Chama cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 endapo Chama chake cha CCM kitampitisha kuwa mgombea .
Maamuzi hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo Jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wake katika kipindi cha miaka mitano.
"Namsifu Magufuli kuweka Mazingira mazuri hospitali karibu na wananchi,kutuimarishia miundombinu ya Barabara na Reli," amesema John Cheyo na kuongeza kuwa
"Tumeamua kumuunga mkono Rais Magufuli endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema
0 comments:
Post a Comment