Monday, 11 November 2019

Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mlali Morogoro Yachomwa Moto

...
Watu wasiojulikana wamevamia na kuchoma moto Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mlali wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, na kuteketeza Nyaraka na baadhi ya samani ambapo tayari watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi wakihusishwa na tukio hilo la kiharifu akiwemo Diwani wa kata hiyo,Frenk Mwananjinje.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa ofisi hiyo, limetokea majira ya  saa 9:00 usiku wa kuamkia Novemba 11, 2019, ambapo zimeshuhudiwa nyaraka mbalimbali zikiwa zimeteketea vibaya na baadhi ya samani ikiwemo Viti, Meza.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata ole Sanare amefika katika eneo la tukio na kuweka wazi kuwa watu waliotekeleza uharifu huo watakamatwa mara moja na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Afisa Mtendaji wa kata hiyo ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi, amedai kuwa hivi karibuni alipokea vitisho kutoka kwa mmoja wa wagombea akimtuhumu kutotenda haki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger