Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona, hii ni baada ya watu 632 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya wealioambukizwa kufikia 607 .
Wagonjwa hao ni wakenya 22,raia mmoja wa Tanzania,mmoja wa Uganda na mmoja wa China.
Naibu waziri wa afya Dkt Rashid Aman ametoa wito kwa wakazi wa Mtaa wa Eastleigh kufuata kanuni zilizotangazwa na wizara ya afya kusalia nyumbani baada ya idadi kubwa ya watu kudaiwa kuhamia mitaa mingine.
Aidha idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 29 baada ya watu watatu zaidi kufariki.
Idadi ya waliopona imefikia 197 baada ya watu 7 zaidi kupona.
0 comments:
Post a Comment