Wednesday, 6 May 2020

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA VITI NA NGAO ZA USO 'FACE SHIELDS' KUKABILIANA NA COVID 19 KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA

Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Ngao za uso 'Face Masks' kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.

***


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) pamoja na Ngao za Uso 'Face Shield'kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari vyote vikiwa na thamani ya shilingi 444,000/=.

Mhe. Azza amekabidhi vifaa hivyo leo Jumatano Mei 6,2020 kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga ,Kadama Malunde katika ofisi hiyo ya waandishi wa habari.

Mhe. Azza amesema Waandishi wa habari ni wadau muhimu katika mapambano ya Virusi vya Corona ndiyo maana ameona ni vyema awachangie vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Sote tunajua tupo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na tunatambua mchango mkubwa wa waandishi wa habari,mnafanya kazi kubwa katika kuhakikisha kwamba mnaielimisha jamii…Nimewaletea hizi ngao za uso ‘Face Shield’ ili angalau muweze kufunika uso wote..utakuwa umevaa barakoa ndani lakini unafunika uso wako wote ili uweze kufanya kazi zako vizuri”,alieleza Mhe. Azza.

“Kila mwandishi wa habari atapata Ngao ya uso ‘Face Shield’ moja. Ikichafuka unasafisha kwa kitambaa laini kwa maji na sabuni kisha unaendelea kutumia..Ni kitu ambacho siyo cha kutumia na kutupa, unaweza kutumia kwa muda mrefu”,aliongeza Azza.

“Niwasihi tujikinge, tujilinde na tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya. Hakuna ambalo linashindikana iwapo tutafuata masharti ya wataalamu wa afya”,alisema Azza.

Mbunge huyo pia amekabidhi viti vitano kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga baada ya kuombwa na Mwenyekiti wa SPC kuongeza viti kutokana na idadi kubwa ya waandishi wa habari wanaotumia ofisi hiyo.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyekiti wetu wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,aliniita siku moja nikaja hapa ofisini,lakini nilipofika tu akaniambia kuhusu upungufu mkubwa wa Viti katika ofisi kutokana na idadi kubwa ya waandishi wa habari…Sikumjibu kitu chochote niliondoka lakini baadaye nikasema niwaletee angalau hivi viti ili kuwaongezea katika ofisi ili muweze kupata sehemu za kufanyia kazi vizuri”,alisema Mhe. Azza.

“Leo nimeleta viti vitano kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga naamini vitawasaidia katika shughuli zenu za uandishi wa habari”,alisema Azza.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa SPC, Kadama Malunde alimshukuru Mbunge huyo wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad kwa msaada wa viti na ngao za uso kwa ajili kujikinga na maambukizi ya COVID 19 kwa waandishi wa habari.

“Mhe. Azza wewe ni mdau mkubwa katika Tasnia ya Habari mkoa wa Shinyanga,tunakushukuru kwa msaada huu wa viti kwa ajili ya ofisi ya waandishi wa habari lakini pia tunakushuru kwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya COVID 19”,alisema Malunde.

ANGALIA PICHA HAPA
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Ngao za Uso ' Face Shields' alizoleta kwa ajili ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona pamoja na Viti vitano alivyotoa kwa ajili ya Ofisi ya Waandishi wa  Habari  mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 6,2020. Picha zote na Marco Maduhu,Suleiman Abeid na Frank Mshana
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Ngao ya uso ' Face Shield' kwa ajili kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde akivaa Ngao ya uso ' Face Shield' kwa ajili kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona. Ngao hiyo ni sehemu ya ngao 36 zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ili kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Ngao za uso 'Face Masks' kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Ngao za uso 'Face Masks' kwa ajili ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kujikinga na maambukizi ya COVID 19 wanapotekeleza majukumu yao ya uandishi wa habari.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Viti kwa ajili ya Ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde Viti kwa ajili ya Ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza baada ya kutoa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) pamoja na Ngao za uso 'Face Shields' kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog akimshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) pamoja na Ngao za uso 'Face Shields' kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari wakiwa wamevaa ngao za uso baada ya kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) pamoja na Ngao za uso 'Face Shields' kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari wakiwa wamevaa ngao za uso baada ya kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya Ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) pamoja na Ngao za uso 'Face Shields' kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Awali Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (kulia) akipokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde alipofika katika ofisi ya SPC leo Jumatano Mei 6,2020 kwa ajili ya  kukabidhi msaada wa Viti kwa ajili ya SPC na ngao za uso 'Face Shields' kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi Vya Corona kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Awali Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kuwasili katika ofisi ya Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga. Aliyevaa nguo nyeusi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) - Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog

Picha zote na Marco Maduhu,Suleiman Abeid na Frank Mshana


Share:

Mchezo wa Ngumi Warejesha Heshima ya Tanzania Kimataifa

NGUMI ni miongoni mwa michezo ambayo imeitangaza na kuipa heshima Tanzania duniani kutokana na mabondia wake kuonyesha uwezo mkubwa na kushinda katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa.
Kutokana na sababu mbalimbali za kiutendaji wa viongozi wa mchezo huu, ulipoteza sifa yake Kitaifa na Kimataifa na kudidimiza maendeleo yake hapa nchini. Eleuteri Mangi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dodoma anaelezea jinsi mchezo huo unavyorejesha heshima iliyokuwa nayo Tanzania Kitaifa na Kimataifa katika miaka ya 1970.
 
Mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo inayofahamika na kupendwa sana na watu wengi duniani. Kama ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa miguu, mchezo huu umekuwa ni chanzo cha ajira na hivyo kujipatia umaarufu mkubwa ambapo vijana wengi wanajiunga kwa lengo la kujipatia kipato. Ndiyo kusema, michezo ni kiwanda kikubwa kinachobeba ajira lukuki kwa vijana na wataalam wa michezo mbalimbali nchini na duniani kote.
 
Mchezo wa ngumi nchini Tanzania ulianza kufahamika katika miaka ya 1950 ambapo miaka ya 1970 mabondia wake walianza kufahamika katika mashindando mbalimbali ya Kimataifa. Medali ya kwanza ya Kimataifa ililetwa na Titus Simba mwaka 1974 katika michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika nchini Uingereza na mwaka 1998 bondia mwingine Michael Yombayomba aliiletea Tanzania medali nyingine katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika nchini Malasia. 
 
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Tanzania kufahamika Kimataifa katika medani ya mchezo wa ngumi ambapo wanamasumbwi wengine kama vile akina Makoye Isangula, Stanrey Mabesi, Benjamin Mwangata, Shaaban Matumla na wengine walitamba na kuiletea Tanzania medali mbalimbali. Hata hivyo, kuzuka kwa vyama vingi vya ngumi nchini kumekuwa chanzo cha kushuka kwa mchezo huo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kutokana na viongozi wake kutoelewana kiutendaji kutokana na sababu mbalimbali.
 
Kwa kulitambua hili, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Johh Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kuchukua hatua kadhaa kuweza kurejesha heshima ya Tanzania Kitaifa na Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi.
 
Kuundwa kwa Kamisheni ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) ni mwanzo mpya unaodhihirisha nia ya dhati ya Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb). Utekelezaji wa agizo la kuanzisha TPBRC nchini umeanza kuleta manufaa kutokana na shabaha ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020 katika kukuza michezo.
 
Ilani hiyo katika ukurasa wake wa 218 Ibara ya 161 imetamka “Katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 imebainisha CCM itaielekeza Serikali kuimarisha sekta ya  michezo ili  kuinua kiwango  cha michezo  nchini ikiwa  ni  pamoja kuifanya sekta ya michezo kutoa  fursa  za ajira hususani kwa vijana”.
 
Kama michezo mingine, mchezo wa ngumi za kulipwa unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971 pamoja na kanuni za Usajili Na. 442 za mwaka1999.
 
Sheria hiyo iliyofanyiwa marekebisho ya Sheria Na. 3 kifungu cha 18 ya mwaka 2018 kwa mamlaka aliyonayo Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini yameongeza wigo na kutambua michezo ya ridhaa na michezo mingine ambayo yamepelekea kuundwa kwa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini.
 
Chombo hicho kimeleta mafanikio katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini na umekuwa na mchango mkubwa katika kuajiri vijana ambao wamekuwa na mafanikio kwa mtu mmoja mmoja akiwa mchezaji na taifa kwa ujumla.
 
Katika kuthamini michezo nchini ikiwemo masumbwi, Rais Dkt. Magufuli ni mpenda michezo amekuwa mstari wa mbele katika kutambua na kuwatuza wanamichezo wanapofanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. 
 
Mapema mwezi Machi mwaka 2019, Rais alidhihirisha uzalendo wake kwa michezo nchini kwa kuwapa wachezaji, viongozi wao na bondia Hassan Mwakinyo zawadi ya viwanja vya kujengea nyumba mkoani Dodoma kama ishara ya kuonyesha alivyofurahishwa kwa juhudi za wachezaji na viongozi wao kuipa Tanzania ushindi.
 
 “Nimeamua niwape zawadi kidogo kwa niaba ya watanzania, nitawapatia viwanja vya kujenga nyumba wachezaji wote wa Taifa Stars na viongozi wao, bondia Hassan Mwakinyo pamoja na mwalimu wako, zawadi hiyo pia kwa Peter Tino na Leodegar Tenga” alisema Rais Dkt. Magufuli.
 
Bondia Hassan Mwakinyo anapongezwa kwa kazi nzuri anayoendelea kuliwakilisha taifa vema katika mashindano mbalimbali duniani ikiwemo kumtwanga Amel Tinampay raia wa Ufilipino kwa point katika mchezo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Novemba, 2019.
 
Hakika mchezo wa ngumi za kulipwa umekuwa mwanzo mpya wa mabondia nchini kufanya vizuri katika mapambano waliyoshiriki. Bondia  Abdallah Paziwapazi alimchapa Zulipikaer  Maimaitiali raia wa China kwa Knock Out katika  pambano  la  WBO  Asia  Pacific Super  Middle  Title  lililofanyika  nchini China mwezi Agosti, 2019 wakati Hamis Maya alimtwanga Piergiulia Ruhe raia wa Ujerumani kwa Knock Out katika pambano la Global Boxing Council Intercontinental Welter lililofanyika nchini Ujerumani mwezi Novemba, 2019.
 
Mabondia wengine waliofanya vizuri na kuliletea Taifa sifa nzuri ni pamoja na Bondia Bruno Melkiory Tarimo (Vifua Viwili) ambaye alimpiga Nathaniel May raia wa Australia kwa point katika pambano la Boxing Federation International Super Feather Title lililofanyika nchini Australia mwezi Desemba, 2019 na Bondia Salimu Jengo aliyemchapa Suriya Tatakhun raia wa Thailand kwa KO katika pambano la Universal Boxing Organization World Light Title lililofanyika Jijini Tanga mwezi Januari, 2020.
 
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2020/2021 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewapongeza wachezaji wa Kitanzania wanaozidi kuongezeka na kufuzu vigezo vya kimataifa  na kucheza michezo ya kulipwa katika  nchi mbalimbali na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. 
 
“Nawapongeza wanamichezo wote nchini kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yetu katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na hivyo kuitangaza na kuiletea heshima kubwa nchi yetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
 
Waziri Mwakyembe aliendelea kusema “Namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake thabiti na hatua anazochukua kuimarisha michezo nchini. Nampongeza Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa kuipa wizara yangu ushirikiano mkubwa na msaada katika kuendeleza michezo nchini. Pia niwapongeze watanzania kwa hamasa na uzalendo wanaouonesha kwa timu zetu”. 
 
Kwa upande wake Promota Shomari Kimbau ambaye ni mdau wa mchezo wa masumbwi ameipongeza Serikali kwa kwa nia yake ya dhati ya kusaidia na kusimamia mchezo huo na kuamini usimamizi bora wa mchezo huo nchini ni mwanzo mpya wa Mchezo wa Ngumi za Kulipwa.
 
“Lazima yawepo mazingira mazuri ya kusimamia mchezo huu, ili upendwe na watu wengine pamoja na kurudisha imani kwa wadau na wawekezaji waweze kuwekeza fedha zao. Hiki kinachofanywa na Serikali ni kitu kizuri na kinafaa kuungwa mkono na wadau wa mchezo huu” anasema Kimbau.
 
Awali Ngumi za Kulipwa zilisimamiwa na Vyama tofauti tofauti ikiwemo Chama cha Wataalamu wa Mchezo wa Ngumi Tanzania (TPBO), Pugilistic organization of Tanzania (PST) na Tume ya Wataalamu wa Mchezo wa Ngumi Tanzania (TPBC). 
 
Mtindo huo wa kuongoza mchezo wa ngumi za kulipwa ulikuwa na namna ya vionozi na wachezaji kutoelewana wenyewe kwa wenyewe kabla ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuingilia kati mgogoro huo na kuamua kufanya mabadiliko katika mchezo wa Ngumi za Kulipwa ndipo TPBRC ilipoanzishwa na kupewa mamlaka ya kusimamia Ngumi za Kulipwa mnamo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa BMT, baada ya kuundwa Kamisheni  ya Ngumi za Kulipwa yapo mafanikio  yanayodhihirisha kuimarika kwa mchezo huo yanayochagizwa kuwepo kwa viongozi waliopatikana kwa uchaguzi uliofanyika Machi 31, 2019 ambao ni Joe Anea (Rais), Agapita Basil Jambwale (Makamu wa Rais), Yahya Poli (Katibu Mkuu), Bakari Songoro (Mweka Hazina), Hamisi Kimanga na Nassoro Chuma (Wajumbe).
 
Aidha, kuunganishwa kwa wadau wa ngumi za kulipwa umeibua mwamko mpya kwa wadau hao, mabondia wanafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ndani na nje ya nchi, kuongezeka kwa idadi ya wakuzaji wa mchezo wa ngumi, kuongezeka kwa  mapambano 35 ambayo yamefanyika kati ya Aprili, 2019  hadi Machi, 2020.
 
Fauka ya hayo, wadhamini kujitokeza kuwekeza katika kusimamia na kuhakikisha haki za mabondia zinazingatiwa ikiwemo kupitiwa kwa mikataba yao ya mapigano kabla ya pambano pamoja na kuimarika kwa mahusiano ya vyombo vya kusimamia michezo katika nchi tofauti pamoja na vyama vinavyoshindanisha mikanda tofauti duniani ikiwemo, WBO, WBA, WBC, ABU na UBO.
 
Hatua hiyo imesaidia wanachama wa Ngumi za kulipwa waliosajiliwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2019 kufikia 22, taswira ambayo inaonesha kuongezeka kwa mwamko wa kuanzisha na kusajili vikundi vya sanaa na michezo nchini.
 
Kulingana na takwimu hiyo, kati ya vikundi 22, vikundi 17 vinajihusisha na mchezo wa ngumi, sanaa na michezo mingine wakati vikundi vitano tu vilivyoanzishwa na kusajiliwa vinajihusisha na mchezo wa ngumi pekee.
 
Kwa hakika jambo hili linaonesha wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza agizo  la CCM  katika ilani yake iliyotolewa wakati wa uchaguzi wa 2015 kwani  kwa takwimu hizo ni kweli Serikali kwa kishirikiana na sekta binafsi imeweza kuanzisha vituo vya kuendeleza vipaji vya wanamichezo mahiri na kutumika kama vituo vya maandalizi ya wanamichezo wanaoiwakilisha Tanzania katika michezo ya kimataifa.
 
Kwa mantiki hiyo, mwandishi wa makala hii amebainisha kuwa mwamko wa kuanzisha michezo shirikishi ni mkubwa zaidi kuliko mchezo mmoja mmoja na hatua hii Serikali inapaswa kupongezwa kwani  chanda  chema huvishwa pete.
 
Kwa nafasi mafanikio haya na nafasi hii, mwanamichezo anayeshriki katika mchezo wa ngumi akiwa katika kikundi mazoezi (gym) anayonafasi kubwa zaidi ya kuwa mwanamasumbwi bora zaidi ya yule ambaye yupo kweye masumbwi pekee. 
 
Hatua hiyo inamsaidia mwanamichezo kuwa bora katika mchezo katika kikundi ambacho kinahusisha mchezo zaidi ya mmoja ana fursa ya kupata vifaa vinavyomsaidia kufanya mazoezi ya uhakika, utimamu wa mwili na kupata msaada wa kitaalamu katika mchezo husika kutoka kwa walimu mbalimbali wanaokuwepo wakati wa mafunzo na mazoezi yanayompa motisha unaompelekea kuwa mwanamichezo bora.
 
Hakika Kamisheni ya Kusimia Ngumi za Kulipwa imekuwa mwarobaini wa mchezo huo ambapo migogoro ya mara kwa mara imekuwa ni historia ikiwemo mapromota kuvamia tasnia hiyo na kuharibu mustakabali mzuri wa mchezo huo nchini.
 
Ni ukweli usiopingika, kila lenye mafanikio halikosi kuwa na changamoto, mchezo wa ngumi za kulipwa bado unakabiliwa na changamoto ya kutokuwepo kwa makocha wenye viwango vya kimataifa wenye nyota zinazotakiwa, vifaa vya kufanyia mazoezi, uhaba wa wadhamini pamoja na maeneo ya kufanyia mazoezi na ulingo unaotumika wakati wa mashindano. Kwa hakika Serikalia ya Awamu ya Tano itaendelea kuzitatua changamoto zote zilizosalia na kwa hakika mambo yatakuwa mazuri hivi punde.
 
Mafanikio haya yaliyofikiwa ni makubwa mno kwa mchezo huu ulionza kuchezwa hata kabla nchi yetu haijatawaliwa na wakoloni katika karne ya 19. Mchezo huu ulichezwa katika viwanja vikubwa vyenye mikusanyiko mikubwa ya watu (Coliseum) huko Roma na (Arena) huko Athina, iliyokuwa katika hekalu kubwa la ufalme wa Wayunani (Ugiriki) la Akropolis. Viwanja hivyo vilikuwa ndio mwanzo wa ulingo wa kisasa kwani japokuwa ulingo wa kisasa ni wa mraba lakini mwanzo wake ni Arena ya mduara.
 
Mwisho.


Share:

Makonda Atoa Masaa 24 Kwa Wabunge wote waliogoma kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar Warudi Bungeni....,Vinginevyo Watakamatwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliogoma kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam  kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji.

Makonda amesema kuwa Mbunge anayepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye kibali au ruhusa ya Spika wa Bunge, tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Mbunge anayepaswa kuwepo ni yule mwenye kibali cha Spika, kipindi hiki ni hatari na tunataka watu wanaotoka majumbani ni wale wanaoenda kufanya kazi, hatujaalika wazururaji kutoka mikoani, inawezekana wakahatarisha zaidi maisha ya wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwaambukiza Corona, kipindi hiki ni muhimu katika Bunge la Bajeti dhidi ya mahitaji ya wananchi" amesema Makonda.

Hata hivyo Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia maisha, badala ya kwenda majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na mafuriko.


Share:

Wizara Ya Viwanda Na Biashara Yaomba Kuidhinishiwa Zaidi Ya Tsh. Bilioni 81.4 Huku Wananchi Wakiaswa Kununua Bidhaa Za Viwanda Vya Ndani

Na.Faustine Gimu,Dodoma
Serikali imeendelea  kuhamasisha wananchi kununua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani  ili kujenga uchumi wa nchi ambapo  Katika mwaka 2019/2020, jumla miradi mipya 303 imesajiliwa .

Hayo yamesemwa jana  Mei,5,2020  jijini Dodoma na   Waziri wa  Viwanda na Biashara Mhe. Innocent   Bashungwa  Wakati akiwasilisha Bungeni  Hotuba ya Makadirio Ya Mapato na Matumizi Ya Fedha Kwa Mwaka 2020/2021   ambapo amesema Serikali imeendelea kuvilinda viwanda vya ndani kwa kuhakikisha vinapata malighafi ya kutosha kwa kutoza ushuru mkubwa, kuweka katazo kwa baadhi ya malighafi kwenda nje ya nchi na kutoa vibali maalum kwa baadhi ya bidhaa.

Katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu unayosababishwa na virusi vya Corona  [Covid-19 ], Mwezi Machi 2020, Wizara ilikutana na wazalishaji wa malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono na wazalishaji wa bidhaa hizo ambapo inaendelea na  ufanyaji tathmini ya mahitaji ya vitakasa mikono nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Mkemia Mkuu wa Serikali, Wazalishaji wa Vitakasa mikono , TMDA na TPMA.

Aidha,  Waziri Bashungwa amesema kupatikana kwa takwimu halisi  kutasaidia Serikali kufanya maamuzi ya haraka hususan ya kuagiza Ethanol ambayo ni malighafi muhimu katika kutengenezea vitakasa mikono  huku akitoa onyo kwa wafanyabiashara wanaotumia mazingira ya ugonjwa huo kama fursa ya kujinufaisha badala ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na Janga hili .

 Akiwasilisha Taarifa Ya Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu Ya Wizara Ya Viwanda na Biashara, Fungu 44-Viwanda Na Fungu 60-Biashara Kwa Mwaka 2019/2020 na Maoni Ya Kamati Kuhusu Makadirio Ya Mapato na Matumizi Fungu 44 Na 60 Ya Mwaka Wa Fedha 2020/2021 Makamu Mwenyekiti Kamati Ya Bunge Ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kanal Mstaafu,Masoud Ally Khamis ameishauri serikali kufuatilia kwa ukaribu mapato ya  makusanyo ya maegesho ya Magari na Makontena katika eneo la  Kurasini ili kubaini  kama fedha zilizokuwa zinakusanywa zilikuwa zinafika katika mfuko mkuu wa serikali.

Wakichangia hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara  ,Mbunge  wa Geita Vijijini Joseph Msukuma ametaka serikali kuchukua maamuzi ya kuwafungulia wawekezaji,ambapo mbunge wa viti Maalum Zainab Mndolwa ameishauri serikali kuona namna ya kuwapunguzia kodi  wafanyabiashara kutokana  janga la Corona huku Mbunge wa Bagamoyo akishauri wananchi kurejeshewa kurejeshewa maeneo ambayo hayakuendelezwa .

Kwa mwaka 2020/2021, Wizara ya Viwanda na Biashara  imeomba kuidhinishiwa  jumla ya Shilingi  Bilioni  themanini na moja ,milioni  mia tatu sitini na sita  ,laki tisa na elfu mbili [ 81,366,902,000] ambapo  Kati ya fedha hizo, zaidi ya  Shilingi  Bilioni 51.7 ni za Matumizi ya Kawaida na Shilingi  bilioni 29.7 ni za Matumizi ya Maendeleo.

Aidha,Katika mwaka 2020/2021, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi  Bilioni 15 kutokana na uuzaji wa nyaraka za zabuni .

MWISHO.


Share:

Waziri Nchemba Awaponda Baadhi Ya Wabunge Wa Upinzani Kususia Vikao Vya Bunge....Awataka Watanzania Wawapuuze

Waziri wa Katiba na sheria Mhe.Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha baadhi ya Wabunge wa Upinzani kususia vikao vya Bunge  kwa kuogopa Corona ni ishara ya kutengeneza madaraja na mpango wa kushusha uchumi wa nchi.

Waziri Nchemba amesema hayo jana Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya     wizara ya       Viwanda na Biashara ya makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha,2020/2021 ambapo amewataka Watanzania kuacha kusikiliza miluzi  ambayo inapotosha taifa.

Waziri Nchemba amesema  Maisha ya Watanzania mara nyingi hayana akiba hivyo kitendo cha watanzania kujifungia ndani  bila kufanya kazi kwa tahadhari ya Corona  kama wanavyoshauri baadhi ya wabunge wa Upinzani panaweza kutengeneza majanga mengine hivyo wanatakiwa  kufuata ushauri uliotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli wa kuchapa kazi na kuondoa hofu juu ya Corona na kubainisha kuwa janga halikimbiwi.

Waziri Nchemba ameteuliwa na Rais Dokt John Pombe Magufuli hivi karibuni kuiongoza Wizara ya Katiba na Sheria tukio lililofanyika Mjini Chato mkoani Geita baada ya aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo  Dkt.Balozi Augustine Mahiga  kufariki Dunia


Share:

Serikali Yaendelea Kushughulikia Changamoto Zinazojitokeza Mipakani

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema changamoto zinazojitokeza katika mipaka mbalimbali ya Tanzania wakati wa usafirishaji wa bidhaa hususan katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 zinaendelea kutatuliwa kwa majadiliano.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert Ibuge ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Mhe. Benson Keith Chali ili kuangalia namna ya kutatua changamoto mbalimbali za usafirishaji wa bidhaa hususani zile zinazotoka katika bandari ya Dar es Salaam kuelekea katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha janga la COVID – 19 unaosababishwa na virusi vya Corona changamoto mbalimbali zimejitokeza katika utoaji wa huduma za usafirishaji wa huduma na bidhaa mbalimbali na hivyo serikali inafanya jitihada za majadiliano na baadhi ya nchi katika mipaka ili kutatua changamoto zinazojitkeza na kuwezesha huduma ya usafirishaji kuendelea bila ya vikwazo.

Nae Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Chali amemuahidi Balozi Kanali Ibuge kuwa Serikali ya Zambia imeshaanza kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza. "Suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi na kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni," amesema Balozi, Chali. 

Katika tukio jingine Balozi Kanali Wilbert Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Christine Musisi ambapo katika mazungumzo hayo wameongelea zaidi namna ya kushirikiana na kuwezesha kujenga uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa wawekezaji wadogo na wakati wa Tanzania na kuwa na ubia na wawekezaji wakubwa hususani katika kipindi hiki cha COVID – 19 na baada ya COVID – 19 ili kuunusuru uchumi wa Taifa kuanguka.

"Tumekubaliana kuongea ushirikiano katika sekta za afya, maji, maendeleo na uwekezaji …….kwa hili tunawashukuru sana UNDP kwa kazi wanayoifanya lakini pia hata katika ushirikiano wa kisera tumekuwa tukishirikiana nao jambo ambalo linazidi kuimarisha uhusiano wetu hasa katika wakati huu wa COVID - 19 kwani jambo hili linasaidia kunusuru uchumi wa taifa kuanguka," amesema Balozi, Kanali Ibuge.

Katika hatua nyingine, Balozi Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke pamoja na Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania Bw. Zlatan MiliÅ¡ić ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano hususani katika kipindi hiki cha janga la COVID – 19.

Tarehe 6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulijadili janga la COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka nchi 16 wanachama wa SADC. 

Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu na Huduma katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona. Mwongozo huu unatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari zisizo za lazima na kuwezesa usafirishaji wa bidhaa muhimu wakati huu wa janga la COVID - 19.


Share:

Ajali Mbaya ya Gari Yaua Watu 6 Pwani

Watu sita wamefariki dunia mkoani Pwani katika ajali iliyoua watu sita .

Ajali hiyo ilitokea  usiku wa kuamkia jana eneo la Vigwaza, Chalinze barabara kuu ya Morogoro na kusababisha vifo vya watu sita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo  akibainisha kuwa tukio la ajali lilihusisha gari lenye namba za usajili T299 AGE aina ya Toyota Prado, lililogongana na gari la mizigo lenye namba za usajili T469 DCP/T 996 BHH aina ya Scania lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara.

Kamanda Wankyo alisema, gari hiyo aina ya Prado ambalo dereva wake bado hajafahamika, lililigonga Scania lililokuwa likiendeshwa na Edger Mbilinyi (30), mkazi wa Njombe.

Alisema, watu waliofariki dunia wote ni wanaume na kati yao yupo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 6-7.

Alisema majina yao hayajafahamika na majeruhi mmoja amefahamika kwa jina la Adinani Mresi (30), anayedaiwa kuwa askari wa JWTZ Ngerengere Morogoro aliyeumia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Wankyo alisema, chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni dereva wa gari T 299 AGE, Toyota Prado kuendesha kwa mwendo kasi bila kuchukua tahadhari.

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani Tumbi na majeruhi anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Mlandizi, huku Jeshi la Polisi likiendelea kumshikilia dereva wa Scania kwa tuhuma za kuegesha gari bila kuchukua tahadhari.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano May 06


















Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Vifo Vya Watoto Wachanga Vimepungua Kutoka 25 Kwa Kila Vizazi Hai 1000 Hadi Saba Kwa Kila Vizazi Hai 1000

Na WAMJW – Dar es Salaam
Vifo vya watoto wachanga wenye umri wa chini ya siku 28 vimepungua kutoka 25 kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwaka 2015/16 na kufikia saba  kwa kila vizazi hai  1000 kwa mwezi Machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo  jijini  jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea msaada wa vifaa kinga, mabango,vipeperushi na vifaa vya  kutoa elimu kwa Umma kuhusu ugonjwa wa Corona kutoka kwa Benki ya Absa Tanzania Ltd na Shirika  la UNESCO.

Waziri Ummy alisema kupungua kwa vifo hivyo kumetokana na jitihada zilizofanywa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini hii ni pamoja na kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba.

“Kwa namna ya kipekee niwapongeza na kuwashukuru wakunga wote hapa nchini kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kila siku ya kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano”,.

“Pamoja na kuwa maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19) yapo na watu wanaumwa ugonjwa huu, lakini tusisahau kuwa kina mama wajawazito wanajifungua kila siku na wakunga  wanaendelea kuwahudumia kinamama hawa”, alisisitiza Waziri Ummy.

Waziri huyo aliwahakikishia wananchi kuwa pamoja na kuwa ugonjwa wa Corona upo   huduma zingine zinaendelea kama kawaida  katika vituo vituo vyote vya kutolea huduma za afya zikiwemo huduma za kliniki za akina mama wajawazito na watoto, upimaji wa magonjwa mbalimbali pamoja na upasuaji.

“Ninawashukuru wadau mliotoa vifaa hivi, ninawaomba wadau wengine waendelee kuiunga mkono Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona ambao ni janga la Dunia”,.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara  hiyo Prof. Mabula Mchembe alisema  vifaa hivyo vitaboresha  utoaji wa huduma za afya katika vituo vilivyopo Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine nchini.

“Ninawahakikishia wananchi pamoja na wadau mliotoa vifaa hivi kuwa  vitatumiwa na wataalamu wetu katika kutoa huduma mbalimbali za matibabu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika vituo vyetu vya afya”, alisema Prof. Mchembe.

Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Rasiliamali watu wa benki ya Absa Tanzania Ltd. Patrick Foya alisema vifaa kinga walivyovitoa vyenye thamani ya milioni 20 ambavyo ni glovu, barakoa na vitakasa mikono vitawasaidia watoa huduma za afya wakati wanawahudumia wagonjwa.


Share:

Vyuo Vya Kilimo Nchini Vyatakiwa Kujiimarisha Kimapato

Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo ( MATI) vimeagizwa kuhakikisha vinatumia wataalam wakufunzi na rasilimali ardhi kuzalisha mazao mengi bora ili kuwa na uhakika wa kipato na kujiendesha kibiashara. 

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya wakati alipotembelea Chuo cha Kilimo Mubondo Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma. 

" Tumieni sayansi kuzalisha mazao ya kilimo kwa kuhakikisha mnapima udongo na kujua virutubishi vinavyofaa ili mjue zao gani na aina gani ya mbolea ili kuwa na mavuno ya kutosha kuwezesha vyuo kujipatia mapato " Kusaya 

Katibu Mkuu huyo alisema lengo la serikali kuanzisha vyuo vya mafunzo ya kilimo ni kufundisha vijana na wakulima wengi kanuni bora za kilimo ili waweze kutoa mchango katika kukuza sekta ya kilimo nchini. 

Amevitaka vyuo hivyo kutumia vema ardhi iliyopo na teknolojia  kutoa mafunzo bora na kuzalisha mazao kibiashara  ili wanafunzi wanaohitimu waweze kuwa mahili katika kujitegemea na kuongeza ajira kupitia kilimo na chuo kupata mapato . 

" Vijana wengi watakapofanya vema na kufanikiwa katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kupitia kilimo ndio itakuwa nafasi ya vyuo hivi kujitangaza na kuvutia vijana wengine na wakulima kuja kujifunza " alisisitiza Katibu Mkuu huyo 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kilimo MATI Mubondo Hanif Nzury aliomba serikali ikipatie Chuo hicho trekta ili kiweze kutumia kuongeza uzalishaji zaidi wa mahindi, alizeti na michikichi ombi ambalo Katibu Mkuu alilikubali na kuahidi kulifanyia kazi. 

Aidha Katibu Mkuu Kilimo amewataka Maafisa Ugani kote nchini kuwasaidia wakulima kwa kuwatembelea na kuwapa ushauri juu ya kanuni bora za kilimo . 

Katika hatua nyingine Kusaya ameziagiza taasisi zote chini ya Wizara ya Kilimo kuhakikisha wanashirikiana na Halmashauri nchini kupima maeneo hayo na kupata hatimiliki ikiwa na lengo la  kuyaepusha na uvamizi toka kwa wananchi 

Wizara ya Kilimo inasimamia vyuo 14 vinavyotoa Mafunzo ya stashahada (Diploma) na astashahada ( Certificate)  pamoja na vituo vya utafiti 17 nchini. 

Awali Katibu Mkuu Kusaya alitembelea Shamba la mbegu bora la Bugaga lililopo Kasulu chini wa Walaka wa Mbegu (ASA) ambapo ameagiza wahakikishe miche 5000 ya michikichi iliyopo tayari hapa kituoni inawafikia wakulima kama alivyoagiza Waziri Mkuu. 

“ Waziri Mkuu yuko mstari wa mbele kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa mafuta ya kula hivyo endeleeni kuzalisha miche mingi ya michikichi ili wakulima wapande na hatimaye tupate mavuno mengi yatakayotosheleza mahitaji ya mafuta” alisema Kusaya. 

 Mwisho
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo


Share:

Tuesday, 5 May 2020

Waandishi wa habari watakiwa kuandika taarifa sahihi kuhusu ugonjwa wa Corona

Na WAMJW – Dar es Salaam
Waandishi wa Habari nchi wametakiwa kuandika habari sahihi kuhusu virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19) ili wananchi wapate taarifa ambazo zitawasaidia  kujikinga na ugonjwa huo.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea msaada wa vifaa kinga,vifaa vya kupima joto la mwili, vipeperushi,  mabango na vifaa vya  kutoa elimu kwa Umma kwa ajili ya waandishi wa Habari vilivyotolewa na Shirika la UNESCO.

Waziri Ummy alisema wizara yake imekuwa ikishirikiana na  vyombo vya habari  kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati  kuhusu ugonjwa wa Corona na kufahamu hatua za kufuata ili wajikinge na ugonjwa huo.

“Msaada huu unagusa wadau muhimu sana kwani hawa ndiyo wanaotusaidia kupeleka taarifa kwa wananchi. Mmenifurahisha zaidi kuzifikia  redio za jamii 34 ambazo zitapata vifaa vya kupima joto la mwili pamoja na vifaa kinga vingine. Redio hizi ni za muhimu sana kwani zinawafikia wananchi wengi waliopo vijijini”,.

 “Kwa upande wa waandishi wa habari , pamoja na majukumu yenu ya kazi za kila siku mnazozifanya hakikisheni mnatoa taarifa sahihi za Corona na siyo habari za kuwatisha wananchi bali waelimisheni. Nanyi hakikisheni mnafuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kujikinga na ugonjwa huu hii ikiwa ni pamoja na kusimama umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu wakati mnapotekeleza majukumu yenu”, alisema Waziri Ummy.

Akikabidhi vifaa hivyo mwakilishi mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania Tirso Dos Santos aliipongeza Serikali kwa hatua zinazochukuwa katika kupambana na ugonjwa wa Corona.

“Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za ugonjwa huu kwa wananchi, nasi tumeona tuwape vifaa kinga, mabango na  vipeperushi ambavyo zitawasaidia kuufahamu zaidi ugonjwa wa Corona na kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi kwa wakati”, alisema Santos.

Vifaa vilivyotolewa na Shirika la UNESCO ambavyo vitatolewa kwa waandishi wa habari ni vitakasa mikono, barakoa, mashine za kupima joto la mwili, mabango na  vipeperushi.



Share:

Simiyu Yazindua Mkakati Wa Wanafunzi Kusoma Kipindi Cha Likizo Ya Tahadhari Ya Corona

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkoa wa Simiyu umezindua mpango mkakati wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kusoma katika kipindi hiki cha likizo ya  dharula ya tahadhari ya ugonjwa   wa homa ya mapafu ( COVID 19) inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Akizindua mkakati huo, Mei 04, 2020 katika Shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amesema kuwa mkakati huo utawasaidia wanafunzi kupata masomo wakiwa nyumbani kutoka kwa walimu wao huku ukiwa na malengo makuu manne yatakayoifanya Simiyu iendelee kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

" Malengo makuu ya mkakati huu ni kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza,walimu kuwa na mawasiliano ya kitaaluma na wanafunzi  wao, wazazi kufanya ufuatiliaji wa taaluma kwa watoto wao pamoja na watoto(wanafunzi) kutulia nyumbani wakijisomea kipindi hiki cha likizo ambayo wako nyumbani;  tahadhari zote za maambukizi ya Virusi vya Corona zitazingatiwa, "alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewataka wazazi na walezi kuwahimiza wanafunzi  kutulia nyumba kujisomea na kufuatilia vipindi vya masomo mbalimbali vinavyorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari  nchini, huku akisisitiza maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa afya na viongozi juu ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona yazingatiwe wakati wa kujisomea.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl Ernest Hinju amesema Mkoa utaendelea kufanya mawasiliano na wazazi ili siku tatu baada ya shule kufunguliwa wanafunzi wapewe mitihani ili kuwapima.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge  ametoa msaada wa kompyuta tano na printa kwa Shule ya sekondari Simiyu kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa wote ambazo zimekabidhiwa na Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa, Christina Chenge (mke wa mbunge huyo) kwa niaba ya mbunge.

Akikabidhi kompyuta hizo, Mama Christina Chenge  amesema mbunge ametoa msaada huo na ametoa wito kuwa kompyuta hizo zitumike kwa kazi na malengo yaliyokusudiwa ili mkoa wa Simiyu uendelee kufanya vizuri katika sekta ya elimu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mhe. Chenge kwa msaada huo na misaada mingine ambayo amekuwa akiitoa kwa shule ya Sekondari Simiyu na shule nyingine ikiwemo saruji na mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni na kusisitiza msaada huo kutumika kama ulivyokusudiwa.

Akiongea mara baada ya makabidhiano ya msaada huo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuwa hategemei kuona shule hiyo (Simiyu sekondari) iliyokabidhiwa vifaa hivyo kupata wanafunzi wenye daraja sifuri kwani tayari wana walimu  na vifaa vya kutosha sambamba na madarasa ya kutosha.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Simiyu, Paul Susu amemshukuru Mhe. Chenge kwa kutambua uhitaji walionao kwani utawasaidia katika kutekeleza shughuli zao za ufundishaji huku akiongeza kuwa pamoja na kuwa shule ya Simiyu ndio imekabidhiwa shule nyingine zitanufaika pia kwa kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano na shule nyingine.

Nao baadhi ya walimu wa shule hiyo akiwemo Dorine Bella na John Mogela wamesema kuwa ujio wa  kompyuta hizo utakuwa chachu ya kurahisisha ufundishaji na kutekeleza mkakati wa mkoa wa wanafunzi kusoma katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu na baada ya ugonjwa huo.

MWISHO.


Share:

TRA Kagera Yavuka Malengo Ya Serikali Yakusanya Billion 16 Kwa Robo Ya Mwaka Wa Fedha 2019-2020.

NA Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Jumla ya shilingi Bilioni 16.18 zimekusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania mkoani Kagera kwa upande wa kodi za forodha na kodi za ndani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari-Machi 2020 sawa na 110.03% ikiwa lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi bilion 14.7 

Hayo yamebainishwa na Meneja wa T.R.A mkoani Kagera Bwana Adam Mtogha wakati akizungumza na mwandishi wa kituo hiki akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari –machi mwaka huu. 

Bwana Mtogha amesema kuwa kwa kipindi cha Januari –machi 2020 mkoa wa Kagera ulipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 14.7 kwa upande wa kodi za forodha na kodi za ndani na wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni16.18 na kuvuka lengo walilopewa na serikali .

Aidha ameongeza kuwa ni mafanikio makubwa  kwa kipindi  hiki kwa kuwa kipindi kilichopita kuanzia mwezi Januari –machi mwaka jana  utendaji kazi wao ulikuwa ni 94.5%. 

Bwana Mtogha amesema kwa upande wa kodi za ndani mkoa wa Kagera ulipangingiwa kukusanya jumla ya shilingi billion 9.1 na wamefenikiwa  kukusanya shilingi bilioni 9.8 sawa na jumla 107.5% ya  kwa kodi za ndani Wakati kwa upande  forodha mkoa wa Kagera ulipangiwa kukusanya billion 5.6 na walifanikiwa kukusanya billion 6.4 sawa 114.16%

Bwana Mtogha amesema wamefikia mafanikio hayo kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari mkoani humo pamoja na kuwatumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwa wateja wote ili kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati. 

Sanjali na hayo amebainisha kuwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali wameweza kufanikiwa kuondoa malimbikizi ya kodi . 

Kwa upande mwingine amewapongeza wana kagera kwa ushiriki wao katika shughuli za ulipaji kodi ikiwa nipamoja na kulipa kodi kwa muda muhafaka hasa katika kipindi hiki cha kupambana na virusi vya corona na kuwataka wananchi mkoani humo kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi hivyo zinazo tolewa na serikali.


Share:

Serikali Yavifyeka Vyama 3,348 Ni Baada Ya Kwenda Kinyume Na Uanzishwaji Wake

Na Charles James, Dodoma
SERIKALI imetangaza kuvifuta rasmi vyama vya Ushirika 3,348 ambavyo vingi ni hewa huku ikisema zoezi la kufuta vyama hivyo litakua endelevu Kwa vyama vitakavyoshindwa kutekeleza majukumu ya kuanzishwa kwake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Josephat Hasunga wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo pamoja na kufuta vyama hivyo pia amevitaka vyama vilivyosalia kuimarisha mwenendo wao.

Vyama ambavyo vimefutwa ni Saccos 2,513, AMCOS 229, Mifugo 77, Vyama vya walaji 27, Vyama vya huduma 70, Vyama vya ufugaji Nyuki 15, Vyama vya wenye nyumba 9, Vyama vya Madini 22, Vyama vya wenye Viwanda 79, Vyama vya Uvuvi 32, Vyama vya Umwagiliaji 31 na vinginevyo 244.

Kabla ya kufutwa kwa vyama hivyo, Idadi ya vyama vya ushirika ilikua 11,626 hivyo baada ya kufutwa kwa vyama 3,348 sasa vyama hivyo vya ushirika vinabaki kuwa 8,611.

Waziri Hasunga amewataka wanachama na wakulima wanaotumia vyama vya ushirika nchini kufunga akaunti Benki ili mkulima kujihakikishia malipo yake.

Amesema kama wakulima wakifanya hivyo itakua ni mojawapo ya suluhu kwa udanganyifu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wasio waaminifu wakati wa malipo.

Akizungumzia mfumo wa ununuzi wa mazao Nchi nzima, Waziri Hasunga amesema njia pekee ya kumkomboa Mwananchi ni kupitia ushirika hivyo kuwataka wananchi wajiunge na vyama hivyo ili wanufaike na ushirika.

" Wananchi wakiuza Kwa pamoja ni rahisi kupata bei nzuri, hata hivyo kumetokea malalamiko mengi katika baadhi ya mikoa kuwa wananchi wananyanyasika sana na mfumo wa vyama vya ushirika na stakabadhi ghalani.

Sasa ili mfumo wa stakabadhi ghalani uweze kufanyika sawasawa naagiza kuwepo kwa chama cha msingi kilichosajiliwa katika kijiji husika, kuwepo kwa ghala lililosajiliwa na Bodi ya Maghala, kuwepo kwa mfumo wa kufanya minada kwa njia ya ushirika na kuwepo kwa wanunuzi wa kununua kwa minada," Amesema Waziri Hasunga.

Kutokana na changamoto hizo, Waziri Hasunga ameagiza kuhakikisha kuwa katika kila kijiji kunakua na soko la awali ambalo wananchi watauza mazao yao lakini pia kuwe na soko la upili ambalo wananchi, vyama vya ushirika na wafanyabiashara wa ndani wataruhusiwa kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara wa nje.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vyama vya Ushirika nchini Titus Kamani ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekua ikizingatia maslahi mapana ya wananchi na kwa kusimamia vema uendeshaji wa vyama hivyo.

" Niipongeze sana serikali imekua mara zote ikiwajali sana wanachama wa Ushirika ambao wengi wao ni wananchi wanyonge na ndio maana tunaona mara kadhaa vyama hivi vinapoenda kinyume basi serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekua ikichukua hatua kali ikiwemo kuvifutia usajili vyama vinavyoenda kinyume na uanzishwaji wake," Amesema Kamani


Share:

DIWANI AISHUKURU KAMPUNI YA GP KWA KUWASAIDIA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA

  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kushoto akimkabidhi vyakula vya futari na vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Corona Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Makorora Ramadhani Badi
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kushoto akibidhi mmoja wa wananchi wa Kata ya Makorora Futari yenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo ikiwemo vifaa vya kujikinga na Virusi vya Corona
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akikabidhiwa vitakasa mikono (Sanitize ) na vyakula kutoka kwa  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo
 Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akigawa msaada huo kwa wananchi wa mitaa mbalimbali kwenye Kata hiyo kulia ni  Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed

 Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed akiwaaonyesha waandishi wa habari vitakasa mikono ambavyo vimetolewa


DIWANI wa Kata ya Makorora Jijini Tanga (CCM) Omari Mzee ameishukuru Kampuni ya Mafuta ya GP kwa kutoa msaada futari kwa kaya 150 kwenye kata yake ikiwemo vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Corona.


Huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha watoto wao ili kuona ile mikusanyiko isiyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambayo kwa sasa vinaitikisha dunia.

Omari aliyasema hayo leo wakati akipokea msaada huo wenye thamani ya Milioni 16 vilivyotolewa na kampuni ya Mafuta ya GP vilikabidhiwa na Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kufuatia ombi la kumtaka ashirikiana nao kwenye kukabidhi vyakula na vifaa hivyo..

Alisema vifaa hivyo vitawasaidia wakati huu wa mwezi wa ramadhani ikiwemo katika kukabiliana dhidi ya Ugonjwa huo wa Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa Afya hapa nchini.

Aidha alisema kwa sasa shule zimefungwa na watoto wamekuwa wakizagaa mitaani hivyo wanapaswa kuchukua tahahdari kwa kuwaelimisha ili kuona ile mikusunyiko ilisyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo kwa lengo la kuwaepusha na maambukizi ambayo wanaweza kukumbana nayo.

“Nishukuru sana kwa furari hii kwa zile kaya ambazo hawajiwezi zitawasaidia kupunguzia makali ya maisha lakini wazazi tutambue ugonjwa huu wa Virusi vya Corona upo hivyo niwasihi wazazi na jamii nzima kwa ujumla tuweza kuchukua tahadhari kukabiliana nao “Alisema Diwani huyo.

Awali akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed alisema kwamba wamekabidhi vyakula hivyo kwenye kaya masikini 150 ambavyo vimetolewa na kampuni.


Ambapo alisema kutokana na ukongwe wangu wa kampuni za Oili Mkoa wa Tanga wamemuomba washirkiane nami kukabidhi vyakula hivyo kwa waliofunga mwezi mtufuku na vifaa vya kujikinga dhidi ya Corona vyenye thamani ya milioni 16.

Vifaa hivyo alivikabidhi kwa diwani wa Kata hiyo Omari Mzee ili aweze kuvikabidhi kwa wananchi kwenye mitaa ili kuweza kuwapunguzia makali ya maisha waliokuwa nao baadhi ya jamii maeneo hayo kutokana na kushindwa ukata ambao wamekuwa wakikumbana nao.
Share:

Kenya Yarekodi Idadi Kubwa Zaidi Ya Maambuzi ya Corona Ndani Ya Saa 24....Maambukizi Sasa Yamefika 535

Waziri wa Afya  nchini Kenya Mutahi Kagwe almetangaza kwamba visa vya maambukizi ya corona  nchini humo  vimefika 535 baada ya watu 45 zaidi kupatikana na maradhi hayo. 

Kwenye hotuba yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne, Mei 5, Kagwe amesema hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu kisa cha kwanza cha COVID-19 kuripotiwa Machi 13, 2020. 
 
Kati ya visa hivyo 45, 30 ni wanaume na 15 ni wanawake. Mutahi amesema kwamba watu 29 ni wakaazi wa Nairobi, 11 kutoka Mombasa na watano kutoka Wajir.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger