Sunday, 8 March 2020

Watu 10 wafariki baada ya kuporomoka kwa hoteli iliyokuwa ikitumiwa kama eneo la karantini nchini China

...
Idadi ya watu waliofariki baada ya kuporomoka kwa hoteli moja iliyokuwa ikitumiwa kuwaweka watu chini ya karantini kutokana na virusi vya corona katika mji wa Quanzhou nchini China, imefikia watu 10. 

Mamlaka nchini humo zimesema watu wengine 28 bado wamekwama kutokana na ajali hiyo. 

Awali zaidi ya watu 70 waliaminika kukwama katika jengo hilo la ghorofa saba lililoporomoka jana jioni. 

Wakati wa mkutano na wanahabari uliondaliwa na serikali katika eneo la Quanzhou hii leo, maafisa wa serikali, wamesema kuwa kikosi cha uokoaji cha zaidi ya watu elfu moja ikiwa ni pamoja na maafisa wa zima moto, vikosi vya polisi pamoja na wahisani wengine, walifika katika eneo hilo jana usiku huku watu 43 wakiokolewa na 36 kati yao kupelekwa hospitalini. 

Shirika la habari nchini humo Xinhua, limeripoti kuwa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo ilikuwa chini ya ukarabati wakati wa tukio hilo.

-DW


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger