Tuesday, 12 November 2019

Video Mpya : ELIZABETH MALIGANYA - HAKI ELIMU


Msanii Elizabeth Maliganya kutoka Bariadi mkoani Simiyu ametualika kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Haki Elimu. Video hii imetengenezwa katika studio za Kalunde Media zilizopo Magu mkoani Mwanza... Itazame hapa
Share:

YANGA YATANGAZA KATIBU MKUU MPYA


Makao makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani Dar es salaam.

Klabu ya soka ya Yanga Novemba 11, 2019, imetangaza uteuzi wa Katibu Mkuu mpya, ambaye anakuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo.

Taarifa ya Yanga imemtaja David M. Ruhago kuwa ndio Katibu Mkuu, ambaye ameteuliwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Mshindo Msolla.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo unaongeza idadi ya watendaji ndani ya klabu hiyo.

Ruhago amekuwa mjumbe wa kamati mbalimbali za klabu hiyo katika vipindi tofauti tofauti.
Share:

LIVE: Uzinduzi Wa Kitabu Cha "My Life My Purpose" Cha Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anashiriki hafla ya uzinduzi rasmi wa kitabu cha Historia ya maisha ya Mhe. Benjamin William Mkapa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.Kitabu kianitwa "MY LIFE MY PURPOSE"


Share:

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waongezeka Hadi Asilimia 3.6 % Kutoka Asilimia 3.4

Na: Mwandishi Wetu, MAELEZO -Dodoma
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2. 
 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba2019. 
 
Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209 
 
“Ongezeko hili la mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi  ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba, 2019.” Alisema Bibi. Ruth. 
 
Aidha amesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo hazijumuishi chakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6 kutoka  asilimia 2.7 Septemba, 2019 
 
Fahirisi za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na mwezi Oktoba, 2019 zimepungua kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na badiliko lilivyokuwa kati ya mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019 
 
Alizitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirishi kuwa ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa asilimia 2.1, petrol kwa asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa kama kompyuta kwa asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi. 
 
Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo ndiyo mamlaka ya kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa bei  kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa bei katika nchi hizo utangazwa. 
 
Mwisho



Share:

Wimbo Mpya: Rayvanny – I Love You

Wimbo Mpya: Rayvanny – I Love You


Share:

Waziri Mbarawa Afuta Mamlaka Za Maji 36

Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu mkuu wizara ya Maji Profesa Kilila Mkumbo,amesema serikali imefuta mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 36 na sasa zitahudumiwa na mamlaka za makao makuu ya mikoa 25, zilizoundwa na kuongezewa majukumu ya utoaji huduma katika maeneo yake

Hayo ameyasema jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Wizara juu ya maboresho ya muundo mpya wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini.

Prof.Mkumbo,amesema kuwa katika kuimarisha uendesahiji wa sekta ya usambazaji maji na usafi wa mazingira mijini, Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa, kwa mamalaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria ameongeza maeneo ya huduma za maji.

“Kwa mujibu wa sheria ya huduma za maji na iusafi wa mazingira Na 5, ya mwaka 2019 ameongeza maeneo ya huduma kwa baaadhi ya mamalaka za maji na usafi wa mazingira nchini aidha Waziri wa maji ameanzisha na kufuta baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini”amesema Prof.Mkumbo

Hata hivyo amesema kuwa kwenye mabadiliko hayo kutakuwa na mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 25, katika ngazi ya makao makuu au miji mikuu ya mikoa.

Hata hivyo ameongeza kusema kuwa mamlaka hizo zitahudumia halmashauri zilizopo katika miji mikuu,makao na makuu ya mikoa husika.

“Aidha baadhi ya mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira katika ngazi hii zimeongezewa maeneo ya huduma na kuunganishwa na baadhi ya miji midogo katika mikoa husika au mikoa ya jirani,”amesisitiza

Prof.Mkumbo amezitaja baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira za mikoa zilizoongezewa majukumu kuwa ni pamoja na mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Dar es saalam (DAWASA) ambayo itahudumia hadi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga.

Nyingine ni Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma (DUWASA), ambayo nayo pia itahudumia eneo lake la jiji pamoja na miji ya Kongwa, Bahi na Chamwino

Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mrogoro (MORUWASA) ambayo imeongezewa miji ya Kilosa na Mikumi.

Nyingine ni Mamalaka ya maji na usafi wa mazingira ya Mwanza (MWAUWASA) ambayo itahudumia halmashauri ya jiji la Mwanaza na manispaa zake na mji wa Magu, Nansio na Ngudu

Hata hivyo amesema kuwa Vmamalaka za maji na usafi wa mazingira za miji midogo ya wilaya 40, zitasimamiwa na mamlaka ya maji vijijini (RUWASA).

Baadhi ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira zilizofutwa kati ya 36, ni pamoja na Kibaha WSSA, Kongwa WSSA, Chamwino WSSA, Kilosa, Kyela WSSA, Mikumi WSSA, Pangani WSSA, Magugu WSSA.

Amesema kuwa lengo la Serikali kufanya hivyo ni kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya fedha .


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne November 12





















Share:

Monday, 11 November 2019

Aliyekuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi afungiwa na FIFA miaka 10

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemfungia kwa miaka kumi (10) aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal Malinzi baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.

Mbali na adhabu hiyo, Malinzi pia amepigwa faini ya CHF 500,000 za Uswisi ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.1 za Kitanzania, baada ya uchunguzi wa Kamati ya Maadili ya FIFA uliobaini kuwa Malinzi alihusika katika matumizi mabaya ya fedha za FIFA (FIFA Financial Assistance Programme (FAP) funds), fedha za CAF.

Matumizi mengine aliyohusishwa ni fedha za TFF pamoja na kughushi nyaraka za maazimio ya Kamati ya Utendaji ya TFF kati ya mwaka 2013 na 2017.

Adhabu hiyo inaanza kufanya kazi kuanzia Novemba 8, 2019 na tayari Malinzi mwenyewe ameshajulishwa.

“Kamati imemkuta na hatia ya kuvunja kanuni ya 24 inayohusu kughushi nyaraka, na kanuni ya 28 inayohusu matumizi mabaya ya fedha katika kanuni za maadili ya FIFA toleo la mwaka 2018 na hivyo inamfungia miaka kumi kujihusisha za shughuli zote za soka Kitaifa na Kimataifa”, imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na FIFA.


Share:

CAG Kichere atambulishwa Bungeni

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere leo Jumatatu Novemba 11, 2019 ametambulishwa rasmi bungeni jijini Dodoma, ambapo Spika Job Ndugai ameahidi kuwa, bunge litampatia ushirikiano mkubwa. 

"Nataka nimuhakikishie kuwa, Bunge litakupa ushirikiano wa kila aina na wala hatuna tatizo na ofisi ya CAG kwa hiyo tutakuwa pamoja," amesema Ndugai.

Spika amesema leo mchana atakutana na CAG na wenyeviti wa kamati pamoja ili wajadiliane pamoja na kuzungumza baadhi ya mambo.


Share:

SERIKALI YAPIGA HATUA KUBWA UREJESHWAJI WA KODI YA ONGEZEKOLA THAMANI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imefanikiwa kuwarejeshea wafanyabiashara na wawekezaji Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT baada ya uhakiki wa madai yao kwa lengo la kuimarisha kipato cha mtu mmoja mmoja na uwekezaji nchini.
Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Khadija Nassir Ali, aliyetaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wawekezaji ili kuimarisha uwekezaji.
Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali imelipa zaidi ya asilimia 90 ya VAT kwa watu waliokuwa wakidai Serikali baada ya kufanyika kwa uhakiki wa madai hayo, uhakiki unaendelea kwa asilimia kumi iliyobaki ili kujiridhisha kabla ya kufanya malipo.

“Tulikua na changamoto kubwa ya udanganyifu kwenye eneo la urejeshwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, hivyo Serikali ilianza mkakati wa kujiridhisha na kila muamala unaoletwa ili kuweza kuirejesha kwa wazalishaji, wanunuzi pamoja na viwanda vilivyopo nchini”, alieleza Dkt. Kijaji.
Aidha, akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni, aliyetaka kujua maana ya dhana ya ukuaji wa uchumi kwa kuoanisha na Maisha ya wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa dhana hiyo inatafsiriwa kwa kuangalia upatikanaji, ubora na gharama ya huduma za jamii zinazotolewa na Serikali.
Alisema baadhi ya huduma hizo ni pamoja na elimu, afya, maji, umeme na miundombinu ya usafiri na usafirishaji inayosaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa na na matengenezo ya vyombo vya usafiri.
Dhana nyingine ya kutafsiri ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi ni ushiriki wa wananchi wenyewe katika shughuli za kiuchumi hivyo ukuaji wa uchumi ni matokeo ya ushiriki wa wananchi katika uzalishaji mali na huduma.
Alisema kuwa wananchi wanaoshiriki katika shughuli za uchumi wananufaika kwa tafsiri ya dhana ya ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kijamii zinazotolewa na Serikali pamoja na matokeo ya shughuli zinazofanywa na mwananchi.
Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kufanya jitihada za kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara ili kila mtanzania aweze kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika uzalishaji na huduma.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji katika viwanda utaongeza ajira na uzalishaji katika Sekta ya kilimo kwa kuwa Sekta hiyo inaajiri idadi kubwa ya watu nchini.

Share:

Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mlali Morogoro Yachomwa Moto

Watu wasiojulikana wamevamia na kuchoma moto Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mlali wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, na kuteketeza Nyaraka na baadhi ya samani ambapo tayari watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi wakihusishwa na tukio hilo la kiharifu akiwemo Diwani wa kata hiyo,Frenk Mwananjinje.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa ofisi hiyo, limetokea majira ya  saa 9:00 usiku wa kuamkia Novemba 11, 2019, ambapo zimeshuhudiwa nyaraka mbalimbali zikiwa zimeteketea vibaya na baadhi ya samani ikiwemo Viti, Meza.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata ole Sanare amefika katika eneo la tukio na kuweka wazi kuwa watu waliotekeleza uharifu huo watakamatwa mara moja na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Afisa Mtendaji wa kata hiyo ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi, amedai kuwa hivi karibuni alipokea vitisho kutoka kwa mmoja wa wagombea akimtuhumu kutotenda haki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.


Share:

Polisi Arusha Wafanikiwa Kukamata Bunduki Mbili Za Kivita Na Nyara Za Serikali

Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata bunduki mbili za kivita pamoja na nyara za serikali ambazo ni nyama ya twiga pamoja na vipande viwili vya meno ya tembo sanjari na silaha za jadi yakiwemo mapanga,sime na visu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Jonathan Shana alizitaja silaha hizo kuwa ni AK 47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6 kwenye magazine na G3 yenye namba A36011858 ikiwa na risasi 9ndani ya magazine na kwamba zilikamatwa katika eneo la Naani lililopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya tarafa ya Loliondo Mkoani hapa.

Alisema kukamatwa kwa silaha hizo kunatokana na ushirikiano kati ya jeshi la polisi,Tanapa,Hifadhi ya Ngorongoro,kikosi dhidio ya ujangili(KDU)Kanda ya kaskazini na kikosi kazi cha taifa kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika operesheni inayorndelea huko Loliondo.

“Bunduki hizo zilipatikana baada ya majibizano ya risasi baina ya kikosi kazi hicho kabambe na majangili mara baada ya kuona mashambulizi yamezidi majangili hao walitelekeza silaha hizo na kukimbilia nchi jirani,hata hivyo kikosi kikosi hicho kilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi jangili mmoja ambaye pia alifanikiwa kukimbia huku akivuja damu”alisema Shana.

Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa mnamo tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu katika eneo la Oleng’usa kijiji na kata ya oloipiri ndani ya eneo la pori tengefu la Loliondo walifanikiwa kukamata watu wawili wanaojihusisha na ujangili ambao ni Yamhanga Mwita(19)na Chacha
Marwa(20) wakazi wa Serengeti Mkoani Mara wakiwa wameuwa Twiga.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama hizo porini kwa ajili ya kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande vipande ambapo ndio waliokutwa na panga,sime mbili,kisu tochi pamoja na nyaya za kutegea wanyama zikiwa katika mafungu saba.

Kuhusu meno ya tembo alisema kuwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu majira ya 17:40,maeneo ya mbuyuni wilayani Arumeru waliwakamata watu watano wakiwa na meno hayo pamoja na pikipiki mbili aina za Kinglion namba T917 BUA na Sunlag namba MC 819 ACD ambapo walitokea wilayani Simanjiro mkoani Manyara walipokuwa wameyahifadhi na kwamba walikuja
Mkoani hapa kwa ajili ya kuyauza.

Kadhalika Kamanda Shana alisema kuwa polisi inawashikilia Juma Yahaya(33)na Amani Mbise(32) wanaojishughulisha na kusajili laini za simu,wakazi wa jijini hapa kwa tuhuma za kutumia jina la Gavana wa benki kuu ya Tanzania(BOT)Profesa Frorence Luoga katika mitandao ya kijamii na kuwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina hilo ambapo baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.

“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Sombetini jijini hapa hali ambayo aiendani na kipato chake”alisema

Aliongeza kuwa pia jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ya ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati masoko mbalimbali ya jijini hapa ambapo waliwakamata watoto 105 ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi ya
miaka 18.


Share:

ATHARI ZA MFUMO DUME KWENYE JAMII NI KUBWA-TGNP

Share:

Serikali Yatoa Kauli Mahindi Kupanda Bei

Serikali imesema licha ya bei ya mahindi kuwa juu, haitaingilia kupunguza bei kwani ni nafasi ya wakulima kupata bei wanayotaka.

Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe ametangaza msimamo huo bungeni leo Jumatatu Novemba 11, 2019 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Dk Rafael Chegeni.

“Sasa hivi bei ya vyakula inazidi kupanda na ukiangalia wananchi wengi wanaadhirika na hali hii, gunia la mahindi sasa ni karibu Sh. 100,000 je serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama hizi kwa wananchi,” alihoji Dk. Busega.

Akijibu swali hilo Bashe amesema msimamo wa serikali ni kutokuingilia kushusha bei ya mazao kwa kuwa wakulima wameshapata hasara na hivyo watapunguza gharama za uzalishaji na kuruhusu ushindani katika soko.

“Hatutaingilia kupunguza bei ya mazao kwasababu wakulima wa nchi hii kwa muda mrefu wamepata hasara, huu ni msimamo wa serikali na ieleweke hivyo, njia ya pili tunahamsisha Watanzania kuongeza uzalishajikwani supply ikiwa kubwa demand ikiwa ndogo mazao yatashuka bei.

“Ni bunge hili hili mwaka jana wakati bei ya mahindi kwa mkulima ilikuwa sh. 150 wakasema kwanini tunafunga mipaka, sisi kama serikali hatua tunazozichukua kupunguza gharama za bei sokoni ni pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji, kuruhusu soko kushindana, kwahiyo hatutaingilia kushusha bei, tunayo National Food Reserve Agency na niwaambie wabunge na wakuu wa mikoa pale wanapoona kuna upungufu wa mazao ya chakula sokoni wawasiliane na mawakala hao ili wasambaze chakula katika maeneo hayo,” amesema Bashe.


Share:

DC SAME ATANGAZA VITA NA MAJANGILI WANAOUA WANYAMA KWENYE HIFADHI

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Sitaki ametangaza vita mpya na majangili wanaoingia kwenye hifadhi na kuua wanyama kwamba hawatapata nafasi kutokana namna serikali ilivyojipanga kukabiliana nao huku akieleza watakaokamatwa watashughulikiwa kwa hatua kali za kisheria.

Pia amewataka wabadilishe biashara hiyo na sasa waanza kujikita kwenye kufanya ujenzi wa hoteli za kitalii ili waweze kujiingizia kipato badala ya kufikiria kuendelea kufanya vitendo vya ujangili kwenye hifadhi.

DC Sitaki aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu namna kama serikali walivyojipanga kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ujangili vilivyopo kwenye maeneo yao ambapo alisema watu hao hawana nafasi kwenye wilaya hiyo.


“Labda tu niwaambie kwamba hifadhi zote zina askari nikihesabu majeshi yote niliyokuwa nayo hatutawapa nafasi kwani serikali wamejipanga na ukienda kwenye hifadhi zote ni askari kwa maana ya kuzuia watu wasiingie na kuuwa wanyama na kuharibu mazingira hivyo na ambao watasubutu kufanya hivyo tutawachukua hatua kali kama tukikuta mvua anadhamira mbaya na hifadhi zetu tumesimama imara tunataka vivutio hivyo vizazi vya sasa na na vijavyo vivikute”Alisema DC Sitaki.

Alisema kwamba kasi ya serikali ni kuhakikisha inafanya utalii unakuwa sehemu ya kiuungia mapato kwenye nchi hivyo wo hawawezi kufanya uzembe ambao utafanya vivutio hivyo kupunguza hadhi yake  au kupunguza sifa yake ikiwemo wanyama na kuharibu mazingira.

Hata hivyo alisema kwamba hivi sasa wanafuatilia maeneo ambayo wanyama walikuwa wanapita waone kama maeneo hayo yameendeleza kiasi gani au hayaendelezwa kama hayajaendelezwa yaachwe wazi kusiwe na muingiliano kati ya shughuli za binadamu na wanyama ili kuona namna ya kufanya ili kuondoa hali hiyo.

Akizungumzia suala la wafugaji kuingia mifugo kwenye hifadhi hiyo Mkuu huyo wa wilaya anasema kwamba changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa ilikuwa inawasumbua sana lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa za kusimamia sheria na kutoa elimu kwa wafugaji mifugo idadi ya mifugo inayoingia ngombe na mbuzi wanaoingia kwenye hifadhi hiyo.

Share:

Finance Assistant Job at WHO

Finance Assistant, (Special Services Agreement) – (1905202) Grade: No grade Contractual Arrangement: Special Services Agreement (SSA) Contract duration: N/A Job Posting: Nov 8, 2019, 10:49:50 AM Closing Date: Nov 29, 2019, 10:59:00 PM Primary Location: Tanzania, United Republic of-Dar-es-Salaam Organization: AF_TZA Tanzania Schedule: Full-time IMPORTANT NOTICE: Please note that the deadline for receipt of applications indicated above […]

The post Finance Assistant Job at WHO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Health Policy planning Coordinator Job at WHO

Health Policy planning Coordinator (Roster: Botswana, Eritrea, eSwatini, Gambia, Ghana, Lesotho, Liberia, Malawi, Mozambique, Sierra Leone, Tanzania, South Africa, Uganda, Zambia, Zimbabwe) – (1905039) Grade: P4 Contractual Arrangement: Fixed-term appointment Contract duration: Two (2) years Job Posting: Nov 8, 2019, 7:14:43 PM Closing Date: Nov 30, 2019, 1:59:00 AM Primary Location: Botswana-Gaborone Other Locations: Lesotho-Maseru, […]

The post Health Policy planning Coordinator Job at WHO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger