Saturday, 18 April 2020

Senior Technical Advisor – Health Workforce Capacity Building at IntraHealth International , Dar es Salaam, Tanzania

Why join IntraHealth? IntraHealth International is a global health nonprofit that has worked for 40 years in over 100 countries. We improve the performance of health workers and strengthen the systems in which they work so that everyone everywhere has the health care they need to thrive. IntraHealth’s programs generate long-term social and economic impact to keep communities… Read More »

The post Senior Technical Advisor – Health Workforce Capacity Building at IntraHealth International , Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema apiga marufuku mikusanyiko kwenye baa....Aagiza Wanywaji Wanunue Wakanywee Nyumbani

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amepiga marufuku mikusanyiko kwenye baa zote wilayani humo kuanzia jana  Ijumaa Aprili 17 ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona. 

Amewataka waendesha baa hizo, kuhakikisha wanauza vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi akanywee nyumbani na kwamba atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo haya kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa,” amesema Mjema.


Share:

Muhimbili washona mavazi kwaajili ya wahudumu wa afya wanaokabiliana na corona

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshona vazi maalumu (coverall) ambalo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) kuvaa ili kujikinga wakati wanatoa huduma kwa Watanzania na raia ya kigeni watakaobainika kuambukizwa ugonjwa wa Corona (COVID 19) hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai amesema jitihada hizi ni katika kuunga mkono kauli ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Tanzania, tunaweza na siyo kila kitu lazima kitoke nje kwani malighafi zilizotumika zote zinapatikana katika viwanda vilivyopo hapa nchini.

Amesema PPE zinazotoka nje ya nchi hugharimu fedha nyingi za Tanzania ambapo vazi moja tu ni kati ya TZS. 350,000 hadi TZS. 500,000 ikitegemea imenunuliwa nchi gani,  ambapo lililoshonwa na Muhimbili limegharimu TZS. 30,000.

“Tumeamua kushona vazi hilo ambalo linakaribiana na viwango vya WHO na sisi kama watoa huduma tulioko msitari wa mbele kuwahudumia, tumeridhika kuwa vazi hili linakidhi viwango na mahitaji yetu hapa nchini” amesema Dkt. Swai

Amesema katika kukabiliana na changamoto ya kutokapatikana kwa urahisi mavazi haya, Hospitali ya Taifa Muhimbili ina wajibu wa kutoa mwelekeo, ubunifu wa namna ya kutoa huduma nchini na hii ni sehemu ya wajibu huo.

“Tunatoa wito kwamba sasa viwanda vya ushonaji vinaweza kuja kupata sampuli ya aina ya vazi na malighafi zinazotumika ili bidhaa hii iweze kuzalishwa kwa wingi na kupatikana kwa gharama nafuu zaidi”, amesema Dkt. Swai

Amesema, MNH inaipongeza Serikali kwa jitihada inazofanya na hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kukabiliana na ugonjwa huu ambao umeingia nchini nasi tunaendelea kushirikiana katika mapambano hayo.


Share:

Kirusi cha corona kinavyobadili namna tufanyavyo biashara

Na Mwanaheri Khamis, Unguja 17.04.2020
Tangu nchi za bara Afrika kuanza kutangaza visa vya wagonjwa wa kirusi cha homa ya corona, shughuli za biashara zimeathirika kwa namna mbalimbali barani hapa. 
 
Kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani, Tanzania nayo inapata changamoto hii. Katika miaka ya karibuni, Tanzani imeingia kwa nguvu zote kuhakikisha inakuwa nchi ya viwanda yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025. Kufikia hilo kila juhudi inawekwa katika kujenga uchumi wa taifa, wenye biashara na viwanda mbalimbali. 
 
Huku  nchi yetu Tanzania ikiendelea na nia yake hiyo kufikia lengo lake,  COVID-19 imekuwa changamoto  hasa kwenye eneo la utalii  ambapo baadhi ya hoteli za zilisitisha huduma zake kwa muda ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa corona unaotokisa dunia kwa sasa.
 
Katika hatua nyingine, juma hili Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kuahirisha sherehe za Mei Mosi ambazo hufanyika Mei 1 kila mwaka. Waziri Mkuu kaongeza pia kuwa mikusanyiko isiyo lazima isitishwe na kutaka watu kukaa nyumbani kama hakuna jambo ambalo ni muhimu kuwafanya kutoka nje.

Biashara nyingi duniani zimechukua hatua kupunguza kukutana uso kwa uso wengi wakitaka wafanyakazi kufanya majukumu yao kutokea nyumbani au kuahirisha shughuli ambazo zinahitaji watendaji kukutana. 

Aina hii ya maisha itatawala biashara na shughuli zetu nyingi sasa na siku zijazo wakati tunapigana na kirusi huyu. 

Naiwaza kwa mfano shughuli ya kampuni ya Tigo Tanzania kuweka hisa zake sokoni (IPO) katika soko la hisa la Dar es Salaam. Katika biashara hii ni shughuli ya kuleta watu pamoja, mikutano, majadiliano na safari za kutosha. Je shughuli kama hizi ziendelee? 

Busara yaweza kuwa kuahirisha shughuli kama hizi na kukusanya nguvu pamoja kupigana na kirusi huyu kwanza kisha kurejea tukiwa salama na utulivu hili likishapita.


Share:

Majambazi 7 wauawa wakipambana na polisi.

Watu 7 wanaotuhumiwa kuwa majambazi, wameauawa katika eneo la Kata ya Kumwambu, Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma baada ya kukabiliana na Polisi wakati wakijiandaa kufanya uvamizi na kupora katika kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sino Hydro Engineering Company Ltd.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Otieno, alisema tukio hilo limetokea juzi saa tano usiku baada ya jeshi hilo kupokea taarifa ya kikundi kinachopanga kwenda kutekeleza uhalifu huo.

Kamanda Otieno alisema kufuatia taarifa hizo, kikosi kazi kilijipanga kwenda kuimarisha ulinzi katika maeneo ambayo walipanga kujificha na baadaye kuona kundi la watu 12 wakitembea kuelekea kutimiza adhima yao na walipobaini kuwa wanafuatiliwa walianza kuwarushia risasi askari na kuibuka majibizano ya risasi yaliyodumu kwa takribani dakika 25.

Pia, Kamanda Otieno alisema katika majibizano hayo askari waliwaua majambazi watatu hapo hapo na wanne walikufa njiani wakati wakipelekwa hospitali ya wilaya ya Kibondo huku wengine watano wakikimbia kusikojulikana.

Jeshi hilo pia limekamata bunduki tatu zilizotengenezwa kienyeji, pisto moja, risasi 89 za SMG, 15 za pisto na kofia za kuficha sura ambazo zilikuwa zikitumika katika uhalifu.


Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO


Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

RWANDA YAONGEZA SIKU 11 ZA WATU KUBAKI NYUMBANI ILI KUKABILIANA NA CORONA

Baraza la mawaziri nchini Rwanda limepitisha kuendelea kutekelezwa kwa amri ya kusitishwa shughuli za kawaida nchini humo siku zingine 11.

Hii inajiri wakati idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo ikifikia 143 , huku watu wengine 65 wakithibitishwa kupona.

Nchini Rwanda polisi wameanza kutumia ndege ndogo zisizo na rubani, kuwahamasisha watu mitaani kuheshimu amri ya kubakia nyumbani kama mkakati wa kuzuia kusambaa kwa virusi virusi vya Corona.

Hata hivyo hakuna kifo kinachohusiana na ugonjwa aw Covid-19 ambacho kimetokea nchini Rwanda


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa April 18



















Share:

Friday, 17 April 2020

MGANGA WA KIENYEJI AJIUA BAADA YA KUSUMBULIWA NA KIBUYU KUKOSEA MASHARTI ..AACHA UJUMBE AKIOMBA MSAMAHA MIZIMU


Katika hali isiyo ya kawaida mwanaume aliyejulikana kwa jina la Kaido Mfilinge (30) aliyedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji amekutwa amejinyonga mpaka kufa katika mtaa wa Nazaleti mjini Njombe baada ya kuchukua dawa kwa mganga mwenzie kutoka mkoani Ruvuma na kukiuka masharti ambayo alikuwa amepewa na kuacha ujumbe wa maandishi wa kuomba msamaha kwa mizimu.

Inaelezwa kuwa mganga huyo amejinyonga baada ya kukiuka masharti ya mganga aliyedaiwa kumpa kibuyu ambacho kinatajwa kuwa ndicho kimepelekea kifo chake.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema jeshi la polisi limefika katika eneo ambalo kijana huyo amejinyongea na kumkuta ameacha barua ambayo inasema "Nimejinyonga baada ya kusumbuliwa na kibuyu ambacho nilikuwa nimepewa na mganga na kusababisha mizimu kuanza kusumbua".

“Huyu kijana yeye ni mganga wa kienyeji kwa asili yake na amejinyonga baada ya kwenda mkoa wa Ruvuma akapewa dawa iliyokuwa na masharti,ile dawa aliyoenda nayo nyumbani kwake kibuyu kimoja kikaanza kumsumbua akamuuliza Yule aliyempa akaambiwa akatupe kwenye njia panda yoyote”,alisema kamanda Hamis Issa

Kamanda Issa ameongeza kuwa “Lakini yule kijana akaamua kuchukua maamuzi magumu akajinyonga na haya maneno ninayoyaongea ameyaandika mwenyewe kwenye karatasi yake "Samahani mizimu nimekosea masharti,samahani familia yangu,samahani mganga wangu uliyenipa masharti nimekosea nimeaamua kujitoa duniani kwa kujinyonga" na hiyo karatasi ipo imeandikwa hivyo ,alisema Kamanda Issa.
Share:

WAHUDUMU WA HOTELI WAAMBUKIZWA CORONA


Idadi ya visa vya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia visa 246, baada ya hii leo kutangaza visa vipya 12, huku watano kati yao ni wakiwa ni wafanyakazi wa hoteli.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 17, 2020 na Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe, na kusema kuwa kwa kipindi cha masaa 24, nchi hiyo tayari imekwishapima sampuli za watu 450.

"Mpaka asubuhi hii ninavyoongea tayari ndani ya masaa 24 tumekwishapima sampuli 450 na kati ya hao tuliowapima tumepata wagonjwa 12, na siku yenyewe bado haijaisha na watano kati yao ni wafanyakazi wa hoteli" amesema Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.
Share:

Mahakama Kuu Tanzania yatangaza kuanzi Jumatatu watu wote wavae mask Wanapoenda Mahakamani




Share:

Msanii Dudubaya Afutiwa Usajili na BASATA




Share:

Wagonjwa wa Corona Zanzibar Wafika 35....Ni Baada ya Wengine 11 Kuongezeka Leo




Share:

BREAKING: Wagonjwa wa Corona Tanzania Wafika 147.....Ni Baada ya Wengine 53 Kuongezeka Leo

Idadi ya wagonjwa wa Corona Tanzania imeongezeka nakufikia  147 baada ya wagonjwa wapya 53 kukutwa na virusi hivyo .

Akiongea na vyombo vya habari leo Ijumaa April 17,2020, Waziri  wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wote hao ni watanzania ambapo 38 ni kutoka Dar es Salaam,10 Zanzibar,Kilimanjaro 1,Mwanza 1,Pwani 1,Lindi 1,na Kagera 1


==>>Msikilize hapo chini


Share:

China Yapangua Kauli ya Marekani....Yasema Hakuna Ushahidi Wowote Kwamba Virusi Vya Corona Vilizalishwa Maabara

Wizara  ya Mambo ya Nje ya China imesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna ushahidi kwamba virusi vya corona ambavyo vimewaathiri zaidi ya watu milioni 2 duniani vilitengenezwa kwenye maabara.

Msemaji wa wizara hiyo, Zhao Lijian ameyasema hayo jana wakati akijibu swali kuhusu shutuma kwamba virusi vya corona vilianzia kwenye maabara katika jimbo la Wuhan nchini China, ambako janga hilo lilizuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana.

Zhao aliwaambia waandishi wa habari mjini Beijing kwamba maofisa wa WHO wamesema mara kadhaa kwamba hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa virusi vya corona vilitengenezwa kwenye maabara.

Rais wa Marekani, Donald Trump jana alisema kuwa Serikali yake inajaribu kutathmini iwapo virusi vya corona vimetokea kwenye maabara ya Wuhan.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alisema China inahitaji kujisafisha kuhusu kile wanachokijua.


Share:

Baraza la Maaskofu -TEC lasitisha Uimbaji kwenye Ibada za misa Ili Kukabiliana na Corona

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko kutekeleza agizo alilotoa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Aprili 15, juu ya kujilinda na  Corona kwenye masuala ya ibada

TEC imeamua kusitisha mazoezi ya kwaya ili kuepuka mikusanyiko. Pia nyimbo wakati wa ibada zimesitishwa ili Ibada isitumie muda mrefu

Pia mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa. Mafundisho yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea katekisimu au njia ya mtandao

Pia kanisa litazingatia umbali wa mtu na mtu wanapokuwa ibadani, matumizi ya vinasa sauti, watanawa mikono kabla ya kuingia kanisani pia watanyunyizia dawa vifaa vya ibada


Share:

Kampuni Ya Barrick Buzwagi Yatoa Vifaa Vya Kujikinga Na Ugonjwacorona Shinyanga Vyenye Thamani Yashilingi Milioni 48

SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kukabiliana na Maambukizi ya  Ugonjwa uanaosababishwa na virusi vya Corona mkoani Shinyanga, Kampuni ya uchimbaji madini ya Dhahabu ya Barrick Buzwagi imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi  Milioni 48 kwa mkuu wa mkoa huo Bi Zainab Tellack ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya virusi hatari vya COVID 19.

Akikabidhi vifaa hivyo Aprili 18 mwaka huu,wilayani Kahama kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Tellack niaba ya Kampuni ya Barrick Buzwagi Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Afya Kazini Mgodi wa Barrick Buzwagi, Dk. Antoinette George amesema kuwa  msaada huo umejumuisha makontena 25 ya kunawia mikono kwa mkoa wa Shinyanga na 30 kwa wilaya ya Kahama, Chroline ndoo tano zenye kilogramu 45 kila moja, gloves pea 50 zitakazotumika kwa watoa huduma, Barakoa (mask) 400, Chemical Suits 40, chemical googles 40 na vipimia joto saba.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo  vitatumika katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi mkoani humo  hususani katika  Masoko, Minada, Vituo vya Mabasi, Magerezani, pamoja na  Vituo vya Afya ili kuwakinga wananchi dhidi ya janga la kidunia la Ugonjwa  COVID 19.

“Sisi kama Barrick tumetoa   magari manne ya kutoa elimu juu ya ugonjwa huu hatari wa COVID 19 ambayo yatatoa  matangazo  katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga kwa muda wa miezi miwili sambamba na  kutoa mafunzo kwa maofisa afya 204 kwenye vijiji vyote wilayani Kahama”, alisema Dk George..

Awali  akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi  Zainab Telack ameishukuru Kampuni ya Barrick Buzwagi kwa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhindi ya Ugonjwa huu na kuwataka wananchi pindi vifaa hivyo vitakapowekwa kwaajili ya matumizi ni budi wananchi wakazingatia maelekezo ya Serikali ili kujikinga  na COVID 19. 

Mbali na hilo Bi  Tellack ametoa onyo kali kwa wananchi mkoani humo kuacha kutoa taarifa za uongo kuhusiana na ugonjwa huo huku akitolea mfano tukio la kukamatwa kwa mkazi  Mwakitolyo , Mussa Kisinza aliyempigia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimdanganya kuwa  anaugonjwa wa COVID 19

"Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wotw watakaobainika kusambaza taarifa uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ugonjwa huu tutahakikisha tunawashughulikia wote wanaoleta mizaha tunahitaji wananchi wetu wabaki salama na janga hili”,alisema Tellack.

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha alisema kuwa  katika wilaya ya kahama kuna  mwingiliano mkubwa wa watu na uwepo wa mabasi mengi ya abiria yanayoanzia safari zake mjini hapo kuelekea mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Bukoba, Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

Amefafanua kuwa   wameendelea kuchukua tahadhari katika maeneo yote yenye mikusanyiko na wananchi wameonyesha mwitikio kwa kuunga mkono jitihada hizo za serikali isipokuwa bado changamoto ipo kwa waendesha pikipiki (bodaboda) na wamiliki wa Baa ambao hawataki kufuata maelekezo ya serikali.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger