Sunday, 8 March 2020

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA VIFAA VYA KAZI 'EPLONI' KWA MAMA LISHE 300 SHINYANGA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad(CCM) ametoa msaada wa vifaa vya kazi ‘Eploni’ zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kwa wajasiriamali 300 wanaojihusisha na uuzaji vyakula ‘ Mama Lishe’ mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Azza amekabidhi taulo hizo leo Jumapili Machi 8,2020 wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mhe. Azza amesema Eploni hizo zitawasaida katika masuala ya kuboresha usafi kwa Mama Lishe katika maeneo yao kazi.

“Leo tukiwa tunaadhimisha siku ya wanawake duniani,natumia fursa hii kuwakumbuka wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara ya chakula ‘Mama Lishe’ kwa kuwapatia eploni 300 zenye thamani ya shilingi Milioni 2 na laki nne ambazo zitagawiwa kwa wanawake 50 katika kila halmashauri ya wilaya mkoani Shinyanga”,alisema Azza.

Mbunge huyo aliwaomba Wakurugenzi 6 wa Halmashauri za wilaya kuzigawa eploni hizo kwa usawa kwa wanawake wanaouza vyakula ‘Mama Lishe’.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad(CCM)  akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kazi ‘Eploni’ zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kwa wajasiriamali 300 wanaojihusisha na uuzaji vyakula ‘ Mama Lishe’ mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Machi 8,2020 kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi ' Eploni'.
Mama Lishe wakiwa wamevaa Eploni
Mama Lishe wakiwa wamevaa Eploni
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Prisca Musoma kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Verena Peter Ntulo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kahama, Ashura Hoja kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Eploni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu, Rehema Edson kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo. 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na Wakurugenzi/Wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 6 za mkoa wa Shinyanga waliopokea vifaa vya kazi vya Mama Lishe na watakwenda kuzigawa kwa Mama Lishe waliopo katika halmashauri zao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi ' Eploni'.
Picha zote na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog
Share:

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA TAULO LAINI 'PEDI' ZA MIL 7.8 KWA WANAFUNZI WA KIKE DARASA LA SABA 2020

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa ameshikilia Taulo laini za kike na wanafunzi wanaosoma darasa la saba katika shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 bog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) amegawa Taulo laini za kike ‘Pedi’ zinazofuliwa zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Azza amekabidhi taulo hizo leo Jumapili Machi 8,2020 wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mhe. Azza ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi,amesema taulo hizo laini zinazofuliwa ni kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.

“Takwimu zinaonesha kuwa watoto wengi wa kike wanapokuwa katika siku zao ‘Hedhi’ huwa hawaendi shuleni kutokana na mazingira wanakotoka hivyo kupoteza masomo yao. Kutokana na hali hii nilikaa nikafikiria namna ya kuwasaidia watoto wetu,nikashirikisha wadau mbalimbali ambao waliniunga mkono,tukaanza kuchangishana na kufanikiwa kupata shilingi Milioni 7, laki 7 na 78 elfu kwa ajili ya taulo laini”,amesema Azza.

“Nimefanikiwa kupata maboksi 66 yenye pakti 12 ambapo ndani ya kila pakti kuna taulo nne. Taulo hizi tunazigawa katika halmashauri zote 6 za wilaya mkoa wa Shinyanga,kila halmashauri itapata taulo laini 130.Tutawapatia wanafunzi 780 kutoka shule 30 ambapo tutatoa kwa shule 5 zilizopo pembezoni kwa kila halmashauri”,ameeleza Mhe. Azza.

Mbunge huyo alisema kila mwanafunzi apatiwa pakti moja ambayo ina taulo laini za kike nne ambazo atazitumia kwa kipindi cha mwaka mzima kwani kila taulo laini inatumika kwa muda wa miezi mitatu.

“Naomba Wakurugenzi wa halmashauri mhakikishe mnagawa hizi taulo laini kwa watoto wa kike wanaotoka katika mazingira magumu.Tunataka watoto wa kike wakae darasani muda wote ili waweze kufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba vizuri”,ameongeza Azza.

Mhe. Azza ametumia fursa hiyo kuwapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kumuunga mkono kufanikisha Kampeni yake ya kumuandaa msichana kufanya mtihani wa darasa la saba 2020 kwa kumpatia Taulo za kike.

“Miongoni mwa wadau walioniunga mkono ni serikali ya mkoa wa Shinyanga,Shirika la VSO, Agape,Life Water International,Benki ya CRDB na Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd pamoja na marafiki zangu ,viongozi,wananchi na wadau wa maendeleo mbalimbali wa maendeleo” ,amefafanua Mhe. Azza. 

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale amesema taulo  laini za kike zinamfanya mtoto wa kike kujiamini na kuhudhuria masomo yake bila kikwazo hivyo inaongeza nafasi ya watoto kufanya vizuri katika masomo yao.

Aidha amewaomba wadau wasaidie kutoa elimu ya matumizi sahihi ya pedi kwa watoto wa kike ikiwemo kuwashauri kutozianika uvunguni bali sehemu yenye jua na mwanga wa kutosha na wazifue pedi hizo kwa maji moto.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumapili Machi 8,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza wakati wa zoezi la kugawa taulo laini za kike ambapo amesema taulo  laini za kike zinamfanya mtoto wa kike kujiamini na kuhudhuria masomo yake bila kikwazo hivyo inaongeza nafasi ya watoto kufanya vizuri katika masomo yao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea namna alivyoshirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea namna alivyoshirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7. Kushoto ni sehemu ya maboksi 66 yenye taulo hizo laini za kike.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia fedha na hatimaye kupatikana kwa taulo laini kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Muonekano wa boksi lenye taulo laini za kike.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia fedha na hatimaye kupatikana kwa taulo laini kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi taulo laini ya kike mmoja wa wanafunzi wanaosoma darasa la saba katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akigawa taulo laini za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa ameshikilia Taulo laini za kike na wanafunzi wanaosoma darasa la saba katika shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakishuhudia zoezi la ugawaji taulo laini za kike.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi boksi la Taulo laini za kike Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe.Hoja Mahiba. Kila halmashauri imepewa taulo laini 130 kwa ajili ya kuzigawa katika shule tano kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi boksi la Taulo laini za kike Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga. Kila halmashauri imepewa taulo laini 130 kwa ajili ya kuzigawa katika shule tano kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi boksi la Taulo laini za kike Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Verena Peter Ntulo.  Kila halmashauri imepewa taulo laini 130 kwa ajili ya kuzigawa katika shule tano kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi boksi la Taulo laini za kike Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kahama, Ashura Hoja.  Kila halmashauri imepewa taulo laini 130 kwa ajili ya kuzigawa katika shule tano kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi boksi la Taulo laini za kike Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu, Rehema Edson. Kila halmashauri imepewa taulo laini 130 kwa ajili ya kuzigawa katika shule tano kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali waliofanikisha kupatikana kwa  Taulo laini za kike ‘ Pedi’ zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali waliofanikisha kupatikana kwa  Taulo laini za kike ‘ Pedi’ zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wakishuhudia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa zoezi la ugawaji taulo laini za kike.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza muziki na wanawake  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga ambapo Mbunge huyo ametumia maadhimisho hayo kugawa Taulo laini za kike ‘ Pedi’ zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

YANGA SC WAIPA KICHAPO SIMBA SC 1-0 MBELE YA RAIS MAGUFULI NA RAIS WA CAF, AHMAD


Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
YANGA SC imefuta uteja uliodumu kwa miaka minne mbele ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Yanga SC ni leo kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 44 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 25.

Morrison, mchezaji wa zamani wa Heart of Lions, Ashanti Gold za kwao Ghana, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Delhi Dynamos FC ya India na Orlando Pirates ya Afrika Kusini alifunga bao hilo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kungo Jonas Gerlad Mkude. 
Na Yanga walipata bao hilo baada ya beki tegemeo wa kati wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni kuumia na kushindwa na kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Kennedy Juma Wilson dakika ya 23 tu.

Pamoja na Yanga kumaliza dakika 45 za kwanza ikiwa inaongoza, lakini ni Simba SC waliotawala zaidi mchezo huo na kutengeneza nafasi nzuri zaidi za kufunga, wakashindwa kuzitumia.

Na sifa zimuendee mlinda mlango, Metacha Boniphace Mnata aliyeokoa michomo mingi ya hatari, ingawa na walinzi wake wanastahili sifa kwa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Kipindi cha pili Simba SC waliingia kwa kasi zaidi na kuendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa Yanga, lakini kikwazo kikawa kile kile – kupoteza nafasi ama kwa wapinzani kuokoa, au kupiga nje.

Mfungaji wa bao la Yanga, Morrison naye akashindwa kuendelea na mchezo baada ya takriban saa moja, kufuatia kuumia pia na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana.

Kwa sehemu kubwa ya kipindi cha pili, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Luc Eymael anayesadiwa na mzawa, Charles Boniface Mkwasa ilicheza kwa kijihami na kushambulia kwa kushitukiza.

Dakika ya 70, kocha wa Simba SC, Mbelgiji pia Sven Ludwig Vandenbroeck anayesaidiwa na mzawa pia, Suleiman Matola alimpumzisha mshambuliaji wake wake wa kimataifa wa Rwanda, Medde Kagere na kumuingiza kiungo Hassan Dilunga.

Bado haikuizuia Simba kuendelea kushambulia lango la Yanga, lakini pamoja na umakini wa wapinzani wao – bahati pia ililalia upande wa Jangwani leo.

Mchezo wa leo umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na Wenyekiti wa klabu zote, Dk. Mshindo Msolla wa Yanga na Mohamed ‘Mo’ Dewji wa Simba. 

Yanga inafikisha pointi 50 baada ya ushindi wa leo katika mchezo wa 25 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi moja Azam FC inayoshika nafasi ya pili ingawa mecheza mechi mbili zaidi.

Mabingwa watetezi, Simba SC wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa mbali, wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum/Kelvin Yondan dk90+4, Papy Tshishimbi, Haruna Niyonzima, Bernard Morrison/Patrick Sibomana dk56, Ditram Nchimbi na Balama Mapinduzi/Deus Kaseke dk86.

Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni/Kennedy Wilson dk23, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Luis Miquissone, Clatous Chama, Meddie Kagere/Hassan Dilunga dk70, John Bocco na Francis Kahata/Deo Kanda dk62.
Chanzo - Binzubeiry
Share:

Baba Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba Afariki Dunia

Baba Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amefariki leo Machi 8, 2020, saa nne asubuhi akiwa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Mdogo wake Kanumba, Mjanaeli Kanumba amethibitisha. 

Mzee Kanumba kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la nyonga lililosambabishwa kushindwa kutembea kwa muda mrefu na uvimbe katika kibofu cha mkojo pamoja na shinikizo la damu.

Amesema msiba upo nyumbani kwa baba huyo  Ngokolo mkoani Shinyanga na utaratibu wa ratiba za mazishi bado zinaelendea.


Share:

Makamu wa Rais Samua Suluhu Akemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa wakiume

Na Mwandishi Wetu Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa wakiume ambao wamekuwa wakidhalilishwa kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.

Ameyasema hayo leo mkoani Simiyu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani humo.

Amewataka watanzania kusimama pampja kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kila mmoja kuwa katika mapambano haya ya kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Sasa hii tabia ya kuwageuza watoto wa kiume.tumatengeneza taifa gani la kuwaharibu watoto wa kiume na hili haliwapi uhalali kuwafa yia vitendo hivyo watoto wa kike" alisema

Amezitaka Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto kufanya kazi na kuacha kujuana ili Sheria ichukue mkondo wake pale inapotokea mtu amefanya kitendo cha kikatili.

Ameisisitiza jamii kusimama pamoja katika kupinga na kupambana na vitendo vya ukatili katika maeneno yao kwani vitendo vingi hufanywa na watu wa karibu wa familia hivyo kuvifumbia macho na wahanga wa vitendo hivyo kukosa haki zao.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa agemda yabusawa wa kijinsia sio ya wanawake peke yao ila ni ya kwa wote yani wanawake na wanaume ili kuweza kuleta usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa chachu kwa watoto wa kike na wanawake wa Tanzania katika kuwaza makubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ya kijinsia.

"Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wanawake katika uongozi na hakika hatujamuangusha tumezitendea haki nafasi zetu" alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu na kuwa na maendeleo kwani mtazamo na elimu itamsaidia mtoto wa kike katika kupambanua mambo na kujiletea maendeleo.

"Tukiweza kumsaidia mtoto wa kike kufika katika maendeleo yake ni kumsaidia kuondokana na changamoto zinazomkwamisha kufikia malengo yake" alisema

Ameongeza kuwa muhimu ni kwa wadau kushirikiana na Serikali kuwezesha mabweni yatakayosaidia watoto wa kike kuondokana na vishawishi vitakavyowasababishia kuwarudisha nyuma katika kufikia ndoto zao.

Mhe. Mtaka amewataka wazazi na walezi kuzingatia elimu ya jinsia kuanzia kazi ya familia ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia kuanzia katika familia ili kuweza kumkomboa mtoto wa kike na ukandamizaji na unyanyasaji.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa yamefanyika katika mkoa wa Simiyu yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadaye.

 


Share:

WANAWAKE MKOANI TANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UCHUMI WA VIWANDA

 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
 Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
 Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga

 Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
 
NA MWANDISHI WETU,TANGA

WANAWAKE Mkoani Tanga wametakiwa kuchangimkia fursa ya kauli mbiu ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga.

Alisema wakina mama wasilaze damu kwa kuhakikisha wanachangamkia fursa ikiwemo kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha viwanda ambavyo vitakuwa chachu kubwa ya kufikia mafanikio na kuweza kuwainua kiuchumi.

“Wakina mama tunaweza kufanya hivyo kwani tuna vikundi vidogo vidogo tunavyoweza kujipatia fedha ikiwemo vikoba tutumie fursa hiyo kwa kuunganisha nguvu za pamoja kufikia malengo yetu”Alisema Meneja huyo.

“Lakini pia tuhakikishe wanawake tunalipa kodi kwa hiari kwani ndio jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu pia tujikite kwenye ujasiriamali ambao utakuwa chachu kubwa “Alisema

Aidha alisema kwamba pia wakinamama wajikite kufungua viwanda kikubwa na vidogo ili kuweza kuwasaidia na kutoa ajira na hivyo kuepukana na kuwa tegemezi kwa wanaume ili uchumi wa viwanda usiwapite.

“Leo ni siku ya wanawake duniani wanawake ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote lile sisi TRA tumeungana na wanawake wenzetu lakini pia niwahimize mlipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu”Alisema

Hata hivyo alisema katika jamii watu wanaoingaika na mambo ya kiuchumi ni wanawake kuanzia ngazi ya familia mpaka maofisini hivyo wakina mama wanamcvhango mkubwa kwa maendeleo.

“Kwenye familia mwanamke ndio Waziri wa fedha na mipango, mama kama nguzo ya familia kutengewa siku yake ni jambo muhimu sana anayefahamu vizuri umuhimu wa mama ni yule ambayo mama yake ameshamtoka”Alisema

Meneja huyo alisema jamii nzima inatambua juhudi kubwa ambazo wakina mama wanafanya na sapoti wanazofanya wakina mama ambao unaweza kuwafananisha na majembe. “Pia wakina mama wanahainagika, wakina mama ni walipa kodi wazuri wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa,wakina mama wajikite kwenye shughuli za kujenga uchumi wa nchi kwa kulipa kodi kwa hiari na wakati.
Share:

Wajumbe Wa Baraza La Wafanyakazi Ofisi Ya Waziri Mkuu Wahimizwa Kutekeleza Majukumu Kwa Ufanisi

Na: Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wamehimizwa kutekeleza majukumu kwa ufanisi na weledi ili kuimarisha utendaji kazi wao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Arusha alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo uliyofanyika katika ukumbi wa Mkutano uliyopo katika hoteli ya Gold Crest, Machi 8, 2020.

Alieleza kuwa uwepo wa Baraza la Wafanyakazi katika sehemu za kazi unasaidia kuongeza ushirikishwaji wa watumishi katika kupanga na kutekeleza majukumu yao, kuleta usawa katika kujadili mambo muhimu, kutoa ushauri juu ya tija na ufanisi wa kazi ikiwemo kukumbushana, kuelimishana na kuweka mazingira bora ya utendaji kazi na kuweka umoja kati ya wafanyakazi na viongozi.

“Ni matumaini yangu Baraza hili litakuwa na mijadala yenye uwazi na mambo yote yatakayojadiliwa yatasaidia kuimarisha utendaji wa majukumu ya Ofisi kwa lengo la kuhakikisha mazingira ya utendaji kazi yanaboreshwa kwa manufaa ya kutoa huduma bora kwa wananchi, inajulikana kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ina mambo mengi yanayogusa jamii moja kwa moja na hasa masuala ya Kazi, Ajira, maendeleo ya vijana na watu wenye ulemavu,” alisema Mavunde.

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa kila mjumbe wa Baraza hilo kutumia nafasi aliyopewa ili uwakilishi wake uweze kuleta tija na kuwa chachu katika kuleta maendeleo ya watumishi wote kwa ujumla.

Sambamba na hayo Naibu Waziri Mavunde alitoa maagizo kwa Wajumbe wa Baraza ikiwemo suala la kusimamiwa vizuri sekta ya kazi hususani kuongezwa jitihada za zaidi katika kufanya kaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha sheria na kanuni za kazi hapa nchini zinafuatwa.

Pia alitilia mkazo juu ya matumizi ya teknolojia katika kuwahudumia wananchi kwa haraka na wepesi, hivyo alihimiza Baraza hilo kuandaa mpango endelevu utakao wawezesha watumishi kujifunza matumizi ya teknolojia mpya ambayo ni dhabiti katika kutoa huduma.

Aidha, Mheshimiwa Mavunde alitoa wito kwa kila mjumbe wa baraza hilo kushirikiana na watumishi wenzao na wote kwa pamoja watambue kuwa wanao wajibu wa kufanikisha malengo ya Serikali na Ofisi hiyo.

Halikadhalika aliwasihi wajumbe wa baraza hilo kuendelea kutekeleza taratibu na sheria za kupambana na masuala ya rushwa katika maeneo ya kazi. Pamoja na hayo alipongeza utendaji wa watumishi wa ofisi yake kwa utekeleza wa majukumu mbalimbali ikiwemo ubunifu katika kuratibu programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, kwa lengo la kulinda mazingira ya kazi na ajira nchini, kuanzishwa kwa mfumo wa kielektroniki wa vibali na uratibu wa mfuko mfuko wa maendeleo ya Vijana ambao unawezesha vijana kiuchumi.

Awali wakati wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wafanyakazi alisema kuwa majadiliano ambayo yamekuwa yakifanyika katika mkutano wa baraza hilo yamekuwa yakisaidia kutatua changamoto zinazojitokeza sehemu ya kazi na pia kuboresha mazingira ya utendaji na kazi. 


Share:

Watu 10 wafariki baada ya kuporomoka kwa hoteli iliyokuwa ikitumiwa kama eneo la karantini nchini China

Idadi ya watu waliofariki baada ya kuporomoka kwa hoteli moja iliyokuwa ikitumiwa kuwaweka watu chini ya karantini kutokana na virusi vya corona katika mji wa Quanzhou nchini China, imefikia watu 10. 

Mamlaka nchini humo zimesema watu wengine 28 bado wamekwama kutokana na ajali hiyo. 

Awali zaidi ya watu 70 waliaminika kukwama katika jengo hilo la ghorofa saba lililoporomoka jana jioni. 

Wakati wa mkutano na wanahabari uliondaliwa na serikali katika eneo la Quanzhou hii leo, maafisa wa serikali, wamesema kuwa kikosi cha uokoaji cha zaidi ya watu elfu moja ikiwa ni pamoja na maafisa wa zima moto, vikosi vya polisi pamoja na wahisani wengine, walifika katika eneo hilo jana usiku huku watu 43 wakiokolewa na 36 kati yao kupelekwa hospitalini. 

Shirika la habari nchini humo Xinhua, limeripoti kuwa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo ilikuwa chini ya ukarabati wakati wa tukio hilo.

-DW


Share:

Serikali Yapiga Marufuku Mwananchi Kumsajilia Laini Ya Simu Mtu Mwingine

Na Prisca Ulomi, WUUM, Iringa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga marufuku kwa mwananchi yeyote kumsajilia laini ya simu ya mkononi kwa alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakati akiwa kwenye mikutano ya hadhara kwenye kijiji cha Idodi na Isoliwaya mkoani humo wakati akizindua minara ya mawasiliano kwenye kata ya Idodi, Kihesa na Ihimbo zilizopo wilayani Kilolo na Iringa mjini.

Nditiye amesema kuwa ni marufuku kwa mwananchi yeyote kumsajilia laini ya simu ya mkononi mtu mwingine kwa alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA hata mtu huyo akiwa ni mkeo au mumeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria kupitia sheria zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amefafanua kuwa Serikali imebaini kuwa kumeibuka tabia kwa baadhi ya wananchi kuwasajilia laini za simu watu wengine kwa kisingizio kuwa hawajapata namba au kitambulisho cha taifa cha NIDA ambapo amesema kuwa tayari Serikali imetoa namba hizo au vitambulisho hivyo kwa wananchi wengi kwenye maeneo mbali mbali nchini.

Pia, amesema kuwa Serikali iliongeza muda wa kuzima laini za simu ambazo wahusika hawajazisajili kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA ili kuhakikisha kuwa wananchi walio na laini hizo wanakamilisha zoezi la usajili kwa kutambua umuhimu wa huduma za mawasiliano na matumizi ya simu za mkononi kwa kuwa hivi sasa wananchi wanatumia simu kwa shughuli mbali mbali ikiwemo za kiuchumi na kijamii.

“Ujue kitambulisho kinachotumika kusajili laini ya simu kwa alama za vidole ni kimoja tu ambacho ni kitambulisho cha taifa cha NIDA na kinatolewa na Serikali kwa mtu mmoja tu, kama kuna kosa linatokea la matumizi mabaya ya mawasiliano na laini yako ndio imetumika kwa kuwa ni kitambulisho chako kimetumika, sisi tunaifunga hiyo laini na hutasajili tena, mwananchi nenda kwa kampuni ya simu iliyokusajili ili kuhakikisha na kujiridhisha laini ulizosajili na sio vinginevyo,” amesisitiza Nditiye.

Naye Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TCRA, Mhandisi Asajile John amesema kuwa wanaendelea kushirikiana na kampuni za simu za mkononi kusajili laini za simu za mkononi kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA ambapo hadi sasa asilimia 81 ya laini zimesajaliwa na kwa waliobaki wanaendelea kusajiliwa kwa wale walikuwa na laini hizo tangu hapo awali na zoezi litakuwa endelevu kwa wanaochukua laini mpya.

Amewataka wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia na kuendesha huduma za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano yanatumika kwa shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa hivyo wananchi wajiepushe kutumia mawasiliano hayo vibaya ili waendelee kunufaika na huduma za mawasiliano.

“Mwezi Desemba mwaka 2019 kulikuwa na akaunti za benki kwenye mitandao zipatazo milioni 25 kwenye simu za mkononi na katika kipindi hicho miamala milioni 248 ilifanyika na miamala hiyo ilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi trilioni 9.5 na zote kwa ujumla wake zinaonesha umuhimu wa Sekta ya Mawasiliano kwenye uwezeshaji wa kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati,” amefafanua Mhandisi Asajile.

Aidha, Nditiye ametoa rai kwa mawakala wote wa kampuni za simu za mkononi nchini kuwasaidia wananchi kusajili laini za simu zao kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA kwa kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na TCRA.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili March 8













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger