Monday, 10 February 2020

Wakulima Wa Mahindi Tabora Waomba Kupatiwa Mbolea Ya Urea

SALVATORY NTANDU
Uhaba wa mbolea aina ya  UREA katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/20 mkoani Tabora  umetajwa kuchangia  wakulima wa zao la mahindi kuzalisha kwa kiwango cha chini na kusababisha baadhi ya wakulima kuiomba kampuni ya usambazaji pembejeo za kilimo ya PETROBENA kuanza kuwakopesha kwa msimu ujao.

Hayo yalibainishwa febuari sita mwaka huu na Wakulima wa zao hilo kwenye mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) ambapo walidai mwaka huu uzalishaji wa mahindi umeshuka kutoka na kukosekana kwa mbolea aina ya UREA.

Juma Madoshi ni mmoja wa wakulima wa zao la mahindi mkoani humo alisema kuwa familia nyingi huenda zikakabiliwa na uhaba wa chakula mwaka huu kutokana na  uhaba wa mbolea hiyo na kuiomba kampuni ya usambazaji Pembejeo za kilimo ya PETROBENA kuwakopesha UREA kwa msimu ujao.

“Sisi wakulima wa zao la mahindi mwaka huu tutapata chakula kidogo,tumezoea kuzalisha kwa wingi,tunaiomba serikali kupita viongozi wetu wa chama chetu (WETCU) kufanya mazungumzo na PETROBENA ili msimu ujao tusipate changamoto hii” alisema Madoshi.

Nae Monika Manwali mkulima wa zao la tumbaku mkoani humo alisema awali walikuwa wanakopeshwa mbelea na kampuni za ununuzi wa zao hilo ambazo walikuwa wanazitumia katika kilimo cha cha mahindi lakini mwaka huu imekuwa tofauti ikilinganishwa mwaka huu ambapo utaratibu umebadilika.

“Tunaomba kukopeshwa mifuko miwili ya UREA ambayo inatosha kuitumia kwenye hekari mbili na itasaidia wakulima kupata mahindi  yakutosha ambayo yatasaidia familia zetu kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha kwa mwaka mzima”alisema Manwali.

Akizungumza kwenye mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri alizitaka kampuni za usambazaji wa pembejeo za kilimo kuhakikisha wanasambaza mbolea kwa wakati ili kwenda sambamba na msimu wa kilimo wa mwaka huu.

“Msimu wa kilimo umeanza muda mrefu sisi kama serikali hatukubali kuona wakulima wetu wanaendelea kuteseka kwa kukosa mbolea aina ya UREA licha ya kuwa na mashamba ya kutosha na nguvu kazi ipo”alisema Mwanri.

Katika hatua nyingine Mwanri alisema kuwa kwa msimu ujao wakulima watakaobainika mwaka huu hawajapanda miti katika mashamba yao hawataruhusiwa kulima zao la tumbaku hivyo ni budi wakulima wote wakazingatia maelekezo ya serikali.

Mwisho.


Share:

Crew Scheduling Officer Job at Precision Air

Precision Air Services Plc is a fast growing private Tanzanian airline which operates in Partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction, We wish to invite applications from suitably qualified candidates to fill in this… Read More »

The post Crew Scheduling Officer Job at Precision Air appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales & Business Development Manager at Tancoal

Tancoal is a limited liability company incorporated and operating in Tanzania. Tancoal is largely a Coal mining and trading company with its mine situated at Ngaka, Mbalawala Area, Mbinga District, Ruvuma Region. ’Tancoal welcomes candidates to join the company to fill the below mentioned post. Title: Sales & Business Development Manager Department: Sales & Marketing Overall Purpose of… Read More »

The post Sales & Business Development Manager at Tancoal appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales And Commercial Officer Job at Netis Tanzania LTD

JOB TITLE: POSITION SALES AND COMMERCIAL OFFICER INDUSTRY: Telecommunication DUTY STATION: DAR ES SALAAM PURPOSE Sales and Commercial Officer is responsible for generating revenues for the company through new business opportunities with a particular focus on securing and managing business opportunities, set out short and long term strategies for business expansion at minimal costs with effective achievements. The… Read More »

The post Sales And Commercial Officer Job at Netis Tanzania LTD appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wanajeshi na Polisi wavamia bunge la El Salvador Wakitaka Muswada Wao Upitishwe

Wanajeshi na maafisa wa polisi waliojihami nchini El Salvador wamevamia bunge , wakitaka kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu.

Waliingia katika jengo la bunge wakati rais Nayib Bukele alipokuwa anakaribia kuwahutubia wabunge .

Siku ya Ijumaa aliwapatia siku saba za kuunga mkono mpango wake wa kuchukua mkopo. Viongozi wa upinzani walitaja uvamizi huo wa wanajeshi bungeni kuwa kama kitendo cha kutishia.

Taifa la El salvador lina viwango vya juu vya mauaji duniani. Ghasia nyingi hutekelezwa na magenge ya uhalifu ambayo hufanya kazi katika eneo la Marekani ya kati.

Rais Bukele ambaye alichukua mamlaka mnamo mwezi Juni 2019 , anataka kutumia mkopo huo kuimarisha vifaa vya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vita dhidi ya uhalifu.

Ameahidi kukabiliana na ghasia zinazotekelezwa na wahalifu pamoja na ufisadi katika taifa hilo lenye viwango vya juu vya umasikini.


Share:

Wizara Ya Kilimo Yasema Tanzania Haijavamiwa Na Nzige wa Jangwani

Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet N.Hasunga (Mb) jana Jumapili anawafahamisha wakulima na wananchi kwa ujumla kuwa taarifa zinazoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa nzige wa Jangwani nchini  hususan mkoa wa Kilimanjaro siyo za kweli.

Mhe.Hasunga amesema hayo wakati alipoongea na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1) na kusema “ hakuna taarifa za kitaalam zilizothibitisha uwepo wa nzige kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ila ni kweli Kuna nzige wameonekana Kaunti ya Kajiado nchini Kenya takribani kilomita 50 toka mpakani na Tanzania”  alisema Waziri wa Kilimo

Wataalam wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo duniani (FAO) linaendelea na ufuatiliaji wa viashiria vya uwepo wa nzige na tayari hatua za awali za kuwadhibiti endapo wataingia nchini zimechukuliwa. Hatua hizo ni pamoja na Mashirika ya kimataifa ambayo sisi ni wanachama kutuahidi ndege tatu maalum za kunyunyizia dawa na uwepo wa dawa za tahadhali kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Wizara inatoa wito kwa wakulima, maafisa ugani na kilimo na wadau wote wa kilimo kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa sahihi kwa serikali endapo kutajitokeza viashiria vya nzige kwenye maeneo ya mashamba.

Aidha,vyombo vya habari vinasisitizwa kutoa taarifa sahihi na za ukweli ili kuepusha sintofahamu kwa wakulima.

Imetolewa na ;
Prof. Siza D. Tumbo
KAIMU KATIBU MKUU


Share:

Wananchi Kijiji Cha Kalenge Waishukuru Serikali Kuwajengea Zahanati

Na.Catherine Sungura-Uvinza
Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani hapa wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yamebainishwa jana  na wakazi wa kijiji hicho wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya usimamizi shirikishi mkoani kigoma ambayo inafanywa na wizara ya afya pamoja na TAMISEMI.

Akiongea kwa furaha bi. Marystela Chishako alisema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani kwa kupata zahanati hiyo imewasaidia kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya kujifungua ambayo awali walikua wakiifuata kigoma mjini.

"Tunashukuru kwa serikali hii kutukumbuka mkoa wa kigoma,siku za nyuma mama akitaka kujifungua ilibidi aende kigoma mjini,ila hivi sasa tunajifungulia hapa hapa kwenye zahanati na tunapata huduma muhimu hapa hapa".

Aidha, alisema zahanati hiyo imewasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani kipindi cha nyuma walikua wakipata matatizo njiani kwa sababu walikua wakisafiri umbali mrefu na kupelekea kupata matatizo wakiwa njiani.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt.Chaula aliwahidi kulifanyia kazi ombi lao la kupatiwa kituo cha afya kwani wameshaomba kwa kufuata utaratibu kupitia mkoa.

"Ninawapongeza kwa sababu mmejua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya,kwahiyo maombi yataletwa wizara ya afya kutoka TAMISEMI,na katika ziara yangu nimeongozana nao hapa na nimepokea ombi hili najua ukitoa ahadi lazima utimize".Alisema Dkt. Chaula

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amesema atahakikisha wanapata fedha ili kutimiza ndoto za wananchi hao"mmefanya wajibu wenu na uzalendo mkubwa wa kuipenda nchi yenu kwa kujituma mpaka mmetenga eneo na kuweka mawe na mchanga, hivyo serikali itaongezea nguvu pale mlipoanzisha.

Wakazi wa kijiji hicho wametenga eneo la hekari ishiriki,kukusanya mawe pamoja na mchanga kwa kujitolea ili kuweza kujenga kituo cha afya ikiwa ni juhudi za kuiunga mkono serikali kwa kutatua changamoto za huduma za afya karibu na wananchi.

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu February 10



















Share:

Sunday, 9 February 2020

LIFAHAMU KABILA LA WASUKUMA...AINA ZA WASUKUMA, MILA NA DESTURI ZA WASUKUMA


WATU WENGI WAMEKUWA WAKILIPONDA KABILA LA WASUKUMA LAKINI HUU NDIO UKWELI KUHUSU WASUKUMA NA HII NDIO HISTORIA YAO TAFADHALI JITAHIDI KUISOMA HADI MWISHO ANGALAU UPATE KITU.

Wasukuma limetokana na neno SUKUMA(KASIKAZINI).Hivyo Msukuma ni mtu wa Kasikazini.

Lakini Wasukuma haimaanishi tu watu wa kaskazini bali wanajumuishwa pia watu wa 

1.Mashariki(Bhanakiya:Ntuzu):Mkoa wa Simiyu.

2.Kusini(Wadakama,hawa wanaweza kuwa Shinyanga ama Tabora kutegemeana upo wapi). 

Msukuma wa Mwanza yeye ndio anaona yupo kaskazini hasa kuliko wote kwa hiyo akiwaita watu wa Shinyanga ni wa Kusini(Wadakama) hawezi kuwa amekosea.

Japo ukiwa Shinyanga napo utawasikia watu wa Shinyanga wakisema wao wapo kaskazini hivyo ni wasukuma na kusini yao ndio kuna wadakama(Mkoa wa Tabora ndio upo kusini).

 Inajulikana zaidi kuwa Wenyeji wa Tabora ni Wanyamwezi.Usukumani hakuna kabila la Wanyamwezi bali wanaitwa Wadakama. Japo ukifika Tabora wilaya ya Sikonge na Urambo hasa yenye Wanyamwezi huku wilaya zingine zikiwa kwa kiasi kikubwa zimekaliwa na wasukuma waliotokea Shinyanga na Mwanza miaka mingi iliyopita.

3.Magharibi(Bhanang'weli). Huku utakutana na Wasumva/Wasumbwa. Hawa ndio wanachukua sehemu ya watu wa Magharibi.

Wasumbwa kama ilivyo kwa Wanyamwezi wao wanaonekana kama si sehemu ya Wasukuma lakini ni sehemu ya wasukuma na karibu kila kitu kinafanana kuanzia lugha,mila na desturi na utamaduni wao.

4.Kaskazini(Wasukuma).
Kwa hiyo Wasukuma wamegawanyika katika pande kuu nne za dunia na jina la pande moja ya Kaskazini ndio lililochukua nafasi ya pande zingine zote.

Kabila la wasukuma linapatikana mikoa mitano Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu na Tabora.

Hii ni mikoa ya Wasukuma. Japo mkoa wa Tabora unajulikana zaidi kama mkoa wa Wanyamwezi na si wasukuma. Japo wanyamwezi asili kabisa ni wachache na wanachukua wilaya ya Sikonge na Mirambo, wilaya zingine zikikaliwa na Wasukuma kuanzia Igunga na Nzega ama mchanganyiko kama Uyui.

hii ni mikoa asili ambayo wasukuma wanatokea.Lakini Wasukuma wengi pia wanapatikana katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Morogoro.Ambapo wamehamia huko kwa ajili ya kufata kilimo na malisho ya mifugo.Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi nchini Tanzania likifuatiwa na Kabila la Wahaya na baadae Wachagga.

KILIMO NA MIFUGO.
Wasukuma wanafuga kwa wingi ng'ombe,mbuzi na kwa uchache kondoo.

Kwa harakaharaka wasukuma ndio kabila linalofuga ng'ombe wengi zaidi kati ya makabila yanayofuga.mfano sensa ya mwaka 2002 ilionesha kuwa mkoa uliokuwa na ng'ombe wengi zaidi ulikuwa mkoa wa Shinyanga(Shinyanga+Simiyu kwa sasa).

 Kwa kawaida makabila mengine yote ya wafugaji ukiwatoa wasukuma hakuna kabila lingine ambalo linachukua mkoa mzima. hakuna ubishi kuwa ng'ombe wengi zaidi katika nchi yetu wanamilikiwa na jamii ya wasukuma hasa ukizingatia kuwa mbali na Shinyanga kabla ya kugawanywa bado mkoa wa Mwanza(Mwanza na Geita) na Tabora nayo ilikuwa sehemu ya mikoa ambayo wasukuma wanaishi na kufuga.

Wasukuma pia ni wakulima wa mahindi na mpunga.Zao la biashara Usukumani ni pamba lakini hasa katika wilaya moja ya Maswa iliyopo mkoa wa Simiyu.
MILA NA DESTURI.
Kama ilivyo makabila mengine ya Kiafrika wasukuma wana mila zao na tamaduni zao.Mila za wasukuma zimegawanyika sehemu mbili.

1.Mila za koo ama familia.Hizi hazifanani kabisa kati ya koo na koo.
2.Mila za jumuiya. Hizi zinafana na zinajulikana kwa wanajumuiya/wanachama bila kujali ni wasukuma wa Mwanza,Simiyu(Ntuzu),Tabora(Wanyamwezi),Shinyanga ama wamagharibi(bhanang'weli=wasumbwa).
Jumuiya za mila zipo mbili.

(i)Bhakango,hawa wanafanya kitu kinaitwa bhukango. Mila hizi zinahusu wazazi na watoto wa aina:-

kwanza watoto mapacha. Ukizaa watoto mapacha ni mkosi hivyo lazima ufanye bhukango kuondoa mikosi.wa pili ni watoto waliozaliwa wametanguliza miguu(Kashinje/kashindye). 

Mtoto akitanguliza miguu kwa maana ya kuzaliwa kinyumenyume huo ni mkosi na lazima ufanye bhukango.Wazazi wa mtoto ama watoto mapacha hupelekwa kufanyiwa matambiko maeneo kama mtoni na huko wao watakuwa uchi kabisa huku wakifanyiwa hayo matambiko na wanajumuiya wenzao.

Katika matambiko haya matusi yote husemwa na ndio lugha rasmi inayotumika hata kama wakiwa njiani wanarudi.Matusi ya kutaja majina viungo vya siri hutamkwa bila aibu yoyote mwanzo mwisho.

Kwa wasioshuhudia siku ukibahatika kukutana nao barabarani wanatukana matusi makubwamakubwa njia nzima wala usishangae.
Kwa kawaida kama si mwanajumuiya wa Bhukango hata ukizaa mapacha ama kashinje mila hii hufanyi.Labda mpaka upate mikosi ama matatizo na uelekezwe na wataalamu wa mila kuwa hao mapacha ama huyo kashinje ndio tatizo basi utalazimika na wewe kuwa mwanachama/mwanajumuiya.

Ili uwe mwanachama sharti uzae mapacha,kashinje,ama wewe ni pacha,ama waliokutangulia ni mapacha mfano ni Shija ambaye huzaliwa baada ya mapacha naye ana sifa ya kuwa mkango.
(ii)Bhasweji, hili ni kundi la pili la wanamila wa kisukuma.
Kundi hili ndio hushughulika na matambiko ya kila aina iwe ni kuondoa mikosi,neema ,nk

Hapa si lazima uwe mwanachama wa moja kwa moja kufanya matambiko haya. Ukipata mikosi,laana nk na njia pekee ni ya kuondoa mikosi hiyo ni matambiko basi hawa mabwana watakuja kukufanyia hata kama si mwanachama.Ila matambiko na ngoma watacheza na kufanyia kwako.

Chakula chao hawali kitu kingine zaidi nyama. Fanya ufanyavyo nyama isikosekane. Kama unapika ugali mboga ni nyama. Kama wali mboga ni nyama.Na wanatabia huwa hawaondoki na wanaweza kukaa kwako hata mwezi wanatambika tu.Usipopika nyama siku hiyohiyo wanaondoka.

WASUKUMA NA NDOA.
Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitaala(mke zaidi ya mmoja).

Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahari ya ng'ombe kati ya ng'ombe 7 mpaka 20. hii ni kawaida.lakinia mahali inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 kutegemeana na mazingira ya anaeolewa na muoaji.Lakini kubwa kuliko yote ni uzuri na tabia nzuri ya mwanamke.

Wasukuma huzaa watoto wengi. Kwa wastani watoto kati ya 6 mpaka 8 ama zaidi na hao ni wa mama mmoja.
WASUKUMA NA WANAWAKE WEUPE.
Ni kweli wasukuma wanapenda wanawake weupe ila weupe natural.

Lakini hili la wanawake weupe si la Wasukuma peke yake bali ukweli ni asimilia kubwa ya wanaume wa makabila yote wanapenda wanawake weupe ila wasukuma ndo wanasingiziwa zaidi utazani wengine hawawapendi wanawake weupe.

CHAKULA CHA WASUKUMA.
Ugali wa mahindi,Ugali wa muhogo na mahindi,Wali,Ugali wa mtama(kipindi cha njaa),maziwa,mboga za kisukuma na nyama. Mboga za kisukuma hasa ni mlenda(rangi=kijani:wakati wa masika),Mkalango(rangi=nyeusi:wakati wa kiangazi) na mzubo(rangi=kijani:wakati wa kiangazi).

NGOMA.
Wasukuma wana aina ya ngoma za burudani zaidi ya 15.

USHAMBA WA WASUKUMA.
Kuna mambo mawili hapa.
1.Wasukuma wana watani wao.
Ushamba wa msukuma umejengwa juu ya watani wa msukuma. Ambapo ni kawaida sana kwa makabila watani wa msukuma kumtania msukuma japo utani unaweza kuwa unabeba sehemu ya ukweli kwa anaetaniwa ila haimaanishi ndo wasukuma wote wapo hivyo.Nje ya makabila watani wa msukuma hata makabila mengine yanatania wasukuma hasa kutokana na ukweli kuwa msukuma kwa kiasi kikubwa hanaga tatizo na jamii yoyote ukiacha wamasai waliokuwa wanatuibia ng'ombe zetu enzi na enzi japo hili sasa ni kama halipo.

2.Maisha ya kijijini. Kama ilivyo makabila mengine wasukuma wengi zaidi wanaishi vijijini na maisha ya vijijini yanafanana kwa karibu makabila yote nchini. kama ni uduni wa mavazi na malazi yanafanana na watu wa vijijini katika jamii zingine,Kama ni kutoyafahamu vyema maisha ya mjini basi ni sawa na watu wa vijijini katika makabila mengine hata kwa watani zetu wagogo.kwa hiyo ieleweke kuwa kila kabila lina washamba na wasio washamba kutegemeana na aina ya ushamba na mazingira ya huyo mshamba.

HAKUNA MAUAJI YANAYOLENGA VIKONGWE BALI KUNA MAUAJI YANAYOLENGA WACHAWI NA ALBINO.

Katika jamii ya wasukuma kama ilivyo jamii zingine kuna wachawi.Suala la wachawi limebakia kuwa suala tete toka enzi na enzi.Utamaduni wa toka zamani kuhusu wachawi ni kuwa ukijulikana ni mchawi uliyeshindikana basi utafukuzwa katika utemi(tawala za kitemizamano)huo na kulazimishwa uvuke temi zingine si chini ya tano.

Na ukikaidi unauawa hadharani na jamii kwa kuwa sehemu kubwa hawapendi uchawi na wachawi. Utamaduni huu wa kuwafukuza wachawi walioshindikana ulikuwa ni wa zamani sana na baadhi ya wachawi walilazimika kuishi kwenye mapango kwa kuwa kila sehemu akienda anakataliwa.

Katika mazingira ya sasa mchawi aliyeshindikana kabisa hafukuzwi kama zamani kwa sababu ya mambo ya sheria bali mtu anayerogwa atajaribu kutafuta dawa za kuzuia uchawi na ikishindikana kabisa basi chaguo la mwisho huwa ni mauaji ambapo atalazimika kukodi watu wa kuua(Kama wahalifu wengine wapo watu wamejiajiri katika uhalifu huu wa kufanya mauaji ya kikatiri kwa hawa wanaodhaniwa ni wachawi).Wanaouwawa huuwawa kwa sababu ya uchawi ila imepotoshwa sana kuwa wanaouwawa ni vikongwe wenye macho mekundu.yapo mauaji mengi yametokea ya watu wasio vikongwe kabisa na wala hawana macho mekundu na pia macho mekundi si ishara ya uchawi usukumani ila imepotoshwa sana na ule wimbo wa kusema ana macho mekundu mleteni hapa ale mapanga.

Mauji ya albino ni jambo ambalo halina taarifa za kina hata kwa wasukuma wenyewe tofauti na mauaji ya wachawi ambayo yanaeleweka kabisa katika jamii ya usukumani.Hakuna taarifa za kueleweka kuhusu jambo hili na huenda ni siri iliyobakia kwa watu wachache miaka mingi.Katika usukumani taarifa za biashara ya viungo vya binadamu zimekuwepo toka zamani lakini zikieleza kuwa biashara za viungo kama ngozi zilikuwa zikiiuzwa kongo kwa ajili ya matumizi ya dawa za kichawi huko.Kuna muda hofu ya wachuna ngozi ilikuwapo kubwa miaka ya 90 na ngozi zilizokuwa zinahusishwa na biashara hiyo ni ngozi za binadamu wa kawaida ambaye si albino.

Swala la albino nalo lilipoibuka taarifa nyingi zilikuwa ni zilezile kuwa viuongo hivyo vina soko kubwa katika nchi ya Kongo. Kuna wakati Kongo iliituhumu Tanzania kuwa biashara ya viungo inafanyika nchini kwetu na wanaouwawa Kongo viungo vinaletwa Tanzania huku na Tanzania pia kuna taarifa kuwa soko ni Kongo.Baadae ikaja kudhihirika kupitia vyombo vyetu vya usalama kuwa waganga wa kienyeji ndio wananunua viungo vya albino. Swala hili bado limebakia kuwa na usiri mkubwa na hakuna taarifa za kueleweka ni nini hasa chanzo chake na soko hili liko wapi?

Ukweli uliowazi ni kuwa mauaji yanatekelezwa na watu wachache waliojivika unyama na kujiajiri katika kazi ya kuua ili wapate kipato chao. Na hawa mtandao wao ni mtandao wa kihalifu na si mtandao wa wasukuma Na ndio sababu ikitokea muuaji akajulikana basi anaweza kuuwawa na wanachi wenye hasira kali kwa kuwa hakuna anayependa haya mauaji katika jamii ya usukumani.ukumbuke pia kuwa kanda ya ziwa ndio ina albino wengi zaidi.

UPOLE WA WASUKUMA.
Mwisho kabisa asili ya wasukuma wengi ni wapole,wakarimu na si wachoyo ama wabahiri kama wengi wanvyofikiria pia siyo washamba kama ambavyo wengi wamekuwa wakisambaza picha halisi lakini pia wasukuma huwa na mapenzi ya ukweli akipenda amependa haswa haswa.

Japo haimanishi kuwa hakuna wakali,wachoyo na wabahiri. Nao wapo japo ni wachache sana.

Share:

MZEE WA MILA ZA KISUKUMA AWAMWAGIA SIFA WANAWAKE....AWAPA MBINU ZA KUSHIKA NAFASI ZA UONGOZI

Mzee Mila na Tamaduni za Kabila la Kisukuma Sonda Kabeshi.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtafiti wa kujitegemea wa masuala ya mila na tamaduni za kabila la Wasukuma mzee Sonda Kabeshi ambaye ni Mkazi wa mtaa wa Mwasele kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga ameitaka jamii kuwapa nafasi za uongozi wanawake kwani ni waaminifu na waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ukilinganisha na wanaume. 

Akizungumza na Malunde1 blog leo Jumapili Februari,2020 Mzee Kabeshi amesema masuala ya uongozi katika dunia ya sasa ni ya wote,wanaume na wanawake, hatupo kwenye enzi za utawala wa Kitemi ulioambatana na mila zilizokuwa zinakandamiza wanawake na kuwa na mtazamo kuwa hawawezi kuongoza jamii. 

Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Tanzania,kuchagua madiwani,wabunge na Rais, Mzee Sonda Kabeshi anavikumbusha vyama vya siasa kuwapa nafasi za uongozi wanawake huku akiwasisitiza wanawake kuacha uoga,wajiamini kuwa wanaweza kugombea na kushinda katika uchaguzi na kuwa viongozi. 

“Mwanamke ni mtu mwaminifu sana katika masuala ya utekelezaji,apewe uhuru,nafasi ya kutobanwa.Kitendo cha kumchukulia kuwa mwanamke ni mtu wa kuongozwa tu huo ulikuwa ni mfumo wa kitemi uliokuwa unamkandamiza mwanamke”,amesema Kabeshi. 

“Katika enzi za utawala wa Kitemi, wanaume walikuwa wamejiwekea sheria zao na baadhi ya watu bado wanarithi baadhi ya mila. Mila hizo za zamani zilikuwa zinabagua na kukandamiza kwa mfano Mwanamke hakutakiwa kula hata nyama ya ulimi kwa madai kuwa atamtawala mwanamme,atakuwa sauti ‘ataongea’ kuliko mwanaume. Dunia ilipofikia sasa mila na tamaduni hizo zimepitwa na wakati”,ameeleza Kabeshi. 

Mzee Kabeshi amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwapa nafasi za uongozi wanawake kutokana na uchapakazi na uaminifu wao katika utendaji kazi akibainisha kuwa hata Watemi waliwaamini wanawake, ndiyo maana mtoto wa mwanamke ndiyo alikuwa anapewa Utemi badala ya mtoto wa mwanaume kwa sababu mwanamke wanajua kutunza siri. 

Amebainisha kuwa wanawake wana huruma, wanajua kupanga bajeti na wanafanya kazi kwa nidhamu kubwa kuliko wanaume ambao mara nyingi ndiyo wamekuwa wakijihusisha na ufisadi,ubadhirifu wa mali za umma.

"Endapo mwanamke akifanya kazi bila kuingiliwa na mwanaume utendaji kazi wake utakuwa mzuri sana. 
Ukikuta mwanamke anafanya kazi vibaya,anaharibu kazi ujue kuna mkono wa mwanaume,pengine anapewa maelekezo na ushauri mbaya na mwanaume au pengine ni visa tu vya mwanaume pale anapokataliwa na mwanamke hivyo anaanza kumkwamisha mwanamke huyo”,amefafanua Kabeshi. 

“Muda wa kazi huwezi kumkuta mwanamke yupo baa na sare zake lakini Mwanaume huwa ni mtu wa kwanza kutoka ofisini kwenda kutafuta mambo yasiyohusiana na mambo ya ofisi,mfano kwenda kwenye vijiwe vya kahawa na pombe”,amesema Kabeshi. 

Amewashauri wanawake wenye kiu ya kuwa viongozi katika jamii hususani ngazi za kisiasa kujitafakari na kujiamini kuwa wanaweza kuwa viongozi wazuri wenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii hivyo kuwataka wanaume kuwaunga mkono na kuwapa ushirikiano wanawake. 

“Wapo baadhi ya wanawake wanahofia kugombea nafasi za uongozi katika jamii kwa kuogopa kuvunja ndoa zao kwani kuna wanaume wanahofia wake zao wakiwa viongozi ndoa zao zitavunjika wanadhani wake zao wakiwa viongozi watawasaliti na kuwadharau.Bado kuna wanaume wana mawazo hasi,wanawazia zaidi kuhusu wake zao badala ya kazi za wake zao”,ameeleza Kabeshi. 

“Naomba wanaume waondoe mawazo hasi kwani mwanamke akipata nafasi ni faida yako,ni faida yako. Mke wako akiwa kiongozi mwanaume unapata sifa na unachukuliwa pia kama kiongozi,kama mkeo ni mbunge basi nawe unapata heshima,unakuwa nusu mbunge”,ameshauri Kabeshi. 

Aidha amesema msingi wa uongozi unaanzia nyumbani na baraka inaanzia nyumbani.

 “Mwanamke usitafute uongozi kama unatoroka,mshirikishe mme wako,ndugu zako,wakupe baraka usije akatoka tu na kumwambia mme wako kuwa tayari umejaza fomu,utaleta balaa utaonekana umemdharau mmeo na atasema umepata washauri wengine”,amesisitiza Kabeshi. 

Aidha mzee huyo wa mila amewasihi wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi,pale wanapoona dalili za malengo ya kuonekana yanataka kushindika waombe ushauri kwa watu wanaowazunguka badala ya kukata tamaa. 

“Mwanamke mwenye kiu ya uongozi ukiona mmeo hakupi ushirikiano tafuta watu walio karibu na mme wako ili wakupe ushauri na wamshauri na kuwe na mifano hai kwa kuelezea juu ya wanawake walioshika nyadhifa za uongozi.

“Ewe Mwanaume usimpe kikwazo mkeo. Kama wewe hujaandikiwa kuwa kiongozi,hujapangiwa na Mwenyezi Mungu kuwa kiongozi,muachie nafasi mkeo,kwani yeye ana karama zake na niwakumbushe kuwa nyota ya mme na mke ukizichanganya familia inakuwa bora",amesema Mzee wa mila Kabeshi.

Amebainisha kuwa mambo ya uongozi hayana jinsi ni ya kila mtu, ni akili yako,kipaji chako na karama kutoka kwa mwenyezi Mungu na kwamba unaweza kufanya karama yako isionekane kwa kutojiamini kutenda jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako. 

Mwanaume usimzuie mke wako kwa sababu anaweza kuwa na karama ya uongozi,amejaaliwa karama ya uongozi wewe ukawa kikwazo kwa sababu Mungu kampa karama hiyo….Wanaume waunge mkono wanawake,ikiwezekana wanaume wawe wapiga debe wa wake zao”, ameongeza.

Mzee Kabeshi amesema wanawake wana marafiki wengi zaidi kuliko wanaume katika jamii hivyo endapo watagombea nafasi za uongozi watapata mashabiki wengi na watasaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii. 

“Wanawake ni mama zetu, tukiwapa uongozi wao watatuhesabu sisi kama watoto wao,kwa sababu wana huruma na siku zote kile anachokipata mwanamke huwa anakileta katika familia na jamii tofauti na wanaume ambao wao ni kutoa tu”,amesema. 

“Wanawake wanalindana na kuhurumiana,lakini wanaume wanazomeana pale mwenzao anapopata tukio au balaa.Hata kwenye msiba wanaolia wenye uchungu zaidi ni wanawake.Sisi wanaume hatuna huruma”,ameeleza Kabeshi. 

Mzee Sonda Kabeshi ni Mtafiti wa Kujitegemea wa Mila na Tamaduni za kabila la Wasukuma, mkazi wa mtaa wa Mwasele kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga anapatikana kwa simu namba 0785009781 

Share:

Tanzania Yataka Zifanyike Jitihada Za Kuleta Amani Burundi Na Congo- Drc Kupunguza Mzigo Wa Wakimbizi

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta amani katika maeneo yenye migogoro Barani afrika hususani katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuipunguzia Tanzania mzigo wa wakimbizi ulioubeba kwa muda mrefu hivi sasa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 33 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Nchini Ethiopia ambapo ameongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ya kunyamazisha silaha (silencing the gun) umekuja wakati muafaka kwa kuwa mapigano na kutokuwepo utulivu katika baadhi ya nchi za Afrika zinachelewesha maendeleo katika Bara hilo.

Ameongeza kuwa endapo Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa zitaongeza nguvu katika kunyamazisha silaha na kukawepo amani na utengamano,ni dhahiri viongozi wataelekeza nguvu kubwa  katika maendeleo endelevu ya wananchi na hivyo kupunguza umasikini katika Bara la Afrika ambalo linaonekana kama Bara lililoghubikwa na migogoro na mapigano.

Mhe. Samia Suluhu Hassani pia ameuahidi Umoja wa Afrika kuwa Tanzania itatekeleza kwa kasi mpango wa Umoja huo katika Mapambano dhidi ya Malaria na kwamba Tanzania imedhamiria kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

Katika Mkutano huo wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wameshuhudia mabadilishano ya uenyekiti ambapo Mwenyekiti anayemaliza muda wake  Mhe.Abdel Fattah el-Sisiambae pia ni Rais wa Misri amekabidhi Uenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini Mhe. Cyrill Ramaphosa ambae anakuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.


Share:

Video Mpya : MOTO NKALI - BHASHABIKI

Hii hapa ngoma mpya ya msanii wa nyimbo za asili Moto Nkali inaitwa Bhashabiki...imetengenezwa na Director Manwell...Itazame hapa mtu wangu
Share:

Video Mpya : KUNDI ONG'WAMOTO - NITANAGI

Ninayo ngoma mpya ya msanii wa nyimbo za asili Kundi Ong'wamoto kutoka Misungwi mkoani Mwanza inaitwa Nitanagi...Imetengenezwa na Director Migera wa Mbasha Studio..Tazama video hapa chini

Share:

Video Mpya : KUNDI ONG'WAMOTO - NSEKO


Msanii wa Nyimbo za asili Kundi Ong`wamoto anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Nseko..Ngoma hii imetengenezwa na Director Migera wa Mbasha studio..Tazama video hii hapa chini


Share:

Video Mpya : KUNDI ONG'WAMOTO - LAWAMA



Ninayo hapa Video mpya ya msanii Kundi Ong`wamoto kutoka Misungwi mkoani Mwanza inaitwa Lawama...Imetengenezwa na Directo Migera wa Mbasha Studio itazame hapa chini 

Share:

Mwamposa asitisha makongamano Yake Kutokana na Tukio la Watu 20 Kufariki kwa Kukanyagana

Kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na Mtume Boniface Mwamposa amesema kwa sasa amesitisha makongamano yote kutokana na tukio lililotokea hivi karibuni lililosababisha vifo vya watu 20.
 
Mwamposa  amesema hayo leo Jumapili Februari 09, 2020 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe muda mfupi kabla ya kuanza ibada  ya Jumapili ambayo amesema ni ya upako, ya kufunguliwa na kuponywa.

Watu 20 walifariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa Jumamosi Februari Mosi, 2020 mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro waliposhiriki ibada ya kiongozi huyo katika uwanja wa Majengo, wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyomwagwa milango ya kutokea uwanjani.


“Makongamano mengi nimeyasimamisha kwanza. Tunaomba neema ya Mungu ikapate kusimama na watu, na baada hapo ndipo nitaweka ratiba ya makongamano. Leo lilikuwa liwe kongamano kubwa la kukanyaga mafuta, kwa sababu ya shida iliyotokea tulisimamisha yote, tunataka utulivu na kumuomba Mungu atupe neema ya kupanga mipango mipya.” amesema Nabii na Mtume Mwamposa.

Ametoa pole kwa Watanzania wote kufuatia tukio hilo la Waumini kukanyagana na hatimaye kusababisha vifo na kuongeza kuwa anatambua kuwa tukio hilo limewaumiza Watu wengi pamoja na Serikali.

“Namuachia Mungu yeye mwenyewe asimame, kwa sababu lilikuwa jambo sio dogo, ni zito, limewaumiza Watanzania, serikali imeumia, viongozi wameumia lakini mengi tutayajua hapo mbeleni,” ameeleza Kiongozi huyo wa Kanisa la Inuka Uangaze.




Share:

Nyamapori Sasa Kuuzwa Kihalali Kwenye Mabucha.....Bei ya Wanyapori wa Mbegu nayo Imeshuka

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepitisha kanuni za kuanzisha mabucha ya nyamapori, na pia imerekebisha kanuni za uanzishaji bustani, mashamba, na ranchi za wanyamapori.

Hayo yamesemwa leo Jumapili (Februari 9, 2020) na Waziri Hamis Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewataka Watanzania kuchangamkia fursa hizo za kuichumi za kuuza nyama za wanyamapori kihalali pamoja na kufungua bustani za maonesho ya wanyamapori.

Kigwangalla amesema kuwa kupitia ridhaa iliyotolewa na Rais John Magufuli sasa mwananchi mwenye hamu na nyamapori anaweza kuipata kihalali.

“Tuliahidi kuanzisha mabucha ya nyamapori, tumetekeleza. Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kutoa ridhaa yake tuweze kufanya hivi. Sasa ukiwa na hamu ya nyamapori utaweza kuipata kihalali. Wajasiriamali hii nayo ni fursa mpya, changamkieni,” ameandika Kigwangalla.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger