Friday, 8 May 2020

TAKUKURU Dodoma Yamkamata Mwanaume Mmoja Kwa Kujiita Afisa Wa Takukuru Chamwino Ikulu Huku Ikiokoa Milioni 194 Kutoka Kwa Wanachama Wa Saccos.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Mkoa wa Dodoma  inamshikilia Bw.Simon Mapunda  Jumbe[43]mkazi wa Kisasa jijini Dodoma  anayejishughulisha na kazi za ufundi ujenzi ,kwa kosa la kujifanya afisa  wa TAKUKURU   kinyume na kifungu cha 36 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya  329 marejeo ya mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa Habari ,Mei 7,2020,mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo amesema katikati ya mwezi April,mwaka huu walipokea taarifa ya mtuhumiwa Bw.Jumbe kuwa anajiita Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  ambapo amekuwa akiwalaghai  watu na kuwadai  fedha akisingizia kuwa atawasaidia kuwapatia ajira ndani ya TAKUKURU  na Ofisi zingine za serikali.
 
“Ufuatiliaji wetu umeonesha kuwa mtuhumiwa alimwahidi kaka  mtoa taarifa wetu kazi ya udereva  ndani ya TAKUKURU na baada ya mtu huyo kumweleza kwamba hana leseni ya udereva  daraja C ndipo mtuhumiwa  akataka apewe shilingi laki tatu na nusu[350,000/=]ili amsaidie kupata leseni .Baada ya kupata taarifa hii na sisi tukaweka mtego wa kumnasa mtuhumiwa akiwa eneo la Kisasa jijini Dodoma  tarehe 14/4/2020”amesema Bw.Kibwengo.
 
Mkuu huo wa  TAKUKURU ameendelea kufafanua kuwa ,awali mtuhumiwa alimweleza mtoa taarifa kuwa TAKUKURU imetangaza nafasi za kazi nane za ajira ya madereva na kwamba  kwa kuwa nafasi nne zimeshachukuliwa  ,yeye atamsaidia mdogo wake  kupata nafasi moja katika zile nafasi zilizosalia.
 
“Baada  ya hapo tuliendelea na uchunguzi na kubaini kwamba mtuhumiwa alishawahi kujiita afisa wa TAKUKURU Chamwino IKULU  na kumtapeli rafiki wake wa kike ambaye alimtumia Shilingi laki mbili na elfu kumi na nne[214,000/=]ili amsaidie dada yake amsaidie dada  yake kupata ajira serikalini na fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya mafaili  na sare za kazi.
 
Ufuatiliaji zaidi ukatuwezesha kumbaini pia kijana mwingine ,mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma[UDOM] ambaye yeye  na baba yake wametapeliwa na  Bw.Jumbe ambaye alijiita afisa wa TAKUKURU Chamwino  Ikulu jumla  ya Tsh.Milioni mbili laki nne na hamsini na mbili elfu na mia tano [2,452,500/=]fedha hizo zilitolewa ili awasaidie kumwezesha mwanafunzi huyo kupata ajira kama msaidizi wa mkurugenzi wa TAKUKURU .
 
Mtuhumiwa alidai kupatiwa fedha hizo alizokuwa analipwa kidogokidogo  na kwamba zilikuwa kwa ajili ya gharama mbalimbali zikiwemo kufungua akaunti ya kupokelea mshahara,sare za kazi,silaha na mafunzo ya kuitumia ,matumizi wakati wa mafunzo,ukarabati wa nyumba atakayoishi akianza kazi,tiketi ya ndege ya wazazi wake  kwenda DSM Kushuhudia akiapishwa na kuja Dodoma kutoka DSM na TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tunaendelea nauchunguzi.”Amesema.
 
Wakati huohuo Bw.Kibwengo amesema  TAKUKURU mkoa wa Dodoma imewafikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma na kuwafungulia shauri la jinai  Na.80/2020 watu watatu ambao ni Bw.Chizenga Masagasi Chimya [56] ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Muungano wilaya ya Chamwino na Wistone Chagulula[45] mwenyekiti wa kijiji hicho kwa makosa kuomba na kupokea  hongo ya Tsh.elfu sabini[70,000/=]ili waweze kuhamisha lalamiko la mtoa taarifa kwenda polisi kwa hatua zaidi.
 
Wa tatu ni Bw.Ivani Nganje [48]ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Iyoyo kilichopo katika kijiji cha Muungano wilayani Chamwino naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na kupokea Tsh. Elfu ishirini na tano [25,000/=]kutoka kwa mtoa taarifa huyo ili aitishe baraza la kitongoji  kwa lengo la kusikiliza lalamiko lake makosa hayo yote ikiwa ni kinyume  na kifungu cha 15[1][a] cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa,sura ya 329 marejeo ya 2018.
 
Aidha,Bw.Kibwengo amebainisha kuwa katika kuendelea kutekeleza agizo la serikali la kufuatilia madeni ya vyama vya ushirika ,kwa kipindi cha April,2020 TAKUKURU mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha shilingi Milioni hamsini na saba laki tano sitini na sita elfu mia mbili themanini na mbili na  senti hamsini[57,566,232.50/=]kutoka kwa  viongozi na wanachama  41 wa vyama sita  vya akiba na mkopo[SACCOS]Waliochukua wakidaiwa kwa muda mrefu.

Kutokana na takwimu hizo Bw.Kibwengo amesema hadi sasa TAKUKURU mkoa wa Dodoma imeshaokoa Jumla yaTsh.milioni mia moja tisini na nne na kuanzia wiki ijayo  kwa kushirikiana na Mrajis wa Msaidizi wa vyama vya ushirika  watakabidhi fedha hizo kwa SACCOS husika  zinazostahili.
 
Pia.Bw.Kibwengo ametumia fursa hiyo kukikumbusha chama cha Walimu Tanzania[CWT] mkoa wa Dodoma   ambacho kinaendelea na chaguzi kwa ajili ya kupata viongozi wapya  kufanya uchaguzi uhuru na haki bila mianya ya rushwa ili kupata viongozi bora na TAKUKURU inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchaguzi huo.


Share:

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela Atoa Siku Tatu Watumishi Warudishe Milioni 22 Walizotumia

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walio tumia fedha za makusanyo ya ndani kiasi cha shilingi milioni 22.083 wametakiwa kuzirudisha ndani ya siku tatu huku Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU ikielekezwa kusimamia hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa agizo hilo  wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje la kujadili  hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Brig. Jen, Mwangela amesema hakuna mtumishi au mtu yeyote atakayetumia fedha za Serikali kwa Mkoa wa Songwe akabaki salama hivyo wote wanaodaiwa kukusanya mapato ya ndani na kuyatumia waziridishe au wakamatwe hadi watakapo zirudisha fedha hizo.

Amesema TAKUKURU hawapaswi kucheka na wala fedha za serikali kwakuwa madiwani wanahangaika kwa kushirikiana na serikali kubuni vyanzo vya mapato ili fedha hizo zitakazo kusanywa ziboreshe huduma za jamii na kukuza uchumi hvyo wanaozitumia hawapaswi kuvumiliwa.

Brig. Jen Mwangela ameongeza kuwa katika taarifa ya CAG Halmashauri ya Wilaya Ileje imepata hati yenye mashaka katika kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi hivyo Mkurugenzi ahakikishe wataalamu wake wanafuata sheria na taratibu za Manunuzi pia madiwani wahahakishe wana simamia watumishi wasikiuke taratibu hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji Mnasi amemshukuru Mkuu Wa Mkoa wa Songwe kwa kushiriki kikao hicho na kuahidi kuwasimamia watumishi wafuate taratibu na sheria.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa MaY 08




















Share:

Thursday, 7 May 2020

PROFESA ALIYEKUWA ANAFANYA UTAFITI KUHUSU VIRUSI VYA CORONA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAREKANI

Mauaji ya raia wa China, mtafiti wa masuala ya virusi vya corona kwenye ardhi ya Marekani yamesababisha nadharia mbalimbali duaniani kuwa kuna sababu iliyojificha kuhusu kifo chake.

Bing Liu, profesa msaidizi mwenye miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Pittsburgh, Marekani alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake siku ya Jumamosi.

Wenzake walisema alikuwa karibu kupata "matokeo muhimu" ya tafiti kuhusu Covid-19, tukio lililosababisha kuwepo kwa maoni mitandaoni yanayoeleza kuwa yawezekana bwana Liu aliuawa lakini polisi wanasema ni tukio la kujiua.

Kwa nini Liu aliuawa?

Alikutwa akiwa na majeraha mengi ya risasi kichwani,shingoni katika eneo la Pittsburgh yalipo makazi yake kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo.

Mtu aliyekuwa na silaha alitambulika kuwa na miaka 46, mhandisi wa programu ya kompyuta, Hao Gu. Mamlaka zinasema muuaji naye alijiua baada ya kurudi kwenye gari lake.

Liu na Gu walikuwa wanafahamiana, maafisa wapelelezi wa mauaji walieleza.

Uchunguzi umebaini kuwa lilikuwa tukio la kuua na kujiua lililotokana na ''mgogoro wa muda mrefu wa masuala ya kimapenzi''.

Wamesema ''hakuna ushahidi'' wa kuhusisha tukio hilo na utafiti wa Liu na mazingira ya sasa ya changamoto za kiafya.
Liu ni nani?

Katika taarifa yao , wenzake wamemwelezea kama mtafiti wa kipekee ambaye ''alikuwa ukingoni kufanikisha kupata matokeo muhimu '' ya kuelewa maambukizi ya Covid-19.

Waliomboleza kifo cha Liu na kuahidi kumalizia utafiti wake ''zikiwa ni juhudi za kuenzi ubora wake katika uwanja wa kisanyansi''.

Liu, raia wa China alipata shahada yake ya kwanza na shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi ya kompyuta nchini Singapore kabla ya kufanya utafiti nchini Marekani.

Aliwahi kuungana na wanabaiolojia wengine kufanya utafiti kuhusu kinga ya binaadamu, kwa mujibu wa wasifu wake mtandaoni.

Yanayozungumzwa mitandaoni.

''Mungu wangu'' mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii wa Weibo aliandika. '' Labda alibaini kuwa virusi vilitengenezwa kwenye maabara nchini Marekani.''

Maoni kama hayo yalieleza kuwa Liu aliuawa kwa sababu pengine aligundua chanzo cha virusi vya corona.

Maafisa wa China na vyombo vya habari vya habari vya serikali vilisema kuwa madai yakuwa virusi vilitengenezwa Marekani na kupelekwa Wuhan na wanajeshi wa Marekani hayana msingi.

Wengine walisema ni tukio ambalo lina sababu iliyojificha.

''Inawezekana kuwa kuna siri iliyojificha gizani''. Alieleza mtu mmoja kwenye mtandao huo.

Maoni mengi ya watu kwenye mtandao huo yanasema kuwa historia ya Liu inaweza kuwa ndio iliyomuweka hatarini nchini Marekani, ingawa hakuna ushahidi ulioibuka kuwa Liu alikuwa akilengwa kwa sababu ya asili yake.

Gazeti ka Global Times linalofungamana na chombo cha habari cha taifa nchini china, lilichapisha makala kuhusu mazingira ya kifo cha Liu.

Kwenye mtandao wa Twitter, baadhi wameeleza hisia zao kuwa huenda serikali ya China ina mkono wake kwenye tukio hilo.

Kutokana na janga la Covid-19, nadharia mbalimbali kuhusu virusi na asili yake zimeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Nyingine zikiwa na madai yasiyothibitishwa zimekuwa zikiungwa mkono na wanasiasa na vyombo vya habari vya China na Marekani.
CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

WAGONJWA WA CORONA ZANZIBAR WAFIKA 134






Share:

Picha : WATOA HUDUMA ZA AFYA KAHAMA WAPEWA ELIMU YA CORONA..MGANGA MKUU ATAKA WAGONJWA WAPEWE HUDUMA STAHIKI


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akifungua Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya kutoka katika vituo vya afya halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amewashauri watumishi wa sekta ya afya kutumia taaluma zao vizuri kuwa na ujasiri na moyo wa kulitumikia taifa katika kipindi hiki cha Janga la Corona huku akisisitiza kuwa siyo kila mgonjwa mwenye dalili za Corona na ana Corona hivyo asinyimwe haki ya kutibiwa magonjwa mengine. 

Dkt. Ndungile ameyasema hayo leo Alhamis Mei 7,2020 wakati akifungua Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira. 

Alisema katika janga hili la Corona matumaini ya Watanzania yapo kwa watumishi wa sekta ya afya hivyo msingi mkubwa ni kutoa matibabu sahihi kwa mgonjwa bila kujali rangi,kabila ,dini ,uwezo wake ama mahali anapotoka ili kuzuia vifo visivyokuwa vya lazima. 

“Sisi watumishi wa afya ni sawa na pale inapotokea vita matumaini ya wananchi yanakuwa kwa askari. Kwenye janga hili la Corona sisi ndiyo kimbilio. Tunatakiwa kuwa na ujasiri na moyo wa kulitumikia taifa letu. Hatutarajii mtu amekuja kwenye kimbilio halafu na wewe unamkimbia au unamnyima huduma stahiki au unamtenga au unamnyanyapaa kwa sababu umehisi ana Corona”,alisema Dkt. Ndungile. 

Aliwataka wataalamu wa afya kutumia taaluma yao vizuri ili kuokoa maisha ya Watanzania huku akiwataka kuondoa hofu,wasiwasi na mashaka akisisitiza kuwa kitendo cha mtu kuwa na dalili za Corona kisimnyime haki ya kutibiwa magonjwa mengine. 

“Kuna wagonjwa wengine watakuja na magonjwa mengine tofauti na Corona. Historia ya mgonjwa ichukuliwe kwa mujibu wa taratibu za kitabibu,huenda mtu ana homa,anakohoa, ana kifua Kikuu,Maleria, shinikizo la damu,tatizo la moyo,Kisukari, Aleji, Pumu, HIV nk. Kwa hiyo lazima tutambue kuwa mgonjwa atatibiwa kwa ujumla wake na siyo tu kuangalia kipengele cha Corona”,alieleza Dkt. Ndungile. 

“Niwaombe sana wataalamu tusiwanyanyapae wagonjwa maana unaweza kuzuka mtindo..Hivi wewe umetokea wapi? Dar wiki mbili zilizopita..Aaah! kaa huko kwenye hicho chumba! Na pengine anaweza tu akawa na hofu kuwa ana Corona…Yaani wewe hujachukua hata historia ya mgonjwa,hata vipimo tayari wewe unamtenga,halafu humpi huduma yoyote akisubiri mpaka vipimo vya Corona”,alisema Dkt. Ndungile. 

“Kuna mwingine unakuta ana pumu, mwingine matatizo tu ya presha,hajatumia dawa,presha imepanda na presha ikiwa juu sana mtu anaweza kubanwa na kifua,mbavu na wakati mwingine vichomi, Sasa wewe ukisikia tu mbavu zinauma unasema hii ni Corona halafu unamfungia hapo unasubiri hadi DMO akupe maelekezo matokeo yake mtu anapoteza maisha”,aliongeza Dkt. Ndungile. 

Mganga huyo wa Mkoa alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo juu ya Corona kwa watoa huduma za afya mkoani Shinyanga ili wawe na uelewa mzuri kuhusu namna ya kutambua na kubaini mgonjwa wa Corona,kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa,namna ya kuzuia maambukizi yasienee na kujilinda wasipate maambukizi.

"Ninalishukuru Shirika la LifeWater International kwa kuwezesha mafunzo haya ya Corona kwa watoa huduma za afya mkoani Shinyanga.Tayari tumetoa mafunzo kama haya katika halmashauri ya Shinyanga,Manispaa ya Shinyanga na Kishapu na kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Mji, Msalala na Ushetu mafunzo yanafanyika leo na kesho",alisema Dkt. Ndungile. 

Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima alisema wameamua kushirikiana na serikali kutoa mafunzo ya COVID -19 kwa watoa hudumza a afya kwa sababu wapo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya COVID- 19. 

“Tumeona nyinyi ni watu muhimu sana ambao mnatakiwa kupata mafunzo haya na mkayafanyie kazi kwa kujilinda nyinyi wenyewe na kusaidia wale mnaowahudumia. Bila wataalamu wa afya pengine tunaweza kuwa na tatizo kubwa sana la COVID -19”,alisema Malima. 

“Nyinyi ndiyo mnakutana na wagonjwa,nyinyi ndiyo mnakutana na washukiwa kwa hiyo msipokuwa na uelewa mpana kuhusu COVID 19,msipotoa huduma kwa kuwajali na kujijali nyinyi wenyewe inaweza kuwa tatizo jingine”,aliongeza Malima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati akifungua Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira leo Alhamis Mei 7,2020 kwenye Ukumbi wa Kahama College of Health Sciences mjini Kahama. Kulia ni Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga,Benety Malima,kushoto ni Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga, Neema Simba Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akiwasisitiza wataalamu wa afya kutumia taaluma yao vizuri ili kuokoa maisha ya Watanzania huku akiwataka kuondoa hofu,wasiwasi na mashaka akisisitiza kuwa kitendo cha mtu kuwa na dalili za Corona kisimnyime haki ya kutibiwa magonjwa mengine.
Watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya wilayani Kahama wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ambaye alisema katika janga la Corona matumaini ya Watanzania yapo kwa watumishi wa sekta ya afya hivyo msingi mkubwa ni kutoa matibabu sahihi kwa mgonjwa bila kujali rangi,kabila ,dini ,uwezo wake ama mahali anapotoka ili kuzuia vifo visivyokuwa vya lazima.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' ambapo alisema wameamua kushirikiana na serikali kutoa mafunzo ya COVID 19 kwa watoa hudumza a afya kwa sababu wapo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya COVID 19.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya wilayani Kahama "..alisema “Tumeona nyinyi ni watu muhimu sana ambao mnatakiwa kupata mafunzo haya na mkayafanyie kazi kwa kujilinda nyinyi wenyewe na kusaidia wale mnaowahudumia. Bila wataalamu wa afya pengine tunaweza kuwa na tatizo kubwa sana la COVID 19”
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya wilayani Kahama 
Watoa huduma za afya katika vituo vya afya wilayani Kahama wakiwa ukumbini.
Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga, Neema Simba akizungumza wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira.
Mratibu wa Huduma za Afya mkoa wa Shinyanga, Dkt. Daniel Mzee akitoa mada wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira.
Watoa huduma za afya katika vituo vya afya wilayani Kahama wakiwa ukumbini.
Afisa Afya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Musa Makungu akijibu swali la mshiriki wa mafunzo hayo.
Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada wakati wa Mafunzo juu ya ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma za afya 43 kutoka katika vituo vya afya vya serikali na watu binafsi wilayani Kahama 'halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Msalala' yaliyofadhiliwa na Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira.
Watoa huduma za afya katika vituo vya afya wilayani Kahama wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya katika vituo vya afya wilayani Kahama wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA OFISI YA UWT SHINYANGA NA FEDHA OFISI YA CCM KITANGILI






Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi. 

 Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, ametoa msaada wa seti moja ya Kompyuta kwa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga, pamoja na fedha taslimu shilingi 180,000/= kwa ajili ya kununua mifuko 10 ya saruji ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili.

Zoezi la kukabidhi Kompyuta na fedha hizo za kununua saruji limefanyika leo, Mei 7, 2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, na kushuhudiwa na wajumbe wa chama hicho akiwamo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ambaye ndiye aliomba msaada wa Kompyuta hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Kompyuta hiyo na fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 10 ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili, Mhe. amesema yeye ni mbunge wa mkoa mzima, hivyo ana jukumu la kuhudumia wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga pamoja na chama chake kwa ujumla.

Amesema baada ya kuambiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kuwa Kompyuta ya UWT Wilaya ya Shinyanga ni Mbovu, akaguswa na kuamua kutoa msaada huo ili kazi za Chama zisiweze kulala sababu ya ubovu wa kifaa hicho na kutoa huduma kwa wananchi.

“Nimeamua kutoa msaada wa Computer kwenye ofisi hii ya UWT wilaya ya Shinyanga, na mimi UWT ndiyo wamenilea hadi nikapata ubunge, na baada ya kuambiwa na DC kuwa Computer yao ni mbovu ikabidi niitafute haraka, na leo hii naikabidhi rasmi ili iweze kufanya kazi za chama,” amesema Mhe. Azza.

“Computer hii ina thamani ya Shilingi Milioni 2, ambapo pia natimiza na ahadi yangu ya kutoa mifuko 10 ya saruji ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili, ambapo natoa pesa Taslimu Shilingi 180,000 ,” ameongeza.

Aidha amesema ameshachangia pia vifaa tiba katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga, ambapo ametoa vitanda vitatu kwa ajili ya wazazi pamoja na mashuka 30.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Shambuo Katambi, amempongeza Mbunge huyo kwa kutoa msaada wa Computer ambao utasaidia kusaidia kazi za chama kusonga mbele, huku akimuomba aendelee na moyo huo huo wa kujitoa kusaidia jamii pamoja na chama.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amempongeza mbunge huyo kwa kuitikia ombi lake na kutoa msaada huo wa Computer, pamoja na kuwabeba kidedea wanawake kwenye nafasi za uongozi kwa kuchapa kazi kwa bidii.

Pia Mboneko ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Shinyanga, kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kuacha kufukiza watoto wadogo na kuwazuia wasizurure hovyo mitaani.



TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog.

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya yaShinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 180,000 katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Gregrory kwa ajili ya ununuzi wa mifuo 10 ya saruji ambayo itasukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza mara baada ya kukabidhi Computer na fedha Taslimu Shilingi 180,000 ahadi yake ya ununuaji wa mifuko 10 ya saruji.

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Mjini  Hadija Magoma Hassani, akimshukuru mbunge Azza kwa msaada huo alioutoa.

Mwenyekiti wa umoja wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi akishukuru kwa msaada huo kutoka kwa Mbunge Azza.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Gregory akishukuru kwa msaada ambao ameutoa mbunge Azza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akimshukuru Mbunge Azza, kwa moyo wake wa kujitoa kusaidia jamii na chama katika nyanja mbalimbali zikiwamo huma za afya na elimu.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog.

Share:

Vifo Vya Corona Kuchunguzwa

Na WAMJW – Mwanza
Vituo vya kutolea huduma za afya nchini vyatakiwa kufanya uchunguzi juu ya kifo chochote kitakachotokana na ugonjwa wa corona ili kubaini kama mgonjwa alihudumiwa ipasavyo kabla ya kifo kutokea.
 
Agizo hilo limetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akiwa Jijini Mwanza mara baada ya kuagana na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa – Bugando alipokuwa akifanya kazi awali kama Mkurugenzi Mtendaji kabla ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
 
“Kwakweli tusingependa kuona mgonjwa anafariki kwa sababu zisizo na msingi, naagiza hospitali zote zenye kamati ya uchunguzi (Clinical Audit) kufanya uchunguzi wa vifo vinavyohusiana au kutokana na corona ili kuona kama kulikuwa na tatizo lolote katika kumpokea mgonjwa au katika kumhudumia” alisema Prof. Makubi
 
Prof. Makubi amewataka wananchi kuelewa kuwa sio kila kifo kinachotokea hivi sasa kinasababishwa na ugonjwa wa corona kwa kuwa yapo magonjwa mengine pia ambayo yanatushamblia binadamu. 
 
“Siyo kweli kwamba mgonjwa akiwa na presha, kisukari, figo au kansa akifariki iwe imesababishwa na corona, tuendelee kuwahudumia wananchi, kuepusha vifo vinavyoweza kuwa na uhusiano wa corona”. Alisema Prof. Makubi.
 
Aidha, Prof. Makubi ametoa rai kwa vituo vya afya kuwapokea wagonjwa wote na kuwapatia matibabu bila kuwabagua kuwa na dalili za corona.
 
“Serikali inapenda kuona wagonjwa wa corona wanapokelewa nakupata matibabu, tuendelee kuwapokea na kuwahudumia huku tukichukua tahadhari ya maambukizi”. Alisema Prof. Makubi.
 
“Watumishi wa afya wasiwe na ubaguzi wa kuchagua wagonjwa wa kuwahudumia au mpaka apimwe kipimo cha covid-19 ndio ahudumiwe, tuwapokee wote lakini wakati huo tukichukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa”.  Alisisitiza Prof. Makubi.
 
Katika hatua nyingine Prof. Makubi amesema kuwa Serikali inaendelae kusambaza vifaa kinga kwa ajili ya kuwawezesha watoa huduma kujikinga na ugonjwa huo wakati wakitoa huduma.
 
“Serikali imeanza kugawa vifaa kinga kama vile PPE, masks pia sanitizer kwa ajili ya vituo vyote vya afya Tanzania, kwahiyo pasiwepo kisingizio chochote cha kushindwa kumhudumia mgonjwa wa corona kwa sababu ya vifaa kinga”


Share:

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 607...Ni Baada ya Wengine 25 Kuongezeka Leo

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona, hii ni baada ya watu  632 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita  na kufanya jumla ya wealioambukizwa kufikia  607 .

Wagonjwa hao ni wakenya 22,raia mmoja wa Tanzania,mmoja wa Uganda na mmoja wa China.

Naibu waziri wa afya Dkt Rashid Aman ametoa wito kwa wakazi wa Mtaa wa Eastleigh kufuata kanuni zilizotangazwa na wizara ya afya kusalia nyumbani baada ya idadi kubwa ya watu kudaiwa kuhamia mitaa mingine.

Aidha idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 29 baada ya watu watatu zaidi kufariki.
 
Idadi ya waliopona imefikia 197 baada ya watu 7 zaidi kupona.


Share:

Dkt. Ndugulile: Endeleeni kutibu watu wenye magonjwa mengine na si wa Covid -19 tu

Na John Stephen, WAMJW – Dar es Salaam
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wataalamu wa afya kuendelea kutibu watu wenye magonjwa mengine kama vile matatizo ya moyo na figo katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kuitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kuwaona wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo.

Dkt. Ndugulile amesema pamoja na kuwapo kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona, watu wenye matatizo ya moyo, kupumua, figo, kisukari pamoja na matatizo mengine wanapaswa kupatiwa matibabu.

“Tunaweza tukawa tunapambana na Corona, tukawapoteza wagonjwa wengi kwa sababu tu hatujaweza kuwapatia huduma ya matibabu ya kisukari, figo, presha au moyo, hivyo nitoe rai kwa wahudumu wa afya wahakikishe wanaendelea kuwatibu watu wenye magonjwa haya pamoja na magonjwa mengine,” amesema Dkt. Ndugulile.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile amewapongeza wataalamu wa JKCI kwa kufanya upasuaji wa kupandikiza mishipa kwenye moyo kwa wagonjwa waliokuwa na matatizo ya moyo.

 “Sisi kama Wizara ya Afya, tunapata faraja sana, mambo kama haya ni mazuri na lazima tuseme kwa hiyo hii operesheni mliofanya ni kubwa na nje ya nchi ingetugharimu shilingi milioni 80 hadi 90 kwa mtu mmoja, lakini hapa tumefanya kwa shilingi milioni 29 kwa kutumia wataalamu wetu na wagonjwa wetu wanaendelea vizuri,” amesema Dkt. Ndugulile. 

Amesema awali wataalamu kutoka nje ya nchi walikuwa wanakuja kufanya upasuaji kama huo, lakini sasa Watanzania wazalendo wanafanya baada ya kutoa mishipa kwenye paja na kwenye kifua cha mgonjwa husika.

“Leo nimekuja kuona kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wazalendo wa JKCI ya upasuaji wa kupandikiza mishipa kwenye moyo ili uweze kufanya kazi kwa wagonjwa waliokuwa wakikabiliwa na matatizo ya moyo,” amesema Dkt. Ndugulile.

Naye Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI, Dkt. Angella Muhozya amesema kuwa wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji na wataalamu wazalendo wanaendelea vizuri na kwamba wataruhusiwa muda wowote kuanzia sasa.

Mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo, Bw. Hamid Nassoro amesema baada ya kufanyiwa upasuaji hivi sasa anaweza kuzungumza vizuri tofauti na awali alikuwa hawezi kuzungumza na kwamba tayari ameshaanza mazoezi.


Share:

Tanzia: Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Hamim Buzohera Gwiyama afariki dunia

Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoa wa Geita,  Hamim Buzohera Gwiyama, amefariki leo Mei 7, 2020 Saa 5:00 Asubuhi katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa ya msiba huo imetolewa na Waziri wa Nchi - TAMISEMI Selemani Jafo.

Marehemu Hamim Buzohera Gwiyama aliteuliwa na Rais John Magufuli Juni 26, 2016 kuwa mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale.

Aidha Waziri wa Nchi - TAMISEMI Selemani Jafo ametoa pole wa familia na ndugu na kueleza taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger