Friday, 17 April 2020

MGANGA WA KIENYEJI AJIUA BAADA YA KUSUMBULIWA NA KIBUYU KUKOSEA MASHARTI ..AACHA UJUMBE AKIOMBA MSAMAHA MIZIMU

...

Katika hali isiyo ya kawaida mwanaume aliyejulikana kwa jina la Kaido Mfilinge (30) aliyedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji amekutwa amejinyonga mpaka kufa katika mtaa wa Nazaleti mjini Njombe baada ya kuchukua dawa kwa mganga mwenzie kutoka mkoani Ruvuma na kukiuka masharti ambayo alikuwa amepewa na kuacha ujumbe wa maandishi wa kuomba msamaha kwa mizimu.

Inaelezwa kuwa mganga huyo amejinyonga baada ya kukiuka masharti ya mganga aliyedaiwa kumpa kibuyu ambacho kinatajwa kuwa ndicho kimepelekea kifo chake.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema jeshi la polisi limefika katika eneo ambalo kijana huyo amejinyongea na kumkuta ameacha barua ambayo inasema "Nimejinyonga baada ya kusumbuliwa na kibuyu ambacho nilikuwa nimepewa na mganga na kusababisha mizimu kuanza kusumbua".

“Huyu kijana yeye ni mganga wa kienyeji kwa asili yake na amejinyonga baada ya kwenda mkoa wa Ruvuma akapewa dawa iliyokuwa na masharti,ile dawa aliyoenda nayo nyumbani kwake kibuyu kimoja kikaanza kumsumbua akamuuliza Yule aliyempa akaambiwa akatupe kwenye njia panda yoyote”,alisema kamanda Hamis Issa

Kamanda Issa ameongeza kuwa “Lakini yule kijana akaamua kuchukua maamuzi magumu akajinyonga na haya maneno ninayoyaongea ameyaandika mwenyewe kwenye karatasi yake "Samahani mizimu nimekosea masharti,samahani familia yangu,samahani mganga wangu uliyenipa masharti nimekosea nimeaamua kujitoa duniani kwa kujinyonga" na hiyo karatasi ipo imeandikwa hivyo ,alisema Kamanda Issa.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger