Tuesday, 10 March 2020

Waziri mkuu wa Sudan arejea ofisini baada ya jaribio la kumuua

...
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amerejea ofisini  baada ya jaribio la kumuua kushindwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum. 

Msemaji wa baraza la mawaziri, Faisal Mohamed Salih amesema kiongozi huyo anaendelea na majukumu yake ofisini kama kawaida. 

Hamdok ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anawahakikishia watu wa Sudan kuwa yuko salama kabisa. 

Amesema shambulizi hilo halitorudisha nyuma harakati za Sudan kuelekea katika demokrasia. 

Faisal amesema vikosi vya usalama vinawatafuta magaidi walioushambulia msafara wa Hamdok. 

Shambulizi hilo lilitokea karibu ya gari la kiongozi huyo wakati msafara wale ukipita kuingia kwenye daraja la Kober, kaskazini mwa Khartoum akiwa anaelekea ofisini kwake. 

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger