Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameishauri Serikali kuweka taasisi au mamlaka ya kuweza kusimamia kwa ukaribu masuala ya majanga yanayotokea nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na mvua zilizosababisha mafuriko na watu kadhaa kupoteza maisha.
Aidha alisema sheria ya mwaka 2015 walishauri kuwepo na mamlaka kamili ya kukabiliana na majanga hayo na inatakiwa kusema ni lazima isimamie majanga yote na iwe inachukua hatua haraka.
Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alisema kuwa suala la maafa ni suala la kitaalamu, hivyo mamlaka hiyo ikiundwa inakuwa na wataalamu maalumu ambao watakuwa maalum kwa kusimamia majanga hayo.
0 comments:
Post a Comment