Friday, 14 February 2020

Infinix Kuipamba Valentine Kwa Uzinduzi Duka La Pili La Kisasa-Infinix Smart Hub.

Katika Kusheherekea sikukuu ya wapendanao, kampuni ya simu, Infinix Mobile Tanzania imezindua rasmi duka Jipya, maarufu kama Infinix Smart Hub, lililopo China Plaza Kariakoo. Hili ni duka la pili la kuzinduliwa na kampuni hiyo huku lengo kuu ni kuwafikia wateja wake kwa urahisi zaidi.

Katika uzinduzi huo afisa wa mahusiano wa kampuni ya simu ya Infinix, Aisha Karupa alivieleza vyombo vya habari kuwa, “Infinix imejipanga vizuri katika kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu wa maeneo mbalimbali pasipo kuwa na hofu ya kutufikia kwa uharaka zaidi na katika kuhakikisha tunafanikiwa katika hilo Infinix Smart Hub itakuwa ikitoa huduma kwa siku saba za kila wiki yani jumatatu hadi jumapili kuanzia saa 9:00 asubuhi hadi saa 11:30 jion”.
 
Aisha aliwashukuru watanzania kwa kuzipokea bidhaa za Infinix na kuwa wateja wazuri kwao, kusema “kwa mapenzi yenu tutaendelea kutanua wigo ili kuhakikisha mnapata huduma stahiki kama vile simu na bidhaa nyingine za Infinix zenye ubora zaidi zikiwa chini ya warranty ya mwaka mmoja na mwezi moja pamoja na elimu ya bure kuhusiana na utunzaji na utumiaji wa simu za Infinix kwa muda mrefu pasipo kuwaletea shida ya aina yoyote”. 
 
Vile vile Meneja wa Masoko Bwana Saiphone Asajile alieleza machache kuhusiana na mauzo ya Infinix tangu kuingia kwake rasmi Tanzania mwaka 2018 na ni nini watanzania wategemee kutoka Infinix hasa kwa kipindi hiki cha valentine,
“Watanzania wameonyesha upendo wa hali ya juu sana kwetu na hadi kufikia hatua ya kuzindua duka la pili la kisasa sio hatua ndogo, kwani kuna kampuni nyingi za simu tumezikuta lakini hawajafanikiwa kufanya hili tunalolifanya Infinix, hiki ni kiashirio tosha Infinix imeliteka soko la simu kwa asilimia kubwa lakini vile vile katika kuendeleza upendo kama ilivyo kawaida yetu katika Msimu huu wa Valentine Infinix inakupa ofa ya 10%, Infinix gift package na chakula cha usiku kwa wewe na umpendaye katika restaurant ya kisasa”.
 
Uzinduzi huo ulishamirishwa na michezo mbalimbali pamoja na muziki wa live band na kuufanye uwe wa kipekee.



Share:

Bashe:Hakuna Maeneo Yaliyoshambuliwa Na Nzige Nchini

Na Faustine Gimu
Naibu waziri wa kilimo MHE.HUSSEN BASHE amesema kuwa hakuna eneo lolote ambalo limeshambuliwa na nzige hapa nchini kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikizagaa mitandaoni.

MHE.BASHE amesema hayo mkoani Dodoma katika kongamano la wachambuzi  wa sera za kilimo nchini ambapo wadau hao wamekutana na kujadili mwenendo wa hali ya kilimo nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo MHE.BASHE amesema kuwa serikali imejiandaa kwa ajili ya kupambana na janga hilo kwa kupeleka wataalamu maeneo mbalimbali pamoja na kuandaa dawa ili kupambana na tatizo hilo.

Katika hatua nyingine MHE.BASHE amesema kuwa kumekuwa na changamoto kwa watafiti na wachambuzi wa udongo ambao unafaa kutumia mbolea ambayo hali ambayo imeipelekea changamoto wizara hiyo jinsi ya kumfanya mkulima aweze kumudu gharama ya sampuli ambazo anatakiwa kutumia.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa jukwaa huru la kilimo nchini ANSAF AUDAX RUKONGE ameeleza kuhusu soko la kahawa hapa nchini na kuwashauri wawekezaji kuwekeza zaidi kwa kufungua makampuni mengi.

Nao baadhi ya washirikio wameomba masuala mbalimbali yajashughulikiwe ili  kukuza sekta ya kilimo na ufugaji

Pia Wadau wa sekta ya kilimo wamejadili changamoto zanazoikabili sekta hiyo pamoja na kupatiwa ufumbuzi kupitia kongamano la sita la sera za kilimo ambapo linahitimishwa leo Februari 14,2020.


Share:

Mkurugenzi CRDB , Dk. Shein Wateta Ikulu Zanzibar. Aimwagia Sifa Tele Benki Hiyo.

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja kwa Benki ya CRDB kuendelea kutoa huduma zake kwa pande zote mbili za  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wananchi  wote wafaidike na matunda ya benki hiyo.

Dk. Shein aliyasema hayo , Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha akiwa amefuatana na uongozi wa Benki hiyo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ally Hussein Laay.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein aliipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutoa huduma zake hapa Zanzibar sambamba na mikakati na malengo yake iliyoyaweka katika kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dk. Shein alisisitiza haja kwa Benki hiyo kuongeza matawi yake hapa Zanzibar pamoja na kuipongeza azma yake ya kushirikiana na Serikali katika kuendeleza na kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

Pia, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa mipango waliyoipanga ya kuhakikisha Benki hiyo inaleta tija kwa nchi na wananchi wake huku akieleza matarajio yake makubwa katika uongozi wa Mkurugenzi huyo mpya wa Benki hiyo ya CRDB.

Alisisitiza kuwa iwapo Benki hiyo itaendelea  kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi Benki nyengine hapa nchini zitaweza kupanua wigo kutoka Benki hiyo hatua ambayo itapelekea kufuatwa ile dhana ya uzalendo kwani wananchi, Makampuni na hata Serikali wataitumia benki hiyo ikiwemo kukopa fedha badala ya kwenda kukopa kwenye benki za nje ya nchi.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza kuwa Benki ni taasisi ya kiuchumi hivyo, kuongezeka kwa benki hapa Zanzibar ambapo hivi sasa zipo Benki 13 kutaendelea kuongeza ushindani wa kibiashara sambamba na kukuza uchumi wa Zanzibar ambao umekuwa ukiimarika kila uchao.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza uzoefu alionao wa Benki hiyo kutokana na shughuli zake inazozifanya kwa muda mrefu hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuunga mkono sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo kilimo, afya, viwanda, biashara, miundombinu ya barabara, wajasiriamali na mambo mengineyo.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Benki hiyo ya CRDB kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Benki hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela alimueleza Rais Dk. Shein kuwa atahakikisha anatekeleza vyema majukumu yake ili benki hiyo iendelee kupata mafanikio zaidi.

Alieleza jinsi Benki hiyo inavyofanya kazi zake hapa Zanzibar pamoja na Tanzania Bara na kueleza azma ya Benki ya CRDB ya kuunga mkono miradi mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aliongeza kuwa Benki hiyo inayomilikiwa na Serikali imekwua ikipata mafanikio makubwa katika utoaji wake wa huduma hali ambayo ilitokana na hatua iliyochukuliwa ya kwenda kwa wananchi.

Alieleza kuwa kwa upande wa Zanzibar Benki hiyo ina matawi mawili hapa Zanzibar ambapo tawi moja liko Unguja na jengine liko Pemba na ina wafanyakazi 42 hapa Zanzibar na wateja wapatao 30,062 ikiwa na Mawakala kwa ujumla 145 (128 kwa Unguja na 17 Pemba) sambamba na kutoa huduma za kifedha katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo alieleza azma ya Benki hiyo ya kufungua tawi lake jipya hapa Zanzibar huku akionesha maeneo ambayo Benki yake imedhamiria kushirikiana na Zanzibar yakiwemo miundombinu, kilimo, utalii na ukusanyaji mapato.   

Mkurugenzi huyo pia, alitumia fursa hiyo kumueleza Rais Dk. Shein jinsi Benki ya CRDB ilivyodhamiria kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi ya kimkakati kwa lengo la kuendelea kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ally Hussein Laay kwa upande wake alisema kuwa Benki hiyo inayofuata misingi ya Utawala Bora imekuwa na mikakati na Sera madhubuti katika kuhakikisha inabadilishana madaraka huku akieleza namna Benki hiyo inavyochangia uchumi wa Tanzania.

Aidha, alieleza mafanikio makubwa yaliopatikana tokea kuanza kazi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya Abdulmajib Mussa Nsekela ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Charles Kimei ambaye amestaafu.

Mapema Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akiutambulisha uongozi huo kwa Rais Dk. Shein alieleza jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyoshirikiana na Benki hiyo ya CRDB katika mambo mbali mbali.

Pamoja na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi, Benki ya CRDB imeendelea kutumia mfumo wake imara wa kibiashara ili kutekeleza mkakati wa kuimarisha biashara na uendeshaji wa shughuli zake za kibenki.

Hivi karibuni Benki hiyo imepata tuzo ya Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira ambapo ikidhihirisha utekelezaji wa falsafa yake, imekuwa ikiendelea na dhamira ya kutoa huduma bora zaidi kwa wateja pamoja na bidhaa za kifedha za kisasa kwa wateja binafsi na wakubwa kwa kutumia mifumo imara ya tehama na mtandao wake mpana wa huduma.

Azma na dira ya benki hiyo wakati wote imelenga katika kukidhi mahitaji ya wateja huku ikitumia uwezo wa teknolojia kutoa pato zuri kwa wanahisa pamoja na kujali jamii na jumuiya inayowazunguka ikiwa na kauli mbiu yake isemayo “Benki inayomsikiliza mteja”.

Benki ya CRDB ni taasisi ya kibenki nchini Tanzania iliyo na thamani kubwa ya rasilimali, mikopo na amana za wateja ikiwa na lengo la kujipanua katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo mnamo Julai 29, mwaka 2017 Benki hiyo ilizindua Tawi lake jipya kisiwani Pemba. 

Rajab Mkasaba, 

Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. 

Fax: 024 2231822  
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk 



Share:

Idd Simba kuzikwa leo makaburi ya Mwinyi mkuu Magomeni

Msemaji wa Familia ya Marehemu Idd Simba, Ahmed Simba, amesema kuwa mwili wa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, utapumzishwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, lengo likiwa ni kumpumzisha mahali ambapo Baba zake wote walizikwa.

"Sasa hivi tuko hapa Msasani nyumbani kwake, tutaondoka na mwili mpaka Msikiti wa Manyema utaswaliwa pale kisha tutaelekea Magomeni na atazikwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu, anazikwa kule kwa sababu Baba zake wote wamezikwa hapo" amesema Ahmad.

Waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara Iddi Simba, alifariki Dunia siku ya jana Februari 13, 2020, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa akipatiwa matibabu


Share:

Mbatia Aishauri Serikali Kuhusu masuala ya majanga yanayotokea nchini.

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameishauri Serikali kuweka taasisi au mamlaka ya kuweza kusimamia kwa ukaribu masuala ya majanga yanayotokea nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na mvua zilizosababisha mafuriko na watu kadhaa kupoteza maisha.
 
Aidha alisema sheria ya mwaka 2015 walishauri kuwepo na mamlaka kamili ya kukabiliana na majanga hayo na inatakiwa kusema ni lazima isimamie majanga yote na iwe inachukua hatua haraka.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alisema kuwa suala la maafa ni suala la kitaalamu, hivyo mamlaka hiyo ikiundwa inakuwa na wataalamu maalumu ambao watakuwa maalum kwa kusimamia majanga hayo.


Share:

Serikali yamsaka Nabii anayejitangaza kutoa Tiba ya Corona

 Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Serikali ya Tanzania imemuonya vikali mtu anayejiita Nabii Namba saba ambaye jina lake halisi ni Mosses Mollel kuwa itamchukulia hatua kali iwapo atashindwa kuthibitisha madai  kuwa na uwezo wa kutibu virusi Vya ugonjwa wa Corona .

Nabii huyo ambaye taarifa zake zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akidai anayodawa ya kutibu ugonjwa hatari wa Corona ulioanzia nchini China na kusababisha Vifo Vya watu zaidi ya 1100 hadi sasa,ametakiwa kujisalimisha wizara ya afya na kuthibitisha taarifa hizo. 

Akiongea na Vyombo Vya Habari jijini Arusha,Naibu Waziri wa Afya,Dkt Faustine Ndugulile ameeleza kuwa anazo taarifa za Nabii huyo kujitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake

“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu  anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu  atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huyo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo  hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka  Tiba ya ugonjwa huo.

Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa corona na kuweka mawasiliano yake  kwenye mitandao .

“Ninayodawa hapa Arusha ya kutibu virusi Vya Corona inayowaua Wachina na mataifa mengine. ” sauti ya Nabii huyo.


Share:

Israel Yakabidhi Rasmi Kitengo cha Huduma ya TRAUMA Hospitali ya Benjamin Mkapa

Na Jacquiline Mrisho -  MAELEZO
Serikali ya Israel imeikabidhi rasmi Tanzania Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Majeruhi (TRAUMA UNIT) kilichopo katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo jijini Dodoma


Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dodoma baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Naibu Balozi wa Israel nchini Tanzania, Eyal David baada ya kumaliza kuweka miundombinu, vifaa tiba na kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya watakaotoa huduma katika kitengo hicho.

Dkt. Mahenge ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Pombe Magufuli aligawa viwanja vilivyopo jijini Dodoma kwa Taasisi mbalimbali za Kimataifa hivyo kukiwa na huduma dhaifu za afya hakuna taasisi yoyote ya kigeni itakayokuwa tayari kuleta watu wake.

“Kutokana na uwepo wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Majeruhi chenye huduma zenye hadhi ya kimataifa katika hospitali hii kunaifanya Serikali kujiamini katika kuitangaza nchi kimataifa hasa kukaribisha wageni kuja kuwekeza na kufanya shughuli mbalimbali ndani ya jiji hili”, alisema Dkt. Mahenge.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa Israel nchini Tanzania, Eyal David amesema kuwa afya ni sekta muhimu kati ya sekta kubwa ambazo wana ushirikiano nazo hivyo mradi huo ni ushirikiano wa kisekta baina ya nchi hizo mbili.

“Serikali ya Israel kupitia shirika lake la Maendeleo la MASHAV lilitoa msaada wa kujenga miundombinu na kuweka vifaa tiba ambavyo vimegharimu takriban shilingi bilioni 2.2, hii yote ni njia moja wapo ya kuboresha mahusiano yetu pamoja na kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania”, alisema Naibu Balozi, Eyal.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa palipo na msongamano wa watu magonjwa ya dharura hayaepukiki hivyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuamua kukiweka kitengo hicho jijini Dodoma kwani jiji hilo linategemewa kuwa na ongezeko la watu kwa kiasi kikubwa.

“Sote tunafahamu kuwa wagonjwa wa dharura wasipopata huduma ndani ya muda fulani kuna uwezekano mkubwa wa kupata madhara zaidi ikiwemo ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha hivyo huduma hizo ni za muhimu, na kwa hospitali hii huduma zinazopatikana ni sawa na utakazozipata nchi zingine ikiwemo Israeli”, alisema Dkt. Chandika.

Mnamo Januari 22, 2018 Serikali ya Tanzania na Israel ziliingia makubaliano ya kuanzisha kitengo hicho katika hospitali hiyo ambapo hadi sasa jumla ya wagonjwa 3000 wamehudumiwa.

Mwisho    



 


Share:

Mkutano Wa Kwanza Wa Kamati Ya Mawaziri Wenye Dhamana Ya Menejimenti Ya Maafa Kwa Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika

 Ndugu Wananchi,
Serikali ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein. 


Kaulimbiu ya Mkutano huu: “Ushiriki wa Kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa ni njia bora ya kuimarisha ustahimilivu katika ukanda wan chi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika” (SADC). 

Itakumbukwa kuwa Tanzania ilichukua rasmi nafasi ya Mwenyekiti wa jumuiya kuanzia mwezi Agosti, 2019 kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mwezi Agosti, 2020.  Hatua hii inatokana na utaratibu wa kawaida wa mzunguko wa kushika nafasi hiyo kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.  

Mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar tangu Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akabidhiwe uenyekiti wa jumuiya. Kufanyika kwa mkutano huu ni fursa kubwa kwa wananchi wa Tanzania kwani utasaidia kukuza biashara na utalii katika nchi yetu hasa visiwa vya Zanzibar na kuendelea kujitangaza kimataifa.

Ndugu Wananchi,
Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya menejimenti ya Maafa  imeanzishwa kwa lengo la kulishauri Baraza la Mawaziri wa nchi za jumuiya ya SADC kuhusu masuala ya upunguzaji wa madhara ya maafa kikanda. Lengo mahususi pia ni,  kuwa jukwaa la kubadilishana taarifa na uzoefu wa kiutendaji miongoni mwa nchi wanachama ili kutekeleza kwa ufanisi shughuli za usimamizi wa maafa. 

Ndugu Wananchi, 
Mkutano huu unakuja kipindi ambacho nchi nyingi wanachama katika ukanda huu zimekuwa zikiathiriwa na majanga ya asili mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa. Sote tunakumbuka ukame wa mwaka 2016 ambao uliathiri takribani watu milioni 40 katika ukanda huu na kusababisha ukosefu wa chakula. Idadi hii iliongezeka hadi watu milioni 41.6 katika nchi 13 Wanachama kipindi cha msimu wa 2018/2019.  

Ndugu Wananchi, 
Baadhi ya nchi wanachama ikiwemo; (Komoro, Malawi, Msumbiji na Zimbabwe) kwa mwaka 2019 zilipata mafuriko yaliyosababishwa na Vimbunga Idai na Kenneth. Kutokana madhara ya mafuriko hayo, Gharama za misaada kukabilia na madhara zilikadiriwa kuwa dola milioni 323, wakati gharama za kurejesha hali zilikadiriwa kuwa dola bilioni 10.  

Ili kuweza kupunguza gharama kubwa katika urejesahi wa hali ndio maana katika mkutano wa SADC kujadiliana namna ya kuwekeza katika punguza madhara ya maafa, kwa kuwa Gharama za usimamizi wa maafa kama ya ukamae na mafuriko huzilazimu Nchi Wanachama kuelekeza rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za za maendeleo na badala yake kuelekezwa katika shughuli kurejesha hali.  

Sote tunakumbuka, matukio ya Vimbunga vya Idai na Keneth, katika nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe,  zilizoathirika zaidi. Kutokana na madhara ya Vimbunga  hivyo,  Nchi yetu ilishiriki katika hatua za kurejesha hali,  kwa kutoa misaada ya kibinadamu: ikiwemo tani 24  za dawa za binadamu na mahindi tani 200 kwa nchi  hizi 3 (Msumbiji, Malawi na Zimbabwe). 

Ndugu Wananchi, 
Kwa uzoefu wa aina ya majanga ambayo hutokea katika nchi za SADC, yanadhihirisha umuhimu wa ushirikiano wa kikanda ulio thabiti katika kukabiliana nayo. Majanga haya kwa kiasi kikubwa yanatokana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa, Pia yamekuwa yakitokea magonjwa ya milipuko ya wanyama na mazao, katika ukanda huu ambao asilimia kubwa ya wananchi wake hutegemea sana shughuli za kilimo kwa ustawi wa uchumi. 

Hali hii imekuwa ikichangia kudumaza ukuaji wa uchumi wa kikanda, hivyo hatuna budi kuchukua hatua kwa pamoja za kupunguza madhara, kuimarisha utayari wa kikanda na uwezo wa kukabiliana na maafa. 

Aidha, katika kuchukua hatua za kuimarisha ustahimilivu wa kikanda dhidi ya maafa, Sekretarieti ya Jumuiya kwa kushirikiana na nchi wanachama imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuimarisha ustahimilivu kwa kuandaa Mpango wa Dharura wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa,  kushirikiana kuandaa taarifa za utabiri wa msimu na kutoa tahadhari ya awali kuhusu hatari zitokanazo hali ya hewa pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalam wa nchi wanachama katika fani mbalimbali ikiwemo tathmini, utafutaji na uokoaji.  

Aidha, baadhi ya nchi wanachama ikiwemo Tanzania zimefaidika kwa kupata vifaa na mifumo ya kufuatilia majanga ya mafuriko, ukame na moto wa misituni kwa ajili ya kutoa tahadhari ya awali. 

Ndugu Wananchi, 
Ili kwenda sambamba na juhudi za kikanda na kimataifa, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli,  itaendelea kuimarisha uwezo wake wa usimamizi wa maafa katika nyanja zote. Tayari serikali ya awamu ya Tano imetunga Sheria ya Usimamizi wa Maafa ya Kitaifa Na. 7 ya 2015 na kanuni zake, Tunao Wasifu wa Janga la Mafuriko na Ukame wa Kitaifa na Mkakati wa Taifa Kupunguza Madhara ya Maafa;  

Serikali imefanikiwa kuandaa Mpango wa Dhamira ya Taifa wa Utekelezaji wa Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, pia  Mfumo wa Taifa wa Ufuatiliaji na Taarifa za Gesi Joto umeandaliwa pamoja na  Mipango ya Kukabiliana na Dharura za afya ya binadamu, mifugo na wanyama pia na kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvuna. 

Lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha kila sekta inazingatia hatua za upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango ya maendeleo na uandaaji wa bajeti ili kupunguza madhara kwa jamii na hasara za kiuchumi.  

Ndugu Wananchi, 
Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wanaohusika na Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika mwezi Februari, 2020 visiwani Zanzibar unakusudia kuchochea juhudi zilizopo katika kupunguza madhara ya maafa kwa kuteleleza yafuatayo: 
i.    Kujadili na kupitisha Mkakati wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wa Kikanda 2016 – 2030; 
ii.    Kujadili na kuridhia Mfumo Mkakati wa Ustahimilivu wa Kikanda 2020 – 2025; 
iii.    Kupitia maombi ya nchi wanachama kuunga mkono Sekretarieti ya Jumuiya kupata idhini ya matumizi ya Mfuko wa Fedha za Ufadhili wa Mabadiliko ya Tabianchi. 
iv.    Kupokea taarifa za maendeleo juu ya utekelezaji wa Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mpango Kazi;
v.    Kupokea taarifa ya hatua za utekelezaji wa maazimio mbalimbali ikiwemo kuanzisha Mfuko wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wa Kikanda; kuanzisha Kituo cha Kikanda cha Operesheni ya Maafa; Mpango wa Mazoezi ya Nadharia ya Kukabiliana na Dharura; pendekezo la Mfumo wa Ushirikiano wa Rasilimali ikiwemo wataalam, fedha na vifaa wakati wa dharura; na Utafiti wa Njia Mbadala za Ufadhili wa Majanga katika huduma za kibinadamu na urejeshaji wa miundombinu kutokana na majanga ya asili.  

Mhe. Jenista Mhagama (MB)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu 
Sera, Uratibu, Bunge, Uwekezaji, Ajira, Vijana na Wenye Walemavu
 


Share:

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika Ofisi ya Msajili wa Hazina

Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wameelezea kufurahishwa na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, baada ya kutembelea na kukutana na  Menejimenti ya ofisi hiyo yenye jukumu la kusimamia Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa.

Katika mkutano kazi huo, Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka alitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi yake inayosimamia mashirika na taasisi 266.


Share:

Hospitali ya halmashauri ya ushetu suluhisho la wananchi kufuata huduma za afya umbali mrefu.

SALVATORY NTANDU
Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya saba ya  hospitali ya  halmashauri ya Ushetu wilayani kahama kwa asilimia 90 kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga imeagiza kuanza kutolewa kwa huduma za afya kuanzia mwezi machi mwaka huu ili kupunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta  za matibabu.

Hayo yalibainishwa febuari 10 mwaka huu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya hospitali hiyo na kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Michael Matomora kuhakikisha huduma za afya zinaanza kutolewa mwezi machi mwaka huu.

“Anzeni kutoa huduma za afya mara mmoja kwa kutumia majengo haya saba ya awali, tunataka wananchi wetu wapatiwe huduma hapa tunataka kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya halmashauri ya mji kahama ambayo ipo umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka hapa nyamilangano”alisema Mlowa.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kupitia ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015/20 imeahidi kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata ndio maana halmashauri hii ilipatiwa shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Ushetu ambayo itatoa matibabu ya kibigwa katika ukanda huo.

Mlolwa aliongeza kuwa ni lazima wahakikishe wanatumia rasilimali watu ya watumishi wachache walionao kutoa huduma katika hospitali hiyo ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu sambamba kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa miundombinu ya barabara zote za eneo la hospitali hiyo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na ujenzi wa hospitali hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora alisema kuwa watahakikisha mwenzi machi mwaka huu huduma za afya zinaanza kutolewa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za matibabu.

“Kwa mwaka huu wa fedha tumetenga bajeti ya shilingi milioni 500 ambazo zitatumika kukamisha baadhi ya miundombinu ya hospitali hii na tumejipanga kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) na huduma za akinamama na watoto ambazo sisi tuzipa  kipaumbele katika hatua za awali za kutoa huduma za matibabu”alisema Matomora.

Matomora aliongeza kuwa Halamshauri hiyo inayodawa za kutosha na vifaa tiba ambavyo vinatosheleza kuanza kutoa huduma za matibabu kwa kuanzia na watatumia watumishi wachache waliopo katika halmashauri hiyo.

Kuanza kutolewa kwa huduma za matibabu katika hospitali ya ushetu itapunguza msongamamo wa wagonjwa katika hospitali ya mji kahama ambayo inahudumia wagonjwa wa nje zaidi ya elfu 1000 kwa siku kutokana na kuhudumia halmashauri za Mbogwe,Msalala,Ushetu na Nzega.

Mwisho.


Share:

“Tanzania Ni Salama Hakuna Ugonjwa Wa Corona” - Dkt. Ndugulile.

Na Englibert Kayombo, WAMJW, Arusha.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi bado iko salama na hakuna mgonwjwa yeyote mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona. 

Dkt Ndugulile ametoa kauli hiyo akiwa Jijini arusha katika Ziara zake za kikazi ambapo waandishi wa habari walimuuliza juu ya tetesi za uwepo wa ugonjwa huo nchini, pamoja na kutaka kufahamu ukweli wa taarifa za mtu anayedai kuwa na dawa za ugonjwa huo. 

“Niseme tuu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi bado tuko salama na hakuna mgonjwa yeyoteambaye ameripotiwa na amethibitika kuwa na ugonjwa” amesema Dkt Ndugulile. 

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa hawana ugonjwa. 

“Sambamba na hilo tumeendelea kuchukua tahadhari mbalimbali na mimi niko katika Mkoa huu wa Arusha na nitaenda Kilimanjaro kwenda kuangalia utayari” amesmea Dkt. Ndugulile na kuendelea kusema “ Nimepita hapa leo nimeongea na uongozi na nimeridhika na maandalizi ambayo tunayo hapa katika Mkoa huu wa Arusha katika kudhibiti ugonjwa huo” Ameeleza Dkt. Ndugulile 

Akijibu kuhusu mtu ambaye anasema kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo ambaye anajulikana kwa jina la Mosses Mollel maarufu kwa jina la “Nabii namba saba” aliyetoa taarifa za kuwa na dawa yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona, Dkt Ndugulile amesema kuwa anazo taarifa za mtu huyo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akijitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake. 

“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu  anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu  atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile 

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria. 

Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo  hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka  Tiba ya ugonjwa huo. 

Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa virusi vya corona na kuweka mawasiliano yake  kwenye mitandao . 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa mtu yeyote anayetoa tiba asili na mbadala kwanza ni lazima asajiliwe na mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Afya, pili lazima dawa zake ziwe zimesajiliwa na Wizara ya Afya na kusisitiza kuwa nabii huyo pia anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini. 

“Tuepuke kutoa kauli ambazo zinakwenda kuchanganya jamii, na endapo tutabaini mtu huyu hana sifa ambazo anasema kuwa nazo tutamchukulia hatua za kisheria” Amesema Dkt. Ndugulile.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa February 14










Share:

Rais Magufuli Kuzindua Kipindi Cha Pili Cha Awamu Ya Tatu Ya TASAF

Mary Mwakapenda 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam.

Aidha, tukio hili litashuhudiwa pia na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) amesema tathimini ya Utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha Mpango inaonyesha kuwa Mpango huu umesaidia kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini nchini ambapo takwimu zinaonyesha kwamba umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya za walengwa umepungua kwa asilimia 10 na umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa kaya maskini sana nchini.

Mhe. Mkuchika amesema pamoja na mafanikio hayo, walengwa waliofikiwa na sehemu ya kwanza ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini ni asilimia 70% ya wananchi wanaoishi katika hali duni.

“Ili kuwa na maendeleo yanayogusa wananchi wote, Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuendelea na Kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya maskini ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi wa TASAF kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umaskini ikiwa pia ni moja ya agenda kuu katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015.” Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambacho kitazinduliwa na Mhe. Rais kitatekelezwa katika halmashauri 185 za Tanzania bara, Unguja na Pemba kwenye vijiji/mitaa/shehia zote nchini na kujumuisha maeneo ya vijiji/mitaa /shehia ambayo hayakupata fursa hiyo katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wake ambacho kilikamilika mwezi Disemba mwaka jana (2019).

Aidha, Kipindi hiki kitafikia Kaya milioni 1.4 zenye jumla ya watu milioni 7 kote nchini hii ikiwa ni nyongeza ya kaya laki tatu ukilinganisha na kaya zilizofikiwa katika kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu.

Mhe. Mkuchika amesema mkazo mkubwa katika kipindi cha pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango wa KUFANYA KAZI ili kuongeza kipato, pia huduma za jamii zitaongezwa na kuboreshwa ili kuendeleza rasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa elimu na afya.

“Ni matarajio ya Serikali kupitia utekelezaji wa shughuli za TASAF katika kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu kuwa kiwango cha umaskini kitapungua na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi ukiwemo ule wa viwanda ambayo ni agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.” Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Mhe. Mkuchika ametoa rai kwa Watanzaia kuhakikisha wanaosajiliwa kwenye Mpango huu ni wale tu waliotimiza vigezo vilivyowekwa na sio vinginevyo ili kuepuka usumbufu.


Share:

Thursday, 13 February 2020

Procurement Manager at Stanbic Bank

Stanbic Bank Tanzania Limited is a full service commercial bank which specializes m providing facilities and services to public and private sector corporations, diplomatic missions and international organizations Job Title: Procurement Manager Report to: Head of Finance Division: Finance. Procurement Job Purpose: The incumbent will be responsible to ensure that the procurement standards, policies and procedures governing all… Read More »

The post Procurement Manager at Stanbic Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Unit Head, Recoveries Job at KCB Bank Tanzania

Job Title Unit Head, Recoveries Location TANZANIA Organization Name KCB Bank Tanzania Ltd Department Description Brief Description To provide special attention and support to distressed banking relationships by ensuring proper co-ordination and control of all watch list and non-performing loans thereby preventing losses, maximizing recoveries and restoring profits through rehabilitation, restructuring and direct recovery. The role will have… Read More »

The post Unit Head, Recoveries Job at KCB Bank Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Officer at TAMWA

POST: Program Officer Tanzania Media Women’s Association, (TAMWA) calls for applications from committed personnel preferably a woman. ORGANIZATION DESCRIPTION The Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) is a non-profit sharing, non-governmental and non-partisan organization registered under the Societies Ordinance on 17th of November, 1987 with registration number SO 6763. The Association in 2004 complied with the new NGO law… Read More »

The post Program Officer at TAMWA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BENKI YA STANDARD CHARTERED YAIKOPESHA TANZANIA SH. TRILIONI 3.3 KUJENGA RELI YA KISASA

 
Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakionesha Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakibadilishana Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3
ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020.

Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani, wakitia saini makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3, zilizotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto)), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani (wa tatu kulia), wakitia saini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chattered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohusika na kutoa mkopo huo pamoja na utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), wakiwemo Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet (wa pili kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg (wa nne kushoto) baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Doto James mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida
 Baadhi ya Mabalozi na Wadau wengine mbalimbali wa Maendeleo wakishuhudia utiaji saini wa Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida.
 Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi
 Meza kuu ikifurahia kwa pamoja huku wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza jambo na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kusaini Hati za Mkataba wa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR)

***
SERIKALI kupitia Wizara ya fedha imeweza kupata mkopo wa shilingi trilioni 3.3 kupitia waabia 17 wakishirikiana na benki ya Standard Chartered ili kuwezesha mradi wa reli ya kisasa kukamilika kwa wakati.

Akizungumza katika hafla ya usainishaji wa mikataba ya mkopo huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango amesema kuwa kila mara wamekuwa wanaomba mabenki ya hapa nchini kuchangia katika miradi mikubwa ya vipaumbele vya taifa ili kuweza kufikia malengo yetu kama taifa.

“Mradi huu wa kujenga reli ya kisasa ni mradi ambao unakwenda kubadilisha maisha ya wananchi wakitanzania, hivi sasa unavyojengwa unawaajiri watanzania wengi, mradi huu unatumia baadhi ya vifaa ambavyo vinazalishwa hapa nchini hususani saruji, mchanga lakini nguvu kazi ni ya vijana wetu”. Amesema Dkt.Mpango.

Aidha Dkt.Mpango amesema kuwa deni la nchi yetu bado ni himilivu na ni lazima tukope kwasababu reli hii tunawekeza takribani miaka 200 ijayo. Hii reli iliyopo (ya zamani) imekuwepo takribani miaka 100, hii ya kisasa itakaa zaidi ya miaka 200.

“Kuna baadhi ya waabia wetu tena wa siku nyingi tuliwaomba waingie kwenye safari hii ya kuchangia mkopo wala si kama wanatupa bure lakini walinikatalia kwahiyo tunashukuru sana kupitia kwenu serikali ya Denmark  na serikali ya Sweden kuwa waabia wazuri na marafiki wa watanzania”. Ameongeza Dkt.Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani amesema kuwa zoezi la kuwekeana saini ya makubaliano ya mkopo kwaajili ya mradi wa reli ya kisasa ni hatua kubwa hasa katika suala la uchumi pamoja na upande wa uwekezaji.

“Afrika inabaki kuwa kipaumbele kwa biashara yetu na wateja kwa ujumla, tunajivunia kutumia utaalamu wetu kusaidia serikali ya Tanzania na fedha zinazohitajika kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR”. Amesema Sanjay.

Pamoja na hayo Sanjay amesema kuwa upatikanaji wa wawekezaji 17 kusaidia mkopo huo ni juhudi kubwa imefanyika hivyo tutegemee kuwepo kwa maendeleo pamoja na ukuaji wa uchumi.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa mpaka kuwezesha upatikanaji wa mkopo kwaajili ya mradi huo, kutaongezeka kwa kasi ya ujenzi huo kwani mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Morogoro umefikia asilimia 73, hivyo mkopo huo utawezesha ujenzi wa reli hiyo kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger