Friday, 21 February 2020

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane kushtakiwa kwa mauaji ya mkewe

...
Jeshi la Polisi Nchini Lesotho limesema litamshitaki Waziri Mkuu Thomas Thabane, 80 kwa mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane

Thabane ametangaza kuwa atajiuzulu mwezi Julai kutokana na umri wake, lakini Chama chake kilimtaka ajizulu kabla ya Jana Alhamisi.

Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa kwa mauaji hayo..

Thabane atakuwa kiongozi wa kwanza kusini mwa Afrika kushtakiwa kwa mauaji akiwa madarakani, katika kesi ambayo imeishitua nchi hiyo.


Mkewe wa zamani Lipoleo Thabane alipigwa risasi na kufariki nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Maseru siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu 2017.

Wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na kabla ya mauaji hayo walikuwa katika mchakato wa kupeana talaka.

Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana , lakini stakahabadhi zilizowasilishwa mahakamani hivi karibuni na kamishana wa polisi ,zinawatuhumu Waziri Mkuu na Mkewe wa sasa kwamba walihusika na mauaji hayo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger