Tuesday, 10 March 2020

UBA TANZANIA YAKUTANISHA WATEJA WANAWAKE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


WAFANYAKAZI na Wateja wa Benki ya UBA Tanzania ,wakisherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam
 WAFANYAKAZI na Wateja wa Benki ya UBA Tanzania ,wakisherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam


 WAFANYAKAZI na Wateja wa Benki ya UBA Tanzania ,wakisherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam

Na MWANDISHI WETUDAR ES SALAAM

WAFANYAKAZI wanawake wa UBA Tanzania wamesherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake  kwa kuwaalika wateja wanawake kushiriki kifungua kinywa katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo, ikiwa ni kutambua mchango wa wanawake katika jamii.


Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2020 ni ‘Dunia sawa ni dunia iliyowezeshwa'. Kila mmoja kwa usawa.

Siku hii inayosherehekewa Machi 8 kila mwaka, inatoa fursa ya kutafakari maendeleo yaliyopatikana, kutoa wito wa mabadiliko na kusherehekea matendo ya ujasiri na uamuzi uliofanywa na wanawake wa kawaida ambao wametekeleza majukumu katika historia ya nchi zao na jamii.


Katika kuadhimisha siku hii maalumu ya wanawake, Ijumaa ya Machi 6, 2020, UBA Tanzania ilitembelea wanawake wenye matatizo ya Fistula katika Hospitali ya CCBRT na kuchangia vifaa vya matibabu, pampas za wanawake watu wazima pisi 40.


Mbali na hivyo pia walitoa mafuta ya kujipaka 40, sabuni za kufulia pisi 40, dawa za meno pisi 40, miswaki pisi 40, sahani 100 na bakuli 50, vikombe vya chai pisi 100, kanga doti 100, vyandarua vya mbu pisi 100, dawa za mbu za kupuliza katoni 5, mabeseni 100, kandambili pisi 100 na taulo za kike pisi 40.


Wanawake wa UBA Tanzania walitekeleza jukumu lao muhimu kwa kuwawezesha pia wanawake wengine kupitia shughuli mbalimbali zilizofanywa na benki hiyo kusaidia wanawake na wanafunzi wa kike kwa kuwapatia taulo za kike, taulo za wajawazito na vifaa vingine.


Hata hivyo katika hafla iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya UBA Tanzania, Pugu Road jirani na Mfugale Flyover, timu ya viongozi wanawake wa benki hiyo  na wafanyakazi wengine wanawake walitoa elimu na kujadili masuala mbalimbali wanayopitia wanawake na mwisho walipata kifungua kinywa na wateja wote wanawake walioalikwa.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki hiyo, Flavia Kiyanga, aliwataka wanawake kujishughulisha katika shughuli za ujasiriamali na shughuli nyingine za biashara ili kujiwezesha na kujimarisha kiuchumi.


Naye Katibu wa Kampuni, Victoria Lupembe, aliwaeleza wanawake kuwa kwa sasa usawa wa kijinsia umefikia mahali pazuri katika kampuni nyingi, ikiwamo UBA Tanzania ambayo imeajiri idadi kubwa ya wanawake katika nafasi za utendaji na zisizo za utendaji.
Share:

CHADEMA, Polisi wavurugana Mahakamani

Vurugu na kurushiana maneno vimeibuka  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza kesi ya viongozi wa Chadema. 
 
Hayo yote ni baada ya polisi kujaribi kuzuia baadhi ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingia katika chemba za mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri  hukumu ya viongozi wa chama hicho.

Polisi walilazimika kuwazuia wafuasi hao kwa maelezo, kwamba chumba cha mahakama hiyo kimejaa kutokana na watu kuwa wengi.

Kutokana na wafuasi wa Chadema kutokuwa tayari, lakini pia kujiridhisha kwamba nafasi ya kutosha ipo, waliendelea kuwa na msimamo wa kutaka kuingia ndani.

Kutokana na mvutano huo, polisi walilazimika kuruhusu baadhi ya wafuasi hao kuingia huku wengine wakibaki nje.

Leo tarehe 10 Machi 2020, mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya uchochezi Na. 112/2018 inayowakabili viongozi wa Chadema.

==>>Tazama hapo chini


Share:

Ofa! Ofa! Viwanja Vimeshuka Bei Tena: Mapinga na Bunju

Ofa! Ofa! Viwanja Vimeshuka Bei Tena: Mapinga na Bunju

Viwanja vipo Kimele/Mapinga (mpakani mwa Bunju na Mapinga.
Vipo viwanja vya bei zifuatazo:
Mita 10 /20 ni tsh 2.5 mil,
Mita 15/20 ni tsh 3.5 mil,
Mita 20/20 ni tsh 4.5mil,
Mita 20/30 ni tsh 6.5 mi,
Mita 20/40 ni tsh 9 mil,
Robo eka ni tsh 11 mil,
Nusu eka ni tsh 21 mil,
Eka moja ni tsh 41 mil

Viwanja hivi vipo umbali wa km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road) Na huduma zote za umeme na maji zipo.

Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki.

Hakuna dalali/udalali
Mpigie mhusika: 0758603077,
Whatsap 0757489709


Share:

TANGA UWASA YAWEKA BAYANA VISABABISHI VYA BILI KUBWA ZA MAJI

 Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala kulia akitoa ufafanuzi wa huduma za mamlaka hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari wakati alipotembelea banda lao kwenye eneo la viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika eneo hilo
 Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
 Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda lao
 
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeeleza kwamba vitu ambavyo vinasababisha bili za maji kuwa kubwa ni matumizi ya maji na kutokukaguliwa kwa miundombinu iliyopo kwenye nyumba mara kwa mara kama bomba linavuja au limedondokewa na kitu kupasuka na kumwaga maji .

Upasukaji huo wakati mwengine umekuwa hautambuliki mapema na hivyo kupelekea ongezeko la bili kubwa jambo ambalo lingeweza kudhibitiwa iwapo kungekuwa na utaratibu nzuri wa kufanyika ukaguzi huo mara kwa mara kwenye miundombinu hiyo.

Hayo yalisemwa leo na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devota Mayala wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.

Alisema kwamba walitumia siku hiyo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zao za maji safi na uondoshaji wa maji taka ambapo katika suala hilo mtumiaji mkubwa ni mwanamke kwa sababu walipaji wa bili ni wakina baba na watumiaji wakubwa ni wakina mama ndio wanatumia kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

“Bili kubwa inasababishwa na vitu vingi ikiwemo matumizi ya maji, miundombinu iliyopo kwenye majumba yetu kama watu hawana utaratibu wa kukagua mabomba unakuta linamwaga maji au limedondokewa na kitu likapasuka bila watu kujua na hivyo maji yakimwagia kwenye mita inaandika maji yametumika”Alisema

Alisema kitu kingine ni hitilafu kwenye mita hali inayochangia uwepo wa bili kubwa ambazo huzielewi huku gharama unazolipa zisizo sahihi unaruhusiwa kufika ofisini na kuonana na wahusika na kuambiwa ufanye nini ili ikiwemo upimaji wa mita yako.

Hata hivyo alisema mita itapimwa na utaonyeshwa kama inashida na baadae itabadilishwa kwa hiyo wapo kwenye maadhimisho hayo kuwaelimisha wakina mama na wananchi kuhusiana na suala hilo.

Awali akizungumza Afisa Utawala wa Tanga Uwasa Theresia Sanga alisema kwamba wataendelea kutoa elimu kuhusiana na uondoshaji maji taka majumbani ikiwemo kuacha kufanya uhujumu wa miundombinu ya maji na maji taka.

Aliwataka wananchi waliounganishwa na mtandao wa maji taka kuutumia vizuri na kutokuweka taka ngumu kwani inaweza kupelekea kutokupitisha maji vizuri.

“Lakini pia nitoe wito kwa wananchi kwenye maeneo ambayo mtandao wa maji taka umepita wateja wajiunge na mtanda huo pamoja na kuacha kuhujumu miundombinu hiyo kwa kutupa taka ngumu kwani wanakuwa wakiihujumu taasisi hiyo kwani wanatumia fedha nyingi kuirejesha kwenye hali yake ya kawaida”Alisema
Share:

PICHA: Viongozi Mbalimbali wa CHADEMA Na Wafuasi Wao Wafurika Mahakama ya Kisutu ....Hukumu Imesogezwa Mbele Hadi Saa Saba

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefurika wafuasi wa Chadema na ulinzi umeimarishwa kwa askari kila kona  kabla ya muda wa hukumu.
Wafuasi hao walianza kumiminika eneo la mahakama tangu saa moja asubuhi wakisubiri hukumu ya vigogo wa Chadema akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe

Hukumu hiyo  ilitarajiwa kusomwa saa nne na nusu asubuhi   lakini imesogezwa mbele hadi saa saba na nusu mchana



Share:

Waziri mkuu wa Sudan arejea ofisini baada ya jaribio la kumuua

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amerejea ofisini  baada ya jaribio la kumuua kushindwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum. 

Msemaji wa baraza la mawaziri, Faisal Mohamed Salih amesema kiongozi huyo anaendelea na majukumu yake ofisini kama kawaida. 

Hamdok ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anawahakikishia watu wa Sudan kuwa yuko salama kabisa. 

Amesema shambulizi hilo halitorudisha nyuma harakati za Sudan kuelekea katika demokrasia. 

Faisal amesema vikosi vya usalama vinawatafuta magaidi walioushambulia msafara wa Hamdok. 

Shambulizi hilo lilitokea karibu ya gari la kiongozi huyo wakati msafara wale ukipita kuingia kwenye daraja la Kober, kaskazini mwa Khartoum akiwa anaelekea ofisini kwake. 

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.


Share:

TAMISEMI Releases the list of new recruited health workers 2020

TAMISEMI has officially released the list of recruited health workers . For more details , read the official press release notice from TAMISEMI below You can check your name in the attached pdf document below

The post TAMISEMI Releases the list of new recruited health workers 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania Yafanya Vizuri Mfumuko wa Bei

Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa mfumuko wa bei wa taifa umezidi kuimarika kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020 baada ya kubaki palepale kwenye asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioshia Januari 2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi.Ruth Minja alisema kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioushia mwezi Februari, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi ya iliyokuwepo mwezi Januari, 2020.

“Hali hii ya mfumuko wa bei kubaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi Januari imechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Februari 2020”, alisema  Bi. Ruth Minja.

Aidha ameongeza  kuwa kuna baadhi ya bidhaa za vyakula kama nyama ambayo iliongezeka kwa asilimia 1.6, samaki 6.1, mafuta ya kupikia 2.8, maharage 9.3 na viazi vitamu 4.2. Ongezeko la bei ambalo limekuwepo kwa Februari 2020 ni sawa na ongezeko hilo Februari 2019

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Februari, 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2019 kama vile jiko la gesi ya  kupikia lilipungua kwa asilimia 1.6, viatu vya watoto asilimia 1.0, mafuta ya nywele za  wanawake asilimia 2.5 na  gharama za huduma za starehe asilimia 1.0.

Minja alibainisha kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioisha mwezi Februari, 2020 umeongezeka hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka ulioishia Januari 2020.

Aliitaja Tanzania katika Nchi za  Afrika Mashariki kuwa imeendelea kuwa vizuri kwenye mfumuko wa bei kwa asilimia 3.7 ikilinganishwa na Kenya asilimia 6.37 kutoka asilimia 5.78, wakati Uganda mfumuko wa bei umebakia pale pale 3.4 kwa mwaka ulioishia Januari 2020.

Mwisho.


Share:

Mawaziri Sekta ya afya nchi za SADC Wakutana Kwa Dharura Tanzania Kujadili Namna Ya Kukabiliana na Virusi Vya CORONA

Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), imesema imejiandaa kikamilifu kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Virusi vya Corona (Covid-19) ambao umezidi kusambaa duniani na kwamba mikakati madhubuti imeweka tayari kwa kutoa elimu ya kutosha jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wananchi wa ukanda huo wa Afrika.

Akizungumza katika Mkutano wa dharura uliofanyika Jijini Dar es Salaam, ambao uliitishwa kujadili hali ya mlipuko wa ugonjwa huo uliohudhuriwa na nchi 10 kati ya 16 za ukanda wa Kusini mwa Afrika, zikiwemo Angola, Congo DRC, Lethoto, Mauritius, Malawi, Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia Namibia na Tanzania, Waziri mwenye dhamana ya Afya kutoka Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu alisema kuwa tayari nchi hizo zimefanya maandalizi na sasa zimeingia kwenye hatua ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Tupo hapa leo kujadili hali ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona (Covid -19), ambao sisi kama nchi wanachama tumekuja kubadilishana taarifa kuhusiana na ugonjwa huu na kuona kama nchi za SADC tumejipanga kukabiliana nao na sasa imeonesha kuwepo na hali ya utayari kwa kila nchi mwanachama”, Alisema Ummy Mwalimu.

Alibainisha kuwa kati ya Nchi 16 za SADC ni nchi moja tu ambayo mpaka sasa imebainika kuwa na washukiwa wa ugonjwa huo ambayo ni Afrika ya Kusini na nchi zingine ziko salama, lakini walikubaliana kuwa nchi hizo zianzisha utaratibu wa kujipima na kujitathmini badala ya kusubiri tathmini za wadau wa afya.

Katika Mkutano huo, Waziri Ummy alisema nchi hizo zilifikia makubaliano mbalimbali katika kukabili ugonjwa huo ikiwemo hilo la kujitathmini wenyewe, kushirikisha sekta nyingine kama Utalii, Uchumi, fedha pamoja na Uhamiaji, kutoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri wa SADC kutofanya mikutano ya ana kwa ana badala yake njia nyingine zitumike kama vile video conference.

Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuweza kupambana na ugonjwa huo kwani mpaka Machi 9, 2020 kumekuwepo na mabadiliko makubwa ambapo maambukiza mapya yamepungua na kufikia watu 28 tu.

“Ninawashukuru Serikali ya China kwa kudhibiti ugonjwa huu kwani mpaka leo China ina wagonjwa wapya 28 hali hii inaonesha jinsi gani wenzetu wameweza kupambana kwa kiasi kikubwa kwa hiyo sisi kama nchi za SADC tumejipanga kukabiliana na  Corona (Covid -19)”, Alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wa Tanzania mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote wa Corona (Covid 19), lakini Serikali imejiandaa kwa kiasi kikubwa kwa kutenga maeneo iwapo ya  kuwatibu iwapo wagonjwa hao watapatikana na kwa sasa inajenga eneo la kudumu katika Hospitali ya Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

Katika sehemu za kusafiria na kupokea wageni na mizigo ikiwemo Viwanja vya ndege, bandari  na maeneo ya mipakani Serikali imeweka vipima joto vya kutambua ugonjwa huo.

Naye Waziri wa Afya kutoka Zimbabwe, Mhe.Dkt. Obadiah Moyo, alisema kuwa Nchi za SADC hususani nchini kwake zimejiandaa kukabiliana na ugonjwa huo kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wake jinsi ya kujikinga na kuepukana nao.

“Tutatoa elimu ya uelewa kwa wananchi wetu kwani elimu hiyo ni muhimu sana kujikinga na ugonjwa huu na tutahakikisha kwamba tunashirikiana na kushirikishana kama nchi za ukanda huu ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu katika nchi nyingine za  ukanda huu”, Alisema Waziri Moyo.

Aidha katika kuwatambua wanafunzi  wa Nchi za Kusini Mwa Afrika walioko China, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania  Dkt. Damas Ndumbaro alisema kuwa mpaka sasa wanafunzi hao kutoka nchi za SADC wako salama na hakuna aliyeambikizwa.

“Wanafunzi wa SADC walioko China wako salama kabisa hakuna mwanafunzi yeyote aliyeambukizwa ugonjwa huo, lakini tunataka nchi zetu za SADC zibaki salama tunatakiwa kupata elimu na kuelewa tunachofundishwa kuhusiana na ugonjwa huu”, Alibainisha Dkt.Ndumbaro.

aliendelea kusema kuwa Dkt.Ndumbaro kuwa Vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika kutoa taarifa sahihi kuhusiana na ugonjwa huo, hivyo vinatakiwa kushirikiana na mamlaka husika za afya ili kupata taarifa sahihi ambazo zitawatoa hofu wananchi katika ukanda huo wa Afrika.

Mwisho


Share:

Hukumu Ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA ni Leo Mahakama Ya Kisutu

Mahakama ya Kisutu leo March 10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri.

Mbali na Mbowe, wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Katibu Mkuu wa sasa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na mbunge, Halima Mdee.

Wabunge wengine ni Esther Matiko, Esther Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche. Katika kesi hiyo, baadhi ya washtakiwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mitatu kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.


Share:

RC Tabora Aagiza Kukamatwa Kwa Wanaotumia Vyandarua Kinyume Cha Utaratibu Wa Kujikinga Na Mbu

NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wa vijiji na mitaa kuwamata watu wote watakutwa wakitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu.

Alisema matumizi ya vyandarua nje ya kujikinga na mbu yanapingana na juhudi za Serikali za kupambana malaria na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa

Mwanri alitoa kauli hiyo  wilayani Kaliua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.

Alisema kuwa katika baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki katika madimbwi na wengine wanatumia kuzungushia vifaranga vya kuku vishismbuliwe na mwewe.

Mwanri aliongeza kuwa kuna watu wengine wanatumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kuzungushia bustani za matunda na mboga mboga ili kuzuia wadudu waharibifu.

Alisema matumizi hayo ambayo ni kinyume cha kujikinga na mbu ni marufuku mkoani na atakayekuwa atachukuliwa hatua.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa alisema mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa malaria uwe umetokomezwa.

Alisema takwimu zinaonyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa Mkoa wa Tabora bado ni tatizo ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina asilimia 16.7 , kufuatia Uyui asilimia 16.1 na Sikonge ambayo ina asilimia 13.9.

Dkt. Rutatatinisibwa alisema Urambo ina asilimia 12.8, Manispaa ya Tabora asilimia 8.9, Halamashauri ya wilaya ya Nzega asimilia 8.7, Nzega Mji asilimia 6.8 na Igunga asilimia 5.6.

Alisema nguvu zaidi zinahitajika katika kupmbana na tatizo la malaria mkoani Tabora.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne March 10























Share:

Monday, 9 March 2020

Jobs at Morogoro International School

Morogoro International School Job Opportunities at Morogoro International School Morogoro International School invites the suitable qualified Tanzania Citizens to fill the following posts for academic year 2020/21. Job start date is August 2020. MOROGORO INTERNATIONAL SCHOOL -British/Cambridge International Education (CIE) Curriculum. IGCSE & A-Level Position Title: School Driver Qualifications/ Experience.  Safe driving record  At least a… Read More »

The post Jobs at Morogoro International School appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Underwriter at UAP Insurance

UAP Insurance Tanzania is a member of the UAP Old Mutual Group in East Africa, which is a subsidiary of Old Mutual Limited (OML) in Africa. UAP made its entry into the Tanzania market in 2013 after the acquisition of a majority 60% shareholding in Century Insurance Company. We are proud of our contribution in the growth of… Read More »

The post Senior Underwriter at UAP Insurance appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Branch Manager at UAP Insurance

UAP Insurance Tanzania is a member of the UAP Old Mutual Group in East Africa, which is a subsidiary of Old Mutual Limited (OML) in Africa. UAP made its entry into the Tanzania market in 2013 after the acquisition of a majority 60% shareholding in Century Insurance Company. We are proud of our contribution in the growth of… Read More »

The post Branch Manager at UAP Insurance appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania ni nchi ya mfano katika kulinda haki za watu wenye ulemavu wa ngozi

Dodoma, 9 Machi 2020
Tanzania imetajwa kuwa ni nchi ya kupigiwa mfano na inayopaswa kuigwa kutokana na  mikakati mizuri iliyojiwekea katika kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mtaalam wa Kujitegemea anayeshughulikia haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi, Bi. Ikponwosa Ero, alipowasilisha taarifa yake kwenye Kikao cha 43 cha Baraza la Haki za Binadamu kilichoanza mwishoni mwa mwezi Februari 2020 Geneva, Uswizi.
 
Bi. Ero alilieleza Baraza hilo kuwa hali ya haki za binadamu kwa watoto na wanawake wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali duniani bado si nzuri. Hata hivyo, alisema kuwa kuna nchi ambazo zimefanya vizuri katika kuboresha haki za binadamu za wanawake na watoto wenye ulemavu wa ngozi na kuitaja Tanzania kuwa ni moja ya nchi hizo.
 
Mtaalamu huyo alianisha maeneo ambayo Tanzania imefanya vizuri kuwa ni pamoja na kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji takwimu za watu wenye ulemavu wa ngozi na kuzitaka nchi nyingine ziige mfano huo wa Tanzania. Pia alieleza na kusifia Ibara ya 6 ya Katiba ya Baraza la Watoto (Junior Council) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloelezea hatua mahususi kwa ajili ya kuwajumuisha watoto wenye ulemavu katika michakato yake. 
 
Aidha, mtaalamu huyo alitoa mfano wa Kikundi cha Upendo wa Mama kilichoundwa kwa ajili ya kuwawezesha akinamama wenye ulemavu wa ngozi katika kujipatia kipato na kuelezea kuwa kikundi hicho kinatoa elimu ya kuwawezesha akinamama walemavu wa ngozi kujilinda na kujitambua na kusema kuwa hilo ni jambo jema.
 
Mambo meninge aliyoyasifia kwa Tanzania ni pamoja na mifumo mizuri iliyowekwa  katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanasikika au kushiriki kwenye vikao vya maamuzi yanayowagusa moja kwa moja, utengenezaji wa mafuta maalumu ya ngozi (sunscreen) ndani ya nchi na kuyasambaza kwa wahitaji wote nchini, uanzishwaji wa mpango jumuishi wa kitaifa ambao lengo lake ni kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu na hasa wenye ulemavu wa ngozi wanawekewa mazingira mazuri na rafiki ya kuwawezesha kupata haki yao ya elimu na mfumo mzuri wa mashauri/kesi za watu wenye ulemavu wa ngozi kupewa kipaumbele kwa kusikilizwa kwa haraka.
 
Wakati wa majadiliano, Tanzania ilitoa hotuba kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kulinda haki za watu wenye ulemavu wa ngozi. Hotuba hiyo, pamoja na mambo mengine ilieleza kuwa Serikali imetekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Mtaalamu huyo wa Kujitegemea alipoitembelea Tanzania mwaka 2016 na kuwa Serikali itaendelea kushirikiana naye ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanapata ulinzi na kuwa haki zao zinalindwa kama raia wengine. 
 
Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali liitwalo World Barua Organization lenye makao makuu yake Geneva naye alitoa  hotuba kwenye Baraza la Haki za Binadamu na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya takwimu kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali


Share:

Lukuvi Asambaratisha ulaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya maafisa ardhi wa jiji la Arusha.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi amemaliza rasmi ulaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya maafisa ardhi wa jiji la Arusha.

Waziri Lukuvi amesema hayo mkoani Arusha tarehe 8/3/2020 wakati wa ziara yake ya kuanzisha rasmi ofisi za ardhi za mikoa na kuvunja ofisi za kanda ambazo zilikuwa zinahudumia zaidi ya mkoa mmoja, hali iliyokuwa inawasababishia wananchi usumbufu.

Akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati akianzisha rasmi ofisi mpya ya kanda ya mkoa wa Arusha amesema kuanzia sasa ulaji uliokuwa unafanyika na baadhi ya maafisa aridhi wa jiji kwa kudai posho za kwenda kufuatilia hati mkoa wa kilimanjaro ameaumaliza rasmi.

Ameongeza kuwa Huduma zote za utoaji hati, uandaaji wa michoro ya mipango miji, pamoja na huduma za Msajili wa Hati zitatolewa Katika Jiji la Arusha na sio katika makao makuu ya kanda Moshi kama ilivyokuwa hapo awali.

Hadi sasa Waziri Lukuvi ameishafungua ofisi za ardhi ngazi ya mkoa katika mikoa ya Singida, Tabora, Geita, Mara na Arusha na kazi inaendelea katika mikoa mingine yote nchini ambapo huduma zote za uandaaji na utoaji hati kuanzia sasa zinafanyika mkoani.

Hatua hii ya  kuanzisha ofisi za ardhi ngazi ya mkoa imekuja ili kupunguza kero za wananchi kufuata huduma hiyo Wizarani au katika Makao makuu ya Ofisi za Kanda za mikoa mitatumitatu.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger