Saturday, 18 April 2020

RWANDA YAONGEZA SIKU 11 ZA WATU KUBAKI NYUMBANI ILI KUKABILIANA NA CORONA

...
Baraza la mawaziri nchini Rwanda limepitisha kuendelea kutekelezwa kwa amri ya kusitishwa shughuli za kawaida nchini humo siku zingine 11.

Hii inajiri wakati idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo ikifikia 143 , huku watu wengine 65 wakithibitishwa kupona.

Nchini Rwanda polisi wameanza kutumia ndege ndogo zisizo na rubani, kuwahamasisha watu mitaani kuheshimu amri ya kubakia nyumbani kama mkakati wa kuzuia kusambaa kwa virusi virusi vya Corona.

Hata hivyo hakuna kifo kinachohusiana na ugonjwa aw Covid-19 ambacho kimetokea nchini Rwanda


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger