyekiti Kadama Malunde, Makamu Mwenyekiti Shaban Alley, Katibu Ali Lityawi, Mweka Hazina Stella Ibengwe, na wajumbe watano wa kamati tendaji ambao ni Marco Maduhu, Kareny Masasi, Suzy Butondo, Shija Felician na Patrick Mabula.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa uchaguzi huo, David Nkulila alimtangaza Greyson Kakuru kuwa Mwenyekiti mpya wa Shinyanga Press Club (SPC) baada ya kuibuka na ushindi wa kura 12 dhidi ya washindani wake, Stella Ibengwe aliyepata kura 11 na Kadama Malunde aliyepata kura 10.

Pia Patrick Mabula ametangazwa kuwa Makamu Mwenyekiti baada ya kupigiwa kura za ndiyo 28, hapana 3 na moja iliyoharibika.

Vile vile, Ali Lityawi ameibuka kuwa Katibu Mtendaji wa klabu hiyo baada ya kumshinda mpinzani wake, Moshi Ndugulile, ambapo mshindi huyo alipata kura 18, huku Moshi Ndugulile akipata kura 14.

Kasisi Kosta alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi kwa kura za ndiyo 27, za hapana 4 na moja ikiharibika huku  Kareny Masasy amechaguliwa kuwa Mweka Hazina baada ya kupata kura 27 za ndiyo na tano za hapana, huku wajumbe watano wa kamati tendaji wakichaguliwa ambao ni Shija Felician, Suzy Butondo, Marco Maduhu, Marco Mipawa na Frank Mshana.

Mkutano huo wa uchaguzi ulihudhuriwa na wajumbe 33 kati ya wanachama 39 wa SPC ambapo wawili ni wagonjwa, wawili wakiwa na ruhusa na wawili hawakufika, ambapo nafasi nyingine zote zilipigiwa kura na wajumbe 32, kasoro nafasi ya Mwenyekiti ambayo ilipigiwa kura 33 baada ya mwanachama mmoja kuongezeka wakati zoezi la upigaji kura likiendelea.

Pia kabla ya zoezi la upigaji kura, wagombea wote walipewa fursa ya kujinadi kwa dakika tatu kila mmoja, huku wajumbe wakipewa fursa ya kuuliza maswali matatu kwa kila mgombea.

Akiwapongeza wanachama wenzake kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo, Mwenyekiti Mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC), Greyson Kakuru aliwashukuru wanachama kwa kumuamini na kumpa ushindi huo, huku akieleza kuwa kwa sasa safu yake inalo deni kubwa la kuyatimiza yale iliyoahidi na kwamba kila mwanachama atakuwa na nafasi sawa kukijenga chama hicho.

Naye Katibu mpya wa SPC, Ally Lityawi aliwashukuru wajumbe na kueleza kwamba sasa wanakwenda kuchapa kazi kwa kuyatimiza yale yaliyoahidiwa, kuwaunganisha waandishi, kutengeneza mahusiano mazuri na wadau na kutetea maslahi ya wanahabari mkoani hapa.

"Chama hiki ni chetu zote tushirikiane kukijenga, mimi siyo mkamilifu penye mapungufu tufuatane kushauriana," amesema.

Akizungumza na kuwashukuru wanachama, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Kadama Malunde aliwapongeza wajumbe kwa kufanya uchaguzi wa huru na haki ambao umeleta mvuto mkubwa, huku akiwahimiza waliochaguliwa kuzingatia maadili na kuacha kutoa maamuzi ya haraka yatakayowaumiza wanachama wa klabu hiyo.

"Viongozi mliochaguliwa leo hakikisheni mnazingatia katiba ya SPC na msifanye mambo kwa kukurupuka. Pia kamati tendaji isiendeshe SPC kwa chuki bali itoe fursa sawa kwa wanachama na msitengeneze makundi baina yenu, viongozi wapewe ushirikiano na wasisite kutuomba ushauri na mawazo," amesema Malunde.

Msimamizi wa uchaguzi huo, David Nkulila amesema utaratibu wote umefuatwa na hakuna malalamiko yoyote na kwamba SPC imefanikisha uchaguzi huo kwa utulivu mkubwa, ambapo amewasihi wanahabari hao kuendelea kuwa wamoja kukijenga chama chao na kuyapigania maslahi ya nchi.

Pia mkutano huo kwa kauli moja umewapitisha Stella Ibengwe, Simeo Makoba, Suleiman Abeid, David Nkulila na Hakimu Masesa kuwa wajumbe wa Kamati ya Maadili na Usuluhishi ya Klabu hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi huo, David Nkulila akizungumza wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Shinyanga Press Club
Mwenyekiti Mpya wa SPC, Greyson Kakuru akizungumza baada ya kutangazwa mshindi nafasi ya mwenyekiti wa SPC
Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Kadama Malunde (kulia) akimpongeza mwenyekiti mpya wa SPC Greyson Kakuru
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde akiwashukuru wanachama baada ya kumaliza muda wake huku akiwahimiza waliochaguliwa kuzingatia maadili na kuacha kutoa maamuzi ya haraka yatakayowaumiza wanachama wa klabu hiyo.
Katibu Mtendaji mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Ali Lityawi akizungumza
Wajumbe wakifuatilia mchakato wa uchaguzi
Wanachama wa SPC wakiwa ukumbini kukamilisha zoezi la uchaguzi wa klabu yao
Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao (2015 - 2020) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuvunja kamati tendaji kupisha uchaguzi wa viongozi wapya leo Julai 4,2020
Viongozi wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao (2015 - 2020) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuvunja kamati tendaji kupisha uchaguzi wa viongozi wapya leo Julai 4,2020
Safu mpya ya uongozi wa SPC ikiwa katika picha ya pamoja na msimamizi wa uchaguzi huo, David Nkulila (kushoto).
Safu mpya ya uongozi wa SPC ikiwa katika picha ya pamoja
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakifuatilia uchaguzi huo
Baadhi ya wanachama wa SPC wakifuatilia kwa umakini hoja za wagombea wa nafasi mbalimbali
Makamu Mwenyekiti mpya wa SPC, Patrick Mabula (kushoto)
Baadhi ya wanachama wakiwa ukumbini
Mmoja wa Wajumbe wapya wa Kamati Tendaji ya SPC, Marco Maduhu akifuatilia mchakato wa uchaguzi
Mwanachama wa SPC, Moshi Ndugulile akiwashukuru wapiga kura licha ya kushindwa katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Klabu hiyo.

Picha na Marco Maduhu na Salvatory Ntandu
Share:

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba Amsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba  amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Faki Suleiman Khatib kwa alichokidai ni kuimarisha kamati tendaji ya chama hicho.

Taarifa ya CUF kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 4,2020 imesema hatua hiyo ni katika kutekeleza agizo la Baraza Kuu la kuondoa Mapungufu na Kuimarisha Kamati Tendaji.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar itajazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linalotarajiwa kuketi mwishoni mwa mwezi huu.


Share:

Tundu Lissu Achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu,  amechukua fomu ya kugombea urais wa Tanzania, kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
 
Fomu hiyo imechukuliwa leo Jumamosi tarehe 4 Julai 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam na  wakala wa Lissu  David Jumbe

“Nimekuja kwa ajili ya kuchukua fomu kama wakala wa Tundu Lissu, mnafahamu Lissu yuko nje ya nchi.

“Tukitoka hapa, tutaanza kazi ya kujaza na kutafuta wadhamini na kwa mujibu wa maelekezo, tupate wadhamini 100 kwa kila kanda. Tukitoka hapa tutaanza Kanda ya Pwani,” amesema Jumbe.


Share:

Chama cha UDP Chatangaza Kumuunga Mkono Rais Magufuli Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu

Chama cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020  endapo Chama chake cha CCM  kitampitisha kuwa mgombea .

Maamuzi hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo Jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wake katika kipindi cha miaka mitano.

"Namsifu Magufuli kuweka Mazingira mazuri hospitali karibu na wananchi,kutuimarishia miundombinu ya Barabara na Reli," amesema  John Cheyo na kuongeza kuwa

"Tumeamua kumuunga mkono Rais Magufuli endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema


Share:

Tundu Lissu atangaza rasmi kurejea nchini Mwishoni Mwa Mwezi Huu

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu amesema mwishoni mwa mwezi Julai, 2020 atarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kisiasa. 

Amesema, atafanya hivyo ili aweze kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 Julai 2020.

Mikutano hiyo, pamoja na mambo mengine, itampitisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Mchakato wa uchakuaji na urejeshaji fomu za kuwania Urais wa Tanzania unaanza leo Jumamosi tarehe 4 hadi 19,2020.

Wagombea au mawakala wao watakuwa na fursa ya kuchukua fomu kisha kutafuta wadhamini 100 katika kila kanda kumi za chama hicho.

Lissu ni miongoni mwa wanachama ambao wamekwisha tia nia hadharani ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki.


Share:

Takukuru yawajibu CHADEMA Kuhusu Madai Kwamba Inatumika Kisiasa Baada ya Kuwahoji Baadhi wa Wabunge Wa Chama Hicho

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imejibu madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa inatumika kisiasa, baada ya kuwahoji baadhi ya wabunge wa chama hicho kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilizokuwa zikikatwa kwenye mishahara ya wabunge pamoja na michango.

Taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali, John Mbungo imeeleza kuwa Takukuru ni chombo kinachojitegemea na kinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Imewataka wanachama wa Chadema kuendelea kutoa ushirikiano kuhusu tuhuma hizo kwa sababu wanatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007.

“Takukuru inawashauri wanachama wa Chadema kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea,” imeeleza taarifa hiyo.

Kapwani ameeleza kuwa wanachama wa Chadema ndio waliowasilisha malalamiko yao wakihoji matumizi ya fedha zilizokuwa zinakatwa kwenye mishahara ya wabunge wa viti maalum na wabunge wa majimbo.

“Hatua hii ni muendelezo wa uchunguzi unaofanywa na Takukuru Makao Makuu kuhusu malalamiko juu ya matumizi ya fedha za chadema, ambapo hatua ya sasa ni kuwahoji wabunge 69 wa chama hicho pamoja na wanachama wa zamani wa chama hicho,” imeongeza taarifa hiyo.

Takukuru walianza kuchukua hatua kuhusu tuhuma hizi baada ya waliokuwa wabunge wa chama hicho waliohamia vyama vingine kudai kuwa walikuwa wanakatwa mishahara yao tangu Juni 2016.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika malalamiko hayo ilidaiwa kuwa kila mbunge wa viti maalum wa Chadema alikuwa anakatwa Sh. 1,560,000 kwenye mshahara wake wa mwezi, na wabunge wa majimbo walikatwa Sh. 520,000 kwa kila mwezi kwenye mshahara wake.


Share:

Uwezo Wa Kusikiliza Mashauri Ya Jinai Wafikia Asilimia 105.06

Na Magreth Kinabo na Innocent Kansha – Mahakama
Jumla ya mashauri ya jinai 24,698 yalifunguliwa katika ngazi zote za Mahakama nchini nzima isipokuwa Mahakama za Mwanzo kati ya hayo 25,950 yalisikilizwa sawa na asilimia 105.06 ya mashauri yote yaliyofunguliwa katika kipindi cha Januari hadi Julai Mosi, mwaka huu.

Akizungumza wakati akitoa taarifa hiyo leo ya uendeshaji  wa mashauri hayo katika kipindi hicho, kwenye kikao kazi cha robo  mwaka ya pili ya mwaka wa  kimahakama cha mwaka huu kilichohusisha wadau wa Kamati ya Kitaifa ya  Haki Jinai.

Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha Mahakama hivi sasa ina uwezo wa kusikiliza mashauri yote yanayoingia mahakamani ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati.

‘‘Taarifa hii inaelezea hali ya ufunguaji na usikilizaji wa mashauri ya jinai kwa kipindi cha Januari hadi Julai Mosi, 2020 kwa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya nchi nzima.“Kwa upande wa Mahakama ya Rufani Tanzania, jumla ya mashauri ya jinai 297 yalifunguliwa na mashauri 210 yalisikilizwa sawa na asilimia 70.7 ya mashauri yote yaliyofunguliwa katika kipindi hicho,’’ alisema Kamugisha huku akisema wastani wa mzigo wa mashauri ni 737 kwa jopo la majaji wa tatu.

Alisema Mahakama Kuu ya Tanzania, mashauri ya jinai 2,561 yalifunguliwa na 2,618 yalisikilizwa sawa na asilimia 102.2. Wastani wa mzigo wa mashauri ni  345 kwa kila Jaji wa Mahakama     Kuu  ya Tanzania.

Kamugisha alisema katika Mahakama za Hakimu Mkazi jumla ya mashauri 5,338 yalifunguliwa, 5,566 yalisikilizwa sawa na asilimia 104.3 ya mashauri ya jinai yaliyofunguliwa. Hivyo wastani wa mzigo wa mashauri ni  198 kwa kila Hakimu.

“Mahakama za Wilaya mashauri 16,169 yalifunguliwa, mashauri 17,254 yalisikilizwa sawa na asilimia 97.5.Hadi kufikia Julai Mosi, 2020 wastani wa mzigo wa mashauri kwa Mahakama za Wilaya ni 96 kwa kila Hakimu,”alisisitiza

Aliongeza kwamba  mashauri 333 yalifungiliwa katika Mahakama za Watoto, 302 yalisikilizwa sawa na asilimia 90.6.

Kwa upande wa ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai    nchini, ambayo imewakilishwa na Naibu Kamishna wa Polisi Bw.Saleh Ambika alieleza kuwa lengo kuu la ofisi yake ni kuhakikisha upelelezi wa makosa ya jinai unafanyika na unakamilika kwa haraka zaidi kadri iwezekanavyo.

“Upelelezi wa makosa ya jinai una hatua mbalimbali na unahusisha taasisi mbalimbali za mfumo wa haki jinai kuna wakati mwingine Polisi wanahitaji kupata ripoti zinazotoka mamlaka nyingine kukamilisha upelelezi ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa wakati,” alisema Ambika.

Alifafanua kuwa upelelezi unaohusisha sampuli za kitu fulani, Kitengo cha Upelelezi lazima kishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakatiKmwingine sio rahisi kupata ripoti kwa kadri ya matarajio ya upelelezi wako, pia taasisi hiyo inataratibu zake za kiuchunguzi ili kukamilisha hilo,

Ambike alisema ushirikiano wadau hao upo kwa kiwango cha kutosha, hivyo hilo ndio lengo la kamati hiyo ni  kuisaidia Mahakama ya Tanzania kufikia ajenda ya kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani.

Mkurugenzi Msaidizi  kutoka Idara ya Huduma za Uangalizi kwa wafungwa wanaotumikia vifungo vya nje ya Magereza, Bw. Charles Nganze alisema wafungwa 706 walitumikia adhabu mbadala ya kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo ya Makaburi ya Kinondoni, mabwawa ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) , wizara na zahanati mbalimbali.

Naye  Kamishna Msaidizi wa Magereza, Bw,Willington Kamuhuza, alishukuru jitihada zilizofanywa na wadau hao zimesaidia kupunguza msongamano wafungwa kwa asilimia 0.73.Pia  aliongeza kwamba kwa kutumia  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) jumla ya mikoa 16 iliyo na magereza mashauri hayo yamesikilizwa kwa njia ya Mahakama Mtandao baada ya kuwezeshwa kuwa na vifaa vya TEHAMA kutoka Mahakama ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Uondoshaji wa Mashauri ya Jinai, ambaye pia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,  Mhe. Sharmillah Sarwatt alisema  lengo kikao hicho ni  kutathmini utendaji  kazi  na kupanga  mikakati ya kupunguza mlundikano wa mashauri  ya aina hiyo.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 4,2020














Share:

WANACHAMA WA PSSSF WATAKIWA KUFIKA KWENYE OFISI ZA MFUKO KUHAKIKI TAARIFA ZAO


 Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF viwanja vya Julius Nyerere

 Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe, akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kulia) na Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bw. Meseka Kadala
Afisa Matakelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald Meeda (kushoto), akimfafanulia masuala mbalimbali ya huduma za Mfuko, mwanachama huyo aliyepata fursa ya kutembelea banda la PSSSF.
 Afisa wa huduma kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Bi. Nelusigwa Mwalugaja (kushoto), akimfafanulia mwanachama huyu kuhusu michango yake.
 Afisa Mafao PSSSF, Bw.Abddallah Juma Adam (kulia), akitoa huduma kwa mwanachama aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julias Nyerere maarufu Sabasaba.
Afisa Matekelezo PSSSF, Bi. Zainab Ndullah (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo.
Mwanasheria wa PSSSF, Bw. David Mnkande (kulia), akifafanua kuhusu huduma za kisheria za Mfuko huo kwa wanachama hawa waliotembelea banda la PSSSF.
****


WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kufika kwenye ofisi za Mfuko huo zilizoenea katika mikoa yote nchini ili kuhakiki taarifa zao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 3, 2020, Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe alisema mwanachama akifika kwenye ofisi yoyote ya PSSSF utaratibu na mahitaji yako vile vile hivyo amewahimiza kufanya hivyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kutohakiki taarifa.

Lakini pia amewaalika wanachama watakaotembelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere kwenye maonesho hayo ya biashara maarufu kama sabasaba, wataweza kujipatia huduma zote kama zinavyotolewa kwenye ofisi za Mfuko kwenye mikoa yote nchini.

“Tulichofanya mwaka huu tumehamisha miundombinu na vifaa vyote vya kutoa huduma vinavyopatikana kwenye ofisi zetu ikiwemo makao makuu, hivyo mwanachama anapofika kwenye banda letu anapata huduma zote ikiwemo, taarifa za michango, mafao, pensheni na mafao yanayotolewa na Mfuko" alifafanua Bw. Mlowe. 

Maonesho hayo yaliyoanza Julai 1, 2020 yamefunguliwa rasmi Ijumaa Julai 3, 2020 na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa viwanda, ajira na biashara endelevu”.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger