Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang ambapo amesema China inatumai kuwa wakati jumuiya ya kimataifa inapopambana kwa pamoja kukabiliana na ugonjwa huo mpya wa COVID-19, itaendelea kupambana na kuzuia kwa pamoja "virusi vya njama mbalimbali za kisiasa".
Bw. Geng amesema, hivi sasa watu wa China wanapambana na virusi hivyo kwa nguvu zote, hali ambayo inajiwajibika na pia inawajibika na usalama wa afya ya umma duniani.
Amesema kitendo cha baadhi ya watu na vyombo vya habari kutoa kauli kama hizo zinazochochea hofu kina nia mbaya ama kukosa elimu ya kimsingi.