Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko kutekeleza agizo alilotoa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Aprili 15, juu ya kujilinda na Corona kwenye masuala ya ibada
TEC imeamua kusitisha mazoezi ya kwaya ili kuepuka mikusanyiko. Pia nyimbo wakati wa ibada zimesitishwa ili Ibada isitumie muda mrefu
Pia mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa. Mafundisho yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea katekisimu au njia ya mtandao
Pia kanisa litazingatia umbali wa mtu na mtu wanapokuwa ibadani, matumizi ya vinasa sauti, watanawa mikono kabla ya kuingia kanisani pia watanyunyizia dawa vifaa vya ibada
0 comments:
Post a Comment